Dada yangu Hilder, sikufahamu na hata wewe hunifahamu, ila nakusoma sana Twitter kama mmoja wa makamanda.
Kabla sijaendelea, naomba kwanza nikupongeze kwa post zako na msimamo yako kwani unaonekana kupinga na kuchukia udhalimu unaoendelea na hapa ndipo pananifanya nikuunge mkono kwani hata mimi nachukizwa sana na mambo kama uonevu, unyanyasaji, mauaji, utesaji, double standards,usaliti na mengineyo ya aina hiyo ambayo kwa sasa yamekuwa sehemu ya maisha yetu katika Taifa hili.
Hata hivyo, kwakuwa unafahamika kwa maana ya kutotumia ID fake huko Twitter, nakushauri uwe makini katika nyendo zako kwani unagusa watu fulani ambao, kwa hulka zao, wanaweza wasiwe wavumilivi hivyo kuwa makini sana.
Endeleza mapambano ila kuwa macho na watu wasiojulikana.