najiskia uchovu na mihayo napiga, uliza hizi nyayo na nyika/
nimetoka mbali fanya maamuzi tuhitimishe kikao, maana hata mimi nina mishe kibao.../
mishe hata wewe unazo mishe unazo badili, fafanua eleza na uweke mifano isawili.../
huo ubishi wa kujikweza weka kando ukatiii, leo ndio mwisho vina navunja ndoa yako batili.../
andika talaka ili tuondoke, maana maamuzi ni yako au chukua panga unichome.../
haukuitendea haki kura yako, kuchagua ndoa wakati sio jambo kubwa kwako.../
utakapochukua wasaa utagundua ulimpa saa alipohitaji muda wako.../
anajua kua mkoa wa mbali una watoto, anajua kuhusu vikao na safari za uongo.../
anajua kuhusu kondomu ulizobana kwenye nguo, na meseji za wasichana wachuo.../
ulimkuta mwema ukamteka kiakili, ukamshawishi mpaka akakupa shehena ya mwili.../
akakupa moyo akihisi utaweka nadhiri, ukajisahau na ukamuonesha asili...ya kwamba we ni mchafu tu/
kipi unaropoka lakini, ubaya ulipwa wa ubaya unachokonda ni nini.../
mmoja ametupa mwingine ameokota yamkini, aliyetupa ni wewe na niliyeokota ni mimi.../
aah ilikua ni sababu ya msongo wa mawazo, na ndio maana uliona wife sio wamoto kama mwanzo.../
aliteseka kiasi akahisi ndoa ni sumu, na nikaamua kuchukua maamuzi magumu...dongo kwako/
nilimuokoa nikamvusha bahari, maana muungwana vitendo maneno hayata angusha jabali.../
siku mwili hautagusa sayari, utamkumbuka na pengine utajifunza kujali.../
mpunga umeyumba umeanza kujishuku mzee, umerudi nyumbani baada ya kushindwa kumudu starehe.../
haukuwepo kwenye shida ilipofuzu tarehe, ulikimbia na nilikuwepo mimi pekee.../
ngoja nikuudhi unajua mwanao ananiita daddy, nampeleka shule namrudisha nyumbani baada ya kazi.../
nalipa ada, ada usizokumbuka kutoa,, mwanao amefikia balehe nimemfunza kunyoa.../
nimemfunza ushairi nimemfunza kufanya mahesabu, nimemfunza kufunga tai kisha kamba za viatu.../
nimemfuza sheria zinazoongelewa bungeni, na nilienda kumtetea alipoonewa shuleni.../
una hoja yeyote defensively, maana hujui ka wanalala ama wanaamka safely.../
hujui kuhusu family dinner women day birthday zao hujui hata anniversary.../
Hujui kuhusu maumivu aliyopata moyoni, hujui harufu ya chakula alichopasha jikoni.../
hujui kuhusu depression, maana mara mbili nimemkuta amejifunga kamba shingoni.../
Credits: dizasta vina _ kikaoni