Historia na safari ya utumishi wa Generali Jacob John Mkunda

Historia na safari ya utumishi wa Generali Jacob John Mkunda

Jenerali Jacob John Mkunda alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 1968 katika Kijiji cha Chakwale, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kwaru iliyopo Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara, Mwaka 1979 hadi 1985. A
7. Nishani ya Utumishi Mrefu.
8. Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
9. Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne.

Huyu ndio CDF wetu Jenerali Jacob John Mkunda..!!!
We pamba pambua sisi tunamtaka aje mahakamani tuu hizo mwember apeleke unguja kwenye eda..
 
wajifunze kujiwekeza, au wajifunze kuiba ?

kuna mishata ya kujiwekeza sasa ? Hivyo vi mishahara vya 2 million, mtu ana familia hiyo, daily to daily cost anabaki na kipi hapo ? unless wajifunze wizi tu nao ngoma iwe draw
Na huo ndiyo mtihani wenyewe

Hata utumie miaka 10 kumfundisha uzalendo mtu hivi sio rahisi kukuelewa
 
Ukishapokea gawio la mkupuo (Ile 33%) Ile inayobaki inatolewa kidogo kidogo hadi utakapoaga Dunia

Kwahiyo ukifa, ndiyo imetoka hiyo

Hakuna pesa nyingine familia itapewa baada ya kifo chako
Kuna mtu niliwai sikia akisema Kuna pesa ya miezi 10 ambayo mtu hupewa baada ya mtu huyo kufariki sina uhakika unaweza kuliweka sawa hili jambo..

Kwaio baada ya kifo mke wa marehemu hapewi kifuta jasho chochote cha marehemu mumewe ili kimsaidie..
 
wajifunze kujiwekeza, au wajifunze kuiba ?

kuna mishahar ya kujiwekeza sasa ? Hivyo vi mishahara vya 2 million, mtu ana familia hiyo, daily to daily cost anabaki na kipi hapo ? unless wajifunze wizi tu nao ngoma iwe draw
Kwaio mkuu sisi wenye salary ya tarakimu SITA. Bila kujiwekeza hatutoboi hahaha haaaahaa

Kwa dar es salaam naona pesa inatumika sana mfano Mimi kwa wastani kwa siku natumia 40,000 iviii kwa kadilio dogo.

Kwaio hata kama una ingiza 2m unaweza jikuta hufanyi lolote la maana tena kwa sisi tunao piga BIA daily HAPA TUNASINGIZIA TUMEROGWA
 
Some people are very luck, Kuna dogo mmoja wenzake wanamuitaga KITIVO a.k.a Professor

Ukitizama elimu yake imenyooka ila now yupo mtaani ni BODA BODA inasikitisha sana

Ukisoma cvs za BAADHI ya wakuu wa vyombo na viongozi wetu wa nafasi za juuu kimaamuzi

Tumepigwa big time
Nchi inapenda wajinga, na ukiwa na akili kama wanakuchukua ukubali kuwa mjinga. Kuna zee moja kila huwa nikikaa nalo linanisifia sana, kuhusu elimu na akili la ndani ndani huko uchawani, ila kujionesha ile kujitambua na kugomea ujinga, limefungw njia zote za mie kutoboa 😅😅😅.. Uzuri na mie sina tamaa ya mali za utapeli
 
Nchi inapenda wajinga, na ukiwa na akili kama wanakuchukua ukubali kuwa mjinga. Kuna zee moja kila huwa nikikaa nalo linanisifia sana, kuhusu elimu na akili la ndani ndani huko uchawani, ila kujionesha ile kujitambua na kugomea ujinga, limefungw njia zote za mie kutoboa 😅😅😅.. Uzuri na mie sina tamaa ya mali za utapeli
Kwa spirit hiyo utatoboa...Mimi akili zangu Huwa sizionyeshi waziwazi ukiwa na seniors wenye wivuuu ( DO NOT OUTSMART YOUR MASTER) maana CV wataiwekea GUNDU 😁
 
Jenerali Jacob John Mkunda alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 1968 katika Kijiji cha Chakwale, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kwaru iliyopo Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara, Mwaka 1979 hadi 1985. Akajiunga na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mavu mwaka 1986 hadi 1989 na Shule ya Sekondari Ndanda mwaka 1990 hadi 1992.

Baada ya kumaliza Elimu yake ya Sekondari Alijiunga na Elimu ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mwaka 2014 hadi 2017 na kutunukiwa shahada ya sanaa katika Utawala wa Umma na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Jenerali Jacob John Mkunda alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa "JKT" kwa mujibu wa sheria mwaka 1992 na ulijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania "JWTZ " Tarehe 1 Aprili mwaka 1993. Pia alihudhuria mafunzo ya Afisa Mwanafunzi na kutunukiwa kamisheni katika Chuo cha Monduli tarehe 25 Juni mwaka 1994.

Katika utumishi wake Jeshi Jenerali Jacob John Mkunda, Alipata nafasi ya kuhuduria mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo:

Afisa Mwanafunzi Tanzania (1994), Kozi ya awali ya maafisa wa mzinga (1995), Gun Position Officers Course katika Shule ya Mzinga Tanzania (1998), Kozi ya utawala wa kikosi, Shule ya Mafunzo ya Huduma Pangani (2001), Field Artillery Company Commander nchini Marekani (2002), Regimental Survey Officers Course Tanzania (2003), Kozi ya Waangalizi wa Amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania (2007), Kozi ya Makamanda na Unadhimu nchini Uganda (2008), Artillery Battalion Commander Course nchini Bangladesh (2010), Kozi ya Ulinzi wa Taifa nchini India (2016)

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake Jeshini umepandishwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:

1. Luteni: Tarehe 5 - Oktoba 1995
2. Kapteni: Tarehe 21 - Januari 2001
3. Meja: Tarehe 3 - Novemba 2006
4. Luteni Kanali: Tarehe 19 - Machi 2010
5. Kanali: Tarehe 17 - Januari 2015
6. Brigedia Jenerali: Tarehe 30- Juni 2016
7. Meja Jenerali: Tarehe 2 - Julai 2020
8. Jenerali: Tarehe 29 - Juni 2022

Kutokana na kisomo chake Jenerali Jacob John Mkunda aliweza kushika Madaraka mbalimbali katika Jeshi letu la Ulinzi "JWTZ" ikiwemo:

1. Platoon Commander, Shule ya Mzinga (1993–2000)
2.Afisa Tawa 451 Regiment (2001–2006)
3. Battery Commander 451 Regiment (2006)
4. Mkufunzi, Shule ya Mzinga (2007–2009)
5. Kaimu Kamanda 977 Regiment (2009–2011)
6. Kamanda Kikosi 977 Regiment (2011–2018)
7. Kaimu Kamanda Brigedi 202 (2018–2020)
8. Kamanda Jeshi la Nchi Kavu (2020–2021)
9. Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Utendaji Kivita, Makao Makuu ya Jeshi (2021–2022)
10. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania kuanzia tarehe 30 Juni 2022, Madaraka uliyonayo hadi sasa.

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake jeshini, Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikutunuku nishani mbalimbali kama zifuatazo:

1. Nishani ya Miaka 40 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
2. Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro.
3. Nishani ya Miaka 50 ya Uhuru.
4. Nishani ya Miaka 50 ya Muungano.
5. Nishani ya Miaka 50 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
6. Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru.
7. Nishani ya Utumishi Mrefu.
8. Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
9. Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne.

Huyu ndio CDF wetu Jenerali Jacob John Mkunda..!!!
cv yake nyingine ni Shahidi wa Lissu
 
Back
Top Bottom