Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nguruvi3
Nilipata tabu kuweka kitu nadhani hiyo mistari ilikuwa inakorofisha nikaweka hii kwa FF sasa naiweka kwako uwaone wazee wangu walivyokuwa na ari ya maendeleo. Juzi wametoa mitaa na majengo kuipa majina ya wazalendo na waliosaidia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wazee wangu wamesahauliwa tena. Iko list ya waliochangia chuo Insha Allah nikiipata nitaimwaga hapa jamvini:

"Salum Matimbwa anaingia katika historia ya ukombozi wa Tanganyika si tu kama mwanachama wa awali waliojiunga na TANU kabla ya 1958 bali kama mmoja wa wazalendo waliochanga fedha kuanzisha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Fikrra ya kuanzisha Chuo Kikuu inasemekana ilianza na Nyerere akiwa na Dossa. Ilkuwa kawaida ya Dossa baada ya mikutano ya TANU pale Mnazi Mmoja kumchukua Nyerere na gari lake kumrudisha Pugu. Njia ya zamani kwenda Pugu ilikuwa inapita hapo kilipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Sasa ilikuwa kiza kimeingia na walitaka kutoka nje ya gari kuangalia mandhari ya Dar es Salaam maana kutokea pale mji ulikuwa unapendeza sana kwa taa zilizokuwa zikiwaka barabarani. Nyerere alimwambia Dossa, "Dossa tukipata uhuru wetu hapa lazima tujenge Chuo Kikuu."Hili wazo lilifanyiwa kazi na wananchi wakahamasishwa kuchangia ujenzi wa Chuo hicho. Fedha zilichangwa na Chuo kikajengwa pale New Street kwenye kiwanja cha John Rupia alichokitoa kuwapa TANU. Hapo ndipo kilipoanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. (Chuo hiki sasa ni Chuo Cha Watu Wazima).Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo y ash. 50.00 stakabadhi ambayo ina saini ya Bhoke Munanka."

Mohamed
 
Sidhani kama nimesema hivyo.

Ila itoshe tu kusema nchi hii kama zilivyo nchi zingine ina historia pana na ina mengi sana yasiyo wazi kwa wengi, kwa sie tunaopenda kujifunza ni afya kwetu kupata vingi iwezekanavyo.

Butola,
Hata mimi sijasema kwamba ndivyo ulivyosema.
Kwakuwa na mimi najifunza yale yaliyokuwa yamefichika katika historia ya ukombozi wa nchi yetu ndo nikataka kujua ulichojifunza kwa martin shikuku.
 
Samahani kwa kukuchekesha tena. Lakini ungeandika "unanichekesha" kuna "i" inakosekana hapo.

Kwetu Kariakoo, kiswahili nimezaliwa nacho, mtoto wa kike kukaza mdomo ndio nini? turejee kwenye mada. Usinkasirishe!
 

Masanja,

..asante.

..uliyosema ni kweli. LIGI za udini hazina maslahi kwa taifa.​

 
Kweli, Bibie, Kiswahili kinanipa taabu. Mimi ni wakuja.
 
Mohammed,
Nisahihishe kama nimekosea. Katika toleo la kwanza la kitabu chako cha "Life and times of Abdulwahid Sykes" version ya Kiingereza, uliandika kuwa kura tatu zilikuwa zinalenga kuwabagua Waislamu. Baadaye nikashtuka umeandika kitabu au makala nyingine na kuita kura tatu "uamuzi wa busara." Je, unaweza kukiri hapa kwamba ulikosea kuita uamuzi wa kura tatu kuwa ulikuwa ni kuwabagua Waislamu, na ni lini ulipogundua kuwa kumbe uamuzi wa kura tatu Tabora ulikuwa ni uamuzi wa busara?
 
Butola,
Hata mimi sijasema kwamba ndivyo ulivyosema.
Kwakuwa na mimi najifunza yale yaliyokuwa yamefichika katika historia ya ukombozi wa nchi yetu ndo nikataka kujua ulichojifunza kwa martin shikuku.

Kwa ajili ya mada iliyo mbele yetu, ebu hili tuliache kwa sasa..
 
--------------------

Jasusi,

Walichokuwa wanakitafuta Waingereza ni kutia mjiti katika ya Waislam na Wakristo ili ipatikane farka. Waislam wangelikataa kushiriki katika uchaguzi ule chama kingemeguka na Nyerere angepwelewa.

Sasa hapa kigetoka chama kingine ambacho kingeingia katika kura tatu na chama hiki kingelikuwa na Wakristo kwani Waislam wangelibaki wengi katika TANU.

Hili lingetendeka lingevuruga mstakbali wa nchi yetu kabisa.

Kwa wazee wetu kukubali TANU iwalete watu kutoka nje kuja kusimama kuingia katika Legco na Waislam wabaki nje ya chombo hicho ilikuwa busara kwa maana kuwa ile farka iliepukwa na wananchi wakabaki wamoja. Angalia chini hapa:
"Mkutano ule ulitishia kuigawa TANU katikakambi mbili hasimu. Kambi moja ni ile ya wenye siasa za wastani waliopendeleakushiriki katika uchaguzi na ile ya pili ni ile ya wenye msimamo mkaliwaliotaka uchaguzi ususiwe kabisa. TANU ilinusurika na kile ambacho kingewezakuwa mgogoro ndani ya chama ambao ungewafanya wale wenye msimamo mkali kamaSheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU katika makaomakuu, na Zuberi Mtemvu, wakati huo katibu mwenezi wa TANU, kufanya mapinduziambayo yangekigawa chama kama isingelikuwa busara ya Julius Nyerere, Rais waTANU."

Mohamed
 
Kwetu Kariakoo, kiswahili nimezaliwa nacho, mtoto wa kike kukaza mdomo ndio nini? turejee kwenye mada. Usinkasirishe!

Mmmh! Makubwa! Haya ngoja tuendelee kuwasoma wanahistoria wetu haya ya kuzaliwa kariakoo na kukaza midomo hayana tija...
 

Wanaukumbi,

Kuna uzi niliambiwa kuwa mimi sijui chochote kuhusu Sablak na wenzake wa huko Meru. Nikamwaga hapa jamvini habari za Abdulwahid Sykes na Sablak kama nilvyosoma katika nyaraza za marehemu Abdu na Tanzania National Archives. Ninachosikitika ndugu zangu ni ukimya wenu.

Jamani kuweni na huruma kwani mcheza kwao hutunzwa. Hivi imekushindeni hata kusema, "Mkuu Mohamed tumekosoma." Vibaya hivyo ndugu zanguni. Nipeni motisha kidogo.

Hilo kama hamliwezi basi nipeni mji au niruhusini nitoe salam.

Mohamed

PS: Kuna mwingine akaja na Nyerere kuandika katiba nikamwaga data. Katiba ya TANU wazee wamenyanyambua ya Nkrumah. Kimya! Sisikii kitu.
MS
 
Hili la "kutuma salamu" nimelipenda....Mkuu,haya salimia ndugu wa upande ule (kama wanavyopenda kusema wenyewe)
 
Mohmed said ni activist wa mkoa wa dar es-saalam
Mohamedd Said ni Mwanahistori wa mkoa wa dar-s esalaam



Niimemuuliza swali dogo tu kuhusu maoni yake juu mwalimu nyerere kuridhia ushauri wa wataalam na kuhamishia makao makuu dodoma. Akasema hana jibu wala maoni. from that u can sense kuwa hata makao Makuu yangekuwa yemshahamia dodoma basi Mohamed said labda agetafuta namna ya kuonyesha kuwa hiyo ilikuwa ni janja ya nyerere kubadilsiah historia ya Darau kuifini dar na wanadaresalaama sababu ya chuki yake kwa wazee wa dar.


Hili nalo la Dodoma ni sehemu ya mambo ya historia na issue Zilizoanza Chini ya Nyerere .Je lilikuwa jema au baya.? Ebu tupate majibu Mohamed Saidi acha kukwepa kwepa
.
 
Nguruvi3
.Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo ya sh. 50.00 stakabadhi ambayo ina saini ya Bhoke Munanka."

Mohamed
Tangu jana nimekuwa nafuatilia mjadala huu bila ya kuchangia chochote kile lakini huku nikitafakari ni nini hasa hoja ya MS. Jee MS anaamini kwamba wazee wake pekee wa Gerezani wengeweza kuikomboa nchi hii bila ya Watanganyika wa majimbo mengine kushiriki? Ms anataka tuamini hao wazee wake wa Gerezani wote ni wazaliwa wa Gerezani tangu kuumbwa kwa dunia na hawajatokea bara kama vile wamanyema, wanubi, na wanyamwezi ambao walikuwa ni wapagazi wa wajerumani?

Nilirudi kwenye mada. Hapo kwenye nyekundu kuna swali ndugu yangu MS nataka kukuuliza. Umesema Abdalah Salum alikuwa ni "mmoja" wa wachangiaji, hiyo haimaanisha kwamba kulikuwa na wachangiaji wengi waliochangia ujenzi wa Chuo Kikuu Cha kwanza? Na swali la pili ni kama mchango wa sh. 50.00 ambao risiti yake bwana Salum Matimbwa ameihifadhi hadi leo ilikuwa ni asilimia ngapi ya gharama zote za ujenzi wa Chuo kikuu cha kwanza pale Lumumba? Kama unaweza kutuwekea sisi watu wakuja BOQ ya ujenzi wa jengo zima utatusaidia zaidi.
 
M Said wewe mwaga historia ya wazee wako,sisi tutachambua tunapoona au tunapohisi kuna a grain of truth,hili la katiba ya TANU kubanduliwa kwa Nkurumah ni news kubwa kwa wengi wetu
 
K
Mkuu bwana MS ukiacha swala la katiba kkuwa hakuandika mzee nyerere lakini pia ktk kumbukumbu zako zinaonyesha pia hata ile hotuba iliosomwa umoja wa mataifa na mwalimu nyerere pia hakuiandika yeye naomba utuweke sawa katika hilo.ili tuzidi kuiweka sawa historia iliosahaulika kutajwa.
 

Shadhuly,

Hiyo nimeiweka kama saa moja iliyopita na nikaeleza kuwa document hiyo sasa haipatikani Maktaba ya CCM wala National Archives. Mimi kote nimepita huko kuitafuta.

Hebu zidurusu hizi nyuzi zangu utaikuta.

Mohamed
 

Kigarama,

Niruhusu hili la kwanza kukujibu niandike Kingereza maneno machache.

"You are missing the point. It is not the value but the thought behind."

Hela alizotoa Mzee Saluma Matimbwa ni kiasi kidogo sana. Wala mimi
sikuandika yale kwa kufaharisha thamani. Hata kidogo.

Nia na madhumuni ilikuwa kuonysha ari ya wazee wangu katika kila
jambo lililokusudiwa kuleta maendeleo ya Mwafrika.

Safari ya Nyerere UNO Bantu Group na akina Tatu bint Mzee, Kidawa Bint
Abdallah walikuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuchangishana thumni,
thumni. Hii ndiyo ilikuwa "spirit ya TANU."

Wazee wa Gerezani peke yao kamwe wasingeweza kufika popote bila ya
kuungwa mkono na Watanganyika wote.

Hili wazee wakilijua zamani na fika na ndiyo maana kuanzia 1950 Abdu
alikuwa akimshawishi Chifu Kidaha Makwaia aingie TAA wampe urais kwa
kuzingatia kuwa Chifu Kidaha akija TAA Wasukuma watamfuata kiongozi
wao na TAA itapata nguvu.

Hilo lingetendeka wangeliunda TANU na Chifu Kidaha angekuwa rais wa
TANU. Chifu Kidaha aliona yeye maslahi yake yapo zaidi na Waingereza.

Chief Kidaha alikuwa "diner" nyingi nyumbani kwa Abdulwahid lakini kila
Abdu alipomgusia hili hakufua dafu hadi alipokutana na Nyerere 1952.

Hebu staladhi na hiki kijembe cha Nyerere kwa Chifu Kidaha kwenye hafla
moja ya taarab Mtaa wa Mvita mwaka wa 1957:

"Katikahafla hiyo waheshimiwa, wageni waalikwa walipewa vitafunio, vinywaji baridi nachai. Nyerere katika kutoa shukrani kwa wanachama wa TANU alikamata kikombe chachai na kukionyesha juu kwa wasikilizaji wake. Aliwaambia watu kwamba wasidhanikitendo cha kumpa mtu kikombe cha chai ni kitu kidogo. Nyerere aliendeleakusema kuwa watu wameiuza nchi hii kwa kupewa kikombe cha chai na wakoloni.Nyerere alikuwa akitoa maneno hayo akiwa anawapigia vijembe watu maalum.Nyerere kwa maneno yake alikuwaakiwakusudia machifu. Baadhi yao walikuwa pale pale katika meza kuu wakinywachai na yeye. Wakati huo baadhi ya machifu walikuwa wakishirikiana na GavanaTwining na UTP katika hila za kuipiga vita TANU ishindwe kuikomboa Tanganyikakutoka makucha ya ukoloni. Ilikuwa dhahiri kuwa makombo waliyokuwa wakipatamachifu kutoka kwa Mwingereza hayakuwa hata na thamani ya kikombe cha chai.Maneno ya Nyerere hayakuwa fumbo kwa wale machifu. Yalikuwa maneno ya waziambayo waliyaelewa. Machifu walitambua kuwa wao ndiyo walikuwa wakisemwa katikahotuba ile ya shukurani. Lakini kijembe kile kwa hakika yake kilikuwakimeelekezwa kwa Chifu Kidaha. Chifu Kidaha alikuwa na bahati mbaya sana.Abdulwahid Sykes miaka michache nyuma alimbembeleza sana ajiunge na TAAwamfanye rais kisha waje kuunda TANU na yeye wamchague kuwa rais lakinialikataa."

Mohamed
 
Hili la "kutuma salamu" nimelipenda....Mkuu,haya salimia ndugu wa upande ule (kama wanavyopenda kusema wenyewe)

Kwanza salamu zangu ndugu mtangazaji napenda kuzituma kwa Sanda Matuta na wana ukumbi wote!

Mohamed
 
Kigarama, nashukuru sana maana nimeandika kitu kama hiki katika makala ya Mohamed Said ile inayoendelea thread nyingine.

Nimehoji kuwa ni vema kama Matimbwa alitoa mchango huo na tunauthamini sana, lakini kwa bahati mbaya kama ilivyo ada ya Mzee Said pesa hizo sio hoja, hoja ni kuinasibisha na jina la Salum na wala si Matimbwa, hapo unajua kinaendelea nini.
Katika makala zake Mohamed amemtaja John Rupia kama mtu aliyetoa kiwanja cha ujenzi, lakini huwezi kumsikia John akitajwa kwasababu ni John. Hapo ndipo tunapohoji sana makala za Mohamed na 'Biasness'.

Ukitaka kuona mkanganyiko zaidi, ni pale Mohamed Said anaposema hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na Sykes na kufanyiwa editing Mzumbe kabla hajaenda nayo UNO. Hili laweza kuwa ni kweli lakini linazaa maswali mengine. Nyerere alipofika Dar alikuwa ni msomi mzuri tu aliyehitimu Makerere na Edimburgh. Inaingia akilini zaidi kuwa ufahamu wake wa mambo ya kimataifa ulikuwa mkubwa sana kuliko wenzake wengi.

Labda ingeandikwa kuwa hotuba iliandikwa kwa ushirikiano wa abc ningeelewa zaidi. Sidhani Nyerere alikuwa mtu wa kuandikiwa hotuba aende akaisome tu bila ye yeye kuwa na ushiriki wa kujua nini anaenda kuongelea.

Na kuthibitisha kuwa hotuba iliandikwa kwa ushirikiano naomba nimnukuu mzee Said '........Sykes aliandika na kuituma kwa basi Mzumbe na kisha kurudishwa kwakwe.....' Sasa kama aliandika na ikafanyiwa edit Mzumbe ni wazi kulikuwa na ushirikiano wake na wenzake, ushirikiano ambao nadhani ulimgusa aliyetakiwa kwenda kutoa hotuba UNO.

Hii haina maana Sykes hakuandika au hakuna nakala ya hotuba! maana yake halisi na anachotaka kusema Mohamed ni kuendelea kumdhalilisha Nyerere kama alivyowahi kusema ' wazee walimjua Nyerere wakati akiwa si lolote si chochote' na pia ' ......Kiyate akampa pesa za kwenda kariakoo kununua mboga n.k.

Ukisoma makala za mzee Said sehemu inayomhusu Nyerere inanasibishwa sana na ubaya. In short, his intention is to potray the negative image about Mwalimu, despise him, above all to make Nyerere as public enemy number one. Mohamed hates Nyerere to the core.
Mzee Said strives to make his grievance as a 'public issue'.
As long as you stand to correct the history, the same will correct you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…