Hili ni swali langu kwenu mnaosema Israel ni ya wapelestina, Acheni kujitia upofu mtazame uhalisia

Hili ni swali langu kwenu mnaosema Israel ni ya wapelestina, Acheni kujitia upofu mtazame uhalisia

Labda twende kwenye mfano halisi kwa sababu naona logic unataka kuiweka kando.

Ushahidi wa kihistoria mamlaka ya zanzibar yana maeneo mpaka huku kwetu bara.

Unafahamu kuwa Kigamboni ni ya Zanzibar? Na haikuishia hapo, mpaka bandari ya bara Dar es Salaam ni ya wazanzibar. Upo tayari kuwapa eneo lao?

Wazanzibar wakidai hayo maeneo kwa kitumia huo ushahidi wa kihistoria upo tayari kuwapa hayo maeneo?
Swali umeuliza mwenyewe ili tupate jibu unaleta mada nyingine usiponijibu basi sikulazimishi
 
MATHAYO 23:37, 38

37. Ee Yerusalemu, Yerusalemu! Unayewaua manabii. Unawapiga kwa mawe wale ambao Mungu amewatuma kwako. Mara nyingi nimetaka kuwasaidia watu wako. Nimetaka kuwakusanya watu wako kama kuku anavyowakusanya vifaranga wake chini ya mbawa zake. Lakini hukuniruhusu kufanya hivyo.

38. Sasa Hekalu lako litaachwa ukiwa kabisa.

Hao Wayahudi walishalaaniwa hiyo kuishi hapo wanaforce tu walitakiwa waendelee kusambaratika na ndio maana hawana amani hapo ni machafuko kila siku. Waliwakataa manabii wakapewa adhabu ya kusambaratika na kutangatanga
 
Swali umeuliza mwenyewe ili tupate jibu unaleta mada nyingine usiponijibu basi sikulazimishi
Sasa wewe unatafuta ubishani.

Wengine hatupendi ubishani na ndiyo maana hatuchangii tu mada bali tunachangia pale inapotupasa kuchangia.

Kama ndiyo njia uliyoichagua ya kukaa nayo kaa nayo tu: Maarifa ni ya mtu na ujinga ni wa mtu vilevile.
 
Mtu anaishi Tukuyu na mwingine Tandahimba mna ongea in details habari za ardhi iliyopo huko middle east....na bendera za nchi hizo mnapeperusha....utasema mmerogwa
Sio wazima hata kidogo
 
Kanaani ndio nchi waliyopewa wayahudi, waisrael na Mungu wao baada ya kutoka Misri.

Kabla hawajaingia ktk ile nchi, wakiongozwa na Yoshua mwana wa nuni baada ya Musa kufa. Mungu aliwaambia wana wa Israel, mtakapoingia ktk hiyo nchi, waangamizeni wenyeji wote.

Wana wa Israel wakaacha wakanaani na wengine pia. Mungu alikasirika, akawaambia wana wa Israel, hayo mataifa mliyoacha kuyaangamiza yote. Hakika yatakuwa kama mwiba ktk maisha yenu yote.

Palestina ni kama mwiba ktk maisha yote ya Taifa la Israel, na hiyo ni nchi halali kabisa ya Israel sababu Baba yao Ibrahim alikaa hapo na aliimiliki hata.

Baada ya Ibrahim kufa, wakaja watu wengine kuishi hapo, hiko ndicho kipindi cha wana wa Israel walipokuwa utumwani kwa miaka 430 nchini Misri.
Mungu gani huyo unayemzungumzia hapa?? Mungu wa Yakobo??
 
Ukisoma bibilia hasa agano la kale, unaona kama vile ni katiba iliyokuwa inawahusu makabila 12 ya waiziraeli tu. Sisi huku wa tandale kama vile tunajipendekeza tu katika mambo yasiyotuhusu
 
Ngoja mtu siku aje kwenye kiwanja chako au shamba lako akuambie kuna sauti imemjianya Mungu imemwambia hiko kiwanja au shamba lako ni pake.
 
Mtu anaishi Tukuyu na mwingine Tandahimba mna ongea in details habari za ardhi iliyopo huko middle east....na bendera za nchi hizo mnapeperusha....utasema mmerogwa
Hahahahahahahahaha halafu unakuta wanabishana mpaka wanatukaniana mama zao, wa Africa weusi kama tumerogwa hivii
 
Hahahahahahahahaha halafu unakuta wanabishana mpaka wanatukaniana mama zao, wa Africa weusi kama tumerogwa hivii
Ukiwauliza history za makabila Yao hawajui....kabisa kazi kujitoa ufaham Kwa makabila ya watu ambao hawana undugu nao kabisa
 
Wengi ni wafia dini ya mudi,wanajitia uchizi ila ukweli upo wazi na historia ipo wazi kabisa.
Mungu alivyo wa ajabu alimtimua yule kijakazi na mwanaye wakaenda maporini huko hadi ukamilifu wa dahari na dini zote zinajua hivyo!

Sipati picha wangeendelea kubakizwa na kuzalia pale! Hilo timbwili leo lingekuwa balaa! Kwa neema zake hawajaacha uzao pale nchi ya ahadi!
 
Ukiwauliza history za makabila Yao hawajui....kabisa kazi kujitoa ufaham Kwa makabila ya watu ambao hawana undugu nao kabisa
Hahahahahahahahaha sahihi kabisaa, wabongo tuna safari ndefu mnooo ya kujitambua
 
Huu mgogoro una sura nyingi kuanzia ya kisiasa, kiimani, kihistoria n.k
 
Kwa misingi hiyo Wahindu wakisema kwa mujibu wa vitabu vyao vya kidini mungu wao amewaambia Tanzania ni nchi yao ya ahadi watanzania wote kuanzia sasa hamna haki na nchi yenu wewe utakubali kuondoka kwenye hii ardhi na kumuachia Mhindu hii nchi?
jitahidi uelewe kabla ya kubisha , story za wayaudi sio tu za kidini bali kihistoria pia
 
Hawezinjibu Hilo swali kilogically

Ataishia kukuletea nukuu za Biblia tu
maswala ya israel sio kidini tu bali kihistoria pia ambapo hata wapalestina pia wanaamin hivyo , kwann unalazimisha tuitizame kidini zaid?
 
Kwa misingi hiyo Wahindu wakisema kwa mujibu wa vitabu vyao vya kidini mungu wao amewaambia Tanzania ni nchi yao ya ahadi watanzania wote kuanzia sasa hamna haki na nchi yenu wewe utakubali kuondoka kwenye hii ardhi na kumuachia Mhindu hii nchi?
Mkuu umeuliza swali lenye tafakuri kubwa sana sijuwi kama utajibiwa.
 
Tunamsubiri tuone jawabu lake litakuwaje!
kasomeni hata story za falme za jiran na hapo Israel , mjifunze maana dini zimewatia upofu wakati waliowaletea dini wanawatambua uwepo wa waisrael hapo middle east , sio persia au warumi wala mesopotania kote huko wanaitambua israel kuwai kuwepo hapo
 
Back
Top Bottom