Hatia III kaisikilize, vina empty na ndio ngoma niliyokua namlaumu Disasta, hajatembea na vina karap hakuna mizani hakuna vina hakuna stanza, isikilize
Nioneshe verse gani hapa imekosa vina
Dizasta Vina
Hatia iii Lyrics
Ah...
Nakusalimu mwafrika...nakusalimu habari gani.../
Nikaribishe tuketi...niseme yaliyo ndani.../
Sahau kuhusu hadithi za kale...za upendo wako.../
Nataka leo tukae...tuijadili kesho yako.../
Kutoka kupiga ramli...na kutii mizimu.../
Umeanza kufata amri...za TV na simu.../
Na ubaya ni kwamba...umeanza kuikacha sanaa.../
Na kufata siasa...ambayo inakulaza na njaa.../
Na kila unachokiona...unataka kubeba.../
Vichache vimekushinda...na unapanga kuongeza.../
Juzuu,Katekisimu mpaka Novena.../
Sio zako...zako zilikuwa ni kutamba ngojera.../
Umezubaa...majirani wameanza kufika kwako.../
Na unaamini kuwa...watakubebea shida zako.../
Kwa sababu ya ujinga,umezidi umasikini.../
Unamjengea jirani...kwako unachimba unabaki chini.../
Zamani...ulikuwa una sembe ya kusaza.../
Uliabudu kazi...ukaliweka jembe kwenye shamba.../
Ghafla ukauza panga...ukapamba jembe kwenye kabati.../
Ukanunua kioo ujirembe...ili uende na wakati.../
Ume...chagua urembo na umetupa werevu.../
Umeuza mifugo...unafuga kucha na ndevu.../
Familia iwe...mwafrika uzame mitini.../
Au uombe msaada..wakati unakufa na fasheni mwilini.../
Mwafrika..una mzigo mkubwa wa madeni.../
Hauna mali ..ardhi yako ni 'future ya wageni.../
Unalala ndani...kungoja hisani ya wenye nguvu.../
Nyumba iko wazi..wewe uko ibadani unaabudu.../
Ujasili ni kujimudu...mwafrika haujui hili.../
Umejaliwa nguvu...na unashindwa kuzihimili.../
Unavamia diplomasia..unatunga hotuba.../
Na hakuna mwenye hisia...kuwa upo nyuma ya muda.../
Ah..
unapoteza stadi za maisha.../
Kwa elimu ya magharibi...ikuweke ofisini suti kubwa..
ukumbatie dawati la nyazifa.../
Huku unauwa..nguvu kazi ya taifa.../
Umepitiliza nyumbani...hauna vituo.../
Umekuwa mtumwa wa sera zao,kiasi kwamba hauna 'future..
hauna dira,hauna lugha hauna nguo.../
Milango ya fahamu..imefungwa na ufunguo.../
Umepewa karatasi...ukaita jina pesa.../
Ukasubiri ikuletee furaha..ikakutesa.../
ukauza umoja...ukauza amani ukauza utu.../
Ukawashusha mashujaa wako..ukamwinua Yesu wa kizungu.../
Una kucha ndefu ..kushika chungu matusi.../
Hauwezi kuandika history..haumudu herufi.../
Ume-bleech nywele,mdomo mwekundu umebusu baruti.../
Nikuite nani...mwafrika mzungu au mzungu mweusi.../
Ah..
Unadanganywa...rangi yako sio nzuri.../
Ili utafute pesa...ukawaungishe vipuri.../
Ume-switch kutoka Mama Afrika...mpaka drama Queen.../
Una nunua TV...uone Afrika ikizama chini...!/
Mwafrika..umeshakosa mipango.../
Unajua kuchonga ngenga..badala ya kuchonga vinyago.../
Unaacha wanyama Mikumi,Serengeti unasafiri.. unaenda kushangaa ghorofa Chicago.../
Unarudi..unajikuta Mmarekani eti real nigga...!/
Mbona haulili bili nigga...?/
Jasiri..haiachi asili real nigga.../
Kamwe usijiite G nigga.../
Hauwezi kuwa warrior../
Unajua majina ya wasanii..kishinda historia.../
Unasahu mapishi..hauendi jikoni.../
Unakufa na ngoma mwilini...cheni shingoni.../
Kwa heshima na taadhima...unautunza Msaafu.../
Unatupa kitenge..kisha unafunga hijabu.../
Na ubaya ni kwamba...bado haujajua sababu.../
Unapewa Zaburi..utafakari mwenyewe wakichukua dhahabu.../
Ufeli majibu...uishie kubuni.../
Ushindane nani msafi...aende mbinguni.../
Mhanga wewe...rudi uzipitie kanuni.../
Umeshikishwa kitabu...wenzio wakushikie uchumi.../
Mwafrika...hii haikuingii nikichana.../
Unanuka sana...kiasi hauvutii kama Jana.../
Kiburi moyoni..haisikii unapokanywa.../
Unatia aibu..kiukweli sijivunii kuwa mwana.../
na bado unaamini..shahada ya shule ni zana.../
Haujui...ukitaka ule ni shamba.../
Unafunga ubongo...unafungua mikono ili wakupe msaada.../
umesahau kuwa...vya bure gharama.../
Mchezo wako...sheria zao utashindwa.../
Ukiishi porini..kama haiwindi..utawindwa.../
Inasikitisha..wenzako wanaigiza ili waishi...ila we unaishi kwa kuigiza sio...?/
umekuwa dekio..umekubali kuwa soko la pombe
na sigara.../
Soko la risasi bunduki na mabomu...
Soko la madawa ya kulevya..yanauwa waafrika wenzio.../
Soko LA dini zao..soko la picha za uchi .../
Soko la vitukukuziba sauti.../
Soko la sera unevu..na mifumo gombanishi...
Magonjwa batiri..unanunua dawa kwa kuhisi sio...?/
Umezagaa visingizio.../
Haujui akiba..ndio maana unashangaa salio.../
Umegeuzwa kifaa cha majaribio.../
imeandikwa..asiyeandaa silaha ataandaa mapambio.../
Mwafrika...
Nakupa nahau kalili.../
Afrika inakufa..mwafrika unadharau dalili.../
Unasahau wito..unafata mkumbo kwa dau batili.../
Unakumbuka kila kitu..na unasahau asili.../