Hisia za jamii kuelekea 7/7: Je maandamano yapo au hayapo?

Hisia za jamii kuelekea 7/7: Je maandamano yapo au hayapo?

Je maandamano ya 77 yatakuwepo?

  • A. Ndio

    Votes: 64 50.0%
  • B. Hapana

    Votes: 33 25.8%
  • C. Sijui

    Votes: 31 24.2%

  • Total voters
    128
  • Poll closed .
Mkuu kwa generation yetu hii uoga umetutawala sana.

Ila hiki kizazi kinachokuja neno uoga litakosa nafasi kabisa na huo ndiyo utakuwa muda wa watanzania kujikomboa
Hiki kizazi kimegoma kuuziwa bidhaa inayoitwa hofu/uoga
 
Sidhani kama matokeo ya hapa yanaweza kukupa uhalisia wa mitaa.

Nachojua kama kuna watu walikuwa sehemu ya maandamano ya october 29 kutoka humu hawazidi 50.

Sema ninachofurahia serikali ina watu wa hovyo kweli.Just imagine nguvu wanayotumia kujaribu kuzuia maandamano ambayo hayana kiongozi na dhima ya kuandamana zaidi tu ya kila mtu kusikia kwenye mitandao
Kabisa, inatia shaka sana. Sisi huku tunapiga doria na kuwaambia. Sema zinamanufaa zaidi ya mjuavyo.
 
Hakuna maandamano, huku mtaani wananchi hawataki hata kuyasikia, Tanzania hatujazoea hayo mambo na msitupeleke huko, nyanya moja iliuzwa shilingi elfu 2, petrol lita moja iliuzwa elfu 20, hakuna kutoka nje ni ndani tu, bado walioibiwa na kupoteza ndugu zao, HAKUNA MAANDAMANO, period!
Kiongozi huu ni ubinafsi na hakuna sehemu utatupeleka.Nyanya itafika hiyo bei na mafuta yanaweza kuzidi hiyo bei ikiwa mtaendelea na mitazamo hii(Hivi mababu zetu(kwa nchi zilizopigania uhuru achana hii ya kupewa kwa hisani) wangesema tuache mkoloni afanye yake leo hii wewe si ungekuwa unaamushwa na kiboko ukalime kahawa au katani kwenye mashamba yao)

Hakuna anayependa maandamano au vurugu lakini watawala wakiwa na mioyo migumu unategemea nini(Ungekuwa mtoto wa Tundulissu au ndugu yake Pole pole au Mdude,kutaja wachache ungeyasema haya).

Maisha yetu ni magumu hata kama leo kwako ni mazuri nakuhakikishia kesho yatakuwa mabaya zaidi(Watu walishakufa siku nyingi wamebaki miili tu inatembea siku si nyingi utaona maiti zao).

Kuna sababu gani ya kuishi maisha marefu yasiyo na malengo(Kwamba utwambie uliishi miaka mia mbili lakini hakuna kitu ulikamilisha hapa duniani,inakusaidia nini?)

Kataa dhuluma,pigania haki hata ukaishi masaa mawili you will be crowned in your next life.

Asante na jumapili njema
 
Mimi nawa appreciate wana harakati akina Kimambi na Sarungi jinsi wanavyoipelekesha na kuitesa serikali yetu kisaikolojia!
Hakuna Mwizi anayekupa taarifa kuwa tarehe fulani saa fulani atakuja kukuibia.
Maandano hayapo.
 
Sioni kama kuna maandamano, ila tayar watu washaanza kuchukua taadhari, matokeo yake ni kwamba siku ya jumanne, wafanya biashara wataathirika, kule sabasaba maonyesho napo idadi ya watu inaweza kupungua, kwahiyo hii fever ya maandamo ambayo kimsingi hayapo yata athiri watu kiuchumi zaidi siku ya jumanne
 
Jibu la moja Kwa Moja halipo.
Watu wengi wanatamani yawepo lakini wanasubiri nani wa kuyaanzisha, kwa sasa Tanzania ni kama petrol imemwagwa chini nch nzima, tunasubiri tu kibiriti ambacho ccm na vyombo vya ulinzi wanakilinda mtu asikichukue,.
Hapa namaanisha ikitokea watu Wachache wakatoka, basi baada ya muda mfupi watu wengi watajaa kwenye maandamano hayo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa serikali ya ccm.
 
Jibu la moja Kwa Moja halipo.
Watu wengi wanatamani yawepo lakini wanasubiri nani wa kuyaanzisha, kwa sasa Tanzania ni kama petrol imemwagwa chini nch nzima, tunasubiri tu kibiriti ambacho ccm na vyombo vya ulinzi wanakilinda mtu asikichukue,.
Hapa namaanisha ikitokea watu Wachache wakatoka, basi baada ya muda mfupi watu wengi watajaa kwenye maandamano hayo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa serikali ya ccm.
Hapa namaanisha ikitokea watu Wachache wakatoka, basi baada ya muda mfupi watu wengi watajaa kwenye maandamano hayo, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa serikali ya ccm💪🏿🔥
 
Back
Top Bottom