ukuwi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 861
- 1,426
Unashangaa hiyo bado hujaona laki juu ya lami,Wikii kulikuwa na marekebisho ya barabara za mijini hasa zile ambazo zina mashimo mashimo au madimbwi,nikiwa katika harakati za hapa na pale nimeshangazwa na hali ya kuona baadhi ya barabara maeneo ya masaki na Posta zikiwa zinawekwa lami juu ya lami ya zamani.JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.
Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo
Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
Kwa maana kwamba nimezoea kuona ka kipande fulani ka bara bara kinafanyiwa marekebisho utakuta wanafunga njia kisha wanaharibu au kuvunja na kubomoa ile ya zamani kisha wanaanza upya from the scratch kuitengeneza au kama ni issue ya vilaka inafahamika kuwa wanachonga kile kipande korofi kisha wanaweka kilaka ila kwa hii ambayo nimeiona this week ni kitu kigeni kwangu,naomba engineers Waweze kunielewesha hili limekaaje kitaalamu.