Historia ya Sewa Haji Paroo (1851-1897), Muasisi wa Hospitali ya Muhimbili

Historia ya Sewa Haji Paroo (1851-1897), Muasisi wa Hospitali ya Muhimbili

Alijenga jengo ambalo leo ni wodi ya Sewahaji pale hospitali ya Muhimbili sio alijenga hospitali ya Muhimbili
Ungesema hivi; huyo Sheikh Sewa Haji Paroo alijenga jengo la kutolea matibabu miaka hiyo au niseme Hospitali ambapo kutokana na kukua kwa maendeleo limeonekana kuwa dogo na hivyo kufanywa ward.
Kimsingi huyo ni founder wa Hospitali ya Muhimbili na wala huna haja ya kupindisha maneno........
 
HUYU NDIYE MTU ALIYEJENGA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Anaitwa Sewa Haji Paroo Alifika Zanzibar Akitokea Katika Miji Ya Bhuj Na Kutch
Na Mnamo Mwaka 1852 Alifungua Duka La Bidhaa Mbalimbali Huko Zanzibar, Mnamo 1860 Akafungua Duka Lingine Kubwa Bagamoyo na Kuweka Makazi Yake, Biashara Zake Zikawa Kubwa Na Kuwa Tajiri Mkubwa Sana.

Alisaidia Watu Wote Bila Kujali Rangi, Dini Wala Kabila Zao, Alinunua Majengo Mengi Na Kuyafanya Maeneo Ya Watu Wasiojiweza, Alijenga Mashule ba Hospitali Kadhaa, Katika Mji wa Mzizima { Leo Inaitwa Dar es Salaam}.

Alijenga Hospitali Akaiita Sewahaji Hospitali Ikitoa Huduma Bure, Mnamo February 1897 Sheikh Sewa Haji Paroo Alifariki Dunia, Ilikuwa Ni Huzuni na Simanzi Kwa Wakazi Wa Bagamoyo Na Mzizima Kwa Kuondokewa Na Sheikhe Sewa Haji Aliependwa Sana na watu.

Baada ya Kufariki Kwake Wakoloni Baadaye Wakabadilisha Jina Kutoka Sewahaji Hospital Na Kuiita Princess Magreth Hospital, Na Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo ya Wodi Katika hospital hiyo Inaitwa SEWA HAJI,

Sheikhe Sewa Haji Alale Mahali Pema..peponi 🙏

View attachment 2645161
Washia huwa wako makini sana kwenye huduma za kijamii
 
Baada ya uhuru ilipata jina la "Muhimbili", ambalo limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.

Source: Wikipedia

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Swali ni kuwa muhimbili ni nini!!!!
Baada ya uhuru ilipata jina la "Muhimbili", ambalo limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.
 
Ungesema hivi; huyo Sheikh Sewa Haji Paroo alijenga jengo la kutolea matibabu miaka hiyo au niseme Hospitali ambapo kutokana na kukua kwa maendeleo limeonekana kuwa dogo na hivyo kufanywa ward.
Kimsingi huyo ni founder wa Hospitali ya Muhimbili na wala huna haja ya kupindisha maneno........
👏🏾👏🏾👏🏾
 
Kadri ninavyofahamu mimi kuhusu historia ya Tanzania, ambayo sisi vijana wengi siku hizi tunaipuuuza, MWAISELA na SEWA HAJI, walikuwa ni madaktari bingwa wa mwanzo wenye asili ya Kiafrika nchini mwetu. Hospitali ya kwanza kubwa katika Tanzania, ilikuwa inaitwa kwa jina la Sewa Haji, ambayo ilikuwepo kabla ya uhuru katika eneo kati ya Kituo cha sasa cha Kati cha Polisi na Ofisi ya Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam. Baadaye wakati uhuru unapatikana, Sewa Haji, ikahamishiwa pale ambako sasa ni Muhimbili, lakini wakati huo ilikuwa inajulikana kuwa Princes Margaret Hospital, kwa heshima ya Malkia wa Uingereza wakati huo. Ndiyo maana Wodi moja muhimu Muhimbili, inaitwa Sewa Haji. Hospitali nyingine kubwa ni ile ambayo sasa ni Ocean Road, lakini ilikuwa inaitwa European Hospital, kwa ajili ya Wazungu tu.
 
Neno wapagazi limetumika kupunguza ukali wa maneno kwa rafik yetu mtukuka kiufupi hayati alitumia watumwa kupiga fungu ila alikua na utu sana akawajali kwa kuwajengea makaz nk
 
Back
Top Bottom