Historia ya TANU siku zote imeandikwa na makosa

Kwahyo unaona huyo shekh wako alikua sahihi kuleta mada za maslah ya waislamu kwenye harakati za uhuru wa taifa lenye dini nyingi?
Lugoda...
Mimi sina haki ya kumuhukumu Sheikh Suleiman Takadiri kuhusu tatizo lile.

Lakini ni dhahiri yeye alipata wasiwasi kutokana na matokeo ya Kura Tatu na uchaguzi wa wagombea wa TANU kuingia Legco.
 
Kwahyo mzee dhumuni lako ni nini? Yani tufanyaje ili wazee wako nao waheshmike? Mana kama nyuz za kuwahusu ni nyingi ila binafsi sijawahi ona ushauri wako ili watambulike kitaifa. Samahani kama nimekosea.
Lugoda...
Mimi nimeandika kitabu kusahihisha historia ya TANU iliyokuwa na makosa mengi.

Kitabu kipo toka 1998.
Sikuwa na jingine.
 
Sasa utahoji vipi hali ya Waislamu wakati Tanzania ni ya Waafrika na sio ya Waislamu au wakristu. Maswala ya dini ni ya kijinga sana
 
Salamu Mzee wangu ningependa kumfaham zaidi huyu Mzee wetu Ali Migeyo, mana nilipata kusoma elimu yangu ya sekondari bukoba mjini miaka ya 1994 na kuna mtaa ulikua unaitwa Migeyo Street karibu na soko kuu Mohamed Said
 
AHMED ADAM – MNUBI

Tukio dogo la kiburi

Askari mmoja mpita njia

aliingia katika ubishi na kijana mmoja

Hassan Masudi Vuni.

askari huyo alimpiga Vuni kwa kumuonea.

Msepele alitamka kwamba tukio kama hilo kamwe lisingeweza kutokea Dar es Salaam kwa sababu Mwafrika mmoja jina lake Julius Nyerere

Mwafrika huyu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Nyerere

Mohamed Ali alimweleza Nyerere kwamba ukoloni ulikuwa bughudha

Mohamed Ali alikuwa na umri wa miaka 45.

Alikuwa hana elimu kama elimu

Zanzibar ilikuwa ndiyo kitovu cha elimu ya Kiislamu Afrika ya Mashariki

kijana Mohamed Ali alisoma kwa Sheikh Mohamed L’Khamus

Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni.

Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza

kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya Kimagharibi.

Mohamed Ali na akawa mwanachama

na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU

awafahamishe watu kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.

Nyerere aliwahakikishia wasikilizaji wake kuwa kulikuwa na uwezekano mku

mwalimu mmoja wa shule, Abdulrahman Muhibu

Katika hali yake ya ulevi alimpigia kelele Nyerere akamwita muongo.

aliona wazo la mwalimu wa shule Mwafrika kama yeye kuwaongoza watu hadi uhuru upatikane ni jambo lisilowezekana.

Nyerere alipomaliza ziara yake ya Jimbo la Kusini, fikra za watu wengi zilibadilika.
 
Salamu Mzee wangu ningependa kumfaham zaidi huyu Mzee wetu Ali Migeyo, mana nilipata kusoma elimu yangu ya sekondari bukoba mjini miaka ya 1994 na kuna mtaa ulikua unaitwa Migeyo Street karibu na soko kuu Mohamed Said
Nduku...
HAMZA MWAPACHU NA ALI MIGEYO "WAASISI" WA TANU AMBAO HAWAKUHUDHURIA MKUTANO ULIOASISI TANU
Siku zote nimekuwa nikiungua ndani ya moyo wangu kwa nini Hamza Mwapachu na Ali Migeyo hawajapewa heshima wanayostahili katika kuunda chama Cha TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Huu ni mmoja wa misiba ya historia ya TANU.

Lakini pia unaweza ukaniuliza kwani nani kapewa heshima ya kuunda chama Cha TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika hadi leo niwataje Hamza Mwapachu na Ali Migeyo?

Hao wazalendo wengine vipi mbona huwataji ilhali wao ni waasisi wa TANU?

Siku zote mimi nimewahesabu wazalendo hawa wawili, Hamza Mwapachu na Ali Migeyo katika kundi la waasisi wa TANU na kufanya hesabu yangu ya waasisi wa TANU kuwa watu 19 badala ya 17.

Nani Hamza Mwapachu (1913 - 1962)?

Ana mengi sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere.

Hamza Mwapachu ndiye aliyefanya juhudi kubwa sana kuwa TAA iongozwe na vijana na hawa vijana ndiyo waunde TANU na kuongoza harakati za kudai uhuru.

Hamza Mwapachu alikuwa rafiki mkubwa wa Abdul Sykes.

Hamza Mwapachu alikuwako katika TAA Political Subcommittee iliyoundwa mwaka wa 1950.

Hii ilikuwa kamati ya wataalamu na watu wenye sauti katika siasa za Tanganyika na ndiyo waliotengeneza mapendekezo ya katiba ya Tanganyika yaliyowasilishwa kwa Gavana Edward Francis Twining mwaka wa 1950.

Katika mapendekezo haya yalikuyowasilishwa kwa Waingereza katka mapendekezo yaliyoighadhibisha serikali ilikuwa pendekezo la uchaguzi huru na pendekezo la kuwataka Waingereza kuondoka Tanganyika baada ya miaka 13 kuanzia pale uchaguzi utakapofanyika.

Wajumbe wa kamati hii walikuwa: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hamza Mwapachu ndiye aliyempendekeza Julius Nyerere kwa Abdul Sykes kuwa Nyerere atiwe katika nafasi ya uongozi wa juu wa TAA katika uchaguzi wa mwaka wa 1953 na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Ilikuwaje Hamza Mwapachu muasisi wa fikra kama hizi hakuhudhuria uasisi wa chama alichokuwa anakihangaikia kiasisiwe ni kisa ambacho In Shaa Allah tutakisoma katika kumbukumbu za Juma Mwapachu mtoto wa Hamza Mwapachu.

Tuwe na subra.

Ali Migeyo ndiye aliyekuwa akiwasha moto wa ukombozi Kanda ya Ziwa.
Ali Migeyo alikuwa fupa lililokwama kwenye koo la Waingereza.

Siku moja mwaka wa 1953 Ali Migeyo akiwa anahutubia wananchi wa Kamachumu mkutano ulivamiwa na mabomu yakapigwa.

Ali Migemo alikamatwa, akashitakiwa na kufungwa jela ya Butimba, Mwanza.
Wakati viongozi wa TAA walipokutana Dar es Salaam kuunda TANU, Ali Migeyo alikuwa jela anatumikia kifungo chake.

Hii ndiyo sababu hakuweza kuhudhuria mkutano ule.

Kwangu mimi Hamza Mwapachu na Ali Migeyo ni waasisi wa TANU ambao hawakuhudhuria kikao cha kuasisi chama cha TANU.

 
Sasa utahoji vipi hali ya Waislamu wakati Tanzania ni ya Waafrika na sio ya Waislamu au wakristu. Maswala ya dini ni ya kijinga sana
Ed...
Huenda tatizo kwa baadhi yetu ni kukosa kujua somo tunalojadili.

Maswali mengi ninayokutananayo hapa JF ni tofauti sana na mswali ninayoulizwa kwengineko ninakopita kukutana na wanafunzi wa African History.

Umetumia lugha kidogo haipendezi kusema ujinga.

Sikulaumu kwani wewe historia hii na mchango wa Sheikh Suleiman Takadir katika kupigania uhuru wa Tanganyika historia hii umeisikia kwangu.

Umekuja hapa kujadili historia ambayo huijui.

Soma historia hii ya uhuru wa Tanganyika kama nilivyoieleza katika kitabu cha Abdul Sykes utaelewa kwa nini uhuru ulipokuwa unakaribia baada ya Kura Tatu likajitokeza suala la Waislam katika Tanganyika huru.
 
Nelson,
Hapana sina chuki na mtu yoyote.
Nimeandika kitabu kueleza historia ya kweli ya uhuru.

Sikusukumwa na chuki ila nilitaka historia ya wazee wangu waliopigania uhuru isipotee.
Mzee said una chuki ya udini.Sababu nishawahi kukusikia mahala unasifia makanisa kugeuzwa stoo na miskiti huko uingereza.Na pia unalaumu baraza la mitihani linafelisha wanafunzi kimakusudi.
 
Leo anataka kudanganya watu eti vijana wa UD wamechezea picha, huyu jamaa anawafanya watu humu wakuda eeh?.

Yaani anadhani kizazi hiki ndicho kile cha "rudi nyumbani nitakuletea pipi" NO!.
Mzee ana hasira na Nyerere.
 
We mdini sana halafu mpotoshaji sisomagi nyuzi zako, sijui nia ni nini. Wenzako wanakemea udini we unaukoleza je una tofauti na shetani?
 
Nelson,
Hapana sina chuki na mtu yoyote.
Nimeandika kitabu kueleza historia ya kweli ya uhuru.

Sikusukumwa na chuki ila nilitaka historia ya wazee wangu waliopigania uhuru isipotee.
Historia ya kweli we ulikuwepo kwenye michakato ya kutafuta uhuru?
 
Shukran sana Mzee wangu nimepata kujifunza kitu ubarikiwe na uwe na saum njema Mohamed Said
 
Historia ya kweli we ulikuwepo kwenye michakato ya kutafuta uhuru?
Mzee kanidanganya mpaka kuhusu vita vya maji maji kua ni jihad ya waislamu na pia anamsifia yule mfanyabiashara chotara wa kiarabu wa pembe za ndovu na watumwa Abushir bin salim kua alikua anatetea masilahi ya wabantu weusi alipopigana na wajerumani ambao walimzuia asifanye biashara haramu ya kuuza binadamu wenzie.
 
Historia ya kweli we ulikuwepo kwenye michakato ya kutafuta uhuru?
Saig...
Mimi nimezaliwa mwaka wa 1952 na baada ya miaka miwili ndiyo TANU ikaunndwa kwa hiyo michakato ya kutafuta uhuru katika siasa za TANU 1954 hadi 1961 mimi nilikuwa mtoto mdogo.

Lakini babu yangu Salum Abdallah yeye alihusika katika siasa za kutafuta uhuru kutoka miaka ya 1929 wakati African Association inaundwa.

Babu yangu aliongoza migomo mikubwa mitatu (General Strike) 1947, 1949 na 1960.
Bau yangu alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU Tabora mwaka wa 1954 na pia ni mwasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) akiwa Mwenyekiti na Kassanga Tumbo Katibu 1955.

Kwa ajili historia ya uhuru wa Tanganyika kuanzia 1929 imekuwa ikiishi ndani ya familia yangu.

Hivi ndivyo nilivyokuja kuijua historia ya uhuru kushinda watu wengi sana.


Kulia ni Kassnga Tumbo na anefuatia ni Salum Abdallah​
 
We mdini sana halafu mpotoshaji sisomagi nyuzi zako, sijui nia ni nini. Wenzako wanakemea udini we unaukoleza je una tofauti na shetani?
Saig...
Nimesahihisha historia ya uhuru ambayo ilikuwa na makosa mengi sana kiasi historia ya TANU haikuwapo.

Tatizo ni waandishi wakihofu mchango wa Waislam katika kupigania uhuru.

Sidhani kama kuandika historia ya kweli na kuuweka wazi mchango wa Waislam ni udini.
 
Nelson...
Kuna kaburi la halaiki wamezikwa mashujaa yapata 67 wa Vita Vya Maji Maji pale Songea na kuna kaburi amezikwa Abdul Rauf Songea Mbano.

Katika hao walionyongwa kuna mwanamke pekee Bi. Khadija Mkomanile.
Hawa walinyongwa na Wajerumani.

Kabla ya kunyongwa alikuja mmeshionari kutoka Peramiho kuwaambis kuwa ikiwa takubali kubatizwa hawatanyongwa.

Ungekuwa unandika kwa adabu ningekueleza mengi mbayo huyajui.
Lakini kwa kuwa unadhani kuwa unajua basi na twende hivi hivi.
 
Sijui analipwa na nani kwa uptoshaji na udini na anapata faida gani. Anadanganya vijana hasa wa kiislamu kuhusu historia ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…