Kuna Watz wapuuzi sana hasa ma-CCM. Bado wanafikiri hii Tanzania bado ni ya Hayati Magufuli. That's very NONSENSE!!!!. Biblia imesema wazi kabisa kuwa Mungu si Mungu wa WAFU na bado imeende mbele zaidi na kusema AMELAANIWA AMTEGEMEAE MWANADAMU tena marehemu!!!!.
Ma-CCM mtegemeeni Mungu na si Marehemu Magufuli...!!!Over n' Out.
Tanzania ni ya watanzania,si ya ccm au chama chochote cha siasa.Ni muhimu sana kulijua hili
Nchi hii ni yetu sote watanzania .hivyo nashauri tabia ya kutusemea watanzania wenzenu ife.
Mfano mzuri ni maziko aliyoyapata magufuli,huo ni ujumbe tosha kwamba watanzania tunataka kuongozwa kwa mfumo alioutumia magufuli.
Kama uliangalia picha zote za msiba,waliovaa uniform za ccm ni wachache sana ukilinganisha na umati ambao hawakujulikana walikuwa wanachama gani.
Biblia umeinukuu vizuri,lakini ina vipengele vingi vya kunukuu.
kimojawapo ni hiki kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohana " heri wafu wafao katika Bwana,........kwa kuwa matendo yao yafuatana nao" Mdo 14:13. Kama wewe ni mkristo unaelewa fika kuwa watumishi wote walioandika vitabu vya injili walikufa lakini maandiko yao waliyoyaandika kwa kuongozwa na Roho wa Mungu hata sasa yanaishi na yanawavusha wanaomtumaini Mungu.
Kwa hiyo mtu anaweza kufa ndio lakini matendo yake yakaishi. Tumesema mara nyingi kuyaenzi mazuri ya baba wa taifa,
sasa ubaya uko wapi tukiyaenzi mazuri ya Magufuli.
Naomba niwe mkweli kwamba,suala la kusema hili zuri na hili baya inategemea na dhamira ya huyo anayetoa maamuzi ya kusema ni wa mlengo gani.
Mfano,kwenye mtaa kikizinduliwa kituo cha polisi.watu wema wanafurahi lakini vibaka na wauza bangi wanachukia hata kuuhama mtaa.