Hili la watu (wakiwemo viongozi) kudhalilishwa na Watanzania kufurahia linanishangaza sana

Hawakumtukana, walimuita mashamba tu.
 
Huelewi lolote kuhusu siasa wewe, unajua kipindi cha JPM Mange alikuwa analipwa na nani!?,unajua akaunti ya KIGOGO ilikuwa inamilikiwa na nani!?

Mama Samia katukanwa matusi ya nguoni, umeona waziri wa mambo ya nje akichukua hatua yoyote!?,watu hawana shida ya uwaziri, wana shida ya Uraisi, waweza kuita tamaa au vyovyote vile ndo binadamu tupo tofauti.

Mange ana backup kubwa sana ndo maana anajiamini. Vilevile Makonda ana backup kubwa sana ndo maana kaongea vile Jana. Vita ni kubwa kuliko tunavyodhani.
 
Mbona anachokifanya Mange si kigeni, alishafanya Sana huko nyuma.

 
Ila hata kama siyo President ni mke wa mtu na ni mama .

Hii siyo sawa.

Hivi huo usalama wa taifa huwa wao hawana Instagram ?
Hata Magufuli alikuwa Rais na ni baba wa watoto lakini alitukanwa na hadi wakina January na Nape ,Kinana bila kumsahau Mzee Makamba hadi waliomba msamaha…huyo Mange alimdhalilisha sana Magufuli lakini watu mlishangilia sana….
 
Mange ni kichaa tu,Hana anayemtuma yule....akili zake anazijua mwenyewe
 
Mkuu uko sahihi kabisa, mamlaka zinazotakiwa angalau kuchukua hatua dhidi ya matusi ya Mangekimambi hazijawahi hata kuattempt tukaona wamekwama wapi na kwa sbb au sheria zipi. Waziri wa mambo ya nje, waziri wa habari, balozi wa marekani, msemaji mkuu wa serikali, waziri wa mambo ya ndani wote wako kimya sijui wanasubiri Rais ndo awaambie wachukue hatua au wakemee!!??? Sasa kajitokeza mtu ambae ameona ukimya na Rais anendelea kuchafuliwa mitandaoni then watu wanaona nongwa....Why Why between my interview passing around......I hate them.......wamwache Makonda aoneshe ujasiri wake kwa maslahi ya nchi, kama angekuwa mnafiki Rais Jana hiyo hiyo angemkemea......Lazima tuungane kumlinda Rais wetu na kama wewe huwezi acha waliojasiri waseme na kutenda.......siyo kweli kwamba mawaziri licha ya kuteuliwa na Rais wote wanaweza kuwa na nia nzuri na kumtakia mema, waswahili wanasema kikulacho kinguoni mwako
 
Hata Yuda Iskarioti alikuwa ndugu kabisa wa Yesu na ndiye alikuwa Mtunza Hazina wa wale thenashara 🐼
 
Hizi zote ni consipiracy shida ni kwamba watu mmeanza lalamika zama hizi. Na kipindi cha Kikwete je alikuwa analipwa na nani. Maana hakuna awamu amabayo hajaishambulia labda ya Mkapa na akina mwinyi kwa sababu alikuwa mdogo na mitandao haikuwepo.
Awamu ya Magufuli ilianza anamsifia, baadaye akaanza kumshambulia. Same hata hii awamu. Same awamu ya Kikwete.
Wewe unayeelewa hebu tuambie kigogo ni nani na mbona kama mnafahamu hadi leo mmeshindwa kumkamata na abdo anaendelea mashambulizi. Mlianza mara January, ikaenda mkaanza mara nape yani kigogo ashakuwa watu mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…