Hili la watu kula supu ya ngozi ya ng'ombe/mbuzi lina usalama kiasi gani?

Hakuna
Madhara yoyote yale, kwani sisi watu wa kusini ni kawaida yetu tangu zamani sana.

Na sijasikia athari ya aina yoyote ile... Na kama ni Mbuzi basi huwa tamu zaidi ya nyama ya ndani... Jaribu mkuuu ngozi Tamu sana
 
Wewe kula hiyo ngozi haimanaishi nilichoandika ni uongo, tofautisha sana nyama ya kwenye mkia na hiyo ngozi, ngozi ya ng'ombe ina nyama gani me ndani sasa
 
Sasa nyama kilo moja Tsh 10.000 unadhani supu ya buku mbili itakuwa na finyango ngapi? mbona kongoro lina ngozi? acha watu wanywe tena unakuta ngozi ina kupe na papasi basi safi kabisa kwa vitamin x.
Sababu ya yote haya ni umaskini tu unazidi nchini, hakuna mtu mwenye uwezo wa kula nyama au maini akaacha akaenda kula ngozi ya ng'ombe I sio na chochote
 
Mkuu
kuna wale wengine wanakula ngozi ya yule mnyama mwenye mafuta sana, na wao pia inabid tujue usalama wao ukoje.

Na ile nyama yake hawaichuni ngozi kama hizi zingine, ngozi ni sehemu ya nyama na inaliwa kwelikweli.
 
Sio maisha ya chini, wa west africa ni chakula kawaiada tuu, hata kuchwa kinapikwa vizuri
 
Ugumu wa maisha ndio chanzo cha watu kula ngozi na sehemu za siri za wanyama mfano pum*** za mbuzi na ng'ombe zimekuwa maarufu, watu wanagegeda kwa fuji. Turudi kwenye mada. Kazi mojawapo ya ngozi ni kutoa uchafu mwili kwa njia ya jasho. Sumu za mwili pia hutolewa kwa njia ya jasho ingawa zinaweza kutolewa kwa njia nyingine. Hivyo kula ngozi ni sehemu ya kula sumu za mwili wa huyo mnyama
 
Bora hao kuna wengine wanakula utabu tena wanataka usisafishwe kwakuwa viini lishe viko kwenye majani aliyokula mnyama akacheuacheua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…