We mzee ni MPUMBAVU SANA. Unastahili kuwa gerezani kwa hizi akili zako mbovu za kutala Tanzania iwe nchi ya kiislamu. Hii nchi haina udini nakushangaa unavyosukuma agenda zako za kihayawani.
Mama...
Kwa hakika unanitukana bila sababu.
Sijafanya kampeni kutaka Tanzania iwe nchi ya Kiislamu.
Hata wazee wetu walioanzisha harakati za kuwakusanya Waafrika wa Tanganyika kuwa chini ya African Association hawakupata kulifikiri jambo hili.
Sababu ziko wazi kuwa fikra kama hiyo isingefanikiwa kamwe na hiyo African Association yenyewe isingefika mbali.
Ukichukulia kuwa Wamishionari wakiwaonya waumini wao wasijihusishe na siasa.
Hii ndiyo sababu Waislam wakatawala siasa.
Nitakupa mfano uliokuwa ndani ya AA.
Waislam walikuwa wakipitisha madai yao mengi kwa serikali kupitia AA.
Wazee wetu wakaona huo kuwa mushkeli mkubwa.
Wakati huo Mzee bin Sudi alikuwa President na Kleist Sykes Secretary.
Ili kukiepusha chama na tatizo hili ndipo wakaamua mwaka wa 1933 kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Ikawa sasa mambo yote ya Waislam kwenda kwa Gavana yanapitia Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Ninaweza nikakupa mifano mingi.
Ilipoundwa TANU Mufti Sheikh Hassan bin Ameir aliitisha mkutano wa ndani Mtaa wa Pemba usiku kujadili suala la umoja baina ya watu wa imani hizi mbili kubwa.
Ikutoshe tu kwa kuangalia nyuma kuwa hoja ya Hamza Mwapachu kuwa Nyerere atiwe kwenye uongozi wa TAA 1953 kisha waunde TANU 1954 ilikuwa Nyerere ni Mkristo na kwake yeye kuongoza harakati za uhuru itajenga umoja ndani ya TANU kwa kuwavuta Wakristo
Kikao hiki kilifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio na alikuwapo Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Uamuzi huu ulikusudiwa kuondoa ile picha kuwa harakati za kudai uhuru ni za Waislam peke yao.
Historia hii ni maarufu hapa JF kwani nimeieleza mara nyingi.
Ikiwa wewe una ushahidi kuwa katika maandishi yangu nimetaka Tanzania iwe nchi ya Kiislam ulete hapa usomwe.
Masikini ya Mungu wewe huijui historia ya uhuru wa Tanganyika unapandwa na ghadhabu unatoa matusi ilhali hujui wazee wetu waliweka misingi gani kuhakikisha umoja na amani wakati wa mapambano ya uhuru.
Lakini sikulaumu nakuonea huruma.
Itaijuaje historia hii wakati haikupata kuandikwa?
Umepata kuwasikia Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe wakitajwa katika historia ya uhuru wa Tanganyika?
Ushajiuliza kwa nini imekuwa hivi?
Unahamaki unapoambiwa kuwa kadi ya TANU ya Abdul Sykes ni No. 3, No. 2 ni ya mdogo wake Ally Sykes na kadi ya Julius Nyerere ni No. 1 na kaandikiwa na Ally Sykes.
Kwa.kuandika historia hii nimekuwa mdini.
Haitakiwi historia hii kufahamika.
Inatakiwa ibakie historia ambayo si historia ya kweli ya TANU.
Ally Sykes na Julius Nyerere
Kulia Abdul Sykes na Hamza Mwapachu