Hili suala la malezi ya hivi limekaaje?

Hili suala la malezi ya hivi limekaaje?

Joined
Sep 4, 2024
Posts
51
Reaction score
34
Habari za muda huu wanajukwaa?

Ipo hivi niliwahi kuwa kwenye mahusiano na mshichana mmoja anayetokea ukanda wa kaskazini, msichana huyo pia alikuwa akisoma chuo kimojawapo huko Arusha.

Sasa kilichokuwa kikinishangaza licha ya tabia yake kuwa njema na mcha Mungu mzuri lakini bado wazazi wake hasa mama yake ameendelea kumlea kama mtoto mdogo yani bado anamfuatilia sanaa kana kwamba ni binti bado hajavunja ungo.

Jambo hili lilinifanya kujiuliza maswali mengi kwa mfano, je huyu binti anayetarajiwa kuwa mke wa mtu siku chache za usoni anafuatiliwa hivi na mzazi wake ina leta picha gani kwenye jamii?

Soma Pia: Wote wenye tabia mbaya ni malezi mabovu ya mama zao

Jambo jingine mama yake ni mkali sanaa kiasi kwamba akiona tuu kijana yeyote anajisogeza kuongea na mwanaye anamkaripia hadharani sasa najiuliza huyo mama hataki mwanae atongozwe ataolewa vipi? Hata mwanaye anamuogopa sanaa.. Mlio na watoto wa kike hebu mje mtoe uzoefu wenu.
 
Kwanini linapokuja swala la Mtoto wa kike mnakimbilia kwenye kuolewa tu?

Unajuaje kuwa anatarajiwa kuwa Mke wa mtu?

Assumption za ajabu sana
Mpaka yule msichana alikubali kuingia kwenye mahusiano na mimi na pia nilimweleza malengo yangu juu yake na yeye alinielewa na kunikubalia hilo bila shaka linaonyesha yeye alishajiandaa kuwa mke. Changamoto tuu ni treatment ya mama yake anamfuatilia msichana mkubwa wa miaka 24+ kama mtoto wa darasa la nne. Yani kiufupi haruhusu hata nusu ya utashi wa mwanae utumike!!
 
Mtu yuko chuo wewe unawaza kumuoa?

Kwani lazima utumie neno kuoa ili kumpata Mwanamke?
 
Wachafuzi hamchelewi kuharibia binti maisha
Hilo halikuwa kusudio langu, bali nilipanga nije nimuweke ndani ila sasa nikapata mashaka vile mama yake anavyo m-treat. Ni kama hamuamini msichana mkubwa vile anaweza kujisimamia mwenyewe.
 
Mpaka yule msichana alikubali kuingia kwenye mahusiano na mimi na pia nilimweleza malengo yangu juu yake na yeye alinielewa na kunikubalia hilo bila shaka linaonyesha yeye alishajiandaa kuwa mke. Changamoto tuu ni treatment ya mama yake anamfuatilia msichana mkubwa wa miaka 24+ kama mtoto wa darasa la nne. Yani kiufupi haruhusu hata nusu ya utashi wa mwanae utumike!!
Una uhakika utamuoa?
Huna mawazo kama hawa vijana wa ovyo wa kataaa ndoa?
 
Huyo mama ndio anajua maana ya kulea sasa, kwasababu bado yuko mikononi mwake, akiolewa pia uhuru wake unakuwa chini ya mume wake
Duuu, kwangu mimi nilitafsiri kama kumnyima binti yake nafasi ya kufanya maamuzi kwa kujiamini yeye mwenyewe pasina uwepo wa mama. Yaani niliona kunapoelekea mama ataenda kumchagulia nwanae kijana wa kumuoa!😌
 
Back
Top Bottom