Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi


Mh Rais pamoja na wasaidizi wake kama walishauri jinsi Mama alivyotamka lazima tukubaliane amekosea sana tuu kuhusu kauli yake! Yani mwekezaji afanye atakavyo alete awatakao?

Tuambiane ukweli ni mwekezaji gani unayemjua unadhani anapenda kuajiri watanzania hata kama sheria isingekuwa inambana?

Watu wanaofanya kazi viwandani,migodini na makampuni binafsi wanaweza kuwa wanajua madhara ya kauli hii ya Rais!
 
Mimi sipingi kauli
Natamani iwepo clarification..
Je wageni waajiriwe bila kujali idadi?
Au usimamizi uwepo kama enzi za JK..
Sisi kwenye kampuni yetu tuko wabongo zaidi ya 90, wageni wenye kampuni yao ni wachache sana hawazidi watano lkn upatikanaji wa work permit umekuwa ni shida sana, kule wizarani kuna miungu watu, mama kawasema inabidi wajirekebishe kwa kweli
 
Someni sheria inasemaje,kama wakati unawaleta ulisema wanakuja kufundisha wazawa na wataondoka inafika miaka ya kuondoka unagoma

Wengi hapa wanajadili tuu bila kujua wana jadili nini wanasahau kwenye sheria kuna kazi mwekezaji lazima awape wazawa sasa inaposemwa aweke amtakae kwasababu pesa ni yake sasa sijui wanao jadili hapa kama wanaelewa maana ya hii kuweka amtakae....

Sheria iko wazi kabisa kwenye nafasi za wataalam hasa waendesha mitambo migodini na viwandani na kada zingine ambazo experties hapa tanzania ni wachache sana mwekezaji anakuja na watu wake na anakuwa na watanzania wanaopewa nafasi ya kujifunza!

Hivi Hawa Mameneja fedha,Rasilimali watu n.k kuna mwekezaji akiambiwa achague na afanye atakavyo kweli kuna mtanzania atapewa nafasi kweli?


Ukweli ni kwamba kauli ya Mama ni hatari na anapaswa kupitia upya.

Lakini sisi hatukatai kuna urasimu kwenye kutoa vibali bila kusahau rushwa kabisa na hilo linatakiwa kufanyiwa kazi lakini kusema wafanye watakavyo si jambo zuri
 

Bora useme wewe!
 
Mh Rais pamoja na wasaidizi wake kama walishauri jinsi Mama alivyotamka lazima tukubaliane amekosea sana tuu kuhusu kauli yake! Yani mwekezaji afanye atakavyo alete awatakao?
Ndio mwekexaji alete atakao apangiwe tu idadi .Wewe chukulia unaenda kufungua duka kijijini halafu mwenyekiti wa kijiji ndie akupangie umuweke dukani nani kuuza

wapewe idadi tu ambao hawataulizwa chochote wala vyeti ni kuwapa permit tu
 
Kampuni ya kwao mfano umeajiriwa kampuni private IPP unataka ulipwe mshahara dawa na watoto wa Mengi au ndugu zake aliowaajiri hata

ila ungeelewa vizuri zaidi ungetoka juu na mjadala wenyewe

Kampuni ya kwao mfano umeajiriwa kampuni private IPP unataka ulipwe mshahara dawa na watoto wa Mengi au ndugu zake aliowaajiri hata kama hawajui kitu wewe ndio unawaelekeza?
Usingedandia mjadala ungeelewa vizuri zaidi, hapa utachanika msamba bure
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.

Kuna kampuni moja ya utalii imeajiri hadi mfagiaji mkenya.
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
Sio kweli. Walinzi binafsi wa Abramovich hawakuwahi kiruhusiwa kuingia Uingereza kutoka Urusi na sababu ni nyepesi tu; Hata hapa Uingereza wapo wa kutosha!
 
Ndio mwekexaji alete atakao apangiwe tu idadi .Wewe chukulia unaenda kufungua duka kijijini halafu mwenyekiti wa kijiji ndie akupangie umuweke dukani nani kuuza

wapewe idadi tu ambao hawataulizwa chochote wala vyeti ni kuwapa permit tu

Nimegundua hujui tunajadili nini! Yani kwa kauli yako unafikiri kuna mtanzania atapata nafasi ya meneja rasilimali watu na meneja fedha kwenye kiwanda,mgodi au kiwanda chochote?

Hapa tunaongelea vibali vya kazi kwa wageni na hii ipo kwa nchi zote duniani uwezi kufanya utakavyo lazima ufate sheria na lazima wazawa walindwe....
 
Sisi kwenye kampuni yetu tuko wabongo zaidi ya 90, wageni wenye kampuni yao ni wachache sana hawazidi watano lkn upatikanaji wa work permit umekuwa ni shida sana, kule wizarani kuna miungu watu, mama kawasema inabidi wajirekebishe kwa kweli

Work permit kwenye nini? Kwaajili ya kina nani kulingana na sheria?

Mfano kama maneno ya Mama kuwa mwekezaji alete watu awatakao kwa sababu pesa ni zake ,unafikiri hapo ofisi kwenu huyo mwekezaji atabaki na nyie wabongo wangapi kama ni chaguo lake? Na hata akiwaleta wake mkawekwa kwenye usaili ni wabongo wangapi hapo mtabaki?

Yani wewe upo hapo kwakuwa sheria imekusaidia na inakulinda kabisa bila shaka kama ni chaguo la mwenye kampuni ni ngumu ku predict kama ungelikuwepo hapo.....
 
Kuna kampuni moja ya utalii imeajiri hadi mfagiaji mkenya.

Na hapo tuna sheria inayo walinda wazawa je kauli ya Mh Rais ikianza kutekelezwa ya wawekezaji kuwaleta watu watakao na wafanye watakavyo?
 
Mama kwenye maelezo yake mengi anasisitiza suala la kufuata sheria! Bila shaka, alichomaanisha mama ni kuondoa ukiritimba kwenye utoaji wa hivyo vibali lakini sidhani kama anamaanisha vibali vitolewe kiholela!
Sasa hivi ndio Sheria ya kazi na ajira kwa wageni inafanya kazi kidogo maana hapo awali tulikuwa na walinzi wa magetini kutoka UK,Austeria na South Africa na wanalipwa pesa nyingi wakati tuna Askari wetu wanaweza fanya hizo kazi kwa sasa safi.
Kwa kauli hii ya mama naanza kuwa na maashaka nae makubwa ktk uongozi wake wa nchi.
Naona tunaelekea kurudi kule kule
 
Nawe ni wale wale tu mnaojaribu kuaminisha watu kwamba JPM ndio kila kitu kuliko watangulizi wake wote, na bila shaka atakuwa ndio kila kitu hata kwa wale watakaofuata baada yake, lakini cha ajabu, hatuoni kilicho so exceptional kulinganisha na hao wenzake!!!!
 
To qualify to work in any country in the world you need to have certificate,degree or diploma from a recognized university that’s also accredited from recognized institutions.Then if want to practice law,medicine etc you need to pass an exam given to lawyers or doctors in that particular country. Sijui umenielewa?
 
Wachina watarudi tena kuuza maua na karanga mahind, na viatu kariakoo kama henz za kikwete, na kila siku wata kuwa wana kuja Kama henz za jk walijaa mitaan , magufur aliwabana wagen njaaaa naona Sasa mama ana waitaji, sisi hatu katai wagen tuna taka wagen wenye faida kwa jamii yetu, mgen ambaye nyumbani kwake ana weza kumu ajir mpish, shamba boy na yaya na akawalipa mshaara mzur.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenzage aliye pita alibana wagen vizur Sana, Sasa yeye ana fungua milango ovyo Sasa wagen watajaa tutaanza kunyanyaswa tutakuwa wagen kwenye nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Au aende China akafungue duka Kama ata weza kupewa vibal kila isi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…