Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Brother MS et al,

  1. Utafiti (wa ukweli) au ule utafiti (wa kivyako), SI lazima ukosolewe kwa utafiti....na pia SI lazima uandike kitabu ili ukosoe kitabu.....hizi ni FACTS
  2. Kufanya mihadhara Marekani au Ulaya haimaanishi kuwa maandishi yako ni legit...
  3. Mtafiti/Watafiti (wa ukweli) wanapokuwa challenged na maswali au wanapokosolewa.....hu-take their time kutafakari challenges zile na wakiweza hufafanua kile ambacho hakikueleweka au hurekebisha maandishi yake na kutoa toleo litalo-reflect masahihisho.
Kinyume cha hayo juu Brother MS umekuwa ukijigamba........na kuhadaa simple minds......JF ni kikomo.....ukidai unatoa darsa uwe tayari kutoa majibu.....na kutetea darsa/simulizi zako
 
Bw. Said hivi unajua kanuni za utafiti wa historia - the so called 'historical method'?
 
Bw. Said hivi unajua kanuni za utafiti wa historia - the so called 'historical method'?

MM,

Nami nakuuliza.

Mtafanya nini hii leo kuifuta historia hii niliyoandika?
Ile ya kutia moto magazeti haikusaidia sana.

Unadhani haya maswali katika JF itasaidia kitu?

Mohamed
 

Ogah,

Acha maskhara bwana.
JF hapawezi kuwa kikomo.

Sijakuhadthia wasomi walionitoa jasho lakini mwisho nimetoka kichwa juu.
Iko siku nitakupa maelezo hayo.

Mie huchangamsha mijadala si utani hivyo.
Tofauti ya wao ni nyinyi ni kuwa wenzenu hawatukani wala hawakasiriki niliposimama pale naona notebooks tu zinageuzwa kurasa.

Mwisho diners, lunches kutaka kujua mengi.

By the way nimeletewa nyaraka "Tanganyika Intelligence Report" kutoka Rhodes House.
Baada ya miaka 50 nyaraka za siri zinakuwa wazi.

Hizi nyaraka wameniletea rafiki zangu mabingwa wa African History and Islam.
Hii ndiyo faida na manufaa ya kuandika. Watu wanakujua na mnabadilishana taarifa, nyaraka na vitabu.

Utastarehe na nafsi yako ukizisoma...ndani kajaa Abdu Sykes na TAA yake, 1950 yumo Mashado Plantan na gazeti lake la Zuhra...hawa wakiitwa "wachochezi."

Basi kweli historia hii yote tuiache?

Insha Allah nitakuwekeeni zile sehemu muhimu.

Nilimbandikia moja Mag3 hakuthubutu hata kuifanyia "comment.

Mohamed
 
MM,

Nami nakuuliza.

Mtafanya nini hii leo kuifuta historia hii niliyoandika?
Ile ya kutia moto magazeti haikusaidia sana.

Unadhani haya maswali katika JF itasaidia kitu?

Mohamed

Mimi MS sikuelewi kabisa, kama JF si chochote si lolote ni nini kilikutuma ulete makala zako humu wakati unajua humu hakusaidii kitu? Pia nahisi hukudhani wala hukujua kama Moderator ataigandisha (Sticky) hii mada na kupata SAI (Challenge) kubwa kiasi hiki. Nadhani kwa mara ya kwanza katika maisha yako ya kutoa mada hii umekutana na kizingiti ambacho hukukitarajia.

Nikupe ushauri rahisi kwenye kutambua mambo. Mwanamke akienda kwa wanaume kuwaelezea shida, karaha, au raha anazopata mwanamke kwa kubeba mimba bila shaka kila atakachosema hata kama hao wanaume hawakiamini itabidi wakubali kwani anayesema ni mwanamke tena ameshawahi kubeba mimba. Lakini mwanamke huyo huyo akienda kwa wanawake wenzake lazima kuna vitu atabishiwa na kukosolewa.

Wewe wanaokupigia makofi na kukusifia ni wazungu au aghalabu ni "wenzio" katika mkakati ule ule wa uchochezi wa kidini. Sisi watanzania wenzio huwezi kutuambia Nyerere alikuwa "dikteta" au "Mbaguzi wa kidini" bila ya kukuuliza maswali alikuwa dikteta na mbaguzi kidini kivipi.

Siyo kwamba tunakana kwamba hao wazee wako hawakuwepo bali tunachokataa ni kwamba wao walibaguliwa kwa misingi ya dini zao!! HIvi Kiwete hakusoma kwenye shule za Misheni, au Dada yake si alisoma Ashira zama hizo inamilikiwa na kanisa, wote hao uislamu wao mbona haukuwazuia kusoma kwenye hizo shule. Na walilazimishwa kubadili dini? Nenda kawaulize wangali hai siyo ungojee wafe ndiyo uibukie kudai madai yasiyo na mshiko!!


UMEBANWA huwezi KUJIKURUPUSHA!!
 

Mr Right,

Hawa jamaa wameumia vibaya sana.
Hawakutegemea kuwa tulikuwa na mashujaa wetu.

Vipi utamtoa Sheikh Yusuf Badi na mwanafunzi wake Yusuf Chembera katika harakati Southern Province?
Hotuba ya kupokea uhuru kaiandika Sheikh Yusuf Badi ikasomwa na Yusuf Chembera...

Mie nishawarejesha katika historia hawawezi kutolewa kamwa hadi kiama kisimame.

Utapata nao sana tabu.
Ni mkuki katika mioyo yao.

Sanamu yao walioijenga miaka na miaka imeporomoshwa na mvua ya mawe.
Hawajui vipi wataijenga upya.

Batil siku zote ni yenye kutoweka tu...

Mohamed
 
MM,Unadhani haya maswali katika JF itasaidia kitu?Mohamed
Pole Mohamed inaonekana maswali yanakuuma sana, lakini ulipoleta mada hapa ulitegmea nini? watu wakae kwenye gogo na majamvi wakusikilize ukimaliza wasimame wakupigie makofi na kusema sheikh kazi yako tumeiona, mashaalah mwenyezi akujaze heri huku wakibusu mikono yako! hapana hapa si mahali pake, hapa hoja ndiyo inayoheshimiwa. Na maswali yetu hayana dhamira ya kufuta historia au simulizi na tamthilia zozote, hata maigizo ya Pwagu na Pwaguzi bado kumbu kumbu zake zipo na hakuna takayezifuta sembuse kitabu chako kinachosomwa Uchina, Baharain, Saudia Arabia n.k.

Hili la maswali hutalikwepa, tutakuuliza maana ni kutokana na kitabu chako wengine tulichonunua, hatukufanya hivyo kuangalia picha au herufi au jinsi gani mtu anaweza kumtukana Nyerere kwa soksi zake na vitoweo, tulitaka kuelewa. Kwa bahati mbaya hatukuelewa au kuna contradictions nyingi zinazovuruga mtitiriko wa usomaji. Pia kuna hoja zinazokinzana ndani ya kitabu chako kama si ukweli wa kile tunachokijua.
Ni kwa mukatadha huo, hutakwepa mwaswalii yetu na bado yapo yanayokuja. Tunafahamu kuwa maswali yanaharibu ka credibility kaliko baki lakini hatuna jinsi hadi pale utakaoyajibu ili kuonyesha unguli na usomi, ueledi na uerevu wa kutetea masimulizi uliyoandika mwenyewe.

Kwa kiasi gani maswali na hoja yanaharibu heshima yako hiyo si muhimu zaidi ya namna gani unaharibu heshima za wengine na kuwawekea maneno midomoni wenzetu waliotangulia mbele yake(marhum) ili ujenge hoja.

Jibu maswali na hoja ujisafishe, hoja ya 'kaandikeni vitabu au mimi ninakwenda ulaya n.k' hazikidhi viwango vya kisomi na zinazidi kuteremesha hadhi ya mandiko yako. Lakini pia kukaa kimya inaweza kupunguza 'uharibifu' unaojijengea. Dunia haiwezi kuwasiliana kwa kila mtu kuandika kitabu, labda ukienda Cambridge mtafute mtaalamu wa saikolojia ili akueleze kwa undani ukweli wa suala hili.

Si ajabu utakutana na maswali yetu kwa hao wanaotoka ulaya kuja kukutafuta, ni suala la muda tu. Dunia ya leo ni kijiji.
 


By the way nimeletewa nyaraka "Tanganyika Intelligence Report" kutoka Rhodes House.
Baada ya miaka 50 nyaraka za siri zinakuwa wazi.


Mohamed

Mohamed hivi si ni ndiyo hawa ambao kila mara kwenye maandiko yako unawataja kama ndiyo walikuwa wanawapendelea wakristo kwenye mambo mbalimbali, leo iweje nyaraka zao ziwe lulu ya kuaminika? Mitizamo yao kuhusu Tanganyika ya wakati huo unaiunga mkono. Halafu mbona unaongea kama vile hizo nyaraka ni kitu maalumu sana mwingine hawezi kuzipata??!!
 

Kigarama,
Ntakujibu moja tu.

Kilichonituma ni kuiweka wazi historia ya kweli ya TANU.
Fatilia darsa zangu yote utayasoma na utakuwa umepata majibu ya maswali yako.

Subra ni muhimu sana.

Mohamed


Mohamed
 

Hahahaha, darsa limewaingia na JF haisaidii kufuta historia inazidi kufanya darsa linoge. Unabadili badili maneno, sivyema hivyo, hivi ukibadili maneno ndio ukweli utafutika?

Abdul Wahid Sykes kampokea Nyerere, Mshume Kiyate kampa "reshen" ya chakula, Dossa Aziz katumia mali zake, Hassan Bin Ameir katumia umaarufu wake kuinyanyuwa TANU, hata jina la TANU limetolewa na kina Sykes, jee kuna ubishi hapo?
 

Nyaraka zao zisome ukipenda ziamini hukupenda usiziamni, umeambiwa zipo na zimesheheni Abdul Wahid Sykes, sasa hilo nalo hulikubali?
 

Mbona unapenda kleta pumba zisizo na mpango? lete facts, Abdul Wahid alimpokea Nyerere hakumpokea?

Kuhusu dunia ya leo kuwa ni kijiji umesema vyema sana, kwanini hao wa Ulaya wasije kuwatafuta nyinyi wamtafute Mohamed Said?

Hivi wewe ushawahi kuchapisha japo insha kwenye gazeti? wacha kupeleka "mapepaz" na kualikwa vyuo vikuu kuongolea ulijuwalo?
 

Kigarama,

Nyaraka nilizonazo mie hazipo kokote hebu chungulia hapo chini:

"Aliniruhusunisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo zaukoo wa Sykes. Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani yasefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini. Nikiyapitiamajalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu nakila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ulewa harakati. Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli tokakwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo(Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwaAlly Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru;nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabethiliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa RaisAbdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, MwekaHazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwakutawazwa; barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukobakwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa;barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere,Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho. Baadaye nilipofnyautafiti kuhusu maisha ya baba yake, Kleist Sykes, nilikuja kufahamu kwambatabia hii ilirithiwa kutoka kwa baba yake ambae alikuwa akiweka ndani ya jaladakila kipande cha karatasi kilichokuwa na habari iliyostahili kukumbukwa. Nijambo la kuhuzunisha kwamba sikuweza kupewa shajara za Abdulwahid ambazonilielezwa kwamba baadhi ziko katika hati-mkato na hadi leo hazijafasiriwa.Shajara hizi nimezioana kwa macho yangu lakini kwa kukosa idhini sikuwezakuzifungua na kuzisoma. Vilevile vilevile sikuweza kupata kumbukumbu halisi zaVita Kuu ya Kwanza zilizoandikwa na Kleist Sykes kwa mkono wake mwenyewe.Hapana shaka yoyote kwamba nyaraka hizi ni hazina zenye thamani isiyo na mfanowake. Ni matumaini yangu kwamba siku moja nchi yetu itakubali na kuthaminimchango wa Abdulwahid katika taifa la Tanzania na nyaraka hizi kama kielelezocha harakati dhidi ya ukoloni, zitakubalika na zitawekwa chini ya hifadhi yaNyaraka za Taifa kwa faida ya vizazi vijavyo."

Nina nyaraka za Tewa Said Tewa, Sheikh Hasan bin Amir, Bilal Rehani Waikela, Yusuf Chembera, Mashado Plantan...hao wote walikuwa TAA na waasisi wa TANU.

Katika nyaraka hizo ambazo sijazisoma ni shajara (diaries) za Abdulwahid Sykes...

Mohamed
 

Kizingiti ni nani? Kigarama? ambae alileta nyuzi huko kwingine "nikaisambaratisha" within 2 days, akawa hana cha kuongezea? unanchekesha!
 



Nguruvi 3

Nitakujibu moja.
Hilo la heshima wala usiliguse hata kidogo.

Mie kwenye maulid nikitokea kuleeeee...nakimbiliwa nawekwa beneti na kinara.
Nagusana mbavu na masheikh siwezi hata kubeba viatu vyao.

Uliza.

Ningekuwa naumizwa na maswali saa hizi nishasomewa Khitma.
Maswali ndiyo shughuli yenyewe.

Utakuwa mvuvi uogope kulowa?


Mohamed
 
Mohamed,
Nilikuwa napitia makabrasha nikaingia katika sub-folder iliyokuwa na maswali kadhaa, kwa uchache tusaidie haya

1. Kwa vile Bakwata iliundwa na serikali na kukataliwa na waislam, je kwa sasa chombo gani kinaweza kusema kinasimamia masilahi ya waislam?

2. Kwa vile mabucha ya nguruwe yalimilikiwa na 'christiantraders , je bar kama ile ya macheni inamilikiwa na Muslimtraders!

3. Kwa vile Tewa alikubali kwenda China kama balozi na kuacha EAMWS iangamie, huyu ni shujaa au msaliti.

Tutaendelea kidogo kidogo mzee wangu.
 
Ni 'dikteta' Nyerere anayevaa soksi ndeefu! ndiye aliyejenga shule ya Kibaha ambayo rais wa nchi hii amesomea. Sijui Nyerere alisahauje kuwa ni mwislam maana angeondoa jina lake ASAP.

Wapo waliopeleka watoto wao kupata elimu ilikopatikana, Mohamed anawashauri wazee na kusifia kuwa bora hawakupeleka watoto wao kwenye shule za makanisa( jambo jema kama ana mbadala), kinachoshangaza yeye asubuhi na mapema anapanda ndege kwenda Marekani na Ulaya kutoa mihadhara kwenye vyuo vya kanisa na sio Saudia, Bharain, Syria au Yemen.

Wakati Mohamed, anasema lugha ya kiingireza inapanda kwake hadi kumuumbua afisa mhusika, akirudi nyumbani anashauri wenzake wafundishe watoto wao Irab za kiarabu!

Wakati Mohamed anakwenda shule kufuatilia maendeleo ya mwanae na kuona kadhulumiwa na mwalimu asiye na dini(hakusema ana dini gani) mwalimu mkuu akabadili maksi(mwl mkuu hakumtaja dini). Mohamed hajaenda Kilwa kufanya utafiti kwanini sekondari ifungwe kwa kukosa wanafunzi!
 
Kigarama,

Nyaraka nilizonazo mie hazipo kokote hebu chungulia hapo chini:

Mohamed

Usipotoshe Mambo Mohamed, mimi sihoji hizo sajara na nyaraka za wazee wako. Nasema kuhusu"Tanganyika Intelligence Report" ambazo zimetolewa na wale unaowashutumu kuusimika "mfumo kristu" Tanganyika. Jee nyaraka zao unaziamini kwa kuwa zimemtaja Abdluwahid sykes?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…