Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Hili la uwekezaji kupata vibsli.linatakiwa umakini fano ukifungua shule ya msingi au sekondary walimu wa kenya na uganda bei rahisi sana na wako tayari kulala mabwenini kwa mshahara wa laki mbili na nusu kwa mwezi wakila chakula cja wanafunzi.Cheap labor kuliko ukiajiri watanzania

Viwanda ukifungua cheap labour inapatikana India na China .Mishahara yao mifogo na huweza ishi kwa kulala ndani ya kiwanda

Mwekezaji huangalia pia labour cost hilo pia watoa vibali yabidi waa galie kama mtu je labour cost kwa mwekezaji akitumia wazawa itakuwaje na akitumia wageni itakuwaje na matokeo ya kodi yatakuwaje

Hata miradi utekelezaji mwingine waweza kuwa rahisi kwa kutumia wageni kuliko wazawa
 
Niliwahi kufanya kazi kampuni moja wa kichina, hili swala la vibali changamoto sana, wale jamaa wanakuja kazi tunawafundisha sisi hawajui kitu

Mmoja kazi yake ilikuwa kukaa na mihuri ya kampuni, secretary.....yaani nilikuwa nafuatilia vile vibali mnatumia professional za technician,Business Manager etc.......na kutengeneza CV fake na vyeti walikuwa wanatengeneza wenyewe, kama HR ilikuwa inanisikitisha ila ndiyo ivyo tena ilikuwa ndiyo mwendo huo.....kila kitu fake, then naarrange training kwa hao.....yaani wanakuwa hawajui kitu
Uko sahihi mkuu, kwenye hili suala JPM alijitahidi mno. Ofisi za uhamiaji zilikuwa zimejaa Rushwa hatari, wahindi, Wachina na wa Pakistan dah walikuwa wanapishana hewani kuwahi ajira nono bongo. Kuna kampuni moja, Jamaa ana Cheo cha CEO kwenye permit ila anafanya kama accountant, mwingine expart wa instruments kumbe fundi umeme kama wa veta tu. Umakini unahitajika hasa.
 
Tumpe muda, lakini yapo mambo yanatia mashaka. Hilo la vibali vya kazi na jingine alilosema hazina wakiona misamaha ya kodi ipo juu ya uwezo wao wampelekee si mambo ya kushangiliwa.

Nilikuwepo awamu ya Mwinyi, nimeanza kuwa na mashaka huyu anaweza kuwa rais ovyo kabisa kuliko hata alivyokuwa Mwinyi.
Wewe una hasira ya kukosa uteuzi. Tumuache mama afanye kazi.
 
Mwekezeji binafsu hata ndani ya nchi hujaza watu wake anaowaamini
Ukienda IPP wamejaa akina Mengi na nduguzekienda Azam wamejaa akina Bakhresa na nduguze ukienda kwa wawrkezaji wahindi hivyo hivyo na wawekezaji wa nje ni hivyo hivyo

Wacha azalishe akupe kodi yako .Mtaji wa kwake testrictions kali za nini tamka tu kuwa mau be 20 percent ya work force wawe wa mwekezaji 80 percent local content
kusema watano kwa mfano kwa kiwanda kikubwa kama Dangote si sahihi
Point mkuu
 
Mkuu The Boss, nilichomwelewa mama ni kwamba, mwekezaji anakuja na wafanyakaz kutoka nje wale wanaukubalika kisheria, baada ya miaka mitatu wakitaka kurenew vibali, wananyimwa, wanalazimishwa waajiri watanzania. SASA kama ndo mtu anaemwamini vipi umnyime kibali ulazimishe aajiri watanzania na hajavunja Sheria yoyote ile?? Bora mwanzo angeambiwa baada ya miaka mitatu hatutakuruhusu kurenew kibali
Hiki ndicho Mh. Rais Samia Suluhu Hassan alichokimaanisha.
 
Mama yuko sahihi sana anacholalamika ni hizi nenda rudi ambazo hazina kichwa wala miguu mtu ana document zote lakini hapewi haki yake na ni kweli watu wa vibali walijigeuza miungu ili wapate rushwa kama we mleta uzi mmoja wao samahani sana , kama mtu kafuata taratibu zote na anastahili kwanini acheleweshwe mizengwe kibaaaa ili atoe rushwa stupid kabisa
 
Kwa jins nilivyoelewa,kaul ya mama siyo maana katengua sheria zilizopo,bali watu wahusika waondoe urasimu na figusu figusu nchi iendelee
 
kamsikililize vizuri mkuu, kasema kuna nafasi ambazo anatakiwa kuweka watu wake, tena alitaja na idadi, na kusema hao waruhusiwe kwani hata hivyo mtaji ni wa kwake na akipata hasara ni ya kwake hafidiwi na mtu, hAJASEMA KAMPUNI YOTE IJAZWE WAGENI
 
Hajasema wapewe tu vibali kiholela bila bila sheria kuzingatiwa na kufuatwa kikamilifu...
 
Vigezo bado vipo Yaani Mgeni lazima ahakikishe kuwa wale anaowaombea vibali ni wataalam kweli kweli siyo watu magumashi
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama. Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
Local content law inataka wazawa wanufaike na uwekezaji wako. Ikiwa wawekezaji watakuja na watu wao basi tusahau ajira kwa wazawa. Hiyo sheria inamlinda mzawa ili aanufaike na ajira baada ya mwekezaji kuja kuwekeza.
 
Rais yupo sahihi, msisitizo uwekwe kwenye idadi. Sio kumuamulia mwekezaji huyu muajiri huyu usimuajiri.

Muwekezaji apewe idadi ya wageni tu anaopaswa kuwaajiri na asivuke iyo idadi basi. Kumuamuria Nani amuajiri na Nani asimuajiri ilo sio sahihi.
 
Acha tu mkuu, watakuja hadi wapaka rangi kwenye majengo kisa mwekezaji anawaamini,
 
Wewe una hasira ya kukosa uteuzi. Tumuache mama afanye kazi.
Sukuma gang huyo Achana nae. Mama yupo vizuri na ametoa hoja sahihi. Kwa nini TFF aiziamulii timu za mpira kumsajiri mchezaji fulani kwa sababu Kuna mchezaji hapa Tanania ana kipaji sawa na huyo mchezaji mgeni??? Kwa nini kwenye vibali vya kazi ndo wawekezaji wanaoleta mitaji na kulipa kodi ndo wanafanyiwa hivi??? Mama Samia yupo sahihi.
 
Nafikiri kuna jambo hukulikamata vizuri katika hotuba yake. Ameongelea ile namba ya wataalamu iliyoko kisheria anaokuja nayo mwekezaji, wakati wa ku-renew work permit kulikuwa na usumbufu mkumbwa. Hiyo ndiyo aliyoingelea,
 
Mbona wageni hawakuwepo na ajira kwa watanzania hazikuwepo? Sheria ya vibali vya kazi ilibana lakini ajira zenyewe hata kwa watanzania hazikuwepo (hazipo).
Hapana, kuna nafasi Watanzania walikuwa hawashiki! Now tulikuwa tunajenga kizazi kitachoweza kushindana. Angalia hata kauli zake za kama hakuna wataalam tulete wa nje! Hili inataka control kubwa mno!

Hizi ngoma zinarudi hizi ndio zile madeni ya ajabu kwa taasisi za umma kutoka kwa hawa consultants na nyingine tunao hapa wataalam ila watu wanaweka mazingira magumu ili wakalambe 10% zao!

Mama awe makini sana sana, nao anafanyia kazi kila malalamiko! Huwezi kunyosha mambo bila malalamiko! Afanye utafiti kwa umakini! Mama afungui uchumi tu, kwa kauli hizi atafungulia majizi! Tupo hapa tutarudi kulalamika!

Mama achague namna ya kupiga U turn otherwise hawahawa wanaoshangilia leo ndio wataomzodoa kesho.
 
Kazi za kitaalamu ambazo hazina local ndio wageni wanaruhusiwa sio zile ambazo tunao wataalamu hapa ndani,zamani hadi wageni walikuja na HR wao...kuwe na win win situation hata kama wakileta consultants.
Sheria zilikuwa zinanyooshwa tu! Hivi muwekezaji gani ataajiri Finance Manager Mtanzania kama si JPM kukataa hizi mambo? Hawa wanataka all key areas waweke watu wao!

Sidhani kama sheria zetu zikifuatwa kikamilifu zitakuwa kikwazo, kama ndio mkondo tunaotaka tutapata matunda yake! Kuna vitu alifanya JPM hatuwezi kuelewa hivi karibuni! Let's go....
 
Back
Top Bottom