Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Isome tena makala hiyo ndugu yangu. Ulichokimbia kubandika humu sicho kilichoandikwa mle. Ningekuwa na uwezo wa kuishusha yote humu ningewashushia. Bahati nzuri Mzee huyu bado yuko hai. Au naye alisahaulika?
 

WC,

Kama kuna mahali nimesema Kleist alianzisha AA kwa kuwa alikuwa Muislam tafadhali nionyeshe. Lakini hebu msome na msikilize Kleist mwenyewe anasema nini:

"Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafikizake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutokaBelgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchiniSudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi,Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha AfricanAssociation, Kleist akiwa katibu muasisi. Wakati ule Gavana wa Tanganyika alikuwa Sir Donald Cameron ambaealitawala Tanganyika kuanzia mwaka wa 1925 ñ 1929. Cameron alikuwa gavanamliberali na alikuwa akifahamiana na Kleist. Cameron ndiye aliyeanzisha Barazala Kutunga Sheria la kwanza na mfumo wa Indirect Rule katika Tanganyika.Msimamo wake huu ndiyo hasa uliochangia katika kuwezesha kunzishwa kwa AfricanAssociation. Lakini juu ya haya yote, chama hiki kiliaswa kisijiingize kabisakatika siasa. Wakati chama hiki kinaanza tayari kulikuwepo na chama cha Wazunguna Waasia. Lakini katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika walikuwawakiwakilishwa na padri wa Kikatoliki, Father Gibbons, ambae hakuwa hataanaishi na Waafrika bali akikaa Minaki Misheni nje ya Dar es Salaam. Abdulwahidanakumbuka baba yake akimwambia sababu ya kuanzishwa kwa African Association: "Wakati ule vilikuwepo vyama viwili.Kilikuwapo European Association na Indian Association. Vyote viwilivilishugulika na watu wao wenyewe. Lakini Waafrika hawakuwa na chama kama hichokuwatetea. Katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika waliwakilishwa nammishionari Mzungu jina lake Father Gibbons, aliyekuwa akifanya kazi Misheni yaMinaki maili kadhaa nje ya Dar es Salaam. Lakini kwa hakika mzungu huyu hakuwana uhusiano wowote na Waafrika aliokuwaakiwawakilisha. Kwa ajili hii Waafrika walipohisi hawawakilishwi na hawanachama kama kile cha Wazungu na Waasia kutafuta haki zao, walikutana na kuamuakuunda chama chao wenyewe." [1]Kuanzishwa kwaAfrican Association nje ya utaratibu uliokuwapo wa kuwa na vyama vya kidini nakikabila kilikuwa kitu dhidi ya mfumo uliozoeleka na uliojengeka katika utawalawa kikoloni. Ingawaje chama hicho kilikuwa kinaungwa mkono na Gavana DonaldCameroon na kikasajiliwa kama chama cha ustawi wa jamii, wamishionariwaliwatahadharisha Wakristo wasijihusishe na chama: "mara kwa mara Wakristowalikuwa wakitahadharishwa wasijihusishe na harakati zozote zitakazopingana naserikali."[1]Katika kuwatadharisha Wakristo wasijihusishe na siasa, wamishionari walikuwawanayakini labda kutokana na uzoefu wao sehemu nyingine kuwa, vyama kama hivivya ustawi wa jamii hatimae huwakilisha madai ya watu, hili likitokea basi watuhuasi dhidi ya utawala."
(Kipande yaani haya niliyoandika yamo kwenye kitabu cha Abdu Sykes nimeyatoa kwenye kumbukumbu za Kleist Sykes alizoandika kwa mkono wake mwenyewe kabla hajafa mwaka 1949)
Mohamed
 

Duuuuu!

Mohamed
 
Isome tena makala hiyo ndugu yangu. Ulichokimbia kubandika humu sicho kilichoandikwa mle. Ningekuwa na uwezo wa kuishusha yote humu ningewashushia. Bahati nzuri Mzee huyu bado yuko hai. Au naye alisahaulika?

Mkuu WC,

Mimi nakubari kukosolewa na kukubari kurekebika pale nilipo teleza,sasa naomba nieleweshe lilo ambalo sijaling'amua kwenye ile habari?

Nimeileta hapa hiyo tu kwasababu yule Bwn. yu hai na anaweza kuwa source nzuri tu ya yale tunayo pingana hapa
 
[h=2] This message is hidden because FaizaFoxy is on your ignore list. [/h] View Post
 
Mkitaka kujua udikteta wa nyerere chunguzeni habari za Tuntemeke Sanga aliporudi kutoka masomoni kitu nyerere alichomfanya na habari kama hizi zinafichwa na historia inapindishwa ili kumfanya nyerere abaki kuwa juu lakini siku zote haki na batili hutengana au kwa anayebisha akasome vutabu vifuatavyo:THE DARKNESS OF MWL J NYERERE AU THE PATNERSHIP CHA ABDU JUMBE
 
Maneno mazito sana haya ..na yamejaa busara ndani yake...kila la kheri MS
 

Duuuuu!

Mohamed

MS mkuu wetu ...hata mimi nilikuwa nangojea sana jibu la hilo swali kutoka kwa mzee mwanakijiji..nadhani una andaaa nondo za kuja kumjibu..
ahsante!!
 
Hilo swali la mambo ya EPA, ndege ya rais nk kalielekeza sipo.

Mohamed

Sheikh Mohaed,

Bila shaka hili la EPA na ndege ya raisi ni mambo ya juzi juzi hapa kwa kikwete na mkapa!

Hapa tunazungumzia enzi za Nyerere. Lakini si kweli kwamba mfumo huo (wa ufisadi) una athari za moja kwa moja katika mnakasha huu?
 
Sheikh Mohaed,

Bila shaka hili la EPA na ndege ya raisi ni mambo ya juzi juzi hapa kwa kikwete na mkapa!

Hapa tunazungumzia enzi za Nyerere. Lakini si kweli kwamba mfumo huo (wa ufisadi) una athari za moja kwa moja katika mnakasha huu?

=Mohamed
 
Duh watu hamlali, hamli, hamfanyi kazi maana kasi hii inatisha mjadala mpaka saa nane za usiku!!! Mjadala moto kweli kweli. Sheikh Mohamed Endelea kumwaga vitu. Faiza hebu nifahamishe jinsi kuweka picha nina picha za jiji la Dar miaka 1960-1900. Nadhani zitamtoa Mag3 matongo kuhusu mtazamo hasi Dar ilikuwa vipi. Maana amezungumza kauli si nzuri na kudhalilisha kuhusu wakazi wa Dar. Nikipata muda nitazibandika.
 
Kuna mtu nimemuomba amalezo hapo juu,sijapata majibu na kama kuna mtu anaweza tusaidi kwa "lugha nyepesi " afanye hivyo ni maana ya ile makala ambayo mimi sijaelewa ila nimekimbilia "kupost huku"????

FF,wewe mjuzi wa kiswahili tafadhali embu ni juze,nifahamu kosa langu.Hiyo makala ipo kwenye kile kijarida chetu haya yote yalipoanzia katika gazeti la Mwananchi
 
Kwa hiyo kumbe huo "udikteta" anaosemekana kuwa nao Nyerere haukujali dini ya mtu?Au na Tuntemeke Sanga alikuwa muislam..!?
 

Hawana majibu huwa wanasema tu, hata nilipowauliza mimi huko wakaja wanatokwa povu mdomoni, nikawaambia haya, hayo tuyawache kiporo, tuendelee na mengine, wapii? Hakuna.

Sasa wewe huoni ajabu, hapa inajadiliwa mada za Historia na maandiko ya Mohamed Said anakuja mtu anauliza kuhusu EPA na ndege za Rais. Haki ya Mungu, nnacheka maana mengine hata kujizuwia siwezi. Wananchekesha.
 
Tuntemeke Sanga alikuwa Muislamu?
 
Soma tena bango #722 la Nguruvi3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…