Hili la Maalim Seif kupatikana na maambukizi ya COVID19 linatia ukakasi. Ni aibu kubwa kwa Serikali yetu

Hili la Maalim Seif kupatikana na maambukizi ya COVID19 linatia ukakasi. Ni aibu kubwa kwa Serikali yetu

La msing n kujilinda na kuwalinda uwapendao, usitumie nguvu nyingii et mpk serikal iseme covid ipo, serikal ina msimamo wake, na haiyumbishwi na keyboard worriors, 😂
 
Mkuu,

Kwani kabla ya Maalim kusema anaumwa wewe ulikuwa unajua Tanzania hakuna Coronavirus?

Mbona watu wamejaa Aga Khan Hospital haina nafasi? Mbona watu kibao wanaugulia mtaani na kujipiga nyungu tu mpaka wanamaliza ngwe hii?

Yani serikali kuacha kutoa data ukaamini ugonjwa haupo Tanzania?
 
Mnaleta siasa kwenye uhai wa watu kila siku. Tukiwaambia acheni utani linapokuja suala la maisha mnakumbatia vyama. Huyu mtu kwa vile yeye na familia yake wana uwezo wa kutibiwa popote kwa gharama yoyote kwa gharama za serikali, basi hajali maisha ya mwingine tofauti na watu wake.
Watanzania amkeni Corona ipo nchini tena kwa wingi, usipichukua hatua utaiacha familia yako kwenye mateso makubwa maana wengi tunategemewa na watoto, wake/waume na wazazi wetu.
Unafahamu kuwa Covid 19 inashambulia zaidi watu wenye uwezo na kipato kikubwa?
 
Taaarifa siyo za kweli zimelenga kuleta taharuki kwa mujibu taarifa nilizopata
 
Hapo lazima dunia nzima itatushangaa na kutuona sisi ni watu wa ajabu kuwahi kutokea tangu kuumbwa kwa dunia kwani ni juzi tu tulikuwa tunaibeza Chanjo ya corona kwa kutangaza kuwa tupo salama na hatuna Korona kabisa alafu leo Hii Makamu wa Rais anakutwa na virusi vya korona
. Ni aibu ya mwaka
Aibu gani?
Hata waziri mkuu wa UK aliugua corona
Jifukizeni badala ya kusubiri lockdown
 
Back
Top Bottom