Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Hapa ndipo walipohamishiwa Wafanyabiashara wa soko kuu la samaki kutoka eneo la manyema mbuyuni na kuletwa hapa maili sita.
Lengo na kuwahamisha wafanyabiashara hao na kuwaleta hapa ni kile kinachodaiwa kuwa ni katika kuiandaa moshi kuwa jiji na hivyo kuondoa mlundikano wa kuwa sehemu moja.
Lakini cha kushangaza manispaa ya moshi ilichofanya ni kutoa tu eneo na kuwapa wafanyabiashara hao bila kuweka miundombinu yoyote katika soko hilo jipya.
Mfano mzuri hakuna sehemu /mfumo maalumu kwa ajili Ya kuoshea samaki wabichi bali wafanyabiashara hao wamekuwa wakiosha wenyewe kwenye Ndoo zao na kumwaga maji hovyo humo humo sokoni.
Wafanyabiashara hao hawajajengewa vizimba vya kuuzia samaki wabichi na wanaokaangwa hapo sokoni bali kila mtu kajifanyia anavyojua mwenyewe wengine wameweka miavuli wengine meza nk.
Hakuna miundombinu ya. Maji ndani ya Soko hilo wala Choo cha umma ndani ya soko hilo bali wafanyabiashara na wateja wa soko hilo wamekuwa wakitumia vyoo vilivyopo jirani na soko hilo.
Soko hili ambalo kwa sasa ni Maarufu zaidi ya Kule lilikokuwa mwanzo kutokana na Eneo lililopo linachafua taswira ya mji kutokana na kuwa lipo karibu kabisa na barabara kuu ya Moshi Arusha.
Soko hili jipya linahitaji kujengwa kisasa na Kukabithiwa kwa wafanyabiashara hao na sio kama lilivyo hapo maana wafanyabiashara ni Kama wametupwa hapo huku serikali ikichukua ushuru wa Tsh. 500 kila siku kutoka kwa wafanyabiashara hao huo ni sawa na unyonyaji au uporaji