Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Hivi wewe unaweza kukubali uwekeze pesa yako halafu uchaguliwe watu wa kuisimamia? Mwekezaji akija anataka zile key posts kama mkurugenzi mkuu, mkurugenzi wa fedha, mkurugenzi wa production na head wa technical service aweke watu wake. Hapo kuna ubaya gani wakati nafasi zilizobakia wanafanya wazawa.

Pili ujio wa wafanyakazi wa kigeni unazalisha nafasi za kazi indirectly kwa sababu hao wafanyakazi wa kigeni wataajiri mahouse boy na mahouse girls, walinzi na mashambaboi huko nyumbani kwao, hivyo kuzalisha ajira zaidi kuliko kama nafasi zao zingeshikwa na wazawa.
 
Tukisema tuwasikilize WAWEKEZAJI siku watakuja kuomba PASSPORT kwa kisingizio cha kutaka kulinda rasilimali zao.
 
Kama muwekezaji amefungua mradi au ana kampuni yenye watu 700 kuna tatizo gani hata 100 wakiwa ni kutoka nje??
 
Mbona kaeleweka vizuri tu. Kuna baadhi ya nafasi lazima u compromise kwa interest ya mwekezaji. Haina maana kuajili wageni bila ukomo. Maana hata hao wanaoruhusiwa kisheria, ku renew work permit imekuwa ni urasimu mkubwa.
 
Hivi wewe unaweza kukubali uwekeze pesa yako halafu uchaguliwe watu wa kuisimamia? Mwekezaji akija anataka zile key posts kama mkurugenzi mkuu, mkurugenzi wa fedha, mkurugenzi wa production na head wa technical service aweke watu wake. Hapo kuna ubaya gani wakati nafasi zilizobakia wanafanya wazawa.

Pili ujio wa wafanyakazi wa kigeni unazalisha nafasi za kazi indirectly kwa sababu hao wafanyakazi wa kigeni wataajiri mahouse boy na mahouse girls, walinzi na mashambaboi huko nyumbani kwao, hivyo kuzalisha ajira zaidi kuliko kama nafasi zao zingeshikwa na wazawa.
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] msiba huu, kwahiyo waajiriwa wa vyuo watapata kazi za house boy na kufua sidiria za wageni
 
Amesema pia tuangalie mfumo wetu wa elimu tuweze kupata watu wenye ujuzi wa kufanya kazi vyema.
Mimi sipingi kauli
Natamani iwepo clarification..
Je wageni waajiriwe bila kujali idadi?
Au usimamizi uwepo kama enzi za JK..
 
Nchi iko na tatizo kubwa la ajira kwa sababu uwekezaji ni mdogo na viwanda ni vichache. Hilo suala la watu kutoka nje kuja kuchukua nafasi za wenyeji ni tone tu katika bahari ya matatizo ya ajira yatokanayo na uchumi usio na viwanda.
Ni eneo ambalo kauli yake italeta shida. Issues za vibali ilikuwa tatizo zito! Asiturudishe kule, ndio Inawezekana kwenye udhibiti kuna mipaka ilivukwa yafanyiwe marekebisho lakini namna alivyozungumza tatizo la vibali kutoka kama pipi kwa mangi litarudi.

Kwa ufupi zipo sheria nzuri za vibali tusisitize ifuatwe! Malalamiko kwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa na awamu iliyopita lazima yangekuwepo maana zilikuwa ni hatua mpya.

Mama awe makini asichomekewe agenda na watu waliochangia kuvuruga mfumo wa ajira nchini.
 
Kuna wazelendo uchwara wengi sana nchi hii
Mbona wageni hawakuwepo na ajira kwa watanzania hazikuwepo? Sheria ya vibali vya kazi ilibana lakini ajira zenyewe hata kwa watanzania hazikuwepo (hazipo).
 
Nchi iko na tatizo kubwa la ajira kwa sababu uwekezaji ni mdogo na viwanda ni vichache. Hilo suala la watu kutoka nje kuja kuchukua nafasi za wenyeji ni tone tu katika bahari ya matatizo ya ajira yatokanayo na uchumi usio na viwanda.
Sasa kama una degree ya atomic science nani atakupa ajira? Walimu haooo wanalamba ajira zao.
 
Ukiona mchina anakuja na wafagizi wake ni kwa sababu mliwaambia wao ni marafiki zenu wa karibu na hamukuwapa mipaka kama "mabeberu" ya kizungu ambayo wao huwa hawaji na wafagizi wao. Turejeshe uhusiano mzuri na wa faida na mabeberu ya kizungu pia ila tuwe na uwanja mpana kwani Wachina wako mbioni kuifanya Africa koloni lao baada ya kujua wao ndio wamebaki kimbilio la madikteta.
Huna akili wewe.

Yani mtu atoke China aje kufanya kazi ya Procurement bongo ? Hivi huwa mnatumia akili za miguuni kufikiri?

Wewe unaweza kwenda kufanya kazi ya HR south Africa au Rwanda ? Muwe mnasoma na miongozo ya ajira ya nchi zingine ikoje sio mnaandika pumba.

Kuna kazi za Wazawa lazima zilindwe kwa namna yoyote. Muwekezaji anakuja na experts tu ila wafagizi na kazi zingine lazima wawe Wazawa.
 
Mkuu hiyo inafaa nchi za ulaya na Marekani ambapo wapo level nyingine. Kwa nchi zetu za Africa na uchumi wetu kila mtu akae kwao ikibidi. Kwa tulivyo na tatizo la kiingereza na tunavyobabaikia wageni ukitoa vibali vya kazi kiholela tutalia na kusaga meno. Nakuhakikishia watajaa wakenya na wazimbabwe mpaka maredioni sababu tu wanaongea English nzuri. Na hivyo hivyo ukienda kuchukua ajira nchi za Africa zenye shida ya ajira hata wewe unajiona kabisa umechukua ajira zao labda iwe level za juu sana za mishahara minono. Kati ya 2010 na 2015 bongo walijaa waturuki kibao wa fani mbali mbali tena vichwani weupe tu kwa kupitia zile permits za $50 miezi mitatu mitatu.
Naona hamjamuelewa Mh Rais. Yeye kasema kuna maeneo yanahitaji busara ili kulinda interest za mtaji wa mwekezaji. Haiwezekani mwekezaji alalamike vibali vya secretary, wahudumu, madereva, HR Officers n.k. Lazima watakuwa wanaongelea nafasi nyeti kulingana na aina ya uwekezaji. Mfano Director of Operations, Finance Manager n.k ambapo kwa complexity ya project unaweza kukuta watano ni wachache. Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu kudhani eti Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji naye ameelewa kama ninyi hapo.
 
Bado nchi inaongozwa na matamko na hotuba. Kila nchi duniani wamelipa kipaumbele suala la uhamiaji.

Miaka ya nyuma mambo yaliendeshwa kiholela mpaka raia wa kigeni walimiliki pasi za Tanzania.
Kweli kabisa, ni hatari sana kutaka walegeze kamba. Kauli ya Rais ni amri, inabidi achuje maagizo yake maana nina uhakika from Monday vibali vitaanza kutoka kama njugu. Mambo ya uhamiaji na vibali ni sensitive asisikilize kila kilio atawatoa kwenye reli watumishi.

Mambo kama TRA kuvuka mipaka inajulikana sababu ikiwemo task force ya kuvunjilia mbali lakini asipochunga tone yake kwenye maelekezo nyeti tutarudi nyuma hata kwenye mazuri aliyofanya JPM.

Nyakati hizi lazima kuna watu wana set agendas makusudi kwa malengo yao na watu wasio waaminifu wamchomekee mama. Usishangae tukarudi hadi kwenye kununua umeme wa IPTL. Twende taratibu na kwa utafiti wa kina, tusitibue maji yote kufurahisha watu tu.
 
Tuboreshe uhusiano wetu na mabeberu wa kizungu tuache kutegemea Wachina ambao hupenda kuja na vibarua wao katika miradi yao.Inasemekana hawa vibarua wao wanaokuja huku Africa wengine ni wafungwa huko kwao.
Niliwahi kufanya kazi kampuni moja wa kichina, hili swala la vibali changamoto sana, wale jamaa wanakuja kazi tunawafundisha sisi hawajui kitu

Mmoja kazi yake ilikuwa kukaa na mihuri ya kampuni, secretary.....yaani nilikuwa nafuatilia vile vibali mnatumia professional za technician,Business Manager etc.......na kutengeneza CV fake na vyeti walikuwa wanatengeneza wenyewe, kama HR ilikuwa inanisikitisha ila ndiyo ivyo tena ilikuwa ndiyo mwendo huo.....kila kitu fake, then naarrange training kwa hao.....yaani wanakuwa hawajui kitu
 
JPM kwenye maswala ya uchumi kaboronga tu mkuu ,hatuwezi kuja kuelewa mbele kabisa ,yaani uandae task force ya kina biswalo,bashite na dotto kwa ajili ya kupora wafanyabiashara mali zao ndio tuje kumkumbuka? Akumbukwe kwani amekuwa MTOTO WA DANDU?
Ile ilikuwa wrong wrong! Ila kuna vitu vya msingi vibadilishwe kwa tafiti na watu waadilifu. Ukiona unapendwa tu kila unachosema hilo ni tatizo. Huko mbele mzito utamuelemea wanaoshangilia sasa ndio watakuwa wa kwanza kumsulubu.
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
Bonge la point mkuu
 
Mimi nilimuelewa kuwa anapinga ucheleweshaji
 
Kwa nini shule binafsi na hoteli zinapenda kuajiri walimu na wafanyakazi kutoka nje wakati wangeweza kuwaajiri wa hapa nchini na wasiingie gharama za kulipia vibali vya kazi?
Mkuu mnaongea tu, unajua ilifika mahali 95% ya walimu wa English medium pamoja na wafanyakazi wa mahotelini walijaa waganda,wakenya, wazimbabwe etc na wengi walirudishwa kwao 2016!??.. Hatukatai kujichanganya na wageni Ila permits kutolewa holela kutarudi tena na watanzania tuna kasumba ya kujidharau na kubabaikia wageni. Sasa subiri uone mtifuano wake kwa wanaotoka vyuoni kukosa ajira. Watarudi mpaka wachina machinga waliojazana kariakoo kipindi cha JK. Mtu ana mtaji wa milioni 6 tu anakimbilia Tanzania tu.
 
Back
Top Bottom