jay-millions
JF-Expert Member
- Apr 30, 2015
- 3,983
- 10,034
Hao wote uliowataja hawapingi serikali ya kagame Sera zake wao wanapinga umoja wa wanyarwanda wanapanda chuki na kuleta utengano wa makabila, kama unabisha weka hapa Sera za ingabire, weka sera za rwigara hapa tuone, pitia video zao YouTube uone wanahubiri nini? Wanataka kurudisha mambo ya kangura magazine ili nchi irudi 20yrs back? Ungukuwa wewe ndo president ungewachekea? Wakiachwa unajua mwisho wao kutatokea nini? Kumbe demokrasia kwako ni kusema kila kitu? Hao wapinzani waliomsifia kagame kwenye mdahalo sio demokrasia ila wangemponda ndio demokrasia? Mkuu nikiangalia Rwanda miaka 20 iliyopita na miaka 30 ijayo hapo ndo nauona u genius wa kagame, trust me that man sio wa dunia hii, that man is from the futures! He is a true gift from God to the rwandese and AfricansLini nimemchukia kagame?? Mbona thread kibao humu namsifia sana..... Nachopingana na kagame ni eneo la UDIKTETA na UKABILA basi hapo tu mengine yote namuunga mkono hasa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa aliyoyaleta ntakuwa mwendawazimu kupinga hilo
Kwanini nimchukie kwa akili zake kwani ninagombea naye urais 2024 ama mie ni kilaza hadi nimuonee wivu?? Na nani kasema kagame ndio brightest au kisa ni maarufu kuliko wanyarwanda wengine?? Kuna wenye akili wengi tu Rwanda hata nmesoma nao most tutsis are bright sana tu so kagame sio wa kwanza na sio wa mwisho
Embu uache slave mentality ya kuamini wengine hawawezi ila kagame tu...... Na ndio hiki kinaua Afrika mtu mmoja kujiona ana akili kuliko wengine.... Sasa kwa mfano leo akifa ghafla si ina maana Rwanda itaporomoka?? Haijalishi una akili kiasi gani mbona Mahathir mohammed licha ya kwamba aliitoa singapore kwenye jalala na sasa ni top hapa duniani ila aliachia ngazi?? Kwanini unaamini hakuna wengine?? Umewajaribu?? Unajua baraza la mawaziri la kagame au kisa unamjua kagame tu basi ndio unamuona anafaa pekee..... Ni vizuri kufanya succession plan nzuri ili hata likitokea lolote nchi hainguki sio kuaminishana kwa kuwa ana akili sana basi atawale milele BIG NO.... Nchi haitostawi kwa akili za mtu mmoja bali MFUMO otherwise huyo mtu akifa nchi nayo inakufa kama PATRICE LUMUMBA NA ZAIRE
Sina chuki na kagame mkuu ila ukweli lazima usemwe kwenye issue ya UTAWALA amechemka sana.... Hivi kwa maendeleo yote yale alikuwa na haja ya kuogopa wapinzani?? Yule binti si bora angemuibia kura tu kuliko kumtesa vile then wwe huoni shida?? Yukwapi ingabire?? Yukwapi nyamwasa?? Kwanni hataki mawazo mbadala??
Kingine ni issue ya genocide kagame anaficha mengi sana na anapotosha dunia ndio maana kwa hili huwa nampinga wazi wazi bila kupepesa macho hata humu nlitoka mapovu sana maana ni propaganda tupu facts ni 20%....
Mfano Bold anasema eti kagame hakuua ruhengeri?? Ina maana risasi za RPF zililenga wanajeshi wa serikali pekee ila alishindwa kutwambia kivipi wahutu 40,000 walikutwa wamechinjwa na wengine kukimbia makazi!! Kulingana na ripoti za human rights watch!!
Kagame namkubali sana ila kwa hili la genocide hapana ntampinga kma alivyofanya Mch Mtikila hadi anaingia kaburini
Long live East Africa
Long live Rwanda