Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Nguruvi3.

Nakubaliana kabisa na wewe katika para no 1,2 na 3. Lakini ningependa kukutanabaisha kuwa historia lazima ibakie kama ilivyokuwa na kusitokee kuichakachua kwa aina yoyote iwe mbaya au nzuri lazima iwekwe ilivyo. Lakini pia imani lazima ziheshimike na kupewa usawa na haki sawa pasi na upendeleo wa aina yoyote.

Tanganyika ilitakiwa ilione hilo kama janga, hasa pale mnaposema kwa kinywa kipana kuwa waislam wapo nyuma kimaendeleo ukilinganisha na wakristo na sasa mna almost miaka 50. Je serikali ilichukua hatua gani kupunguza gap hiyo ambayo kama mngekuwa serious basi sasa kungekuwa hakuna gap kabisaaaaa kwani popolation yenu ya wasialm na wakristo almost 50% each. Hilo naomba mlione kuwa ni aibu kubwa kwa taifa lenu. Kwan kama sasa kuna kampini maalum kwa elimu kwa jamii za wafugaji na hata uongozi kwa wanawake je vipi kwa waislam mnaliangaliaje. Kumbukeni hilo ni bomu na sasa ndio linakaribia kulipuka mjiandae.

Nilipo Green.

Nafikiri si vizuri kuzungumzia kuhusu Bakwata. Kwani kwa namna yoyote ile hicho ni chombo cha Serikali ingawa Nyerere alipoianzusha alisahau kabisa kuwa Serikali haina dini ila raia wake ndio wenye dini. Kwa waislam Bakwata haia cha kuwaambia zaidi ya kufata mambo ya serikali. Ilitakiwa Serikali ya Tanganyika iwaache waislam wenyewe waunde umoja wao kama walivyofanya wakristo kitu kama Tec n.k. Kumbuka Bakwata haina watu zaidi ya viongozi wa Serikali .

Nilipo RED.

Suluhu ya matatizo yenu nafikiri umebainisha mwenyewe pale nilipo Bold. ni vizuri kuweka mjadala wa wazi kwa kuzishirikisha pande zote mbili na kuichambua historia nzima na kuiweka sawa pale ilipokosewa na kuja na historia iliyo sahihi. Lakini pia kujadiliana matatizo mbalimbali ya imani zenu pasi na kuoneana aibu na kuweka mikakati ya kuyatatua kimazungumzo kama ilivyofanyika katika Serikali ya Zanzibar kuunda umoja wa kitaifa.

Pasi na kuliweka wazi suala hili na kuliona kama kitu kidogo basi mjue sasa wakti umefika na kila mtu ameona dhulma ipo wapi na wamefikaje walipofikia. Sasa kazi kwenu kwani siku zote mficha maradhwi kifo kinamuumbua.

 
Unadhani ni utafiti alifanya? Aliongea tu na "Wazee wake" ambao kwa tayari kwa maoni yake mfumo ulishawatenga. "Machungu" ya wazee wake hawa ndio ukazaa kitabu kile ambacho aliambiwa ni mgodi wa dhahabu. Sasa Nguruvi3 kwa mabandiko yake humu anaonekana sio MDINI ni mfia nchi. Pili, "Wazee kama hawa wa Mohamed atawatoa wapi. Mohamed kajichongea kwa WATANZANIA na hasa WAISLAMU walioko CCM na serikalini kwa vyeo na nafasi kubwa tu nchi hii ukiwemo Urais kwa sasa.
 

Barubaru,

Mungu akujaze kheri.

Mohamed
 
Barubaru,
Waislamu wapo nyuma kimaendeleo kivipi? Matajiri watatu wakubwa nchi hii ni WAISLAMU. Wasomi wakubwa wanaoheshimika nchi hii WAISLAMU ni wengi tu akiwemo Prof Lipumba, Prof Shivji, Prof Abdallah Safari, Jaji wetu Mkuu ndiye huyo anaelekea The Hague,...
UISLAMU wa Mohamed ni Uislamu mwingine kabisa.
 

Tafadhali sana, usitie maneno yako kinywani mwangu, sikumbadilikia mtu bali nami nna haki ya kusema yangu, kitu nnachowalaumu Waislaam wenzangu, ni pale Qur'an inapofanyiwa maskhara na kuwekwa ndivyo sivyo wao wanabaki kulumbana na hivi vitabu vya kidunia. "First and Foremost" ni Uislaam, na Uislaam bila Qur'an, kuihifadhi, kuilinda, na kuitetea, inakuwa hakuna Uislaam.

Leo, mtu anaweka aya ndivyo sivyo, na kila unapomuambia hapo umekosea omba msamaha, Waislaam wengine kimya, wao wako "busy" kutetaa vingine ambavyo vyote vinatakiwa viwe baada ya Qur'an na si kabla.

Mmoja tu humu aliyenyanyua sauti na kuliona hilo, nae ni Topical pekee, baada ya kuona hakunyamaza.

Waislaam mnatakiwa mshikane katika njia ya Mwenyeezi Mungu, hiyo kamba ya kuwashikanisha ni hii Qur'an, na inapofanyiwa mchezo kamba yenu, basi muwe kitu kimoja na kuhakikisha haifanyiwi mchezo. Hapo ndio kwenye yote, leo mtu anakejeli Qur'an kwa kuiweka ndivyo sivyo, unapomuambia anakupuuza na Waislaam wengine wanaendelea kulumbana nae kwenye mengine, huyo mtu na wenzake wanawaonaje? wanawaona wote ni majuha tu, hamna mshikamano.

Nawaambia, sikai kimya itapofanyiwa mzaha Qur'an na panapo uwezo wa kukemea, hiyo ndio kwanza na mengine baadae. Waislaam wasioweza kuliona umuhimu wake hilo, hao nao wako katika unafik.

Q.5:44. It was We who revealed the law (to Moses): therein was guidance and light. By its standard have been judged the Jews, by the prophets who bowed (as in Islam) to Allah.s will, by the rabbis and the doctors of law: for to them was entrusted the protection of Allah.s book, and they were witnesses thereto: therefore fear not men, but fear me, and sell not my signs for a miserable price. If any do fail to judge by (the light of) what Allah hath revealed, they are (no better than) Unbelievers.

Q.5:57. O ye who believe! take not for friends and protectors those who take your religion for a mockery or sport,- whether among those who received the Scripture before you, or among those who reject Faith; but fear ye Allah, if ye have faith (indeed).
 
Sisi wengine Faiza "First and foremost" ni KATIBA ya NCHI yetu. Hayo Qur'an na Biblia yana mahala pake na wakati wake. Kimsingi mimi sisumbuliwi na DINI yoyote ile. Nimepitapita kwenye DINI hizo nimeona niliyoyaona. TANZANIA KWANZA. Faiza unataka kuondoka kwenye mada hii ya Mzee wetu Mohamed kwa staili hii?
 

FF,

Kwa kweli una haki ya kukasirika na kutulaumu pale tulipokaa kimya wakati kitabu cha Allah kinachezewa.

Ilikuwa wajibu wetu sote baada ya kuona bandiko lile tukenda kwenye mashaf zetu na kuangalia je aya zimewekwa sawa?
Hilo hatukufanya tumeghafilika.

Tunamwomba Allah atusamehe kwa makosa yetu.

Hili kwetu liwe fundisho siku yoyote tuionapo Qur'an imebandikwa basi tutazame kama imepewa haki yake.

FF tuwie radhi ndugu zako kwani hakuna mkamilifu ila Allah SW.

Mohamed
 

Nafikiri WC unaleta mas'khara katika issue sensitive kama hii.

Kila pahala unasikia wakristo wanajinasibu tena kwa kinywa kipana sana kuwa waislam wapo nyuma kimaendeleo na kielimu na kuleta sababu mbalimbali kuhalalisha usemi wao.

Lakini ukiangalia sasa mnatimiza miaka 50 ya uhuru wenu na population yenu ipo almost 50% each. Je serikali yenu inalitazamaje hilo. Je malalamiko ya muda mrefu ya waislam kuhusu kudhulumiwa serikali inayaonaje? kumbuka malalamiko yao yapo kimaandishi kabisaaaa na nakumbuka wakti fulani hata Rais Mkapa alipewa na kuahidi kuyafanyia kazi? je yamefikia wapi.

Sasa siku zote dharau hususan kwa jamii moja kudhulumiwa na nyingine kutukuzwa ndiko kunakozaa chuki baina ya jamii hizo na baadae kuzua fujo na hata vita.

Suluhu yake ni kuyaweka mezani mchana kweupeeeee na kuyajadili moja baada ya jingine na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu. Kuakhilisha au kuficha matatizo hakusaidiiiii kwa aina yoyote ile.

Na hilo ndio linaloelekea kwa Tanganyika, kwani sasa hakuna siri tena udini kila pahali na kila mtu analijua hilo.

msipo ziba ufa basi mjue mtajenga ukuta.
 

Allah akuzidishie Bi Faiza.

Hakika Allah ametuita In'san katia Qur'an akiwa na maana ni wenye kughafirika. Na akabainisha wazi kuwa tuwe wenye kukumbushana kila wakti katika mambo mema na kukatazana yale yaliyo mabaya.

naamini hakuna mwenye kuweza kukubali Qur'an ambayo ni maneno ya Allah yachezewe kwa aina yoyote au kubatilishwa kwa aina yoyote ile.

Tulighafirika na labda wengine hatukupitia hizo aya zilizobandikwa kuzihakiki lakini tunashukuru kwa kuliona hilo na kututanabaisha.

Allah azidi kukupa kheir nyingi na afya njema.
 
Barubaru,
Mkianza kujadili haya hamtaishia hapo. Mtajikuta kumbe ni jamii fulani ya watu ndio wako nyuma kimaendeleo. Mwislamu na Mkristo wa Lindi, Mtwara, Mara, Singida, Dodoma,.... wote ni masikini, hawana elimu, hawana vyeo na madaraka makubwa serikalini na taasisi zake, huduma muhimu kwao ni ndoto.
Tatizo sio DINI wala MAKABILA yao. Wakati wa Mwalimu kuna makabila yalipewa upendeleo maalum kuchaguliwa kwenda sekondari. Tukubali jambo moja. Yapo makabila na dini ambazo kwao ELIMU ilikuja baadae sana kwa sababu ya mila, desturi na tamaduni zao. Wengi wameliona pungufu hili. Hawapambani kuwaondoa waliowatangulia kielimu au hawapotezi muda kuwalaumu waliotangulia. Fursa sasa ziko wazi kwa wote. Kama kulikuwa na kasoro katika mifumo ya utoaji ELIMU sasa nyingi hazipo.
Angalia kwa mfano sasa shule nyingi binafsi zinazoanzishwa. Kuna anayekatazwa kuanzisha yake? Nyingi sasa ni St. Nanihii kila mahali hadi Bagamoyo! Vyuo vikuu sasa ni St. John, St. Augustine, Bishop Kolowa,.....Bakhresa yeye ananunua meli!
 
.

WC,
nafikiri sana unaanza kuchanganya mambo. Naomba ujifunze nini wajibu wa Serikali kwa wananchi wake. Jiulize kwanini miaka 50 tokea uhuru wenu mpaka leo baadhi ya sehemu zimeendelea sana kiuchumi na nyingine bado kabisa. Lakini suala la msingi serikali ilikuwa wapi mpaka sehemu moja inandelea sana kuliko nyingine? kwanini isitoe kipaumbele na kuondoa hiyo gap ya maendeleo kwa jamii au wananchi wake?

Jiulize kwanini makanisa yanaanzissha mashule na mahospital? je kwa fedha zao au wanafadhiliwa? Je umepitia bajeti enu (Tanganyika) ya mwaka 2009/2010 na ile ya 2010/2011 kuona misamaha ya kodi hususan kwa hizi taasisi za kidini? vile vile angalia na Mou ya kanisa na serikali ya tanganyika? Je kuna uwiano hapo? Je serikali inalitazamaje suala hilo hicho ndio mjiulize.

Cha msingi ni serikali enu kuwa sikivu kwaa raia wake hususan wale wanaolalama kuonewa na kudhulumiwa haki yao tena wanaweka malalamiko hayo kimaandishi na kuipa serikali. Kumbukeni kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha.

Hakuna amani wala upende penye dhulma na pasipo na haki. Na sasa dalili zote zipo hewani . sasa sijui mnasubiri kifo.
 
Aisee! what a joke!

Tumwamwini mtu moja unknown a.k.a jasusu at JF

tena alimuuliza dreva wake (dereva akamjibu) kweli nyinyi ni scholars
Mbona nyinyi mnataka tumwamini Mohamed Said kwamba aliongea na hao wazee wake?
 

Kwani mbona husemi Gaddaffi alitoa hizo hela lini??
 

Mkuu if u are sincere hebu jiulize ni kwa nini wilaya kama Mbinga ilikuwa ni wilaya maskini kabisa katika kila index miaka 20 iliyopita na sasa inaweza kuwa in the best five au hata kuongoza kabisa katika wilaya zilizoendelea kwa index za maendeleo.
 

Nadhani niliwahi kutoa darsa fupi humu la nini maana ya dini naomba ipitie.
 
Kwani mbona husemi Gaddaffi alitoa hizo hela lini??

Kigarama,

Achana na ya Gaddaffi nakukumbushia ahadi yako ya Mkwawa na wazee waliokaa nae kesho Jumatano umesema utakuja kumwaga madataz. Tunayasubiria mkuu.
 
Nashkuru kwa Allah kuwa kelele zangu zimezaa matunda, japo Waislaam wenzangu wameridhia kuwa kweli kuna masahihisho. Sina kinyongo wala ubaya na mtu lakini hili la Qur'an limeniuma sana, mpaka nikabwatuka na kubwabwaja yote nilioyasema na hakuna cha zaidi ila kama nimetumia lugha mbaya na kali naomba msamaha sana kwa wote humu ukumbini.

Mzee Mwanakijiji haya kazi kwako. Kwa hili nasema sikuachi "mpaka kieleweke".
 

Mohamed,

Sie ni wanadaamu tunaghafilika but sio kutuuita wanafiki hilo sikubaliani nalo. Alichokizungumza Faiza ni cha msingi na kwakweli ana haki ya msingi kutukasirikia kwa kutokuona but sio kutuita wanafiki kwani unafiki ni tabia ya mtu au wasifu wa mtu. Wasifu huo mtume SAW alishatuambia ni watu au mtu wa aina gani kwa kusema mnafiki ana sifa tatu a. Kwanza anasema uongo b. Anafanya hiyana akiaminiwa c. Vile vile hana miadi. Labda tumuuliza tumesema uongo wapi hadi tustahili kuitwa wanafiki? Tumefanya hiyana kwa amana ipi tuliyopewa? Tumevunja miadi ipi.

Lazima tuelewane jamani Quran si kitu cha kuchezea kwani Tafsir ya Quran wanazuoni wanasema kila aya ina maana zaidi ya 50,000. Neno moja laweza kuwa na maana zaidi ya moja mfano hadatha, inaweza kuwa hadithu, inaweza kuwa muhdatha etc. Sasa kama mtu huna elimu nayo si vema ukajiingiza kulisema jambo. Imam Shaffi (R.A) anasema mtu anayesema sijui basi huyo amesema kauli ya kweli. Ndio sababu wengine wetu katika mijadala ya dini tunachangia mara chache sana. Kwani unaweza kupotosha maana ikawa ndivyo sivyo.

Tusamehe kwa kutosema lolote kuhusu Quran lakini hata kama tumeliona hatuwezi kulisemea wengine wetu kwasababu elimu hiyo hatuna. Tunajua kusoma Alif-be basi. Tunajua kuhifadhi quran basi. Lakini maana ya maneno yake wengine ni mafakiri wa elimu hiyo na hilo sio ni unafiki bali ni ujinga wa kutokuwa na elimu hiyo.

FF tuwie radhi kwa kughafilika but sio kutuita wanafiki kwani huo si unafiki bali kughafilika kutokana na uchache wetu wa elimu kuhusu Quran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…