Siyo vema sana kuongelea mambo ya ukabila hapa Tanzania, lakini kwa hakika vitendo vya Rais Magufuli vinatulazimisha tuingie huko.
Magufuli alikuwa very clear katika chuki yake dhidi ya Wachagga. Unaweza kuelewa chuki yake kwa kiasi fulani. Nyerere alikutana na "The Chagga Problem" katika elimu. Kutokana na uchagani kuwepo shule nyingi za msingi, Wachagga wengi zaidi walikuwa wakiingia sekondari kuliko makabila mengine. Hili lilikuwa bomu. Nyerere akaja na solution. Quota system. Idadi maalum ikagawanywa kila mkoa, ili kutoa fursa sawa kwa mikoa yote, hata kama inamaanisha kuna vijana wa kichaga waliofaulu vizuri wataachwa ili kuchukua wa mikoa mingine wenye ufaulu wa chini.
Nyerere alifanya haya bila chuki yoyote dhidi ya Wachagga.
Magu ni tofauti. Alibomoa Kimara kwa ukatili usio na kipimo, akijua wamejaa Wachagga, wakati kule Mwanza alisitisha bomoabomoa, akitangaza bila aibu, mchana kweupe, MSIWABOMOLEE HAWA WALINIPA KURA!!
Magufuli alichukia sana Wachagga. Maeneo mengi kawaondoa, lakini badala yake kajaza wasukuma wengi mno, na kwa hiyo hatatui chochote, bali anatia chumvi nyingi mno kwenye kidonda.
Wakati Nyerere alikuwa anapambana na ukabila, Magu kaurejesha kwa kasi