Hujui unachoongea hapa. Kwa suala la expatriate hilo halina shida, ila wawekezaji wengi wanatumia mwanya huo kuleta vibarua (makanjanja) wenye kufanya kazi za kawaida ambazo graduate wa udsm anaweza kufanya huku zile kazi za vibarua wakipewa wazawa. Kuna kampuni naijua, wao kipindi cha Jk walileta mpaka weighbridge operator, wahasibu, mafundi mchundo, store keepers yani watu kibao kutoka uhindini na Pakistan. Yani mtu anafanya kazi za fundi mchundo ila permit inasoma ni manager expart so n so. Alipokuja JPM, walipukitishwa wote yani wakabaki wale expart kweli na hizo kazi vijana wa veta wakazichukua ila wajamaa hawakupenda na walimchukia mwendazake vibaya mno. So mleta Mada namwelewa vizuri anaposema lazima serikali iwe makini kulinda ajira za wazawa. Hata huko nje unakokusema, wenyewe wanalinda ajira zao vilevile.