Hili la kuweka vibao viwili Kwa Nchi Moja Tanzania na Zanzibar limekaaje?

Wamefanya maksudi ila sio sahihi maana ndani ya Tanzania Kuna Zanzibar kama lengo lilikuwa kuitangaza Zanzibar wametumia njia isiyo sahihi na inaleta taswira mbaya ukizingatia Rais wa Tanzania ni mzanzibar.
Inaleta twasira mbaya kwa kina nani ?
 
Zanzibar Siyo Nchi Haina Kiti UN Japo Bendera Wanayo
Viongozi Wetu Wanaotakiwa Kusimamia Hilo Wamejaa Hofu Bure
Hapo Bango Linalotakiwa Ni Tanzania
wewe ni likichaa kbs siyo nchi kwa vigezo gn? Unaijua katiba ya zanzibar inasemaje khs zanzibar? Inasema zanzibar ni nchi, na kama hujui nimekujuza pia ina bendera, wimbo wa taifa nalo nmekujuza.
 
Inashangaza sana watu kutokujua kuwa Zanzibar ni nchi huru iliyoungana na Tanganyika ambayo nayo ni nchi huru.

Watu wanafikiri eti Zanzibar ni kama mkoa, hawajui Zanzibar ina mikoa yake ambayo wameiweka pamoja na ya Tanganyika ikatoka ya muungano.
 
Hiyo sio sahihi kabisa. Wameanza chokochoko tena. Wanaanza na kibao kisha bendera. Mambo ya nje ni masuala ya muungano tusiwaruhusu kuleta akili na ubishi wao wa kiswahili. Muliona huko nyuma wakisema wanataka muungano lakini hapohapo wanadai wawe na kiti umoja wa mataifa, wakidai mabalozi wao na rais wao akienda nje apigiwe mizinga.
 
KATIBA YA ZANZIBAR INASEMA ZANZIBAR NI NCHI sjui kama unalijua hli.
 
Tanzania ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na zanzibar ila naona kuna Tanzania na zanzbari peke yake ,huwa najiuliza Tanganyika ilienda wap?
Si ndio imewekwa chini ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Ipo ila haitajwi jina isije ikaamka ikawa shida
 
tunangoja samia hatoke madarakanii iwe kivyovyote vile then tunahitaji rais mtanganyika mwenye uchungu na tanganyika yake ndio tunazishe hiyo agenda ya kuvunja huo muungano....tutaona nani huwa anamtegemea mwenzake
Ni rahisi zaidi na hakutakuwa na madhara makubwa kwa raia kutangaza kuwa Tanzania ni moja , serikali moja na dola moja kuliko kuvunja muungano.
 
Huu Muungano ulikua ni wakulazimishwa,Kwa sababu za kiusalama.Ndio maana hata ulikotokea hakujulikani,Karume hakutaka huu Muungano.
 
KATIBA YA ZANZIBAR INASEMA ZANZIBAR NI NCHI sjui kama unalijua hli.
NCHI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ni muunganiko wa nchi mbili(Tanganyika na zanzibar)
so,unataka kusema kuna katiba ya zanzibar na katiba ya bara?
ninachojua katiba iliundwa 1967 kwenye azimio la arusha,badae ikarekebishwa 1977 ndio tunatumia hadi leo
hii katiba ya 1977 ni ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania(katika hii katiba hakuna sehemu inayorefer katiba nyingne ya bara au visiwani)
so kiujumla kwa ninavyojua mimi kikatiba zanzibar ni tanzania visiwani
tofaut ni kwamba wana serikali yao.....
hii ni tofaut na USA
kule wote wapo ndani ya USA ila nevada na washington kila mtu ana katiba yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…