Hili la watu (wakiwemo viongozi) kudhalilishwa na Watanzania kufurahia linanishangaza sana

Mwanasiasa anafanya jambo lolote tena ogopa sana Mtu anayeutamani Urais
Wanaoutafuta urais ni wengi sasa kwanini kidole anyoshewe yeye. Na kama anautafuta urais basi kama anataka kushambulia Rais wa sasa kumshambulia hakuna faida kwake maana kwa siasa za nchi hii zilivyo atamaliza awamu mbili inabidi amshambulie anayeweza kugombea baada ya awamu mbili za Samia. Yani kwa sasa hawezi ahta kuchukua fomu kugombea dhidi ya samia maana lazima tu achukue vipindi viwili sasa kumshambulia kutampa faida gani? Kumbuka pia ndiye kamrudisha kwenye mema ya nchi.
 
Wewe ndio unamnyooshea January

Lema kawataja Watano 🐼
 
Wewe ndio unamnyooshea January

Lema kawataja Watano 🐼
Mimi sijamnyooshea kidole ila naona upepo wa thread hii unamsema January. Lema huyu huyu aliyesema Ni furaha kwa Mungu Lowassa kupigwa mawe halafu baadaye akasema mwenye ushahidi aende mahakamani au lema yupi mkuu? Sijamsikiliza kumbe kataja majina?
 
Sikuona hizi nyuzi awamu ya 5 JPM alipokuwa akitukanwa

Sasa mkae kwa kutulia sindano ziwaingie

What comes around goes around

Mbona inasemakana hata baadhi ya siri za Ikulu yeye ndio alikuwa anavujisha????wacha KARMA imtafune

Muoshwa huoshwa muda wake sasa umefika hana wa kumlaumu atubu kwa muumba wake period
 
Huyo Januari ndo mratibu Mkuu wa matusi enzi za Magufuli na sasa pia
 
Hivi ni mole gani pale ikulu alikuwa anavujisha siri nzito za vikao vya siri vilivyokuwa vinafanyika usiku wa manane lakini kesho yake asubuhi unakuta siri zote zipo kwa dada wa taifa, Kigogo, Sarungi, Ngurumo, Chahali, kule Ubelgiji; na kwingineko? Na Magufuli alipoondoka tu uvujishaji huo ukakoma mara moja?

Nilishangaa sana Mama alipokwenda Marekani na kushikana mkono na dada wa taifa huku akijua matusi na udhalilishaji aliokuwa akifanyiwa bosi wake. Labda alifikiri kwamba akijipendekeza kwa dada wa taifa basi yeye atakuwa salama. Inasikitisha sana.

Huyu mama ni mtu mzima. Na hata ukimwangalia tu unaiona huruma ya umama katika uso wake. Wapo wanaosema eti anavuna alichokipanda yeye mwenyewe lakini kwa kuzingatia ubinadamu tu na hata maadili yetu ya Kiafrika, kabisa kabisa hastahili matusi hayo.

Halafu Kagame yeye huwa anawezaje kuwanyamazisha watu wa aina ya dada wa taifa po pote walipo duniani; na sisi kwa nini hatuwezi?

Your browser is not able to display this video.
 
Dah umeongea point tupu
 
Mkuu ni hasira na upunguani wa Makonda tu, Haamini timing waliomfanyia watoto wa mjini. SG dreams are officially no more!
 
Mkuu Mange hana rafiki wala adui wa kudumu, waweza kufikiria ni mzalendo lakini sio kweli yeye anaangalia maslahi yake binafsi. Huyo KIGOGO alikuwa anapewa details za ndani ikulu ya JPM na nani!?,unadhani Mange angekuwa anayoongea anayatunga kutoka kichwani na ni uongo angekuwa hai leo!?, (hadi picha),Sasa jiulize anapewa information na nani!?,kwa makusudi gani!?,., jibu rahisi, kwenye kila awamu Kuna watu wa ndani wasiopenda mambo yanayoendelea ndani kwa ndani aidha kwa nia nzuri au mbaya, ndo watu wanaomtumia mtu kama Mange, mifumo yetu ingekuwa haijagawanyika huyo Mange angeshakuwa historia siku nyingi. Ila wakipanga hivi, hapohapo kuna mtu anamwambia tumepanga hivi, fanya hivi. Naishia hapa.
 
👍👏
 
Karma kama karma!
 
Duh! Kumbe bitozo ndio alikuwa anavujisha nyaraka nyeti! Au ndio alikuwa anawapa taarifa nyeti akina kigogo 🤣🤣 na mange 🤣🤣🤣
 
Wakati watu wanadukuliwa na taarifa zao kumwagwa mitandaoni ulikuwa upande gani ?
 
Anapotukwa rais ni kuitukana nchi. Ni kuishushia heshima nchi. Baba au mama yako anapokosea kuna namna ya kusema naye na akaelewa.
NB: Si kila unachoshindwa kutafsiri kutoka kwa mtu itakuwa inamaana amekosea kwa kuwa kiongozi hawezi kuwa anaona kama wanavyoona wanaoongozwa. Nikiwa na maana ya kwamba kiongozi ni lazima atangulie miaka kadhaa mbele ndipo anaitwa kiongozi. Kuna vitu utakuja kuelewa baadaye kwamba vilikuwa ni vya muhimu kama kiongozi alivyona. (UKISOMA HABARI ZA FARAO NA NDOTO YA MIAKA SABA YA NJAA NA KILICHOTOKEA KWA WANANCHI KWA KUTOELEWA WALICHOAMBIWA KWA KUWA HABARI ZA NJAA ZILITOLEWA WAKATI WAPO KWENYE MAVUNO)
 
Huyo unayemwomba unamjua vizuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…