Hili limekaaje wadau, Hebu nipeni ushauri kuhusu hili jambo la ndoa

Hili limekaaje wadau, Hebu nipeni ushauri kuhusu hili jambo la ndoa

Tokea Form 6 nimekua nikiwaza kujiajiri tuu, ila vile maisha ya kiyatima na kimaskini yamenichelewesha kidogo.
Ila nashukuru Mungu Nina miaka 30 na mambo yanaenda (I have started Small..!!).

Nilikuaga mwajiriwa wa private nikaenda serikalini, nikasoma na sasa ni Free soul..!!.

SHIDA IKO HIVI...

Tokea mwaka 2018 nyumbani (walezi) wamekua wakiniuliza ""UTAOA LINI?"" sijawahi kutoa jibu kwasababu ""HATA HUYO WA KUOA SINA..!!""

Nilikuaga na mmoja akazingua na kuniita "KAFIR"" sababu ya ukristo wangu japo nilimsaidia sanaa yule fala mpaka akawa na maisha poa.
ALINIFANYA NIPOTEZE HAMU YOTEE NA LADHA YA KOA au KUISHI NA MWANAMKE PAMOJA TENA.
Tokea jambo litokee ni miaka 5 ila SIJAWAHI TENA KUWAZA.

Kuwaambia nyumbani kuwa SINA MPANGO wa kuoa naogopa maana walezi wangu kila Siku wanaongelea ""Marehemu wazazi wangu wanahitaji kuoana wajukuu wakiwa hukohuko peponi..!!""
Halafu huwa nawaheshimu sanaa walezi wangu, maana bila wao NISINGEKUA HAPA KABISAA.
Naogopa kuwavunja moyo na ukicheki ni wazee (60's).

Na sababu hasa ya KUDELETE KUOA ni..

1. Nimeamua kujiajiri kwa kuinvest.
Sasa najiuliza, Unajihangaisha mwenyewe na kupata mali kiasi, halafu unaoa.
Huyo mke baada ya miaka kadhaa anakwambia tuachane..
YAANI MALI NILIZOTAFUTA MWENYEWE KWA MIAKA ZAIDI YA 5 LEO NIGAWANE NA MTU KISA NI MKE WANGU?
•Juhudi zangu zote ziishe kirahisi hivi, KISA NDOA?

2. Wanaonizunguka asilimia kubwaa wanalia na MATESO YA NDOA ZAO.
Hawa walezi wangu sometimes ni wasuluhishi na huwa wananishirikisha nitoa mawazo yangu.
•SASA WANATAKA NA MIMI YANIKUTE AU..??

3. Nimezoea maisha ya ubachelor na free soul.
Tokea nitoke home kwenda kusoma Diploma mpaka sasa Nina Masters of Science in ..... maisha yangu ni kutembea na kuzurula tu mikoani.
Sasa nioe halafu vile nianze kuomba ruhusa kwa mke wakati mi nishazoea nikiwa bored huwa naenda stendi kukata tiketi halafu ndukii...
Sijawahi KUAGA zaidi ya KUTOA TAARIFA kwa watu wa karibu sana ila SIO KUOMBA RUHUSA.
•Sasa nikishaoa si ndio vile unaanza kuomba ruhusa, kunegotiate na mambo kama hayo na Huyo mke!

4. Kama yule dada nilimkuta na stress za un-employment, nikajihangaisha mpaka akapata maisha.
Ila malipo yalikua ni kuitwa KAFIR kisa UKRISTO WANGU na mema yoteee yalisahaulika.
•Sasa Huyo ajae nae si mwanamke kama yule tu?

Najua...
KUOA NI MUHIMU, FAMILIA NI LAZIMA ila MOYO UMEGOMA KABISAAA.

Nakumbuka mwaka 2018 nilijiwekea malengo "Nikifika 2020 lazima niwe na MCHUMBA au NDOA.
Ila hata DALILI SINA..!!

Sometimes kuna kitu ndani kinaniambiaga ""Ole wako ujaribu, You will doomed""

USHAURI TAFADHALI?
Hebu MLIOA naombeni USHAURI na TECHNICS mlizotumia kuondoa hii COMPLEXITY FEAR ya haya maisha..!!!

KUOA NATAMANI ila ""....…..hiii bagosha (in JPM voice)""

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
Sasa unakufuru ulitaka usiambiwe kuwa u kafiri mwenye kukufuru?
 
Kama walezi wako umeshindwa kuuelewa ushauri wao hata hapa naamini hakuna utakae muelewa we endelea kuwa huru tu ila usinyetuke wala usiwe mzinifu maana ni dhambi na we ni mtu wa kanisa

Sent using GunTrigger
 
Oa wewe Mengi ndo bilionea na alioa wee na tuhela twako twa kununulia vibambala na nyanya chungu vinakutia wazimu.
Find a woman and get married.
Oh umetaja vibambala hadi tumbo limeshtuka
 
Msaidizi si beki tatu wapo?
Wengi tu tumelelewa na beki 3.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
Mzee baba hata mchumba huna sasa utaoa nin😁😁 afu sio kila mwanaume ana hadhi ya kuoa,wengine muwe mnakuja kwa mashemeji mnapikiwa mnakula afu mkalale ghetoni
 
Nimeona na nina familia mkuu...but siamini furaha kwenye kuoa...kuna mambo mengi sana tunasucrifise kwa ajili ya kufanya maisha ya songe kiasi kwamba nilipokuwa single ilikuwa tofauti...hivyo yaani.
Hongera kwa hilo Mkuu,furaha inaanzia kwako mwenyewe sio kwa mwenza wako so kama hauna furaha afu unaoa ili upate furaha it will never happen...
 
Usioe mkuu...narudia tena USiOE! Kama watoto tafuta demu piga mimba leo watoto..pambana na life lako as long as unafurahia unachokifanya.... hakuna furaha kwenye kuoa mkuu..belive me!
Aisifuye mvua imemnyea😂😂😂
 
Halafu cha ajabu wanaozaliwaga NJE ya NDOA huwa wana toboa maisha NA wanajielewa kuliko waliozaliwa kwenye ndoa..!!!

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
Hapana nakataa mkuu angalia namba yawaliotoboa hali yakuwa pangu pakavu then linganisha nawaupande wapili utapata jibu.

Hawa wachache waliotoboa hali yakuwa wametokea familia zisizo namisimamo tunawaadmire nakuwa promote kwasababu tunajua aso walizopitia.

Mifano ipo mingi sana angalia hata historia za viongozi wetu waliotuongoza nawanaotuongoza katika nafasi mbalimbali kuanzia serikalini mpaka sector binafsi wengi wao hawajatokea mtaani from no where. Wengi wao unaona kabisa kuna mazingira tayari alikuwa kaandaliwa nawazazi/mzazi wake.

Lengo langu nilitaka nikwambie kuwa, wachagulie watoto wako, kizazi chako mama anayestahili kuwa mama hata kama ukiamua uzae2. Na Mwanamke akishakuwa mama bora basi tayari anastahili kuwa mke bora.

Vuta subira wakati wako sio umri ukifika utaoa2.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisifuye mvua imemnyea😂😂😂
Kwli kabisa...hakuna kipya napata kwenye ndoa ambacho ningekikosa ningekuwa single...ndo maana namshauri jamaa kama ana fraha na life yake kama lilivyo asioee mkuu...
 
Kiaje?
How?

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
Mzee ujana mbaya 30's hata mtoto huna unategemea uje upate mchumba uoe na uzae utakuwa 34...nimekutana na watu wengi waliofanikiwa kimaisha wanajuta kuchelewa kuoa na kuzaa angalia yasikukute kama hayo majuto
 
Kwli kabisa...hakuna kipya napata kwenye ndoa ambacho ningekikosa ningekuwa single...ndo maana namshauri jamaa kama ana fraha na life yake kama lilivyo asioee mkuu...
Duu mkeo angeona hii comment angezimia🙄
 
Back
Top Bottom