Historia ya Sewa Haji Paroo (1851-1897), Muasisi wa Hospitali ya Muhimbili

Alijenga jengo ambalo leo ni wodi ya Sewahaji pale hospitali ya Muhimbili sio alijenga hospitali ya Muhimbili
Ungesema hivi; huyo Sheikh Sewa Haji Paroo alijenga jengo la kutolea matibabu miaka hiyo au niseme Hospitali ambapo kutokana na kukua kwa maendeleo limeonekana kuwa dogo na hivyo kufanywa ward.
Kimsingi huyo ni founder wa Hospitali ya Muhimbili na wala huna haja ya kupindisha maneno........
 
Washia huwa wako makini sana kwenye huduma za kijamii
 
Baada ya uhuru ilipata jina la "Muhimbili", ambalo limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.

Source: Wikipedia

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Swali ni kuwa muhimbili ni nini!!!!
Baada ya uhuru ilipata jina la "Muhimbili", ambalo limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.
 
πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ
 
Kadri ninavyofahamu mimi kuhusu historia ya Tanzania, ambayo sisi vijana wengi siku hizi tunaipuuuza, MWAISELA na SEWA HAJI, walikuwa ni madaktari bingwa wa mwanzo wenye asili ya Kiafrika nchini mwetu. Hospitali ya kwanza kubwa katika Tanzania, ilikuwa inaitwa kwa jina la Sewa Haji, ambayo ilikuwepo kabla ya uhuru katika eneo kati ya Kituo cha sasa cha Kati cha Polisi na Ofisi ya Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam. Baadaye wakati uhuru unapatikana, Sewa Haji, ikahamishiwa pale ambako sasa ni Muhimbili, lakini wakati huo ilikuwa inajulikana kuwa Princes Margaret Hospital, kwa heshima ya Malkia wa Uingereza wakati huo. Ndiyo maana Wodi moja muhimu Muhimbili, inaitwa Sewa Haji. Hospitali nyingine kubwa ni ile ambayo sasa ni Ocean Road, lakini ilikuwa inaitwa European Hospital, kwa ajili ya Wazungu tu.
 
Neno wapagazi limetumika kupunguza ukali wa maneno kwa rafik yetu mtukuka kiufupi hayati alitumia watumwa kupiga fungu ila alikua na utu sana akawajali kwa kuwajengea makaz nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…