Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.

Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo

Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
Unashangaa hiyo bado hujaona laki juu ya lami,Wikii kulikuwa na marekebisho ya barabara za mijini hasa zile ambazo zina mashimo mashimo au madimbwi,nikiwa katika harakati za hapa na pale nimeshangazwa na hali ya kuona baadhi ya barabara maeneo ya masaki na Posta zikiwa zinawekwa lami juu ya lami ya zamani.

Kwa maana kwamba nimezoea kuona ka kipande fulani ka bara bara kinafanyiwa marekebisho utakuta wanafunga njia kisha wanaharibu au kuvunja na kubomoa ile ya zamani kisha wanaanza upya from the scratch kuitengeneza au kama ni issue ya vilaka inafahamika kuwa wanachonga kile kipande korofi kisha wanaweka kilaka ila kwa hii ambayo nimeiona this week ni kitu kigeni kwangu,naomba engineers Waweze kunielewesha hili limekaaje kitaalamu.
 
Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo
Kwahiyo wanaofanya kazi maeneo hayo watakuwa likizo?
 
1737840449102.png

Kwahiyo wagonjwa waendao na wenye wagonjwa Muhimbili, Regency watembee kwa miguu siku hizo?
Hawa watu wana akili kweli?
 
Poleni sana
Wamesha Poa mm ni Jobless na ni naishi uswahilini huku wala hakuna shida kabisa mama mwajuma ratiba yake iko pale pale mihogo au viazi vitamu vya kukahanga kila siku asubuhi,mama manka duka lake litafungiliwa saa kumi na mbili na nusu asubuhi,urio genge atafungua saa mbili na dakika 45 baada ya kutoka mabibo sokoni,James atafungua banda lake la mkaa saa moja na nusu asubuhi,school bus inayompitia Gift na mdogo wake Frank itapiga honi saa kumi na mbili kamili kama kawaida,Bucha la utumbo la mjomba shida litakuwa wazi kuanzia saa mbili kamili baada ya mjomba shida kurudi kutoka vingunguti machinjioni,na mama kwa mama idaya miguu ya kuku itaendelea kuuzwa kama kawaida kuanzia saa tisa kasoro jioni,kijiwe cha Draft kitakuwa wazi kuanzia saa kumi jioni baada ya wabangaizaji kurudi katika vibarua vyao vya ujenzi na karakana bila kusahau Gereji,boda boda na bajaji kama kawaida hua hawalali,Pub ya anti Mishi itaemdelea kupika kazi muda uleule.
 
Kimsingi inabidi iwe hivyo siku zote. Kama tunataka mji wa Dar es Salaam kuwa wa kisasa na world class
Bodaboda na tuktuks hazipaswi kutumia main roads na kuingia city center.

Waboreshe mfumo wa mwendokasi...
Mbadala wake ni nini kwa hili jiji ambalo vichochoro ni vingi kuliko main roads?
 
Unashangaa hiyo bado hujaona laki juu ya lami,Wikii kulikuwa na marekebisho ya barabara za mijini hasa zile ambazo zina mashimo mashimo au madimbwi,nikiwa katika harakati za hapa na pale nimeshangazwa na hali ya kuona baadhi ya barabara maeneo ya masaki na Posta zikiwa zinawekwa lami juu ya lami ya zamani.

Kwa maana kwamba nimezoea kuona ka kipande fulani ka bara bara kinafanyiwa marekebisho utakuta wanafunga njia kisha wanaharibu au kuvunja na kubomoa ile ya zamani kisha wanaanza upya from the scratch kuitengeneza au kama ni issue ya vilaka inafahamika kuwa wanachonga kile kipande korofi kisha wanaweka kilaka ila kwa hii ambayo nimeiona this week ni kitu kigeni kwangu,naomba engineers Waweze kunielewesha hili limekaaje kitaalamu.
Wanakuja kulitolea ufafanuzi wataalam
 
Kiuchumi hapo tumeanguka. Watu itabidi waache kwenda makazini kufanya kazi wakati huohuo hao wageni wanahudumiwa Kwa kugharamiwa na serikali ya Tanzania
 
Back
Top Bottom