Hill water alivyoingia sokoni na kuwapiku wakongwe - Uhai & Kilimanjaro

Sasa unaozungumzia shinyanga usekwen huko
 
Maji ya Kilimanjaro ushindani umekuwa mkubwa mpaka kaamua kushusha bei zimekuwa kama maji mengine
Naamini Maafisa Masoko wa Bonite hapa walifanya kosa. Kilimanjaro ni maji yaliyojenga HIGH STATUS (like Iphone). Hivyo ange deal na customers wakubwa mfano mahoteli—angewauzia retail price kama ya Jambo au Hill water, angeondoa sababu ya wao kukimbilia makampuni mengine, na angemantain wateja wake hao tu. Huku mtaani angekuwa anadokoa dokoa tu.
 
R RIP Dr
 
Jambo product zake huwa zina ladha ya hovyo alaf ni mzee wa kuiga product za azam nae anazo ice-cream kama zile za azam ila ukionja zina kereketa kwenye koo mbaya kabisa
Jamaa bado hawajakaa kwenye mstari vizuri
Kuna mtu alikuwa ananiambia kuwa hiki kiwanda sasa hivi kiko chini ya wachina; Salum, nduguye na mwanae ni wabia tu—wachina ndio largest shareholders.
 
Biashara hizi zina mengi. Compliance kwa wafanyabiashra wakubwa hawa hasa makada ni changamoto. Mmoja ya wadaiwa Sugu wa Ushuru wa Council ni hii Kampuni, mwaka jana MD aliyekuwepo pale Council alianza yabana makampuni mengi sana yanayodaiwa Ushuru, kama ilivyo ada akahamishwa.
 
Kumbe Fredy (FRESHO) alikuwa ndugu wa Hill Water. Jamaa wapambanaji sana. Sema Tanzania ni kujiamini tu na kujua jinsi ya kudeal na Serikali.
 
Mimi tangu nimefika hili nchi lenu la joto sijaona maji matamu! Yote tana ka radha fulani hivi kwa hovyo hovyo! Labda nikijaribu hayo afya? Lakini haya uhai na hill water hapana aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…