Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

Hili la kufungwa barabara limekaaje? Kwa namna hali ilivyokuwa leo kwenye usafiri maeneo ya Posta na Kivukoni mpaka ifike hiyo tarehe 30 tutakuwa hoi

Kiuchumi hapo tumeanguka. Watu itabidi waache kwenda makazini kufanya kazi wakati huohuo hao wageni wanahudumiwa Kwa kugharamiwa na serikali ya Tanzania
kiuchumi hizo siku ni nyingi sana, kuna watu wanategemea kazi walizokuwa wanajishughulisha nazo maeneo hayo.

Changamoto ya usafiri inaongezeka na inasababisha mrundikano wa watu eneo moja kwa muda mrefu.
 
Nimekumbuka kipindi Cha jakaya.ujio wa Obama.
Watu na biashara zao walizolewa,bomoa,fagia fagia Ili kuweka madhari vizuri Kuna mgeni anakuja🤣🤣
Kulifagiliwa mjini kote kusafii
Alivyoondoka tukarudi Tena vilevile
 
Screenshot_20250126_090709_Gallery.jpg


Unashangaa hiyo bado hujaona laki juu ya lami,Wikii kulikuwa na marekebisho ya barabara za mijini hasa zile ambazo zina mashimo mashimo au madimbwi,nikiwa katika harakati za hapa na pale nimeshangazwa na hali ya kuona baadhi ya barabara maeneo ya masaki na Posta zikiwa zinawekwa lami juu ya lami ya zamani.

Kwa maana kwamba nimezoea kuona ka kipande fulani ka bara bara kinafanyiwa marekebisho utakuta wanafunga njia kisha wanaharibu au kuvunja na kubomoa ile ya zamani kisha wanaanza upya from the scratch kuitengeneza au kama ni issue ya vilaka inafahamika kuwa wanachonga kile kipande korofi kisha wanaweka kilaka ila kwa hii ambayo nimeiona this week ni kitu kigeni kwangu,naomba engineers Waweze kunielewesha hili limekaaje kitaalamu.
 
Yaani hii nchi inaongozwa na wajinga na ndio maana ujingaujinga ni mwingi
Ukihoji huu ujinga wanaotufanyia unaonekana mpinzani
 
Nimekumbuka kipindi Cha jakaya.ujio wa Obama.
Watu na biashara zao walizolewa,bomoa,fagia fagia Ili kuweka madhari vizuri Kuna mgeni anakuja🤣🤣
Kulifagiliwa mjini kote kusafii
Alivyoondoka tukarudi Tena vilevile
Huku ni kujidanganya, hii haina tofauti na kufanya usafi ndani alafu uchafu unaukusanyia uvunguni
 
Nje ya bara la Africa; hivi wengine huko duniani nao huaga wanafunga barabara kama huku kwetu? Mfano, mkutano wa marais/nchi za G7 or G8 na wenyewe wanafungaga barabara kama hivi? Kwanini viongozi wa Africa hawanaga imani na wananchi wao? Wanawaibia sana or what? Ingekua enzi za Magufuli nina hakika hu mkutano ungepelekwa Dodoma na sio Dar.
Masikini wakazi wa Kigamboni
 
Hivi Huwa wanakosa kabisa eneo la pembezoni huko wakajifungie wafanye mikutano? Hata huko mbugani huko wangeweza kwenda kukaa mbona?
Kama mjini watu wenye upeo na akili wanahamishwa wakisema wafanyie mbugani na kuna wanyama wasio na akili si ndio watawatoa wote.
 
Yaani hii nchi inaongozwa na wajinga na ndio maana ujingaujinga ni mwingi
Ukihoji huu ujinga wanaotufanyia unaonekana mpinzani
Ukihoji lazima uonekane unataka kukwamisha maendeleo.
 
Back
Top Bottom