Historia kuhusu asili, tamaduni na aina za Wachaga

Historia kuhusu asili, tamaduni na aina za Wachaga

Uchaga siyo Kabila, bali ni makundi mbalimbali yaliounganishwa na Muzungu na kuitwa Wachaga, kabla ya kuja Muzungu hao wengi wanaojiita Wachaga leo hii hawakujiita hivyo!
 
Pata historia ya WACHAGA

Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.

Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000 hata hivyo Wachagga wote duniani wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 2.5 ambapo wengi wao wanaishi nje ya mkoa Kilimanjaro kwenye miji mikubwa wakifanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa biashara.Kwa kasi hii ya ongezeko la watu huenda sasa wachagga wakafikia idadi ya 5.2milioni kati ya mwaka (2003-2016)Wachagga wako wengi zaidi katika miji ya Nairobi, Dar es salaam, Arusha, Mombasa Mwanza, Kampala na miji mingine yote Afrika nzima.Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu,Wa-Kilema, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.

Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katikaKirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.

Historia ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.

Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.

Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu. Hivyo hii imepelekea wachagga kuwa wengi katika nafasi mbalimbali serikalini na kwenye makampuni binafsi huku wengine wakiwa wamiliki wa biashara kubwa na kushikilia nafasi za juu kabisa za kumiliki mali ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe,viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.

Ndizi za Wachagga
Ingawa wachaga wa leo wanakula vyakula mbali mbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko,kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.

Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.
Kuna kitu kingine muhimu sana napenda niwaeleze hakika huwezi kukikuta sehemu nyingine wakati wa kuchinja wanyama; wanawake hawaruhusiwi kupita karibu na sehemu shughuli hii inapofanyika pia maini na nyama kama kidari nk. huliwa na wanaume haswa wazee kwenye eneo la machinjio. Pia wakati wa kugawana nyama mwanaume ambaye hajaoa ( hata kama anaishi na mwanamke) bila ndoa huyu anahesabika ni muhuni na hawezi kupewa fungu sababu ataenda kuchomea baa. Hahahaha
Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa “mchagga halisi, hali muhogo – akila muhogo atakufa”. Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.

Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la “kiti moto” ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji wa “kiti moto” haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa “ruksa”.

Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo:
Mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama.
MACHAME:Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena
OLD MOSHI & VUNJO:Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha.
ROMBO: Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba.
MARANGU & KILEMA: Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau.
KIBOSHO:Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkonyi.

Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao

Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.

Utawala wa jadi ya Wachagga
Watawala wa kichagga waliitwa “Mangi”. Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho – anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao.

Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa “u-Mangi-meza” inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa kichagga.

Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni “kihamba”. Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya wachaga mikoani mbali mbali.

Maoni juu ya Wachagga
Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja.
Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya.
Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi.
Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakula walichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.

I'm proud to be chagga come and join me!
Asante sana kwa kunipa historia ya ujombani. Ubarikiwe.
 
Wachaga sio wabantu na pia katika uchambuzi wa lugha (linguistically) hakuna lugha ya kichaga bali kimashami ( machame) ki uru nk....na lugha hizo sio lugha za kibantu kama watu wake wasivokuwa kiasili ni wabantu
 
Umesahau ndoto za wanawake wa kichaga ni kuolewa na wameru na waarusha.
 
Hapo unaweza kuwa na maana lkn siyo Kabila, huo ni upotoshaji, hakuna Kabila la Kichaga!

Hakuna namna ya kuligawa Taifa la Kichagga. Hili Taifa la Kichagga ni moja, lenye historia moja, tamaduni moja, lugha moja yenye lahaja kadhaa.

Taifa la Kichagga lina umoja kuliko Taifa la Tanzania
 
Wachaga sio wabantu na pia katika uchambuzi wa lugha (linguistically) hakuna lugha ya kichaga bali kimashami ( machame) ki uru nk....na lugha hizo sio lugha za kibantu kama watu wake wasivokuwa kiasili ni wabantu

Unafahamu maana ya "kibantu"?

Unaweza kunipa mfano wa uwepo au kutokuwepo ubantu?
 
Hakuna namna ya kuligawa Taifa la Kichagga. Hili Taifa la Kichagga ni moja, lenye historia moja, tamaduni moja, lugha moja yenye lahaja kadhaa.

Taifa la Kichagga lina umoja kuliko Taifa la Tanzania


Hakuna mwenye hiyo nia, nilitaka kumsahihisha tu mleta mada, kwamba hakuna Kabila la Kichaga Dunia hii, ila kama ukisema ni Taifa hapo unaweza kuwa na hoja lkn siyo Kabila.
 
Et mkuu samahani kwani butiama wote madish yameyumba
Hivi kwanini unapenda kunisumbua hivi?? Hapa si anazungumzia Spika sijui kamwita nani Sauzi Afrika huko kwa tuhuma ya kufanya mambo ya hovyohovyo.... Hako kajamaa eti kanafanya mambo ya hovyo kumzuia bosi wake asigegede michuchu ya ofisi... Kijamaa kina roho mbaya balaa wallah...

Siku nyingine uwe unaniita kwenye mambo muhimu yenye tija kwa taifa kama ya "kwanini Mirembe imejengwa Dodoma na wala sio Butihama"....
 
Ni nzuri, Ila hii sio historia bali ni uchambuzi/simulizi ya maisha ya wachaga. Cultural, social and economic description of the chaga people.
 
Wachaga sio wabantu na pia katika uchambuzi wa lugha (linguistically) hakuna lugha ya kichaga bali kimashami ( machame) ki uru nk....na lugha hizo sio lugha za kibantu kama watu wake wasivokuwa kiasili ni wabantu
mh
 
WACHAGGA
Je unajua kuwa wachagga ni wayahudi?
Kabila la Wachagga linalopatikana Kaskazini mwa Tanzania, asili yao ni Wayahudi wa Ethiopia wanaoitwa Falasha – kutoka Mkoa wa Amhara kwenye kati ya vilima vya kati huko Ethiopia.

Je ni nani hawa falasha
Falasha ni jamii ya kiyahudi ya kundi la Solomonic ambapo Malkia wa Ethiopia alifika Israeli na akazaa mfalme Sulemain na watoto wa, au kizazi kilichotokana na uzao wa Solomon na malkia huyu ndio wanaoitwa Falasha.

Mnamo mwaka 150 kabla ya Kristo kulitokea vita ambayo ilifanya falasha kutawanyika, kisa cha vita hiyo ulikuwa ni wivu tu wa kabila la amhara na tigrey kwa kuona kama falasha wanataka kuwatawala au wameongezeka sana na pia wakaona kama hao falasha wana akili nyingi sana,hivyo wakawafukuza kutoka eneo hilo la Amhara na Tigrey, wengine wakaenda Kaskazini na wengine wakateremka Kusini, walipokuwa wanawafukuza wakawa wanasema chaggy yaani wameteremka kwa lugha ya kitigrey.

Walioteremka wakaweka makazi yao kwenye eneo la waoromo karibu na mpaka wa Kenya, ambapo walikaa takribani miaka 200 na wakawa wengi , na ikaonekana wanataka kuwazidi wenyeji kwa kila jambo, kukatokea tena chuki iliyofanya wazidi kuteremka chini mpaka eneo la Borana, wakaweka tena makazi yao hapo na kuchanganyika na wenyeji wao ambao ni Borana. Eneo la Borana walikaa zaidi miaka 100,chuki na wenyeji ikatokea tena, na hivyo kuwalazimisha kuzidi kuteremka zaidi hadi Ukambani nchini Kenya, hapo walikaa takribani miaka 200 na kuzaliana sana na wenyeji.

Mwaka wa 400 baada ya Kristo walifurushwa tena na wakamba ambapo safari hii walielekea magharibi ya Ukambani na kuwasili eneo ambalo leo hii linaitwa Kilimanjaro, ambapo waliwakuta wenyeji ambao ni watu wafupi wanaoitwa WAMBUTI AU MBILIKIMO. Wakawapiga na kujitwalia eneo lote la Kilimanjaro. Mbilikimo hawo walitoroka na kuelekea Magharibi ya Kilimanjaro kuelekea Kongo.

Kuanzia mwaka huo wa 400, baada ya Kristo Wachagga [Yaani Wayahudi wa Kilimanjaro] wamekuwepo hapo hadi leo.
MIFANO YA MANENO YA KICHAGGA NA KIEBRANIA YANAYOFANANA.
1. YAVE [Kichagga] Ni sawa na YAHWE kwa Kiebrania [ambapo ni jina la Mungu].

2. ELI: Hili pia ni jina la Mungu kwa Kichagga na Kiebrania pia
Majina ya Kichagga yenye neno ELI, Mwisho au Mwanzo wa jina yamekuwepo uchaggani hata kabla ya kuingia Ukristo hapa Kilimanjaro. Mfano: Wangaeli, Elinganya, Shafuraeli. Eliufoo, Elisaria, Apaeli.

TABIA ZA WACHAGGA
Wachagga ni watu werevu sana na wenye Akili nyingi sana
 Wachagga huwa hawapendi kupata usumbufu wanapotafuta maisha
 Wachagga ni watu wachapakazi kuliko kabila lolote lile hapa Africa.
 Wachagga ni watu makini sana na wanajua kutumia fursa yeyote iliyo mbele yao ambayo watu wengine wanaona sio fursa.
 Wachagga wanajua kutunza siri sana na wanajua kupeana habari yoyote ile inayo onekana kuhatarisha maisha yao bila mtu mwingine kujua wanapeana habari.
 Wachagga hawapendi kudhulumiwa au kuonewa [wapenda haki] kwa namna yoyote ile.
Mfano: Mnamo mwaka 1936 wachagga walichukizwa sana jinsi Serikali ilivyokuwa inaingilia Biashara yao ya Kahawa, wakapeana habari bila yeyote nje ya wachagga kujua, kuwa wabomoe Majengo yote yaliyokuwa yanatumika kukusanya Kahawa, Majengo yote yakabomolewa usiku mmoja, kuanzia Rombo hadi Siha, yalibomolewa kuanzia saa sita usiku hadi saa nne usiku huo, yote yakavunjwa.
Jaribu kufikiri wakati huo hakuna Barabara nzuri wala magari, wala simu, lakini waliweza kupeana taarifa juu ya jambo la kufanya, na waliweza kufanya.
 Wachagga siyo watu wanafiki hata kidogo.
 Wachagga wanajulikana kwa uadilifu wao, mchagga huwezi kumhonga ili apindishe Sheria Aslani, maana ni watu makini, na ndio maana wazungu wengi toka Ulaya wanataka kufanya kazi, na wachagga, wanakuwa wameshajulishwa na wenzao kuwa watu makini na waadilifu ni wachagga.
 Wachagga ndio watu wa kwanza Afrika kuanzisha Chama cha Ushirika.
 Wachagga ndio watu wa kwanza kudai Uhuru.
 Wachagga ndio watu wa kwanza kupandisha maji toka mtoni kwa njia ya mfereji kwa ajili ya umwagiliaji.
 Wachagga ndio Kabila la kwanza Afrika kuanzisha gazeti lao lililoitwa KOMKYA [Yaani kumekucha] liloanzishwa mwaka 1920.
 Wachagga ndio watu wa kwanza Afrika kuwa na Baraza lao lililoitwa Chagga Council
 Wachagga ndio watu ambao chakula chao cha Asili kimesambaa Nchi nzima [Mtori] na pia kinapikwa huko Ulaya kwa jina la Kilimanjaro Soup.

GAVANA EDWARD TWINNING NA RICHARD TURNBULL
Wakati gavana Edward Twinning alipokuwa anamkabidhi madaraka Richard Turnbull, alimpa wosia ufuatao.
Mara: ndio mkoa mgumu sana kuutawala [the most difficult region, rule]
MOSHI: ndio eneo lenye watu intellectual, na wanaosadikiwa kuwa ni falasha [wayahudi wa Ethiopia]
Majina ya Koo za Kichagga zinazofanana na za Kiebrania
Mushi, Lema, Kimario, Assey, Shirima, Rabo, Massawe, Lawi.

Dimitris Kimarios: Huyu alikuwa myahudi wa Ugiriki aliyefika Kilimanjaro mwaka wa 540 baada ya Kristo akitafuta wayahudi waliotokea Ethiopia na ndie mtu wa kwanza kuandika Neno, KILIMANJARO kwenye kumbukumbu za Kigiriki.
Ukiibariki Israeli na wewe utabarikiwa na Ukiilaani Israeli na wewe utalaaniwa Asema Bwana.
“Hivyo kumbe pia Ukiilaani Kilimanjaro na wewe Utalaaniwa na Ukiibariki Kilimanjaro na wewe utabarikiwa, hii ni mimi mwandishi nimesema”;

Hebu jaribu kuwaza wewe ambaye sio mchagga ulipomuoa Mchagga ulikuaje kabla hujamuoa na baada ya kumuoa umekuwaje? Tafakari,utafiti wangu unaonyesha wote waliooa wachagga wamebarikiwa. Hebu waza wewe ambaye umewavuruga wachagga ulikuwaje kabla ya kuwavuruga na je baada ya kuwavuruga au kuwasema vibaya umekuwaje? tafakari, mifano ni mingi sana kwa wote walio wavuruga au kuwasema vibaya wachagga waliishia mahali pabaya.
ASILI YA JINA LA WACHAGGA
Jina chagga linatokana na neno la Kabila la Tigrey huko Ethiopia likiwa na maana wameteremka, na hiyo ni wakati wachagga walipokuwa wanafukuzwa na makabila ya Tigrey na Amhara.
MJI WA MOSHI
 Mji wa Moshi ndio sawa na Jerusalem ya pili kwa wachagga.
 Mji wa Moshi ndio ambao unabiashara zinazokwenda kasi kuliko mji mwingine wowote ukiacha Dar es Salaam.
 Angalia mji wa Moshi una matawi ya Benki 20 na unasemwa ni mji sio Jiji? je mji wako una Benki ngapi? Tanga zipo 9 Mbeya ziko ngapi? Mwanza je? Dodoma je? Tafakari
 Mji wa Moshi una Mahoteli mengi sana ukiwa unakaribia Arusha na Dar es Salaam.
 Mji wa Moshi ndio wenye Supermarket nyingi namini supermarket nyingi baada ya Dar es Salaam.
 Moshi ndio mji ambao wenyeji wamewekeza kuliko wageni tofauti na mikoa mingine ambapo wageni ndi wawekezaji.
 Moshi ndio mji ulipangwa vizuri kuliko mji wowote Tanzania.
 Moshi ni mji unaojibeba wenyewe, tofauti na Dar Es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza.
 Moshi ndio mji Msafi kwa asili kuliko mji mwingine wowote Tanzania.
 Moshi ndio mji wenye Bookshop kubwa na nzuri kuliko mji mwingine.
 Moshi ndio mji wenye Masoko mazuri kuliko popote Tanzania.
 Moshi ndio mji wenye maji safi na salama, unaweza kufungua Bomba na ukanywa maji na ukanywa maji bila shida, hakuna pengine Tanzania.
 Moshi ndio mji wa pili kwa utalii baada ya Arusha.
 Moshi ndio mji ambao wakazi wake wana tabia ya kufanya manunuzi na uwezo wa manunuzi.

Wachagga na Thamani ya Nyumbani.
Wachagaa popote walipo au popote walipozaliwa kama walivyo wayahudi wengine wanajua kuna nyumbani na wanapaheshimu sana nyumbani, yaani Moshi.
Mchagga hata azaliwe na kukulia wapi lakini anajua nyumbani ni Moshi.

UPOTOSHAJI WA ASILI YA WACHAGGA.
Historia nyingi zimepotosha sana Asili ya Wachagga. Nyingi zinasema wachagga ni watu wanaozungumza Kibantu_ Lakini hazisemi walikotoka na waandishi wa hizo historia sio kwamba hawajui walikotoka ila wanaficha kwa maana Fulani.

Ni mtu mmoja tu amejaribu kuelezea kwenye encyclopedia kuwa tabia za wachagga zinafanana na mambo ya Agano la Kale kwenye Biblia.

VYAKULA VYA ASILI VYA WACHAGGA.
1. Mapishi ya aina mbalimbali yatokanayo na ndizi.
Mfano: [Ulavi], Machalari, Kimbwe [Kiburu] Makato, Kitawa[Malaa], Kitalolo.

2. Mapishi yatokanayo na aina ya viazi vya Asili kama
- Vibere
- Magimbi machungu
- Fiiye nk.
3. Mapishi yatokanayo na mahindi
- Ngararimu
- Kishanganya, nk

Kinywaji cha Wachagga.
Wachagga wanajulikana kwa Unywaji wa Pombe ya Mbege.

MATUNDA YA ASILI YA WACHAGGA.
Matungusha, Mikodru, Ngomigha, Madala, nk.

Kila zao linalotoka Kilimanjaro ni la THAMANI KUBWA.
 Ukipeleka viazi mviringo Kariakoo vile vinavyotoka Kilimanjaro vinanunuliwa haraka na bei yake ni kubwa kuliko viazi toka kwingine.-
 Mahindi toka Kilimanjaro yanapata bei kubwa kuliko yatokayo sehemu nyingine kwa sababu, hayana mchanga na yamehifadhiwa vizuri.
 Cement ya Moshi cement inapendwa na mafundi kuliko za aina nyingine
 Maji ya chupa ya Kilimanjaro ndio maji Bora kabisa kuliko mengine ya chupa hapa Afrika.
 Kahawa ya Kilimanjaro ndio Bora kabisa hapa Tanzania.
UTUNZAJI WA MAZINGIRA.
Kama hujawahi kufika Kilimanjaro basi siku ukifika utashangaa sana kuwa watu wanaishi msituni yaani miti uchaggani ni mingi kiasi kwamba utaona jinsi nyumba zilivyojengwa chini ya miti.

Vijiji vya Kilimanjaro ni tofauti sana na Vijiji vya maeneo mengine kwani kila mtu amejenga na kuzungukwa na shamba lake, tofauti na vijiji vya maeneo mengine ambapo vimejengwa kama kambi za wakimbizi au miji isiypangwa.
Mfano wake mtu ambaye hajafika Moshi ni kuwa unajua Ostabey ya Dar Es Salaam iliyopangwa? Basi ndivyo vijiji vya Kilimanjaro vilivyo.
UCHUMI WA KILIMANJARO
Zamani wachagga walitegemea mazao ya Kahawa na Ndizi, lakini polepole wameacha kahawa na sasa wanategemea kilimo cha ndizi na zao jipya la Maparachichi, na Macadamia na zaidi sana Biashara.

NYUMBA ZA UCHAGGANI
Unajua nyumba zilizo masaki, Osterbay, Msasani, Ada, Njiro nk? Basi huo ndio mfano wa nyumba zilizopo vijijini hapa Kilimanjaro.
 
Kasome historia tena nenda kasome kuhusu watu wa Yoruba, Igbo, Mali Empire, bila kusahu Songhai Empire halafu uje uandike tena
 
Back
Top Bottom