Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
mziki wa bongo sio kujua tu, inabidi uwe na connection na kina fella,majani,clouds nk.Kama una amini una kitu kizuri kwann uogope, ingia uwanjani tukubonde utoke manundu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mziki wa bongo sio kujua tu, inabidi uwe na connection na kina fella,majani,clouds nk.Kama una amini una kitu kizuri kwann uogope, ingia uwanjani tukubonde utoke manundu.
Yote tisa, lets agree hapa, (na hapa ukibisha utakuwa mbishi)Nioneshe verse gani hapa imekosa vina
Dizasta Vina
Hatia iii Lyrics
Ah...
Nakusalimu mwafrika...nakusalimu habari gani.../
Nikaribishe tuketi...niseme yaliyo ndani.../
Sahau kuhusu hadithi za kale...za upendo wako.../
Nataka leo tukae...tuijadili kesho yako.../
Kutoka kupiga ramli...na kutii mizimu.../
Umeanza kufata amri...za TV na simu.../
Na ubaya ni kwamba...umeanza kuikacha sanaa.../
Na kufata siasa...ambayo inakulaza na njaa.../
Na kila unachokiona...unataka kubeba.../
Vichache vimekushinda...na unapanga kuongeza.../
Juzuu,Katekisimu mpaka Novena.../
Sio zako...zako zilikuwa ni kutamba ngojera.../
Umezubaa...majirani wameanza kufika kwako.../
Na unaamini kuwa...watakubebea shida zako.../
Kwa sababu ya ujinga,umezidi umasikini.../
Unamjengea jirani...kwako unachimba unabaki chini.../
Zamani...ulikuwa una sembe ya kusaza.../
Uliabudu kazi...ukaliweka jembe kwenye shamba.../
Ghafla ukauza panga...ukapamba jembe kwenye kabati.../
Ukanunua kioo ujirembe...ili uende na wakati.../
Ume...chagua urembo na umetupa werevu.../
Umeuza mifugo...unafuga kucha na ndevu.../
Familia iwe...mwafrika uzame mitini.../
Au uombe msaada..wakati unakufa na fasheni mwilini.../
Mwafrika..una mzigo mkubwa wa madeni.../
Hauna mali ..ardhi yako ni 'future ya wageni.../
Unalala ndani...kungoja hisani ya wenye nguvu.../
Nyumba iko wazi..wewe uko ibadani unaabudu.../
Ujasili ni kujimudu...mwafrika haujui hili.../
Umejaliwa nguvu...na unashindwa kuzihimili.../
Unavamia diplomasia..unatunga hotuba.../
Na hakuna mwenye hisia...kuwa upo nyuma ya muda.../
Ah..
unapoteza stadi za maisha.../
Kwa elimu ya magharibi...ikuweke ofisini suti kubwa..
ukumbatie dawati la nyazifa.../
Huku unauwa..nguvu kazi ya taifa.../
Umepitiliza nyumbani...hauna vituo.../
Umekuwa mtumwa wa sera zao,kiasi kwamba hauna 'future..
hauna dira,hauna lugha hauna nguo.../
Milango ya fahamu..imefungwa na ufunguo.../
Umepewa karatasi...ukaita jina pesa.../
Ukasubiri ikuletee furaha..ikakutesa.../
ukauza umoja...ukauza amani ukauza utu.../
Ukawashusha mashujaa wako..ukamwinua Yesu wa kizungu.../
Una kucha ndefu ..kushika chungu matusi.../
Hauwezi kuandika history..haumudu herufi.../
Ume-bleech nywele,mdomo mwekundu umebusu baruti.../
Nikuite nani...mwafrika mzungu au mzungu mweusi.../
Ah..
Unadanganywa...rangi yako sio nzuri.../
Ili utafute pesa...ukawaungishe vipuri.../
Ume-switch kutoka Mama Afrika...mpaka drama Queen.../
Una nunua TV...uone Afrika ikizama chini...!/
Mwafrika..umeshakosa mipango.../
Unajua kuchonga ngenga..badala ya kuchonga vinyago.../
Unaacha wanyama Mikumi,Serengeti unasafiri.. unaenda kushangaa ghorofa Chicago.../
Unarudi..unajikuta Mmarekani eti real nigga...!/
Mbona haulili bili nigga...?/
Jasiri..haiachi asili real nigga.../
Kamwe usijiite G nigga.../
Hauwezi kuwa warrior../
Unajua majina ya wasanii..kishinda historia.../
Unasahu mapishi..hauendi jikoni.../
Unakufa na ngoma mwilini...cheni shingoni.../
Kwa heshima na taadhima...unautunza Msaafu.../
Unatupa kitenge..kisha unafunga hijabu.../
Na ubaya ni kwamba...bado haujajua sababu.../
Unapewa Zaburi..utafakari mwenyewe wakichukua dhahabu.../
Ufeli majibu...uishie kubuni.../
Ushindane nani msafi...aende mbinguni.../
Mhanga wewe...rudi uzipitie kanuni.../
Umeshikishwa kitabu...wenzio wakushikie uchumi.../
Mwafrika...hii haikuingii nikichana.../
Unanuka sana...kiasi hauvutii kama Jana.../
Kiburi moyoni..haisikii unapokanywa.../
Unatia aibu..kiukweli sijivunii kuwa mwana.../
na bado unaamini..shahada ya shule ni zana.../
Haujui...ukitaka ule ni shamba.../
Unafunga ubongo...unafungua mikono ili wakupe msaada.../
umesahau kuwa...vya bure gharama.../
Mchezo wako...sheria zao utashindwa.../
Ukiishi porini..kama haiwindi..utawindwa.../
Inasikitisha..wenzako wanaigiza ili waishi...ila we unaishi kwa kuigiza sio...?/
umekuwa dekio..umekubali kuwa soko la pombe
na sigara.../
Soko la risasi bunduki na mabomu...
Soko la madawa ya kulevya..yanauwa waafrika wenzio.../
Soko LA dini zao..soko la picha za uchi .../
Soko la vitukukuziba sauti.../
Soko la sera unevu..na mifumo gombanishi...
Magonjwa batiri..unanunua dawa kwa kuhisi sio...?/
Umezagaa visingizio.../
Haujui akiba..ndio maana unashangaa salio.../
Umegeuzwa kifaa cha majaribio.../
imeandikwa..asiyeandaa silaha ataandaa mapambio.../
Mwafrika...
Nakupa nahau kalili.../
Afrika inakufa..mwafrika unadharau dalili.../
Unasahau wito..unafata mkumbo kwa dau batili.../
Unakumbuka kila kitu..na unasahau asili.../
Sasa unarap kuhusu mapenzi unataka ujigambe kwa kipi?Options zipo zaidi ya hizo mbili..ila Unajua kabisa hatuwez kulinganisha storytelling na hizi zingine. lets compare apples with apples.
Afu Fid Q sio kwamba zote ni majigambo
Mfano Roho huwezi kusema ni Majigambo ila sio story per se.
Hapa umeamua tu kujikata kichwa.
Hata Dizasta kamsaisia Rapcha kutrendYote tisa, lets agree hapa, (na hapa ukibisha utakuwa mbishi)
Ni kweli rapcha kamfanya dizasta atrend
Saivi Tribulation ina views 24k kwa masaa 5...Dizasta hajawahi kuwa na hiyo traffic
Ngoma kama kiberiti,Mafanikio,Ulimi mbili,sihitaji marafiki,ielewe mitaa,propaganda...nk. nk. zote sio majigambo.Sasa unarap kuhusu mapenzi unataka ujigambe kwa kipi?
Unashindwa hata kuzingatia muktadha?
Mimi nazungumzia aina ya rap yake jinsi ilivyo yani role yake, sijasema kila ngoma au hana ngoma ambayo ka rap nje ya hapo
Kuanzia Augost 13, Hip Hop, I'm professional kuja chini huko asilimia 85 ka rap majigambo
Na usini quote vibaya ukafananisha majigambo yake na hawa rappers wanaosifia mademu na pesa
Majigambo ya Fid Q yapo kwenye category ya MC, nadhani unaelewa utofauti kati ya Mc na rapper japo wote kwenge ku delivery wana rap
Tusisahau rapcha ana hitsong lisa.Hata Dizasta kamsaisia Rapcha kutrend
Unafikiri kabla ya hizi diss huyo Rapcha alikuwa anafikisha hizi numbers kwa muda mfupi kama anavyopata kwenye hizi diss?
Majigambo ni kujiongelea wewe mwenyewe kwa kujikweza zaidiNgoma kama kiberiti,Mafanikio,Ulimi mbili,sihitaji marafiki,ielewe mitaa,propaganda...nk. nk. zote sio majigambo.
au unamaanisha nini unaposema majigambo? Naona kama majigambo ni box dogo sana unalotaka kumuweka fid.
Anyway...hayo 'majigambo' ya fidq ni level moja na Dizasta?
Unamjua vizuri kado au unaropoka [emoji16][emoji16]Huyo Dizasta ata Cado Kitengo haingii
Acha uongo we baba fid Q dot com Ni ya mwaka gani?????Fid Q dot Com huyo ndio alikua Fid,
We huna lolote hata mi nakukalisha kama unajiamini anzisha Uzi ukinishinda nakupa 50kHahaha mi bongo hakuna wa kunichana labda mmkodi Eminem na J.cole
Wewe sema tu ulimchokea hapoMajigambo ni kujiongelea wewe mwenyewe kwa kujikweza zaidi
Kwenye Rap ipo ya namna mbili
Moja kujikweza kwenye mambo yako yanayokuhusu wewe binafsi mambo ambayo hayaigusi bila jamii (hii inafanywa na marapa)
Mbili kujikweza kwenye mambo ambayo yanamgusa kila mtu ndani ya jamii (hii inafanywa na ma MC)
No sina maana ya kumuweka kwenye eneo dogo Fid Q ila ni pale napojaribu kuonesha utofauti kati yake na Dizasta.
Fid Q pia kwenye kuizungumzia jamii pia ni kitu ambachi anakifanya kwenye kila wimbo ila namna anayotumia ku delivery ni mfumo flani hivi wa majigambo
Swala la level nimelikataa kuliongelea hata kwenye post yako ya juu
Ni kwamba hata ungesema Profesa Jay na Fid Q nani mkali bado nisingetoa jibu
Ila ukiniambia nifanye comparison ya kuangalia katika miaka hii nani katoa nyimbo kali naweza kusema flani katoa kali
Na ndio maana nimekuambia Fid Q wa mwisho ni yule kwenye Sumu
Rapcha ana hit song ya Lisa kwanini hana hit song ya nyimbo zingineTusisahau rapcha ana hitsong lisa.
Unazijua numbers za lisa?
Tusimung'unye mung'unye maneno, Rapcha yupo mainstream na anamsaidia kumleta Dizasta mainstream kupitia hizi diss.
Dizasta aspopita na huu upepo ndo bas tena.
Anatakiwa azichange sana karata zake hapa aende mainstream, ila kwa hizi pigo za ngoma ya dakk 11 ndo anafel
nakuhurumia kafifte kako usije laza familia njaa siku 3We huna lolote hata mi nakukalisha kama unajiamini anzisha Uzi ukinishinda nakupa 50k
kitu gan hiko?Yap inaweza ikawa ni hoja kwasababu pengine nilichokuwa nakikubali kutoka kwake sikuwahi kukiona kwenye track zake mpya
Yes kitambo hicho baba Fid hataki mchezo na jukwaa, ana hasira na Jukwaa balaa kabla hajatoa I am Professional,Hapo n kabla hata hajatoa mwanza mwanza miaka Kama minne mbele
Hahhahahah maneno ya nn anzisha Uzi lengo sio hiyo 50k uthibitishe we n mkali hata Simba ya Yanga hutumia mabilioni kushinda NBC tittle yenye hela kiduchu ya kumsajili tu Aziz Ki au Chama... Njo tubato utuoneshe unayoyasemanakuhurumia kafifte kako usije laza familia njaa siku 3