Monstgala
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 1,079
- 1,036
Kwenye nyekundu ungeandika "ladha". Unanchekesha.
Samahani kwa kukuchekesha tena. Lakini ungeandika "unanichekesha" kuna "i" inakosekana hapo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye nyekundu ungeandika "ladha". Unanchekesha.
Nguruvi3[TABLE="width: 100%, align: left"]
[TR]
[TD="class: kaziBody"]By ALVAR MWAKYUSA, 20th October 2011 DAILY NEWS
The two leaders showered praise on the varsity for producing professionals who have played significant leadership roles in their countries.
They made the remarks when addressing delegates in Dar es Salaam on Thursday at the climax of the 50th anniversary of the university.
"I acknowledge the role played by UDSM in training key personnel for other countries in the East African region. A number of experts and graduates from this university have been recognized regionally and internationally," Mr Kikwete said.
His remarks were supported by President Museveni who mentioned some high-ranking people from his country, including himself, as graduates of the renowned university 'Hill'.
Mr Museveni mentioned former East African Community (EAC) Secretary General, Mr Amanya Mushenga, Uganda's Chief Justice Mr Benjamin Odoki as well as his wife who is also the Minister for Karamoja Affairs, Ms Janet Museveni.
"On the list of great people who studied here at the Hill, is Dr John Garang, the late Vice-President of Sudan," he noted.
Mr Museveni said most veteran lawyers in his country were trained at UDSM.
The Ugandan leader also spoke highly of Father of the Nation Mwalimu Julius Nyerere, for establishing a higher learning institution at a time when the region needed educated people.
Mr Museveni, who has been collecting funds in his country for the construction of a students' centre at UDSM, pledged to hand over the contribution to the varsity's authorities.
Meanwhile, the Father of the Nation, the late Mwalimu Nyerere, was among six people who were recognized for their contribution in setting up the university.
Others are Prof Robert Pratt, who was the first Principal of the then University College Dar es Salaam, Chief George Kunambi, who played a crucial role in locating the current site of UDSM.
Others are Justice Julie Manning (Rtd), the first and lone female student at inception, Dr Wilbard Chagula, the first indigenous Principal and Prof Arthur Weston who was the Dean of Law at the inception.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: kaziBody"]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD] My take: Rais Kikwete na Museveni wanasema kuwa UDSM imesaidia kutoa wahaitimu katika ukanda wa Afrika mashariki. Ninahakika aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kenya bw. Kivuitu naye pia ni mhitimu wa hapo.Watu wanaposema kuna nafasi za upendeleo ili kuminya waislam, mbona 'trend' inaonekana kuvuka mipaka?
Lakini kilichonisukuma zaidi kuleta hii habari ni hiyo kauli ya kwamba aliye locate eneo la ujenzi ni George Kunambi kwa mujibu wa UDSM
Mohamed Said anasema ni (Sykes au Dossa sikumbuki vema) aliye muonyesha mwalimu eneo hilo akimpeleka Pugu. Hapa pia historia inatakiwa kurekebishwa! ili tujue ukweli
Ufafanuzi mzee Said.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sidhani kama nimesema hivyo.
Ila itoshe tu kusema nchi hii kama zilivyo nchi zingine ina historia pana na ina mengi sana yasiyo wazi kwa wengi, kwa sie tunaopenda kujifunza ni afya kwetu kupata vingi iwezekanavyo.
Samahani kwa kukuchekesha tena. Lakini ungeandika "unanichekesha" kuna "i" inakosekana hapo.
Masanja said:Hii thread is one of my best have JF in recent years. INAFUNDISHA NA INATOA CHANGAMOTO. Nimejifunza na naendelea kujifunza sana kwa Mag3, Nguruvi, na muungwana Mohamed.
Ushauri wangu, kwa wananchi wenzangu, kamwe hatuwezi kuwa na mijadala endelevu kama hatutavua imani ya dini zetu. Kinachotukwamisha ni hiki. Tujitahidi sana kuheshimiana na tutafute suluhisho la matatizo yetu kama taifa. Umeme ukikosekana anayeathirika ni Hamisi, Said, Mwajuma, Peter, Selina nk. Tujitahidi sana kuepuka hizi emotions za udini. Siku zote nilisema kuna watu walicheza karata ya udini kwa maslahi binafsi lakini kwa uhakika walifungulia pandora`s box maana hawataweza kuuzima. In anycase it is by fate that we are a nation. Kwamba iko Siku TANZANIA inaweza kuwa nchi ya kiislam wote tukavaa kanzu. Never. Forget. Kwamba iko siku wote wataimba mapambio kanisani ya kilokole. Never. Forget it. Kikubwa tujifunze kuthaminiana na ku-celebrate tofauti zetu. Tutafute suluhisho la matatizo ya taifa letu. Kwa yeyote yule anayetaka historia imkumbuke hajachelewa bado. Tanzania kama taifa bado tunachangamoto nyingi sana. Toa mchango wako. WANANCHI tutauuona na tutakuenzi.
Swali kubwa kwetu naomba lisiwe nani alipigania uhuru. Bali tujiulize, kwa nini tulipigania uhuru? na tulipoupata tuliufanyia nini huo uhuru? je huo uhuru umetuletea nini? Mjadala kama huu ni mzuri usipokuwa na sentiments za kidini na kiimani.
Naamini kabisa taifa letu liko katika critical period na ni wasomi kama sisi wenye jukumu la kutafuta majibu ya matatizo yetu kwa kutumia elimu yetu kuliko kujenga chuki na na uhasama. Its unfortunate hizi chuki wengi wetu tunazijenga kwa maslahi binafsi. Sioni logic iko wapi ukafanye PhD Cambridge au kwingineko..halafu uje kuhubiri hapa watu wasome madrasa au mambo ya dini tuu. Its really a tragic. And this goes way far to show how the lites manipulates the poor for their own ends.
Ushauri wangu: tuwekeze katika elimu na mambo mengineyo yanayojenga ustawi wa binadamu. Yes, Iamni ni jambo muhimu sana, lakini tujitahidi kadri tuwezavyo kuwaachia wananchi/waumini wenyewe waamue ni jinsi gani ya kuabudu. Hii ya kujifanya kwamba we know what is good for entire 'we' si jambo la busara. Na ndo maana muungwana mmoja kasema hapo juu..nenda huko ulaya na America..watoto wa hao hao masultani na wafalme wanaolinda msikiti wa Mecca wanasoma top schools za ulimwengu wa leo..Harvard, Oxford, Yale, Princeton, Imperial, LSE, nk...na ndo kesho wanaenda kuwatawala wananchi wao....jamani imani ni muhimu lakini we shouldnt collectivise it. Kila mtu apewe uhuru wa kuwa yeye.
Watanzania tuamke, matatizo tuliyonayo ni mengi mno, dini inabidi liwe swala la mwisho kutufarakanisha.
Kweli, Bibie, Kiswahili kinanipa taabu. Mimi ni wakuja.Sasa hapo umeelewa nini? ni wazi kabisa hayo maneno "kaandika kuhusu TANU lakini hakuandika kuhusu walioianzisha" au na hilo ni tatizo kwako kulielewa?
"He/she wrote about TANU but he/she did not write about those who founded it..." maana naona kiswahili kinakupa taabu kuelewa.
Butola,
Hata mimi sijasema kwamba ndivyo ulivyosema.
Kwakuwa na mimi najifunza yale yaliyokuwa yamefichika katika historia ya ukombozi wa nchi yetu ndo nikataka kujua ulichojifunza kwa martin shikuku.
--------------------Mohammed,
Nisahihishe kama nimekosea. Katika toleo la kwanza la kitabu chako cha "Life and times of Abdulwahid Sykes" version ya Kiingereza, uliandika kuwa kura tatu zilikuwa zinalenga kuwabagua Waislamu. Baadaye nikashtuka umeandika kitabu au makala nyingine na kuita kura tatu "uamuzi wa busara." Je, unaweza kukiri hapa kwamba ulikosea kuita uamuzi wa kura tatu kuwa ulikuwa ni kuwabagua Waislamu, na ni lini ulipogundua kuwa kumbe uamuzi wa kura tatu Tabora ulikuwa ni uamuzi wa busara?
Kwetu Kariakoo, kiswahili nimezaliwa nacho, mtoto wa kike kukaza mdomo ndio nini? turejee kwenye mada. Usinkasirishe!
Kitu kimoja nilicho na hakika nacho kwa asilimia 100% ni kwamba wale wote wenye mapenzi ya kweli kwa taifa letu la Tanzania wanasita sana kuchangia hii hoja inayofinyangwafinyangwa na huyu anayejiita Mohamed Said. Bila kumung'unya maneno nayaita madai ya Mohamed Said la kutoa elimu ya historia ya kweli ni porojo hatari iliyojaa uchochezi ambayo lengo lake hasa ni kuleta uhasama wa kidini miongoni mwa wananchi. Sijui anachotegemea kufaidika nacho kwa kupanda hii mbegu ya hatari ambayo nina hakika mtu kama Mohamed Said anajua fika madhara yake.
Mohamed Said ni kama kipofu ambaye baada ya kusimuliwa na wazee kwamba tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengi anapata nafasi ya kumpapasa tembo. Kwa bahati mbaya anaupapasa mguu wa tembo na si mwili wote halafu katika imani yake anadai anao uwezo wa kutoa somo kuhusu umbo la mnyama tembo na ushuhuda wake, kuwa tembo ni kama gogo la mti mkubwa, ndio ukweli na anayesema tofauti hajui kitu. Watu wote wanaolalamikiwa na Mohamed Said kuwa walisahauliwa, wengi wao walikuwa wakazi wa Dar es Salaam eneo la Gerezani.
Kabla ya uhuru Tanganyika iligawanywa katika majimbo makuu manane na katika majimbo yote hayo, jimbo la pwani kwa ujumla lilikuwa moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma kimaendeleo kiuchumi, kielimu na kisiasa na hiyo ni licha ya kuwa makao makuu ya serikali ya kikoloni yalikuwa Dar es Salaam. TAA ilianzishwa na watumishi wa serikali (civil servants) na kwa wakati wote kazi kubwa ya TAA ilikuwa ni kulalamika ikidai haki ya wafanyakazi bila upendeleo na hasa ubaguzi wa rangi katila utumishi kubwa ukiwa uonevu dhidi ya wazawa, mtu mweusi.
Jimbo la Ziwa ni moja ya majimbo yaliyokuwa mbele kiuchumi, kielimu na kisiasa na kama kuna kitu kinaweza kudaiwa kuwa kilisahaulika katika harakati ya kupigania uhuru ni mchango wa Jimbo la Ziwa (Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) Jimbo la Ziwa ndilo lililoongoza kwa idadi ya watu, idadi ya makabila, idadi ya mali asili na idadi ya machifu ambao nafasi yao ilikuwa kubwa tu katika kuhamasisha watu. Moja wa watu ambao mchango wao nitautaja kidogo tu ingawa alifanya jitihada kubwa labda zaidi ya wazee wa Mohamed Said ni Paul "Kishamapanda" Bomani.
Historia ya harakati za uhuru ni zaidi ya porojo za Mohamed Said, watu walipigania uhuru kama Watanganyika na bila kubaguana kikabila, kidini wala kijinsia. Ndio maana mimi sitaki kabisa kuwa na majibizano na huyu Mohamed Said moja kwa moja ila kwa kuwa hoja ileletwa JF, akae tayari kupewa somo kuhusu umbile zima la mnyama tembo na sio mguu moja wa tembo alioupapasa. Hapa mimi nitaongea sana kuhusu mchango wa Jimbo la Ziwa na baadaye kuonyesha jinsi maadui wa nchi yetu wanavyowatumia kidini watu kama huyu Mohamed Said.
Baadaye nitaeleza jinsi Mkoa wa Mara yenye makabila karibu hamsini yalivyoweza kushirikiana bila mfarakano na kuitikia mwito wa Mwalimu Nyerere katika hizo harakati za kudai uhuru. Je mwamko wa wakazi wa jimbo la Ziwa ulikuwaje na mapokezi gani aliyapata kila wakati Mwalimu aliporudi kwenye hili jimbo ambalo idadi ya wakazi wake kwenye miaka ya 50s ilikuwa mara tatu ya majimbo mengi Tanganyika kama Pwani. Pia nitaonyesha ni wakati gani walianza kuyasikia hayo majina anayodai Mohamed Said ya wazee wa Gerezani Dar es Salaam !
Tangu jana nimekuwa nafuatilia mjadala huu bila ya kuchangia chochote kile lakini huku nikitafakari ni nini hasa hoja ya MS. Jee MS anaamini kwamba wazee wake pekee wa Gerezani wengeweza kuikomboa nchi hii bila ya Watanganyika wa majimbo mengine kushiriki? Ms anataka tuamini hao wazee wake wa Gerezani wote ni wazaliwa wa Gerezani tangu kuumbwa kwa dunia na hawajatokea bara kama vile wamanyema, wanubi, na wanyamwezi ambao walikuwa ni wapagazi wa wajerumani?Nguruvi3
.Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo ya sh. 50.00 stakabadhi ambayo ina saini ya Bhoke Munanka."
Mohamed
Wanaukumbi,
Kuna uzi niliambiwa kuwa mimi sijui chochote kuhusu Sablak na wenzake wa huko Meru. Nikamwaga hapa jamvini habari za Abdulwahid Sykes na Sablak kama nilvyosoma katika nyaraza za marehemu Abdu na Tanzania National Archives. Ninachosikitika ndugu zangu ni ukimya wenu.
Jamani kuweni na huruma kwani mcheza kwao hutunzwa. Hivi imekushindeni hata kusema, "Mkuu Mohamed tumekosoma." Vibaya hivyo ndugu zanguni. Nipeni motisha kidogo.
Hilo kama hamliwezi basi nipeni mji au niruhusini nitoe salam.
Mohamed
PS: Kuna mwingine akaja na Nyerere kuandika katiba nikamwaga data. Katiba ya TANU wazee wamenyanyambua ya Nkrumah. Kimya! Sisikii kitu.
MS
K
Mkuu bwana MS ukiacha swala la katiba kkuwa hakuandika mzee nyerere lakini pia ktk kumbukumbu zako zinaonyesha pia hata ile hotuba iliosomwa umoja wa mataifa na mwalimu nyerere pia hakuiandika yeye naomba utuweke sawa katika hilo.ili tuzidi kuiweka sawa historia iliosahaulika kutajwa.
Tangu jana nimekuwa nafuatilia mjadala huu bila ya kuchangia chochote kile lakini huku nikitafakari ni nini hasa hoja ya MS. Jee MS anaamini kwamba wazee wake pekee wa Gerezani wengeweza kuikomboa nchi hii bila ya Watanganyika wa majimbo mengine kushiriki? Ms anataka tuamini hao wazee wake wa Gerezani wote ni wazaliwa wa Gerezani tangu kuumbwa kwa dunia na hawajatokea bara kama vile wamanyema, wanubi, na wanyamwezi ambao walikuwa ni wapagazi wa wajerumani?
Nilirudi kwenye mada. Hapo kwenye nyekundu kuna swali ndugu yangu MS nataka kukuuliza. Umesema Abdalah Salum alikuwa ni "mmoja" wa wachangiaji, hiyo haimaanisha kwamba kulikuwa na wachangiaji wengi waliochangia ujenzi wa Chuo Kikuu Cha kwanza? Na swali la pili ni kama mchango wa sh. 50.00 ambao risiti yake bwana Salum Matimbwa ameihifadhi hadi leo ilikuwa ni asilimia ngapi ya gharama zote za ujenzi wa Chuo kikuu cha kwanza pale Lumumba? Kama unaweza kutuwekea sisi watu wakuja BOQ ya ujenzi wa jengo zima utatusaidia zaidi.
Hili la "kutuma salamu" nimelipenda....Mkuu,haya salimia ndugu wa upande ule (kama wanavyopenda kusema wenyewe)
Kigarama, nashukuru sana maana nimeandika kitu kama hiki katika makala ya Mohamed Said ile inayoendelea thread nyingine.Nilirudi kwenye mada. Hapo kwenye nyekundu kuna swali ndugu yangu MS nataka kukuuliza. Umesema Abdalah Salum alikuwa ni "mmoja" wa wachangiaji, hiyo haimaanisha kwamba kulikuwa na wachangiaji wengi waliochangia ujenzi wa Chuo Kikuu Cha kwanza? Na swali la pili ni kama mchango wa sh. 50.00 ambao risiti yake bwana Salum Matimbwa ameihifadhi hadi leo ilikuwa ni asilimia ngapi ya gharama zote za ujenzi wa Chuo kikuu cha kwanza pale Lumumba? Kama unaweza kutuwekea sisi watu wakuja BOQ ya ujenzi wa jengo zima utatusaidia zaidi.