HipHop Fans: Ni underground rapper yupi ambaye anafanya vizuri kuliko baadhi ya mainstreams rappers?

Mwezi wa saba tarehe 5 dizasta vina anaachia ngoma stay tuned
 
nishavunja mwamba kaskazini, tanzania hakuna mroma mwenye stamina ya ku-rap na mimi.../

mizuka hewani utadhani anaye-rap ni jini, nusu mtu nusu rap machine.../

najua ushasikia utenzi bro ebwana huu utenzi noma, ita wanafunzi waje waperuzi ngoma.../

we don't play good ukija tuna-execute, ujuzi kama sherry woods naandika zaidi ya daily news soma.../

panda safina imefunguliwa mito, na kingo ni mbovu ukioga tu umechungulia kifo.../

sikudanganyi hamna hewa huku nilipo.../
dizasta vina nobody is safe 3
 
wenzio wameacha mtindo wa kunichukulia simple, sikudanganyi hamna hewa huku nilipo.../
 
Dizasta vina.......Nafika kilele ila sipigi kelele kama nyinyi. Tutawataja wengi ila ni kuanzia wa pili kushuka chini, wa kwanza ndo huyu
 
Harmonize na Marioo wanafanya vizuri
 
code zinafanya wazungu wanazunguka, mafungu yana funguka.../

mazuzu wana zuzuka, nilikua mtupu nikaokota buku nikabukuka.../

leo nasimulia tungo tukufu ni ka' lufufu kafufuka.../

legend kama koffi olomide, naikamata dar kama daudio wa kolomije.../

nawalaza dolo si-follow bata na-follow mishe, na ufundi ni-control verse utasema apollo mishe.../
 
misele hapa mjini, natembea na begi la maiti nachinja bila kwele wala nini.../

busara tele utasema nyerere kama mwinyi, nafika kilele ila sipigi kelele kama nyinyi.../

fuvu limeshiba mautundu kwenye kichwa, niko underground na huku ndiko mitutu inakofichwa.../
 
huwa nashangaa kwa nini Niki Mbishi bado ni underground mpaka sasa. halafu wajinga wajinga tu wanapata airtime.
Sikiliza mistari ya Yote Sawa ndo ujue kama Niki ni giniaz.

Ndo maana niliacha kuchana mapema,nahisi ningepoteza muda tu
 
Diego naladona
 
Dizasta vina hatia iv

Ah sikuwa na hali ya kuikosha roho yake, nilimuacha aende aufuate moyo wake.../

Alipata bwana wa kizungu magharibi, alimuahidi kuishi maisha ya ndoto zake.../

Nilipata uchungu niliishia kuhamaki nilitaka nijiue, nilitaka nimzuie abaki nikakumbuka ukioenda ua haulikati unaliacha likue.../

Duka langu nilifunga biashara niliacha zote, uchumi uliyumba kwa maana nilianza pombe.../

Niliumwa bado kidogo moyo uzime, nilimfanya ndoto yangu kumbe naye ana ndoto nyingine.../

Alisema anakwenda jiji la miami, hakuna alichowaza zaidi ya kuishi kifahari.../

Kamtumia picha na mchizi kazikubali, na yupo tayari kumipia gharama za safari.../

Aliondoka na kipande kimoja cha mwili, nilikonda nilipata ugonjwa wa akili.../

Haikuwahi kupita hata sekunde nisilie, nilitamani mpaka ardhi ipasuke niingie.../
 
Muda ukaenda nikapata mwanamwali, nikamuomba awe mwenza wa maisha akakubali.../

Nikamvisha pete nikalipa mahari, sikumpenda lakni nilijifunza kumjali.../

Aliuliza kama nampenda nilimjibu, sikutaka kuweka moyo wake maumivu.../

Sikutaka kuuweka mtima wake solemba, kiasi aseme hatakuja kupenda forever.../

Ah alinikunbatia nikamfunga kwa ishara, akanikabidhi tunda nikala.../

Akaniamini tukajuana nikapanga kumwoa, akaidhinisha na tukaanza na mipango ya ndoa.../
 
Wakati karne ya 21 inaingia, john alikua miongini mwa vijana waliokuwa fascinated na ukuaji wa teknolojia ya mitandao ya kijamii.

Alijiunga na dunia hii mpya, mara kadhaa alikaa kwenye ubaraza akiangaza simu yake.

Akipapasa kila kitufe ndipo siku moja akapata ujumbe kutoka kwa jane



"Habari naamini u buheri wa afya, unaendeleaje na huyo mpenzi wa sasa.../

Nashukuru nahema ughaibuni sio kwema nakiona cha mtema mpaka naona ni heri nikafa.../

Naisha uliyowaza yote ni uongo, nauzishwa madawa nalazimishwa ngono.../

Nafungiwa ndani kama mtumwa ufungwani roho yangu rehani kiasi naitamani bongo.../

Ukubwa umekuja umenisafisha jicho, ndoto imeisha na taswia imenionesha sivyo.../

Ah naomba unifate uniondoshe kwenye hichi kifo, na hii namba ya msamaria atakueleza nilipo.../"

Sherehe ilikua na mipango madhubuti, kabla mimi kuichukua michango ya harusi.../

Nikatoroka ughaibuni kufwata hisia zangu, kwenda kumfuata njiwa mahususi.../

Nilivuka majangwa na majabali, sehemu ya safari anga sehemu nyingine bahari.../

Niliacha kila kitu nyuma upendo na huruma vilinijaa, penzi likanipeleka mbali.../
 
Nikakutana na bopa la kizungu, lenye sura ya kuichachisha mboga kwenye chungu.../

Kiko kwenye mdomo, tatuu kila kona wapambe na vishoka wenye mtutu.../

Sio siri alizungukwa na wasichana wengi, sikujua umri walikua wadogo ka' madenti.../

Baadhi walikua uchi wanamhesabia chenchi, wengine masaji huku wengine wanamchezea nyeti.../
 
Scars kila ngoma niliyoilike naenda kuidownload

Isipokuwa hiyo baunsa ya Dizasta Vina hiyo ninayo Shaolin aliua sana mle

Nakukubali mwamba
 
toxic fuvu alishampiga cado kitengo wa matitu tatu bila kwenye freestyle ya kumuimbia demu huyu dogo ni sumu kweli kwenye freestyle.
Toxic ni balaa hata kwenye tracks zake alizowashirikisha mainstreams amewatoa kijasho kwa kuchora mistari

Muulize Stamina
 
Vipi dubo jesusson ameishia wapi?
 
Huyo simjui
Nilijua utakuwa unamjua Mzee ..[emoji28] Mbona huyo mwanae Sana dizastavina na nafikiri kipindi cha nyuma waliunda crew Yao inaitwa panorama...Ila Kwasahv naona atakuwa ametulia kidogo na maswala ya mziki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…