Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

Historia fupi ya maisha ya Spika Ndugai aliyoitoa bungeni. Asema alikuwa na maisha ya shida na dhiki

Job alitoka mbali sana spika wetu alipambana kuitafuta elimu kwa nguvu yake yote huku maisha yakiwa magumu ,mbowe pamoja na kuwa na kila kitu nyumbani ila elimu ilimshinda akapata zero ,biashara zimemshinda na siasa pia .

He is professional failure
Bora mbowe biashara zimemshinda kuliko magufuli ambaye hana hata genge la nyanya.
 
Bora mbowe biashara zimemshinda kuliko magufuli ambaye hana hata genge la nyanya.
Hahahaa... aiseee nimecheka sana.

Lakini hawa wanasiasa wengi wao nje ya siasa hawawezi kitu.

Ndio maana wamegeuka kuwa kupe wa madaraka. Wanajijua vizuri kwamba waking'oka hapo ndio kwisha habari yao!
 
Leo Job Ndugai spika wa bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania, anetoa ya moyoni na kuwaaga wabunge akiashiria kumalizika kwa bunge katika kipindi chake cha uongozi.

Kati ya mambo aliyoyaeleza ni:
1. Historia fupi ya maisha yake;
-alipozaliwa
-shule ya msingi aliyosoma
-hali halisi ya mazingira aliyokulia
-maisha yake ya chuo kwa ufupi nk

2. Mafanikio yake kwa kupewa sapoti na raisi

3. Familia yake na hali yake ya kiafya aliyopitia.

4. Mwisho akawaaga wabunge wenzake.

Ninakutakia mema huko uendako na ukavune sawa na kazi ya mikono, ulimi na matendo yako
AMEN



Sent using Jamii Forums mobile app
Bunge la ovyoo kuwahi kutokea ktk historia ya nchi hii
 
Huyu wana angefanya tu aliyoyafanya maana kategeshewa vbya mno kwenye matibabu na uspika enyewe asingeruka ule mtego.jpm mjanja sna
 
Viol,
Maskini wengi wana hasira!
Ndio maana Mwl Nyerere alijenga vyuo vya uongozi kama Kigamboni, Maiwa, n.k ili kuondoa ushamba vichwani mwa viongozi!!

Akawapeleka JKT ili kuwachanganya wawe na umoja, wajifunze kupendana!!
Waliopitia Cadet School za kijeshi ni kosa kubwa kumzalilisha ofisa mwenzako hata awe mdogo mbele ya askari!!
Kidipromasia watu wanaheshimiana, tajiri na maskini, imani tofauti, misingi tofauti, rangi kabila na jinsia tofauti!!

Huyu spika kwanza kampiga mpinzani gongo kazimia, huo sio ustaarabu, hiyo tuu inamdisquarify kuwa kiongozi hafai.
Angekuwa na pisto angeshoot.

Mentaly not fit to be a leader.

Hilo ni galasa, bahati mbaya wako wengi wanafurahia ujinga wanashangilia!!

Watanzania tusikubali kupelekwa huko, tueshimiane tusimame pamoja, tujenge nchi yetu tusiibomoe kwa ujinga huu!!
Tudumishe amani yetu, tupendane hata kama tunatofautiana kifikra kisisa na kidini!!

Mwl Nyerere alitufundisha upendo, sisi sote ni Ndg na Tanzania ni wamoja!!
 
Japo ndani ya masaa 24 yajayo mh Job Ndugai atakuwa siyo Spika tena lakini ametuaga akiwa ametutegulia kitendawili.

Tuliosoma zamani tunajua namna watoto wa maskini walivyojihisi unyonge mbele ya watoto wa maofisa wa serikali achilia mbali wafanyabiashara.

Kama Ndugai hadi anaingia Chuo alikuwa bado ni maskini basi yawezekana wakati akiwa sekondari hali yake ilikuwa mbaya zaidi.
Fikiria wakati huo ndio yuko shule moja na mtoto wa mmiliki wa Mbowe Hotels iliyopo jijini Dsm lazima alijisikia unyonge mara dufu.

Na yeye Freeman watoto wa matajiri hata wakifaulu walisoma shule za private Shaban Roberts Dsm au The Highlands kule Iringa siyo kwenda kujimwambafy kwenye shule za watoto wa wakulima.

Waswahili walisema aliye juu mngoje chini ndio hiyo sasa rungu la Job limesambaratisha Ufipa yote, kisa bifu za sekondari.

Nawatakia wabunge wote vunja jungu njema usiku wa leo.

Maendeleo hayana vyama!
Sioni hoja ya maana hapa..hii ni Afrika yenye mchanganyiko wa watu wenye hali nzuri wachache na wengi masikini?sasa maneno ya Ndugai kuibuka nayo jf si ni sawa na kukosa kazi tu
 
Back
Top Bottom