Hili swali linanitatiza sana, kuna utaratibu wowote wa mwanajeshi kuacha kazi, pale anapotakiwa kwenda vitani?

Kuna siku nimeona jamaa mmoja anahoroja maneno eti vijana wa kirusi wanalalamika Kwamba hawakuambiwa kama wanaingia vitani Ukraine. Ni kweli sometime hutaki kuambiwa unaenda wapi. Unachaguliwa TU we'we, na we'we na Yule kaa pale inakuja gari ingia ndani. Unafika mbele unaambiwa Kuna Jambo ( either Ni operation ya kijeshi) unapewa silaha na mikakati na Hakuna kubishana.
Nb.
Askari halalamiki kupelekwa vitani. Hiyo Ni kazi Kama kupika, kuimba au kuvua samaki.
 
Nimejaribu kufikiria hivyo, baada ya kuona picha za wanajeshi walio-uwawa huko kwenye vita ya Ukraine na Urusi.

Naona vijana wameangamia, huku wakiwa wameacha tegemezi, watoto, wake n.k; huku wanaofanya maamuzi wakiwa ofisini wakipulizwa viyoyozi.

Inawezekana, wakuu? Uhai kwanza, mengine baadaye.​
Sijuh ulikuwa una waza nini.?

Nataman niuluze umri wako unamiaka mingap?

Eb tutoe Mfano hivi hapa tz kila mwanajesh aamue kutetea uhai wake yani wakatae kuhatarisha usalama wao kwa sababu ya familia zao na raia wengine je u nadhan aman na uturivu inge baki hivi??
 
Wanajeshi wameshajitolea kufa kwa ajili ya kulinda wengine sio kwa sababu ya kumchukia adui
 
Nimejaribu kufikiria hivyo, baada ya kuona picha za wanajeshi walio-uwawa huko kwenye vita ya Ukraine na Urusi.

Naona vijana wameangamia, huku wakiwa wameacha tegemezi, watoto, wake n.k; huku wanaofanya maamuzi wakiwa ofisini wakipulizwa viyoyozi.

Inawezekana, wakuu? Uhai kwanza, mengine baadaye.​
Unajua adhabu ya deserters? Kifo!
Nitakubali kwenda vitani endapo kama kweli Vita husika ni Vita ya HAKI, lakini Kamwe siwezi kukubali kwenda vitani endapo kama najua wazi kabisa kwamba VIta husika siyo vita ya HAKI hata kidogo.
VIta ya Haki daima Wapiganaji huwa wanakuwa na Morali (Hamasa) ya kwenda kupigana vitani, lakini Vita isiyokuwa ya Haki daima Wapiganaji huwa wanakuwa HAWANA Morali (Hamasa) ya kupigana vitani.

"Yes, we need war. But not a fracass war."
Barack Obama.
 
Kwanza ujue mwanajeshi si raia ila raia anaweza kuwa mwanajeshi na si kila raia anaweza kufuzu kuwa mwanajeshi. Inachukua mafunzo ya kipekee sana kumbadirisha raia kuwa mwanajeshi. Swali lako umeuliza kiraia ndiomana unashangaa inakuwaje amri inapotoka wanajeshi wanatii bila kupinga.
Just know that It takes special trainings to turn a civilian to be a SOLDIER and once a soldier will always be a soldier.
Ni nani huyo aliekudanganya askari si raia? Askari ni raia kama wengine but yeye ana mafunzo ya kijeshi na uvumilivu wa Kila hali.
Kwa maana ya sentensi yako ni kwamba hata mwalimu so raia kwasababu ya kazi yake!
Wazi?
 
Wanaweza kabisa. Kama Lebanon wanagombania, Ukraine watashindwa?
Tofautisha mission za kulinda amani waendapo wabongo kama huko Lebanon, na Congo .
Ukraine Kuna operation za kivita.
Huko Lebanon Israel wakipiga kambi yenu ya UN peace keeping officers hakuna kujibu mnakaa kimya na mnasuburi UN walaani kama ilivyotokea mwezi wa 11 Kule Lebanon.
Nb hata ukiwa kamanda usililie vita, vita si lelemama nimekuwa nikiona na kufuatilia vita ya Ukraine hali ni mbaya makamanda wanalia bila haya.
 
Nitakubali kwenda vitani endapo kama kweli Vita husika ni Vita ya HAKI, lakini Kamwe siwezi kukubali kwenda vitani endapo kama najua wazi kabisa kwamba VIta husika siyo vita ya HAKI hata kidogo.
VIta ya Haki daima Wapiganaji huwa wanakuwa na Morali (Hamasa) ya kwenda kupigana vitani, lakini Vita isiyokuwa ya Haki daima Wapiganaji huwa wanakuwa HAWANA Morali (Hamasa) ya kupigana vitani.

"Yes, we need war. But not fracass war."
Barack Obama.
Kwa vita zinazoendelea sasa unaweza kutupa mfano ipi haki na ipi si haki
 
Ni nani huyo aliekudanganya askari si raia? Askari ni raia kama wengine but yeye ana mafunzo ya kijeshi na uvumilivu wa Kila hali.
Kwa maana ya sentensi yako ni kwamba hata mwalimu so raia kwasababu ya kazi yake!
Wazi?
Mwanajeshi sio raia
 
Wanajeshi sio raia kwa maana wana majukumu na wajibu tofauti katika jamii, ndio maana wanatofautishwa.

1. Majukumu na Wajibu:
  • Wanajeshi: Jukumu lao kuu ni kuhudumu katika vikosi vya ulinzi ambavyo direct huhusisha mapigano, operesheni za kijeshi, na kulinda usalama wa taifa.
  • Raia: Hata wakifanya kazi kwenye vikosi vya ulinzi hufanya kazi zisizo za kijeshi na shughuli zinazochangia utendaji wa kawaida tu kijamii.
2. Sheria za nchi
  • Wanajeshi: Wao huendeshwa na sheria za kijeshi na kanuni za maadili, ambazo huongoza tabia zao ndani na nje ya kazi isipokuwa kwa baadhi ya makosa ya Jinai Kama Mauaji nje ya kazi, kubaka ila makosa mengine huwa wanahukumiwa na mahakama zao za kijeshi na wana polisi wao Kabisa.(KASOME NATIONAL DEFENCE ACT)
  • Raia: Wao huendeshwa na sheria za kiraia na kanuni zinazotumika kwa watu wote.
3. Mafunzo na Ujuzi:
  • Wanajeshi: Hupata mafunzo maalum ya kijeshi ili kupata ujuzi katika mapigano, utunzaji wa silaha, mikakati, na maeneo mengine yanayohusiana na kijeshi mafunzo yao na mitaala ni Siri. Ndio maana vyuo na shule zao mitaala ya mafunzo ya kijeshi haisimamiwi na Nacte,necta wala Tcu pia hawaruhusu mtu mwenye kasoro yeyote hata mlemavu wa ngozi kuhudhuria mafunzo lakini Huwezi kuona haki za binadamu wakiingilia maana wale sio raia
  • Raia: Wanamiliki ujuzi na utaalamu mbalimbali kuhusiana na kazi zao na maisha ya kila siku, ambayo yanaweza yasijumuishe mafunzo ya kijeshi na mtu yeyote anaweza kusoma,hakuna Siri
4. Haki na Ulinzi:
  • Wanajeshi: Ingawa wanajeshi wana haki, haki zao zinaweza kuwa na mipaka katika hali fulani kutokana na mahitaji ya kijeshi na mahitaji ya operesheni.
  • Raia: Wao hupewa ulinzi mpana chini ya sheria za kiraia na sheria za kimataifa za kibinadamu, hasa wakati wa migogoro ya silaha.(google kitu kinaitwa mikataba ya Geneva iko mitatu au minne Kama sikosei)
5. Ushiriki katika Mapigano:
  • Wanajeshi: Wao wameidhinishwa kushiriki katika mapigano na kushiriki katika vitendo vya vita kama sehemu ya majukumu yao ya kawaida.
  • Raia: Kwa ujumla wamekatazwa kushiriki moja kwa moja katika mapigano. Sheria ya kimataifa ya kibinadamu inapambana mno kulinda raia dhidi ya ushiriki na athari za vita.
 
Tofautisha mission za kulinda amani waendapo wabongo kama huko Lebanon, na Congo .
Ukraine Kuna operation za kivita.
Huko Lebanon Israel wakipiga kambi yenu ya UN peace keeping officers hakuna kujibu mnakaa kimya na mnasuburi UN walaani kama ilivyotokea mwezi wa 11 Kule Lebanon.
Nb hata ukiwa kamanda usililie vita, vita si lelemama nimekuwa nikiona na kufuatilia vita ya Ukraine hali ni mbaya makamanda wanalia bila haya.
Congo peace keeping ilimalizika mwaka Jana mwanzoni baada ya vikosi vya UN kuondolewa sahizi ni mapigano tu.
Tanzania tumeenda chini ya mwavuli wa Sadc
 
Wanajeshi sio raia kwa maana wana majukumu na wajibu tofauti katika jamii, ndio maana wanatofautishwa.

1. Majukumu na Wajibu:
  • Wanajeshi: Jukumu lao kuu ni kuhudumu katika vikosi vya ulinzi ambavyo direct huhusisha mapigano, operesheni za kijeshi, na kulinda usalama wa taifa.
  • Raia: Hata wakifanya kazi kwenye vikosi vya ulinzi hufanya kazi zisizo za kijeshi na shughuli zinazochangia utendaji wa kawaida tu kijamii.
2. Sheria za nchi
  • Wanajeshi: Wao huendeshwa na sheria za kijeshi na kanuni za maadili, ambazo huongoza tabia zao ndani na nje ya kazi isipokuwa kwa baadhi ya makosa ya Jinai Kama Mauaji nje ya kazi, kubaka ila makosa mengine huwa wanahukumiwa na mahakama zao za kijeshi na wana polisi wao Kabisa.(KASOME NATIONAL DEFENCE ACT)
  • Raia: Wao huendeshwa na sheria za kiraia na kanuni zinazotumika kwa watu wote.
3. Mafunzo na Ujuzi:
  • Wanajeshi: Hupata mafunzo maalum ya kijeshi ili kupata ujuzi katika mapigano, utunzaji wa silaha, mikakati, na maeneo mengine yanayohusiana na kijeshi mafunzo yao na mitaala ni Siri. Ndio maana vyuo na shule zao mitaala ya mafunzo ya kijeshi haisimamiwi na Nacte,necta wala Tcu pia hawaruhusu mtu mwenye kasoro yeyote hata mlemavu wa ngozi kuhudhuria mafunzo lakini Huwezi kuona haki za binadamu wakiingilia maana wale sio raia
  • Raia: Wanamiliki ujuzi na utaalamu mbalimbali kuhusiana na kazi zao na maisha ya kila siku, ambayo yanaweza yasijumuishe mafunzo ya kijeshi na mtu yeyote anaweza kusoma,hakuna Siri
4. Haki na Ulinzi:
  • Wanajeshi: Ingawa wanajeshi wana haki, haki zao zinaweza kuwa na mipaka katika hali fulani kutokana na mahitaji ya kijeshi na mahitaji ya operesheni.
  • Raia: Wao hupewa ulinzi mpana chini ya sheria za kiraia na sheria za kimataifa za kibinadamu, hasa wakati wa migogoro ya silaha.(google kitu kinaitwa mikataba ya Geneva iko mitatu au minne Kama sikosei)
5. Ushiriki katika Mapigano:
  • Wanajeshi: Wao wameidhinishwa kushiriki katika mapigano na kushiriki katika vitendo vya vita kama sehemu ya majukumu yao ya kawaida.
  • Raia: Kwa ujumla wamekatazwa kushiriki moja kwa moja katika mapigano. Sheria ya kimataifa ya kibinadamu inapambana mno kulinda raia dhidi ya ushiriki na athari za vita.
Maelezo yako haya kwa kiasi kikubwa Sana yamejikita katika Sheria, Kanuni, taratibu pamoja na tamaduni zilizopo Tanzania, lakini hayajihusisha kwa undani na masuala mtambuka ya kijeshi katika Mazingira ya kidunia kwa ujumla wake. Aidha, ukienda kwenye nchi zingine hali ipo tofauti kidogo na hivyo ulivyoeleza.
 
Back
Top Bottom