Historia ya TANU siku zote imeandikwa na makosa

Watu wenyewe wote anaowatetea Nyerere aliwapa kazi wao na watoto wao. Mohamed Said sijui alikuwa anataka Nyerere awabebe wazee wa Mohamed Said awabebe mgongoni??
Stux...
Haya hayahusiani na kazi.

Nimesahihisha historia iliyokuwa na makosa.
 
Ndo maana tunasema kitabu chako ni cha kuhusu uislamu na sio TANU wala historia ya nchi hii.
Mama...
Kitabu kinaitwa:"The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Catalogue ya Library of Congress ni Islam, Politics.


Library of Congress, Washington DC​
 
Naomba wale Wajuzi wa historia mnielimishe kidogo ilikuwa Watu wa DSM walimuomba Julius Nyerere awasaidie katika mapambano ya kudai Uhuru

Mzee Mohamed Said na Wakili Pascal Mayalla karibuni tafadhali

Mlale Unono 😃
 
Huna uwezo wa kusahihisha historia kwa kuwa uko intoxicated na islamology
Hui...
Nimeisahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika na kitabu kipo toka 1998.
Kiko toleo la nne tunakwenda toleo la tano.

Vitabu nilivyovisahihisha vyote vimekufa vimechapwa toleo la kwanza basi.


 
Mtu mmoja tu uliyekamia kuandika maisha yake hawezi kuwa historia ya Tanzania.
Huihui...
Hakika ni maisha ya historia ya mtu mmoja lakini kupitia maisha yake utasoma maisha ya watu wengi waliokuja kuwa watu maarufu katika historia ya Tanzania.

Kuna picha katika kitabu cha Abdul Sykes na ni picha ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika imepigwa katika miaka ya 1930.

Aliyesimama wa kwanza mstari wa nyuma kushoto ni Maalim Mohamed Matar mwalimu wa Qur'an katika shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Maalim Matar ni kielekezo cha mateso katika jela za utesaji na Zanzibar baada ya mapinduzi.

Katika picha hiyo utaona majina ya Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Kleist Sykes muasisi wa jumuiya hiyo 1933 na mwanae Abdul Sykes.

Ali Mwinyi ni muhimu sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar.

Siku nilipozungumza na Ali Mwinyi aliniambia kuwa Abdul Sykes ni mdogo sana kwake na alinieleza mengi kuhusu African Association.

1953 mwanzoni Abdul Sykes sasa kijana na Ally Mwinyi Tambwe walikwenda Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu kujadili suala la uchaguzi wa mwaka wa TAA uliokuwa unafanyika mwezi April.

Abdul Sykes alikuwa TAA Act. President na Secretary.

Mazungumzo yao hao watu watatu ilikuwa Abdul kumpisha Julius Nyerere katika nafasi ya rais wa TAA na mwaka unaofata 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.

Nadhani hadi hapo umesoma kidogo historia ambayo hukuwa unaijua na maarifa yako yameongezeka.
 
Je ulishafanya tafiti kwanini ilibidi Adbul Sykes ampishe Nyerere?
 
Je ulishafanya tafiti kwanini ilibidi Adbul Sykes ampishe Nyerere?
Huihui...
Kuna sababu kubwa mbili kwa nini Abdul Sykes ilikuwa lazima akae pembeni.

Sababu ya kwanza ilikuwa dini.

Mchakato wa kumtafuta kiongozi wa TAA kisha iundwe TANU ulianza 1951 baada ya viongozi wa TAA kupewa uhamisho kutoka Dar es Salaam kwenda majimboni.

Dr. Vedasto Kyaruzi aliyekuwa President wa TAA aliondolewa Dar-es-Salaam kwenda Kingolwira Prison kisha Nzega.

Hamza Mwapachu akapelekwa Nansio, Ukerewe.

Sababu ni kushiriki kwao katika Mapendekezo ya Katiba ambamo walidai uchaguzi katika wajumbe wa LEGCO na baada ya miaka 13 Waingereza waondoke watoe uhuru kwa Tanganyika.

Gavana Edward Francis Twining alighadhibishwa na haya mapendekezo ya TAA ndiyo akaamua sasa kuidhoofisha TAA kwa kuhamisha viongozi wake Dar-es-Salaam kuwapeleka mbali.

Abdul Sykes sasa akawa TAA Act. President na Secretary.

Earle Seaton aliyekuwa mshauri wa TAA katika mambo udhamini wa Tanganyika chini ya Waingereza akashauri kuwa TAA badala ya kupoteza nguvu kupambana na London wafungue mawasiliano moja kwa moja na UNO, New York kudai uhuru.

Abdul na Hamza Mwapachu wakaamua haraka atafutwe kiongozi iundwe TANU lakini kiongozi huyo lazima awe Mkristo.

Sababu ni kuwa haikutaka kuwepo na picha kuwa harakati zile ni za Waislam peke yao kwani wao ndiyo walikuwa wengi mstari wa mbele.

Abdul Sykes alianza mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia achukue uongozi wa TAA kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze mapambano ya kudai uhuru.

Chief Kidaha hakuafiki na hili na zilikuwapo sababu za msingi.

Alipotokea Nyerere mwaka wa 1952 ikawa imepatikana nafasi mpya.

Nyerere kwa sifa zilezile laiti angekuwa Muislam asingepewa uongozi wa TAA.

Iilikuwa fikra ya Hamza Mwapachu kuwa Tanganyika iingie katika kudai uhuru ikiwa na umoja vinginevyo Waingereza wangewashawishi Wakristo kuunda chama kipingane na TANU iliyojaa Waislam.

India iliingia katika kudai uhuru nchi ikiwa imegawanyika kati ya Wahindu na Waislam; na matokeo yake yanafahamika baada ya uhuru kupatikana.

Hii ndiyo sababu kubwa Julius Nyerere akapewa uongozi ili upatikane umoja wa wananchi.

Pili Nyerere kwa wakati ule alikuwa na elimu kubwa na kwa TAA kuongozwa na mtu kama yeye hilo ndilo lililokuwa likitafutwa.
 
Lakini Mzee Saidi.

Ni kwanini mlimfukuza Mwarabu Zanzibar?

Na mnampigania aje Tanganyika.
Kwanini hamu mpiganii arudi Zanzibar aendeleze Uislamu na Misikiti?

Si Nendeni hapo tu Dubai muka muombe radhi kwa dhuluma mliyomfanyia.

Nyinyi Wazanzibari ndio mliomfukuza Mwarabu kwa risasi. mliwaua hadi Waarabu wasio na hatia. Waliokuwa wanatoka Shambani kwao kulima na kuvuna mazao yao.

Kwa mujibu wa maneno yako, Mzee Saidi Muhammedi.

Sasa unataka sisi Watanganyika tuwasadieje ?

Katu Watanganyika hatujawahi kumdhalilisha Mwarabu.
Kwa namna yotote ile.

Malizeni tofauti zenu na Mwarabu na mumkaribishe tena hapo Zanzibar.

Furaha irudi tena.
 
Che...
Mimi sijamfukuza Mwarabu.
 


First, I state five premises I have extracted from Said’s paper; some are given verbatim, and others are imputed or paraphrased.

A) Authoritarian regimes generally distort national histories.
B) History is made not by one hero, but by a diversity of heroes.
C) Leaders in Africa fear heroes other than themselves.
D) Religion is a primary driver of social change.
E) Islam is a socially progressive religion while Christianity is not.
Second, I state the principal conclusions drawn by Said.
A) Muslims, not Christians, liberated Tanzania from colonial rule.
B) Muslim activists have been written out of the official history.
C) The welfare of the Muslims in Tanzania has been sorely neglected.
D) The religious divide propels the socio-political affairs in Tanzania.
E) Muslims no longer love and respect Nyerere the way they did earlier.
Mzee hapo unaonyesha udini wako, na mnapenda kulialia wakati hamna mipango endelevu kwenye elimu na afya kwa taasisi zenu!
 
Nyioku....
Sijui "lialia," kwa kejeli hii unakusudia kitu gani?

Hili la udini sijui linaingiaje.

Iweje tuwe na mipango ya kuunda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya 1933 na.TANU 1954 na 1962 tuitishe Muslim Congress na kuja na mapango wa elimu tuwe leo hatuna mipango ya elimu.

Tungewezaje kutaka kujenga Chuo Kikuu 1968 sababu iliyopelekea kupigwa marufuku EAMWS?

Ingekuwa hatuna mipango tungejuaje dhulma dhidi ya vijana wa Kiislam ndani ya Wizara ya Elimu?

Tungejuaje hujuma dhidi ya shule za Kiislam zilizokuwa zikifanywa na NECTA?

Hapa nani mdini?

Hakika anaedhulumiwa hawezi kuwa mdini.
 
Utahoji vipi hali ya Waislamu katikati tanganyika wakati taifa halina dini. Kufukuzwa walipaswa wangetaka mambo ya Uislamu wangeenda jenga nyumba Makka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utahoji vipi hali ya Waislamu katikati tanganyika wakati taifa halina dini. Kufukuzwa walipaswa wangetaka mambo ya Uislamu wangeenda jenga nyumba Makka

Sent using Jamii Forums mobile app
Edwayne,
Ikiwa imani moja inahodhi serikali kwa mathalan 80% wako wengi, serikalini, bungeni, fursa za elimu ya juu nk.

Wengine ni minority kila sehemu hii itakuwaje?

Hawa 80% bila shaka ndiyo watakaokuwa na nguvu ya maamuzi na imani yao itatawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…