Historia na safari ya utumishi wa Generali Jacob John Mkunda

Jenerali Jacob John Mkunda alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 1968 katika Kijiji cha Chakwale, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kwaru iliyopo Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara, Mwaka 1979 hadi 1985. Akajiunga na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mavu mwaka 1986 hadi 1989 na Shule ya Sekondari Ndanda mwaka 1990 hadi 1992.

Baada ya kumaliza Elimu yake ya Sekondari Alijiunga na Elimu ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mwaka 2014 hadi 2017 na kutunukiwa shahada ya sanaa katika Utawala wa Umma na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Jenerali Jacob John Mkunda alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa "JKT" kwa mujibu wa sheria mwaka 1992 na ulijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania "JWTZ " Tarehe 1 Aprili mwaka 1993. Pia alihudhuria mafunzo ya Afisa Mwanafunzi na kutunukiwa kamisheni katika Chuo cha Monduli tarehe 25 Juni mwaka 1994.

Katika utumishi wake Jeshi Jenerali Jacob John Mkunda, Alipata nafasi ya kuhuduria mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo:

Afisa Mwanafunzi Tanzania (1994), Kozi ya awali ya maafisa wa mzinga (1995), Gun Position Officers Course katika Shule ya Mzinga Tanzania (1998), Kozi ya utawala wa kikosi, Shule ya Mafunzo ya Huduma Pangani (2001), Field Artillery Company Commander nchini Marekani (2002), Regimental Survey Officers Course Tanzania (2003), Kozi ya Waangalizi wa Amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania (2007), Kozi ya Makamanda na Unadhimu nchini Uganda (2008), Artillery Battalion Commander Course nchini Bangladesh (2010), Kozi ya Ulinzi wa Taifa nchini India (2016)

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake Jeshini umepandishwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:

1. Luteni: Tarehe 5 - Oktoba 1995
2. Kapteni: Tarehe 21 - Januari 2001
3. Meja: Tarehe 3 - Novemba 2006
4. Luteni Kanali: Tarehe 19 - Machi 2010
5. Kanali: Tarehe 17 - Januari 2015
6. Brigedia Jenerali: Tarehe 30- Juni 2016
7. Meja Jenerali: Tarehe 2 - Julai 2020
8. Jenerali: Tarehe 29 - Juni 2022

Kutokana na kisomo chake Jenerali Jacob John Mkunda aliweza kushika Madaraka mbalimbali katika Jeshi letu la Ulinzi "JWTZ" ikiwemo:

1. Platoon Commander, Shule ya Mzinga (1993–2000)
2.Afisa Tawa 451 Regiment (2001–2006)
3. Battery Commander 451 Regiment (2006)
4. Mkufunzi, Shule ya Mzinga (2007–2009)
5. Kaimu Kamanda 977 Regiment (2009–2011)
6. Kamanda Kikosi 977 Regiment (2011–2018)
7. Kaimu Kamanda Brigedi 202 (2018–2020)
8. Kamanda Jeshi la Nchi Kavu (2020–2021)
9. Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Utendaji Kivita, Makao Makuu ya Jeshi (2021–2022)
10. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania kuanzia tarehe 30 Juni 2022, Madaraka uliyonayo hadi sasa.

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake jeshini, Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikutunuku nishani mbalimbali kama zifuatazo:

1. Nishani ya Miaka 40 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
2. Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro.
3. Nishani ya Miaka 50 ya Uhuru.
4. Nishani ya Miaka 50 ya Muungano.
5. Nishani ya Miaka 50 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
6. Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru.
7. Nishani ya Utumishi Mrefu.
8. Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
9. Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne.

Huyu ndio CDF wetu Jenerali Jacob John Mkunda..!!!
Mbona hii Sifa yake Kuu ya kwamba ni Komandoo na hata Makomandoo wa Tanzania wanamkubali sana haujaiweka?
 
Kuna watu wana bahati! Mpaka anafikia nafasi ya CDF hana hata shahada ya uzamili kwenye masuala ya usalama, uongozi, nk!! Nilijua kwa nafasi yake atakuwa ni PhD kwenye masuala ya jeshi!
Hao Wana mfumo wao wa elimu,huko siyo kwa kwenda udsm,saut,mzumbe kupata vyeti vya masters PhD
Hapo 1992-2014 itakua kapiga sana shule ya jeshi,jeshini huhitaji masters ya artillery na fighter jets
 
Sio kweli Mkuu, nimefanya masters na askari wawili hapo jalalani

Elimu ni muhimu kwenye kila Idara ya Serikali
 
Hapo 1992-2014 itakua kapiga sana shule ya jeshi,jeshini huhitaji mas
Tungependa kufahamu matokea ya F4 na F6 alipata daraja gani.
Huyo alifaulu form four ndiyo maana akaenda ndanda,ndanda ya serikali na kipindi hicho sekondari chache
 
2. Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro.
Asante mkuu 'Manyanza' kwa taarifa.
Ni vyema kujuwa wasifu wa hawa watu walio na dhamana muhimu katika jamii ya kiTanzania.

Huko Kilosa kumenikumbusha kwa masikitiko makubwa mtu mwingine aitwae Kabuti la Maganda.

Kamwe sitapenda kumhusisha huyu Jenerarli wetu hapa na mtu kama huyo' ila hiyo Kilosa tu ndiyo nimeona muunganisho wao kwa sasa.

Natumaini kila alipo mkuu wetu huyu wa majeshi, dhamira yake inamweleza mchango wake katika hali yetu tuliyonayo sasa hivi kama taifa. Hayo namwachia mwenyewe na dhamira yake.
 
Sio kweli Mkuu, nimefanya masters na askari wawili hapo jalalani

Elimu ni muhimu kwenye kila Idara ya Serikali
Nakwambia Wana mfumo wao wa elimu tena unakustress vibaya mno,hao wanaokuja kusoma uraiani huwa ni cases chache sana,tulikua nae mmoja,na huenda huambiwa waje kusoma vyuo uraiani
 
Kabla ya hiyo formula yao ya 33%, mtumishi aliyestaafu alikuwa akipata pension yake ya mkupuo yote

Kwasasa, kama ulikuwa unastahili kulipwa 100,000,000 basi utalipwa shilingi 33,000,000

Hiyo nyingine 67,000,000 utaendelea kulipwa kidogo kidogo na Serikali
Wanakulipa kwa namna gani sasa!? Kila mwezi au? Na ukifa mapema je inakuaje, ndugu zako wanapewa hizo pesa unazodai 67% au?
 
Hao Wana mfumo wao wa elimu,huko siyo kwa kwenda udsm,saut,mzumbe kupata vyeti vya masters PhD
Hapo 1992-2014 itakua kapiga sana shule ya jeshi,jeshini huhitaji mas

Huyo alifaulu form four ndiyo maana akaenda ndanda,ndanda ya serikali na kipindi hicho sekondari chache
Umeamua kutetea tu ujinga. Vyuo vya kijeshi vimejaa kote duniani vinavyotoa elimu ya kiwango hicho.
 
Hao Wana mfumo wao wa elimu,huko siyo kwa kwenda udsm,saut,mzumbe kupata vyeti vya masters PhD
Hapo 1992-2014 itakua kapiga sana shule ya jeshi,jeshini huhitaji masters ya artillery na fighter jets
Jeshini unaweza kuwa na Elimu kubwa tu. A iliyonyooka na bado ukawa mtu wakawaida tu, Afu kuna wale wenye Elimu ya Hapa na Pale anakuwa hadi Luten General why kwasababu jeshini kuna vyeo huwa ni vya mwisho kabisa afu viliyobaki ni kama Bahati tu au ukaribu na watu wa mfumo nina wajua askari kibao karibia kila Jeshi wana PHD na ni elimu iliyonyooka ila kwasasa ni SSP tu
 
Nakwambia Wana mfumo wao wa elimu tena unakustress vibaya mno,hao wanaokuja kusoma uraiani huwa ni cases chache sana,tulikua nae mmoja,na huenda huambiwa waje kusoma vyuo uraiani
Okay, huenda hao wawili ilikuwa special case huko jeshini
 
Jenerali Jacob John Mkunda alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 1968 katika Kijiji cha Chakwale, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kwaru iliyopo Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara, Mwaka 1979 hadi 1985. Akajiunga na Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mavu mwaka 1986 hadi 1989 na Shule ya Sekondari Ndanda mwaka 1990 hadi 1992.

Baada ya kumaliza Elimu yake ya Sekondari Alijiunga na Elimu ya chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mwaka 2014 hadi 2017 na kutunukiwa shahada ya sanaa katika Utawala wa Umma na Usimamizi wa Rasilimali Watu.

Jenerali Jacob John Mkunda alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa "JKT" kwa mujibu wa sheria mwaka 1992 na ulijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania "JWTZ " Tarehe 1 Aprili mwaka 1993. Pia alihudhuria mafunzo ya Afisa Mwanafunzi na kutunukiwa kamisheni katika Chuo cha Monduli tarehe 25 Juni mwaka 1994.

Katika utumishi wake Jeshi Jenerali Jacob John Mkunda, Alipata nafasi ya kuhuduria mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo:

Afisa Mwanafunzi Tanzania (1994), Kozi ya awali ya maafisa wa mzinga (1995), Gun Position Officers Course katika Shule ya Mzinga Tanzania (1998), Kozi ya utawala wa kikosi, Shule ya Mafunzo ya Huduma Pangani (2001), Field Artillery Company Commander nchini Marekani (2002), Regimental Survey Officers Course Tanzania (2003), Kozi ya Waangalizi wa Amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania (2007), Kozi ya Makamanda na Unadhimu nchini Uganda (2008), Artillery Battalion Commander Course nchini Bangladesh (2010), Kozi ya Ulinzi wa Taifa nchini India (2016)

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake Jeshini umepandishwa vyeo mbalimbali kama ifuatavyo:

1. Luteni: Tarehe 5 - Oktoba 1995
2. Kapteni: Tarehe 21 - Januari 2001
3. Meja: Tarehe 3 - Novemba 2006
4. Luteni Kanali: Tarehe 19 - Machi 2010
5. Kanali: Tarehe 17 - Januari 2015
6. Brigedia Jenerali: Tarehe 30- Juni 2016
7. Meja Jenerali: Tarehe 2 - Julai 2020
8. Jenerali: Tarehe 29 - Juni 2022

Kutokana na kisomo chake Jenerali Jacob John Mkunda aliweza kushika Madaraka mbalimbali katika Jeshi letu la Ulinzi "JWTZ" ikiwemo:

1. Platoon Commander, Shule ya Mzinga (1993–2000)
2.Afisa Tawa 451 Regiment (2001–2006)
3. Battery Commander 451 Regiment (2006)
4. Mkufunzi, Shule ya Mzinga (2007–2009)
5. Kaimu Kamanda 977 Regiment (2009–2011)
6. Kamanda Kikosi 977 Regiment (2011–2018)
7. Kaimu Kamanda Brigedi 202 (2018–2020)
8. Kamanda Jeshi la Nchi Kavu (2020–2021)
9. Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Utendaji Kivita, Makao Makuu ya Jeshi (2021–2022)
10. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania kuanzia tarehe 30 Juni 2022, Madaraka uliyonayo hadi sasa.

Jenerali Jacob John Mkunda Katika utumishi wake jeshini, Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikutunuku nishani mbalimbali kama zifuatazo:

1. Nishani ya Miaka 40 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
2. Nishani ya Operesheni Demokrasia Comoro.
3. Nishani ya Miaka 50 ya Uhuru.
4. Nishani ya Miaka 50 ya Muungano.
5. Nishani ya Miaka 50 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
6. Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru.
7. Nishani ya Utumishi Mrefu.
8. Nishani ya Utumishi Uliotukuka.
9. Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne.

Huyu ndio CDF wetu Jenerali Jacob John Mkunda..!!!
Tuwekee ya Kingai na IGP
 
Back
Top Bottom