Hili ndio soko kuu la samaki Moshi, Mji unaondaliwa kuwa Jjiji

Hili ndio soko kuu la samaki Moshi, Mji unaondaliwa kuwa Jjiji

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Hapa ndipo walipohamishiwa Wafanyabiashara wa soko kuu la samaki kutoka eneo la manyema mbuyuni na kuletwa hapa maili sita.
DSC_1027.JPG

Lengo na kuwahamisha wafanyabiashara hao na kuwaleta hapa ni kile kinachodaiwa kuwa ni katika kuiandaa moshi kuwa jiji na hivyo kuondoa mlundikano wa kuwa sehemu moja.

Lakini cha kushangaza manispaa ya moshi ilichofanya ni kutoa tu eneo na kuwapa wafanyabiashara hao bila kuweka miundombinu yoyote katika soko hilo jipya.

Mfano mzuri hakuna sehemu /mfumo maalumu kwa ajili Ya kuoshea samaki wabichi bali wafanyabiashara hao wamekuwa wakiosha wenyewe kwenye Ndoo zao na kumwaga maji hovyo humo humo sokoni.
DSC_1023.JPG

Wafanyabiashara hao hawajajengewa vizimba vya kuuzia samaki wabichi na wanaokaangwa hapo sokoni bali kila mtu kajifanyia anavyojua mwenyewe wengine wameweka miavuli wengine meza nk.

Hakuna miundombinu ya. Maji ndani ya Soko hilo wala Choo cha umma ndani ya soko hilo bali wafanyabiashara na wateja wa soko hilo wamekuwa wakitumia vyoo vilivyopo jirani na soko hilo.

Soko hili ambalo kwa sasa ni Maarufu zaidi ya Kule lilikokuwa mwanzo kutokana na Eneo lililopo linachafua taswira ya mji kutokana na kuwa lipo karibu kabisa na barabara kuu ya Moshi Arusha.
DSC_1025.JPG

Soko hili jipya linahitaji kujengwa kisasa na Kukabithiwa kwa wafanyabiashara hao na sio kama lilivyo hapo maana wafanyabiashara ni Kama wametupwa hapo huku serikali ikichukua ushuru wa Tsh. 500 kila siku kutoka kwa wafanyabiashara hao huo ni sawa na unyonyaji au uporaji
DSC_1022.JPG
 
Moshi imerudi nyuma kidogo
Wenyeji wenyewe wamejazana. Sio mji rafiki kwa mgeni. Ukwieka biashara ama hata hiace/coaster wenyeji wakishajua kuwa ni ya chasaka hawapandi kabisa ama hawaji dukani kwako kununua..anasema yaani nikamnyanyue mtu asiye wa nyumbani.
Hata huko mkoani uliko chunguza Kama yupo anayeenda kununua kwa asiye wa kwao,sijui Kama litakuwa jiji kabla ya mpanda , sumbawanga,musoma ama Tabora Mana iyo miji iko afadhali kidogo Ila sio
 
Umeandika uongo mtupu acha ukabila
 
Hapa ndipo walipohamishiwa Wafanyabiashara wa soko kuu la samaki kutoka eneo la manyema mbuyuni na kuletwa hapa maili sita.
View attachment 2152687
Lengo na kuwahamisha wafanyabiashara hao na kuwaleta hapa ni kile kinachodaiwa kuwa ni katika kuiandaa moshi kuwa jiji na hivyo kuondoa mlundikano wa kuwa sehemu moja.

Lakini cha kushangaza manispaa ya moshi ilichofanya ni kutoa tu eneo na kuwapa wafanyabiashara hao bila kuweka miundombinu yoyote katika soko hilo jipya.

Mfano mzuri hakuna sehemu /mfumo maalumu kwa ajili Ya kuoshea samaki bali wafanyabiashara hao wamekuwa wakiosha wenyewe kwenye Ndoo zao na kumwaga maji popote humo humo sokoni. View attachment 2152693

Wafanyabiashara hao hawajajengewa vizimba vya kuuzia samaki wabichi na wanaokaangwa hapo sokoni bali kila mtu kajifanyia anavyojua mwenyewe wengine wameweka miavuli wengine meza nk.

Choo cha umma katika soko hilo hakuna bali wafanyabiashara na wateja wa soko hilo wamekuwa wakitumia vyoo vilivyopo jirani na soko hilo.

Soko hili ambalo kwa sasa ni Maarufu zaidi ya Kule lilikokuwa mwanzo kutokana na Eneo lililopo linachafua taswira ya mji kutokana na kuwa lipo karibu kabisa na barabara kuu ya Moshi Arusha. View attachment 2152702
Soko hili jipya linahitaji kujengwa kisasa na sio kama lilivyo hapo maana wafanyabiashara ni Kama wametupwa hapo huku serikali ikichukua ushuru wa Tsh. 500 kila siku kutoka kwa wafanyabiashara hao huo ni sawa na unyonyajiView attachment 2152706
Lipumba bado ana wafuasi sijui anakwama wapi kuwaunga.huyo mama kavaa khanga yake mpyaaaaa
 
Ngoja waje Sasa ...Umetafuta maneno mwenyewe...huko hawataki kutajwe kwa ubaya
 
Mji wa matajiri huo tatizo moja tu la moshi lingekuwa jiji baada y chuga ishu ni moja tu point bado wako zama za ukabila

Sio rafiki mji huo kwa wageni kabisa wanajichomeka chuga kule bila interaction ingekuwa nyuma pia

Enyi wachaga hamtokuja elimika hata msome vip kukiweka ukabila mbele ruhusuni watanzania wenzenu wafanye biashar hapo muone na muache ubaguzi
 
Wenyeji wenyewe wamejazana. Sio mji rafiki kwa mgeni. Ukwieka biashara ama hata hiace/coaster wenyeji wakishajua kuwa ni ya chasaka hawapandi kabisa ama hawaji dukani kwako kununua..anasema yaani nikamnyanyue mtu asiye wa nyumbani.
Hata huko mkoani uliko chunguza Kama yupo anayeenda kununua kwa asiye wa kwao,sijui Kama litakuwa jiji kabla ya mpanda , sumbawanga,musoma ama Tabora Mana iyo miji iko afadhali kidogo Ila sio
Yani we jamaa unashida mahali
Unaifananisha Moshi na Musoma?

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom