Historia: vituko ulimwenguni

Historia: vituko ulimwenguni

Ukiangalia video ya kunyongwa huyu mtoto inatisha sana, alinyongwa kwa umeme mkali, nililia sana siku naiangalia, kwanini wanadamu wana roho katili namna hii, sikutamani tena kuiangalia na sithubutu kuiangalia tena na ingekuwa ridhaa yangu wangeitoa mitandaoni haifai kutazamwa. Wazungu washenzi sn.
Najua inasumbua Sana nafsi Ila wasiitoe....acha tu watu wajifunze kupitia unyama huo
 
Ukiangalia video ya kunyongwa huyu mtoto inatisha sana, alinyongwa kwa umeme mkali, nililia sana siku naiangalia, kwanini wanadamu wana roho katili namna hii, sikutamani tena kuiangalia na sithubutu kuiangalia tena na ingekuwa ridhaa yangu wangeitoa mitandaoni haifai kutazamwa. Wazungu washenzi sn.
Movue inaitwaje mkuu?
 
Mwaka 2012, Li Xiufeng, mwanamke wa China mwenye umri wa miaka 95, alitangazwa kuwa amefariki na wanakijiji wake baada ya majaribio kadhaa ya kumwamsha kushindikana. Siku mbili baada ya kutangazwa kuwa amefariki, alilazwa kwenye jeneza lake Februari 19, 2012. Kufuatia utamaduni wao, jeneza liliachwa wazi nyumbani kwake kwa marafiki na familia kutoa heshima zao za mwisho. Kama sehemu ya mila, mali yake yote pia iliteketezwa. Tarehe iliyopendekezwa ya mazishi ilipangwa kuwa tarehe 24 mwezi huo huo. Hata hivyo, siku moja kabla ya kuzikwa, jamaa waliogopa sana kugundua kuwa mwili wake haukuwa tena ndani ya jeneza. Walimtafuta na kumkuta anapika jikoni. Alipopatikana alisema: “Nililala kwa muda mrefu. Baada ya kuamka, nilihisi njaa na nilitaka kupika chakula. Nilisukuma kifuniko kwa muda mrefu ili kutoka nje.
20230819_061335.jpg
 
Bibiana, Mlezi Mtakatifu wa Hangover

Aliuawa kishahidi katika karne ya 4, Bibiana alikua mtakatifu mlinzi wa hangover bila sababu nyingine isipokuwa jina lake linatokana na neno la Kilatini la kunywa, "bibulus."


Bibiana aliteswa na Maliki Mroma Julian Mwasi kwa kukataa kukana imani yake katika Ukristo. Imeripotiwa kuwa alikuwa:

*Amefungwa kwenye nguzo, na kuchapwa kwa mijeledi iliyojaa matone ya risasi hadi muda wake utakapomalizika. Mwili wake uliachwa wazi, ili uwe mawindo ya wanyama; lakini akiwa amelala wazi kwa siku mbili hakuliwa na mnyama yeyote yule, akazikwa usiku.

Baada ya mazishi yake, mimea iliyokua karibu na kaburi lake inadaiwa iliponya maumivu ya kichwa - na hangover.

Mahali pa kuzaliwa: Roma, ItaliaView attachment 2705658

Sent using Jamii Forums mobile app
Big no
 
MEYA AFUNGA NDOA NA MAMBA

Meya wa nchini Mexico Kutoka katika Mji wa San Pedro Huamelula, Victor Hugo amemuoa mamba mwenye Umri wa miaka 7. Kabla ya Harusi hiyo mamba huyo alibatizwa na kutambulika kwa jina la Princess, siku iliyofuata ndoa ikafungwa ambapo bwana hurusi alimbusu mamba huyo mdomoni ingawa mamba alikuwa amefungwa mdomo asije kukinukisha katikati ya sherehe na kujeruhi watu

Watu walikula, kunywa na kusaza huku muziki ukipigwa na watu kuserebuka. Mama mtu mzima kwa jina la Elia ambaye alipewa kazi kuhakikisha harusi hiyo inaenda vizuri, alikaririwa akisema aliumiza sana kichwa kujua mamba huyo bibi harusi atavaa nini lakini hatimaye gauni zuri na shela vilishoneshwa kwa ajili ya mamba huyo na kumpendeza vilivyo

Wanakijiji hawakuishia kula na kucheza muziki tu, bali pia walipata nafasi ya kumbeba na kumshika bibi harusi huyo kwa jina la Princess na kuzunguka nae mitaani kwa furaha

Pamoja na hayo, harusi hiyo ni ya kimila mamba anaolewa ambapo watu wa kijiji husika wanaamini kuwa ni muunganiko wa nguvu za kibinadamu na nguvu za kimungu hivyo wanaamini wavuvi wa maeneo yao watavua samaki wengi, watavuna mazao mengi, kupata chakula kingi, mvua nyingi kunyesha na kila aina ya neema

"Tunapendana," meya wa Mexico ameyasema hayo wakati wa sherehe ya ndoa yake na mamba huyo jike..
FB_IMG_1699775566613.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3544] Mwanadada Loveness Tarimo amesema yeye ni mwanamke na ana jinsi ya kike hivyo wenye shaka na yeye waondoe

Loveness ni mwalimu wa mazoezi(gym trainer), aliwahi kushinda taji la Miss Fitness 2019. Pia aliwahi kuwa mshindi wa 2 wa Miss Figure East Africa

C&P
FB_IMG_1699778656763.jpg
FB_IMG_1699778654123.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom