Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?

huondo ukweli, kwan ni uongo
COYssW7UEAAV6Zu.jpg

swissme
 
Mkuu heshima kwako. Bila shaka una kipaji au IQ ya kipekee. Nikiri kuwa mimi ni mmoja wa wenye kufikiri kuwa kauli za rais au kiongozi yeyote wa umma lazima ziwe katika mfumo wa 1+1=2 au 2+5=7 (kwa mfano wako) ili kutoruhusu mikanganyiko yoyote ya uelewa kwa wananchi. Ndivyo tulivyozoea kwa awamu zilizopita na kwa viongozi wa nchi nyingine.

Safari hii itabidi niwe nasoma mabandiko yako kuelewa kauli za Magufuli. Lakini unao uhakika kuwa Mheshimiwa huyu hana mielekeo ya kuachia "gaffes" katika "haraka" zake za kutoa maagizo ya kuvutia wanyonge?


Wazungu wanasema ,,sit back, relax and enjoy the ride" au kwa kikwetu tuliza boli mambo yanakwenda, usiwekeze muda wako kwenye mambo madogo madogo na yasiyo na tija bali angalia bigger picture kama, mishahara hewa iliyokuwa inatafuna mabilioni kila mwezi sasa inakaribia kuwa historia na hizo fedha kuwekezwa kwenye mambo ya kimaendeleo, zaidi ya 40% ya bajeti yetu kwa mara ya kwanza ktk Historia ya nchi yetu inakwenda kwenye mambo ya kimaendeleo, Reli ya kati inajengwa upya ambapo ikikamilika Treni zitakuwa zinakwenda Mwendokasi wa mpaka 120 km/saa, kwa hiyo Dar - Mwanza ni chini ya masaa 10 na fedha za kuanzia tayari zimeshatengwa kwenye Bajeti hii, Meli mpya inaanza kujengwa kwa ajili ya Ziwa Nyanza, mradi mkubwa wa Bomba la mafuta ktk Uganda mpaka Tanga tayari tumeupata ajira zaidi ya 10 000 zitazalishwa na mapato kibao hapo, bei ya umeme imepunguzwa service chaji imeondolewa vile vile mgao wa Umeme uliokuwa unatusumbua umepungua na unakariba kuwa historia, Elimu inaboreshwa sasa wanafunzi wote waliofaulu wanapata mikopo kinyume na zamani kulikuwa na mkanganyiko ambao hawakustahiri walipata na waliostahiri walikosa, Ulinzi unaimarishwa Raisi ameahidi mabilioni kuwekezwa kwenye Jeshi letu la Polisi kwa ajili ya usalama wetu na mali zetu ambazo tumezitolea jasho, Kiwanda kikubwa cha Mbolea cha thamani ya 1 bilion US dollars kinajengwa Lindi, Shirika letu la Ndege linafufuliwa tayari fedha imeshatengwa za kununua ndege hiyo ndiyo bigger picture na haya yote ni ndani ya miezi saba tu ya Uongozi ingawaje pia ni muendelezo ya mengine mengi mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake kama Raisi Kikwete, Mkapa na ndiyo Wananchi masikini na wa kipato cha chini wanachojali TanZania, hivyo acha kupoteza muda wako na mambo ya kijinga ...
 
Kauli kama hiyo aliitoa Mkapa miaka ya 1990 na Vijana wengi waliuawa kwa kushukiwa ni majambazi.

Wengine walipelekwa kwenye mapori na misitu na kupigwa risasi kwa madai walikuwa wanajibizana risasi na Polisi.

Ndugu zangu watatu waliuawa kwa style hii
 
Hakuna haja ya kuzunguka zunguka sana kutafuta ni nini hasa rais Magufuli alimaanisha jana. Simply ni kuwa rais Magufuli amewaagiza polisi kuua majambazi papo kwa papo na polisi atakayeua papo kwa papo atapandishwa cheo.

Naona watu mmajiumauma humu huku ujumbe ukiwa wazi kabisa. Rais ameagiza kuua majambazi yenye silaha hata kama likijisalimisha. Na polisi ukiua tu jambazi tayari una cheo mkononi.

Sasa sijajua polisi wataenda mbali kiasi gani ila ni kuwa hawataenda mahakamani ng'o!
 
mnafiki tu ww, bahati mbaya hauna madhara yeyote kwa andiko lako.
Ni kweli hana madhara, ila wenye madhara wapo. Subiri utawasikia na wengine yawezekana utawaona pia. Once the can of worms, or the pandora box is opened and the hell breaks loose!
 
Back
Top Bottom