Hili suala la Bongo Zozo kujipenyeza kila mahali hadi chumbani kwa baba limekaaje?

Hili suala la Bongo Zozo kujipenyeza kila mahali hadi chumbani kwa baba limekaaje?

Maeneo mengi tu ya huko amefika kwenye museum na maeneo kibao. Ila yote kwa yote bongo zozo ni sawa tu na wazungu Koko wengine japo hofu yako, ni sahihi tu. Hata sisi tungejifunza ujasusi wa hivyo tungekuwa mbali, Leo kununu gari zambia bei rahisi wakati yanapita bandari na Boda za kwetu. Kuna mahali tumekwama
Museum ni jumba la maonesho, tofauti na ikulu
 
TANZANIA na vyombo vya usalama sio wajinga kiasi hicho mnachodhani
Sorry unaongelea vyombo vya jikoni kama sufuria, sahani na vikombe ... ?

... au unaongelea vile VYOMBO vilivyo mteka MOO halafu vikamuokota akiwa ametupwa jalalani GYMKHANA

... au unaongelea vile VYOMBO vilivyovamia CLOUDS FM amabvyo ilifikia boss wao alikua yule M*T*KO makubwa aliekuwa pale Ilala Boma

... au unaongelea vyombo vilivyom'minia risasi yule jamaa wa Singida alipokua kule Dodoma Kutimiza wajibu wa kikatiba

... au unaongelea vile vyombo vilivyojipatia umaarufu wa jina la WASIOJULIKANA

... we unaongelea vyombo gani kwani kama vyombo vya jikoni sawa ni muhimu sana katika maisha yetu watanzania

Ila kama ni hivi VYOMBO vya pale kwenye lile jengo la yule ndege maarufu anaekula viranga vya kuku ... Hamna kitu

Nilichoka siku niliposhuhudia mtoto wa shemeji yake na moja ya chombo alipopata ajira ya kuwa chombo na Div 4 yake ya D mbili hapo ndipo nilipo choka kabisa
 
Intelligence ya Tanzania iliyoasisiwa na Jiwe Magufuli inaangalia kulinda kit cha Rais aliyeko madarakani mengine hayawahusu.
Huyo Bongo zozo siku akiinua kinywa tu kuropoka jambo lolote kuhusu RAIS ataitwa uhamiaji na kupewa masaa 24 tu aondoke haraka
Magufuli ndio aliasisi inteligence?

Aliwakosea nini huyu mzee?

Ifike mahali watu kama nyinyi mkemewe hizo ni chuki binafsi

Magufuli alifanya makubwa sana ambayo wewe na ukoo wako hakuna mwenye akili kumzidi
 
Hata sie pia tulikuwa na mawazo kama yako lakini baadae tukafahamu kwamba jamaa amejitolea tu na kuipenda nchi yetu kwa sababu anaye mwanamke wa kibongo alafu mwenyewe umesikia amesema anatamani ampe mkono kwanza lakini kwa sababu za kiusalama harusiwi kumpa mkono raisi mpaka raisi atoe yeye kwanza naami kwa intelligence ya nchi yetu huyu jamaa kama angelikuwa mtu wa hivyo unavyomchukuria asingefikia hapo halipo.labda nahisi utofauti wa rangi yake nasi ndio inayochangia jamaa kumfikiria kwamba ni jasusi fulani kumbe ujasusi ,ubaya hauna rangi wala ukabila
Ujasusi sio suala la kudhuru tu
 
Huyu j

Huyu jamaa kipindi cha nyuma alikuwa anaishi iringa eneo la wilokesi kazi yake kubwa ilikuwa kununua fedha za zamani.wengi walijua ni fbi
Fbi hafanyi kazi nje ya marekani

Nchi hii ina vilaza wengi na ndio wanaanzisha na kuchangia mada humu
 
Muda mwingine middle class wa kitanzania mna push Ile line ya uwezo wa kawaida wa kufikiri, tupo more concern na mambo ya ajabu huku yanayotuathiri zaidi tunayakwepa au kuogopa vivuli vyetu.

Nchi hii Ina more pressing issues kuliko huyu mzalendo tuliyetofautiana rangi tu, maadui wetu bado ni ujinga, umasikini na maradhi SIO woga kuhusu usalama wa politicians wetu, budgets zao za kiusalama watanzania wengi hatuzijui and we can't ask them.

Mkuu huenda ww ni mgeni au unakwepa kuongea ukweli, hayo mambo ya msingi watu wanahoji na wanaishia kutekwa, kufayiwa ukatili ikiwemo na kuhujumu sehemu zao za vipato.
 
Mkuu huenda ww ni mgeni au unakwepa kuongea ukweli, hayo mambo ya msingi watu wanahoji na wanaishia kutekwa, kufayiwa ukatili ikiwemo na kuhujumu sehemu zao za vipato.
Na matokeo yake wanafwata mkia!uoga na ubinafsi, mimi ni mzaliwa na mkulia wa huku lingusenguse sio mgeni na always ninapenda facts
 
Magufuli ndio aliasisi inteligence?

Aliwakosea nini huyu mzee?

Ifike mahali watu kama nyinyi mkemewe hizo ni chuki binafsi

Magufuli alifanya makubwa sana ambayo wewe na ukoo wako hakuna mwenye akili kumzidi
Nyie ndio mliokuwa mkimwita Magufuli mheshimiwa Mungu huku mkisema kuwa Tanzania haitampata kiongozi mwenye akili kama Magufuli.
Magufuli alikuwa na akili ndogo tu sema tu wengi wa aliowaongoza akili zao zilikuwa ndogo zaidi that's why walimwina genius sana ikiwemo wewe.
Kiongozi atakayeweza kuondoa ufukara na umaskini wa Watanzania ambao wengi vitanda vyao viko juu ya madini na ardhi yenye rutuba huyo ndiye tutamwita kiongozi Bora na mwenye akili sana.
Sio kiongozi mshenzi, muuaji, mwenye matamko na muongo kama Magufuli.
 
Nimebahatika kujuana na waingereza kadhaa, hivyo siwezi kumshangaa Bongozozo, Waingereza wakikipenda kitu wanakuwa na kauchizi Fulani ndani yake. Kilichobaki tuwaachie watu wa ulinzi na usalama wao wanajua zaidi
 
Mwaka Jana kaenda Zanzibar akaambiwa aende Oman Kuna Wazanzibar wanazo hizo hela za wajerumani na dinar za waoman kipindi wanaitawala Zanzibar alienda lakini sijui kama akifanikiwa .Bongozozo kazi yake kubwa hapa Tanzania licha ya kuwa kaoa mwanamke kutoka Moshi ni kutafuta Mali za kale hasa hizi hela za wajerumani.kwenye mpira anazuga tu .
Sio rahisi kufahamu malengo halisi ya mtu mpaka upate muda wa kuwa nae karibu.

Huyu jamaa anatuzuga tu hana jema lolote.
 
Bongozozo ni mjanja sana na kazi kubwa anayoifanya hapa Tanzania ni kutafuta hela za zamani za wajerumani zile zinazoitwa Simba mbili na vitu vingine vya kale kama hivo sema anawazuga wasiojua lakini kazi yake kubwa ni hiyo.Huko kujifanya ni shabiki wa Taifa stars ni uongo tu.
Kumbe anatafuta fedha za kale halafu anatuzuga kuipenda Taifa Stars??

Wazungu bwana.
 
Back
Top Bottom