Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Brother MS.....hilo hapo juu ni moja ya tatizo kubwa sana ulilonalo...na kwa maana hiyo darsa unalotoa lina tatizo na lake si jema kwa Tanganyika yetu

Unapimaje mapenzi ya mtu kwa nchi yake...Sijui ulimuona/julia wapi Nguruvi3
Nikitu gani hasa kinachokufanya uamini wazee wako walikuwa na mapenzi ya Tanganyika kuliko Watanganyika wengine....

Wengine tukisema Wazee wako ni mamluki na walitaka wao waonekane ni bora zaid ya wengine, wapendelewe wao na familia zao na zaidi kwa kuangalia dini yao......(proved by your statements above)....tutakuwa tunakosea?

Hii ni dharau na matusi makubwa kwa Watanganyika wengine wenye mapenzi ya dhati kwa Tanganyika, na waliipigania vilivyo Tanganyika yetu, iwe kwa senti zao (zisizolingana na za wazee wako wa gerezani), mawazo yao, mazao yao...

Brother MS inabidi ututake radhi siye ambao wazee wetu hawakutokea gerezani, na walitoa "senti/mawazo/nia nk" zao kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika...
 
Mkuu nadhani kinachogomba hapa ni matumizi ya lugha halafu alichokiandika Mohammed Said ni kitabu ambacho huwezi kubadilisha yaliyoandikwa kwa kutoa habari nyingine iliyo sawia na hii kutoka bara au mikoani.
Mkuu, nakubaliana na wewe katika ili, kuwa Bwana Mohammed said kaandika kitabu ambacho uwezi kubadilisha aliyo yaandika, ni kweli kabisa. Nadhani na yeye aliliona ilo kwenye hivyo vitabu vilivyo tangulia, ndio maana na yeye akaandika kitabu ili kuelezea kile anacho kiamini na kukijuwa kuwa ndio sahihi.

Mimi hapo wala sioni tatizo, Tanganyika kuna wasomi wengi na wana historia wengi, je hakuna mtu awezaye kuandika kitabu kama alivyofanya bwana Mohammed Said, naye akawataja hao walio achwa na Bwana Mohammed Said!? Sioni kwanini watu wabishane na kuanza kuitana majina mabaya yasio pendeza.

Mkuu, kila mwandishi uwa na lengo lake, na ilo alikwepeki, mwandishi anaweza kabisa kujua mambo mengine ambayo angeyaweka kwenye kitabu chake, lakini kwa kutokana na malengo yake au jamii aliyo ilenga au anayotaka isome kitabu chake basi anaweza kuondoa ili na kuweka lile, lakini hayo yote hayawezi kuondoa ukweli wa historia ya kweli, kwa sababu wazee waliopigania uhuru bado wapo, na hata kama wametangulia mbele ya haki, watoto zao wapo, na nina uhakika kabisa watakuwa wanajuwa moja kama si kumi na moja... Je hakuna mtu ambaye anaweza kuwafuatilia na kuwahoji ili kiandikwe kitabu ambacho kitawataja wale walioachwa na Serikali ya CCM na ambao hawapo kwenye kitabu cha Ndugu Mohammed Said?

Mkuu, ni kweli uyasemayo, lakini kwa kusoma historia hii ambayo mambo mengi hayakuwekwa kwa sababu moja au nyingine, wapo watakao kuja na kusema hawakuwekwa kwa sababu ya aidha dini au kabila zao na hii ni kwa kuangalia wingi wa wahusika... Kwa mfano ikitokea kuwa Wanyamwezi wengi waliopigania uhuru hawakutwajwa wakati huo huo Wachaga ndio wengi wakitajwa pamoja na makabila mengine, ni hakika kabisa itaonekana hapa kuna jambo. Lakini mimi nasema kuwa bado wakati tunao na tunaweza, sasa kwa nini atuthubutu?

Mkuu, tuwe wakweli na tunaposoma mabandiko ya wengi humu kwa mtu yoyote yule ataona wapi wachangiaji wa JF wanaelekea. Inawezekana kabisa ili swala la udini ni swala ambalo lilipandikizwa makusudi ili kuwatenga watu na baadhi wapate kutawala vyema, lakini kwanini wanachama wengi wa JF wanaicheza hiyo ngoma ya Udini?

Ukiwauliza watakwambia kuwa hizi siasa za udini ni kutoka chama tawala, tunasema okay, kama ni chama tawala na tushagundua ilo, zimefanyika jitihada gani kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuyapinga hayo na kuwaelekeza wanachama wake kuhusiana na ilo.

Kila kukicha kelele ni hizo hizo, udini... udini... udini. Lakini wakitokea baadhi ya watu kulipinga ilo anangaliwa kwa mtazamo wa imani yake na anaweza kuonekana kama mnafiki au msaliti... Inavyo onesha wengi wanapenda hao mambo ya ugomvi na si kutafuta suruhisho la tatizo.
 

Ogah,

Sijasema kuwa hawakuwepo wengine waliokuwa na mapenzi na Tanganyika.
Ila bahati mbaya hao wengine mimi siwajui ningefurahi kama nanyi mngefanya utafiti na wao tukawaadhimisha.

Lakini kwa kuwa suala la mapenzi ya nchi limeletwa uwanjani nami nkaona hii ndiyo nafasi ya kueleza mapenzi ya wazee wangu kwa Tanganyika.

Sababu ni hiyo tu.

Wala hapana haja ya kutakana radhi kwa kuwa hajatusiwa mtu.

Ikiwa wapo wengine waliokuwa na mapenzi ya nchi na wakafanya matendo ya kizalendo kama walofanya wazee wangu hakuna tatizo habari zao na ziandikwe na tutawaadhimisha kama mashujaa wa uhuru.

Tusichelewe katika hili maana sasa ndiyo wakati wake tumo katika kusheherekea miaka 50 ya uhuru.

Mwisho umeniuliza kipi kipimo cha mapenzi.
Jibu lake ni VITENDO.

Angalia historia ya Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, John Rupia, Dossa Aziz, Rashid Sisso, Tatu biti Mzee, Titi Mohamed, Bilali Rehani Waikela, Salum Abdallah, Yusuf Ngozi, Said Chamwenyewe,Mshume Kiyate, Sheikh Yusuf Badi...majina ni mengi.

Soma historia za hawa watu ndipo utakapowajua.

Mohamed
 
Mkuu Sija missa point, nimemfuatilia MS toka mwanzo na mara kwa mara nimekuwa nikirudi ktk mada hii pindi napopata nafasi na naelewa kwa nini mada hii imefika hapa ilipo bila watu kukubaliana hata kwa moja..

Historia ya Mohammed said ni ya kusimuliwa na haitoki kwa mtu mmoja wala kumhusu mtu mmoja isipokuwa amekusanya simulizi toka kwa watu tofauti tofauti tena third parties ambao baadhi yao hawakuwa hata rafiki wa AbdulWahid Sykes ama uongozi wa juu wa TANU, isipokuwa ni watu ambao walitegemea fadhila kubwa kutoka kwa serikali yetu baada ya Uhuru kwa sababu wao walikuwa pamoja na kundi hili la wanaharakati.
Hata mzee Ali Sykes ndugu yake hawezi kunambia anajua kilichokuwa rohoni mwa AbdulWahid isipokuwa atazungumzia yale anayoyafahamu na kwa hisia zake yeye..

Na maadam MS kaandika simulizi kwama alivyosimuliwa na Mag3 pia kaja na simulizi inayopingana na hiyo ya MS na taratibu tunapata ukweli wa ujumuisho wa umoja ulotumika kutuletea Uhuru japokuwa chama TAA kilianzishwa Kariakoo sehemu ambayo Waislaam ndio yalikuwa makazi yao. Mkuu wangu enzi za mkolono Kariakoo nzima ilikuwa na waislaam, wakristu unawakuja kuanzia Kota na kwenda bara zaidi kwa hivyo kuanzisha chama au jumuiya hamala gani haina maana yoyote isipokuwa kinachotazamwa ni lengo na jumuiya hiyo. Ayatollah Khomein alianzisha chama chake na harakati za mapinduzi akiwa France (kama sikosei) Je hii ilikuwa na maana gani?..Jamani nani atasahau huzuni alokuwa nayo Nyerere siku alokufa AbdulWahid Sykes lakini waulize wazee wetu watakwambia alikua akilia kichawi tu maanake wao walikwenda msibani kuchunguza watu.

Mii nataka mtu aje hapa aniambie dhulma aloifanya Nyerere kwa Waislaam kwa sababu najua fika kwamba EAMWS ilipigwa vita na waislaam wenyewe sheikh mkuu wa Tanga, Bukoba, Mwanza, Shaban Nassib, Sheikh Kassim na Hemed bin Jumaa, Abeid Abeid Kaluta na wengineo (socialists) wakitaka chombo cha kiislaam kinachoongozwa na wazawa...To them Aghakhan was a foreigner sawa na mkoloni mzungu. Tunachoshindwa kuelewa hapa ni kwamba hata ndani ya waislaam walikuwepo Masocialist kama walivyoshindana huko Zanzibar wakati wote ni Waislaam lakini ajabu ya Mungu lawama lazima apatikane mkristu wa kumlaumu na Nyerer fit the description..
HakunaMuislaam wa kweli ndani ya siasa za Tanzania, they all feed people wrong info kwa sababu tu wao hawakupata kile walichokitaka na wakipewa aaaah hakuna utawala mzuri kama huu. Wako wapi kina Seif Hamad, Bilal, na wengine wote ambao hupiga makelele kutetea Zanzibar na Uislaam leo wanapiga masuti ya nguvu na wananawiri hata sala zinawapita Uislaam pembeni.. Tusidanganyane hapa siasa za Bongo ni UNAFIKI mtupu!
 
Nakubaliana na wewe sana tu na kinachowasumbua wengi ni kwamba lengo la Ms lilikuwa Udini na hilo halipingiki isipokuwa tatizo linalojitokeza ni kwamba hata wanaomjibu ni wadini vile vile na hawaoni sababu ya mchango wa Waislaam kama Waislaam isipokuwa wanajiona wametengwa ili hali hata wao walihusika na harakati hizo..Dini ni kitu very sensitive na haijalishi Uislaam wala Ukristu. Watu husema tu watageuza shavu la pili lakini hakuna kitu kama hicho..

Kitiu kimoja muhimu sana ambacho MS kakitumia nacho ni kwamba siku zote mwalika sherehe ndiye kichwa cha habari. Wewe ukialika watu kuja kula chakula nyumbani kwako sifa na kejeli zote utapewa wewe ikiwa chakula ni kibaya na sii wapishi. Hivyo MS kwa kuelewa uandishi wa best seller na thamthilia na documentary ya kwamba kuandika historia ya wazee wake bila kuhusisha shetani, a villian, Co starring - hii sinema hii haiwezi kuuzika...Yeye ni author wa script nzima na mjuzi wa kazi yake. Anajua maisha ya mwanadamu lazima kuwepo sababu ya kutofanikiwa kwa mtu ktk jambo lolote na mara nyingi huwa kuna mkono wa mtu na sii maamuzi hafifu tulochukua sisi wenyewe..Katika dunia ya leo biashara kwanza na ndio maana kitabu hiki kipo dukani na hapa JF anafanya ads zake mwenywe. He is smart and good at that!

Vitabu vipo vingi sana vimeandikwa kuhusu Uhuru wetu, historia yetu kabla na baada ya Uhuru lakini hakuna mtu aliyechukua mkondo wa MS na ndio maana unaona ubishani ktk historia hii na sii nyingineyo. Vitabu ni vingi sana na vimetajwa humu na watu wa kila aina lakini hakuna kitabu chenye controversials kama hiki maana kinacheza na imani za watu zaidi ya historia yenyewe. Na ndio hapo hata mimi napingana na Ms otherwise kila alichoandika nakikubali isipokuwa pale anapojaribu kuingia vichwani mwa watu na kutafisiri malengo yao wakati hayakuwa hivyo na ushahidi upo mkubwa tu...

Mwisho, kila mtuhapa ataonekana mdini kwa sababu mada yenyewe ina Udini, hivyo mchangiaji yeyote hawezi kuepuka Udini kwa sababu Udini ndio unaozungumziwa hapa. Na hata mimi nimejaribu kutazama pande zote za mjadala lakini nina hakika wasomaji wanaweka akilini mwao dini yangu kwanza kisha wanasoma nilichoandika na kutafsiriwa nimesimama upande gani. Labda tu kitu ambacho wengi wetu hapa hatukitazami MS kaandika kitabu hiki kwa malengo ya kuhakikisha mfumokristu unapigwa vita lakini kafanya makosa makubwa kutumia historia ambayo ilijengwa na Waislaam wenyewe wana CCM kufikia hapa tulipo.
 

Mkandara,

Kuna pande mbili katika mgogoro wa EAMWS upo ule wa dhahir wa akina Adam Nasibu na kuna ule wa siri ambao Nyerere ndiyo alikuwa mfadhili mkuu.

Insha Allah niko katika darsa huko tutafika na wanaukumbi watajionea wenyewe.

Mgogoro wa EAMWS ni mtamu sana kuhadithia kwani una mengi.
Utakutana na Geofrey Sawaya wa CID akipita mikoani kuwahonga akina Adam Nasib na wafuasi wake na kuwatisha wale waliokuwa wakipinga BAKWATA.

Utakutana na Rashid Kayugwa wa Usalama wa Taifa aliyekuwa akiwapangia mipango akina Adam Nasibu.

Utakutana na Martin Kiama Mkurugenzi wa Radio Tanzania akifanya propaganda dhidi ya akina Tewa.
Utakutana na Benjamin Mkapa Mhariri wa "The Nationalist" akifanya propaganda dhidi ya EAMWS.

Si mkono wa Nyerere wala wa Kanisa unaonekana pale lakini Sheikh Hassan bin Amir akiyaona yote hayo na akiwaleza Waislam.

Vuta subira yote Insha Allah nitayasomesha katika darsa yangu.

Kweli wapo wanafik Allah kawataja na hakika Allah vilevile kawataja Waislam wa kweli wanaosimama kama jengo moja kupigania dini yake kwa dhati.

Mohamed



Mohamed
 
Inshaallah! Ila usisahau pia kuandika jinsi Sheikh Hassan Amir alivyoandaa mapinduzi ya nchi kwa kutumia vitu hivi hivi...
 
Inshaallah! Ila usisahau pia kuandika jinsi Sheikh Hassan Amir alivyoandaa mapinduzi ya nchi kwa kutumia vitu hivi hivi...

Mkandara,

Hilo la Sheikh Hassan bin Amir kuandaa mapinduzi mimi silifahamu nitashukuru kama Insha Allah utaliweka hapa ukumbini tunufaike sote.

Mohamed
 
Mkandara,

Hilo la Sheikh Hassan bin Amir kuandaa mapinduzi mimi silifahamu nitashukuru kama Insha Allah utaliweka hapa ukumbini tunufaike sote.

Mohamed
Haaa! haaa Unalijua vizuri sana maadam unaijua historia ya Sheikh Hassan bin Amir akiwa EAMWS na AMNUT...mengine tumlaani shetani dini inapoingizwa ktk siasa.
 
Haaa! haaa Unalijua vizuri sana maadam unaijua historia ya Sheikh Hassan bin Amir akiwa EAMWS na AMNUT...mengine tumlaani shetani dini inapoingizwa ktk siasa.

Mkandara,

Nadhani umekosea kosa la kawaida tu la kukosa kuijua vyema historia ya TANU.

Sheikh Hassan bin Amir hakupata kutoka TANU hakuwahi kuwa mwanachama wa AMNUT.

Dini nikiwa na maana Uislam siku zote ilikuwa ndiyo nembo ya TANU penda usipende.

Mohamed
 

Bob,

kama mwanajamvi wa siku nyingi humu, naomba nikwambie neno moja. I have never seen michango yako JF inayohusu 'udini' (sorry no better word bro) ambayo iko VERY OBJECTIVE kama michango yako kwenye hii thread.

Kwa muungwana Mohamed Said, mengi wameongea wenye ujuzi zaidi yangu. Lakini ninachokiona ni kimoja UMESHINDWA kutenganisha dini/imani za watu na majukumu yao kama wananchi wa taifa letu. Na nadhani wote humu wanao 'kupinga' ni kwa ajili ya dhana hii. Unless and until utenganishe imani za watu na wajibu wao kama watanganyika/watanzania, sidhani kama watu wataiangalia hii thread kwa mrengo 'objective' KAMA AMBAVYO AMEJITAHIDI (NA KUFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA) MKANDARA.

Kwangu mimi naona hili swala la uhuru wa taifa letu umeli 'simplify' sana limekuwa ni kati ya waislamu na wakristo kitu ambacho naona si haki maana kuna watanzania mpaka leo ambao wameifanyia mengi nchi yetu na hawako katika hayo makundi sasa sijui hao siyo wazalendo au vipi. Tafsiri unayo wewe mkuu.

Anyway, wenyewe walishasema 'there is no history..only historians'. But I would add, much as you are entitled to your opinions..you are not entitled to your own facts.


Masanja
 
Ahsantum kwa kutujali sisi tunaofuatilia mnakasha huu kwa makini sana. Kwani kila wakti wenzetu wamekuwa ima wanataka wageuze mada au kurejesha nyuma mnakasha kwa kuuliza masuala yasiyo msingi mkuu wa mada husika.maalim tafadhwal endelea....
Msingi mkuu wa mada kama alivyoleta Mag3 ni .....yakosolewa. Nadhani 'darsa' ni kulee kwa Mohamed na mwananchi na hata huko tutahoji sisi watu wazima , hata hivyo kumbuka kuwa mwanafunzi aliyekaa kimya si kuwa anasikiliza, yaweza kuwa hajui mwalimu anaongelea nini, I mean hakuna connection kati yao na hawana common ground ilimradi tu wameafikiana kukaa sehemu kama tunavyoona wale wa gogo vivu manyema mosque.

Sisi wengine hatulioni hilo darsa kwasababu hata mwalimu anakula darsa JF. Niweke ushahidi?

Mohamed, nchi hii haiwezi kuwa na watu watatu wenye mapenzi, walikuwepo na tupo na watakuwepo. Hao unaowataja ni sehemu tu na sio Tanganyika. Vipi Makaranga na Bhoke, je sio sehemu ya wenye mapenzi!
 

Nguruvi3,

Narudia tena kusema sina tatizo lolote na Makaranga wala Bhoke.
Wenye kujua michango yao katika TAA hadi TANU watuwekee ili tuiokoe historia yetu.

Ama kuhusu darsa ninalotoa atakuwa msomi wa ajabu yule ambae hatataka kusikia kile asichokifahamu.
Na hakika historia hii nitoayo hapo ni ngeni sana kwa wengi.

Ugeni wa historia hii ndiyo ulokipa kitabu changu umaarufu kama nilivyokwishaeleza hapa jamvini.
Swali likawa vipi historia hii ilichelewa kuandikwa?

Mohamed
 

Masanja,

Wala usitaabike kwa hilo la dini na mimi na TANU.

Hicho chama wamekiasisi wazee wangu na hisia za dini yao katika TANU ilikuwapo sana.
Mimi wajibu wangu ulikuwa kuieleza TANU kama nilivyowasikia wazee wangu wakiieleza.

Hili nimelifanya kwa ukamilifu na wameisoma historia hii na wamekubali kuwa nimeiandika sawasawa.
Ikiwa kuna watu historia hii hawaipendi hii ni bahati mbaya.

Ikiwa nyie mna TANU yenu ya sampuli nyingine isiyo hii iandikeni tusome TANU isiyo na Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Abdulwahid Sykes, Dossa Aziz, Sheikh Mohamed Ramia, Bi Tatu biti Mzee, Dharura biti Abdulrahman, isiyo na Al Jamitul Islamiyya na zawiyya za Quadiriyya na Sheikh Hassan bin Amir iandikeni TANU hiyo tutaisoma.

Mohamed
 
Mohammed Said,


Sisi sii waandishi wa vitabu ni wasomaji na unachoambiwa hapa ni mtiririko wa makosa unaotaka ktk kitabu chako..Hivyo kuzungumzia historia ya majina ya watu wengine nje ya kitabu ni sawa kushindwa mtihani maana utakuwa unazungumzia vitu ambavyo havipo ktk usahihisho wa kitabu chako. Binafsi kuna vitabu vingi nimevisoma lakini kinachonipa mwanga zaidi ni kile cha John Lliffe - A modern history of Tanganyika. Hiki kimegusia mambo mengi sana ambayo hakika ndio historia ya Tanganyika na sii historia ya watu.
 

MM,

Nimekusoma.
John Iliffe ndiye aliyeniingiza mimi katika Cambridge Journal of African Histrory.

Mohamed
 
Ahsantum kwa kutujali sisi tunaofuatilia mnakasha huu kwa makini sana. Kwani kila wakti wenzetu wamekuwa ima wanataka wageuze mada au kurejesha nyuma mnakasha kwa kuuliza masuala yasiyo msingi mkuu wa mada husika.

maalim tafadhwal endelea....

Barubaru,

Insha Allah sasa tunaingia katika Muslim Congress, 1963:

Mkutano waPili wa Waislam, 1963"Haiwezekani kuielewa ahadi ya Nyererekatika haki na usawa kwa raia wote kama alivyoahidi wakati wa kudai uhuru, hadiusome hotuba yake aliyoitoa tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakatiTanganyika inakua jamuhuri. Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo yaupogo kati ya Waislam na Wakristo. Nyerere alifanya hivi labda akijua kuwaingawa yeye alikuwa Rais Mkatoliki lakini waliomuweka madarakani kuitawalaTanganyika walikuwa Waislam. Nyerere alikuwa na haya ya kusema:"Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafautibaina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoatofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimuna wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasaina Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa."[1]Hii ilikuwa kauli ya serikali yakudhihirisha nia yake njema. Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini nakuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwaserikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebishahali hiyo. Wakati Nyerere anatoa kauli hii ya kutia moyo, serikali iliyokuwaimejaa viongozi wa Kikristo na taasisi za Kikristo zilikuwa imejaa hofuwakiogopa harakati za Waislam za kujiletea maendeleo zilizokuwa zinatapakaanchi nzima kwa kasi. Walifahamu fika nguvu na umoja wa Waislam ukitumiwa vyemahapana shaka Waislam watakuja juu. Kwa viongozi wa Kikristo waliokuwa wameshikamadaraka ya serikali hii ilimaananisha kugawana madaraka sawa na Waislam, kwaowao harakati hizi mpya ziliashiria kuanguka kwa himaya yao katika madaraka kamaviongozi. Hii ilionekana kama harakati za pili zaWaislam, safari hii kuchukua serikali kutoka kwa Wakristo. Harakati za kwanzazilikuwa zile za kumngíoa Mwingereza katika ardhi ya Tanganyika. Bila yakutegemea, serikali ikajikuta inakabiliana ana kwa ana na na jumuiya ya Kiislamiliyokuwa na nguvu ambayo kwa dhahiri yake kila Muislam alikuwa ni mwanachama,na ndani yake imejumuisha wana-TANU shupavu pamoja na wapinzani wa TANU. Wakatihuo huo Baraza la Wazee wa TANU katika nafasi yake ya ushauri likawalinaishinikiza serikali ifanye mabadiliko haraka kutokomeza mabaki ya ukoloni.Serikali ikaona harakati hizi ni sawasawa na kuendesha nchi katika misingi yaUislam. Baraza la Wazee wa TANU lilikuwa sasa limejigeuza kutoka kundi dogo lawazalendo na kuwa kundi lililokuwa likishinikiza serikali ndani ya TANU.Serikali ilikuwa ama ikubali matakwa ya Waislam au ikatae na ipambane naupinzani kutoka kwao. Kuanzia hapa mambo yakaanza kwenda kwa kasi yakushangaza. Tarehe 11 Machi, 1963, Kamati Kuu ya TANUiliyokutana Dar es Salaam ilipiga kura kuvunja kamati ya wajumbe kumi na mojaya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Idd Tulio. Wazeewalikusanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na wakasomewa uamuzi wa Kamati Kuu yakulivunja Baraza la Wazee. Taarifa ilisema wazee hao ni kero kwa sababu ëdinina siasa vilikuwa vitu viwili tofauti na hawa wazee walikuwa wanachanganya dinina siasa.í [1]Hiki kilikuwa chombo cha ushauri ambacho wajumbe wake wote walikuwa Waislam;chombo kilichokuwa ndani ya TANU ambacho kilimuunga mkono Nyerere na TANU tangusiku za mwanzo kabisa, kwanza chini ya uongozi wa Sheikh Suleiman Takadir nakisha chini ya Idd Tulio baada ya kufukuzwa kwa Sheikh Takadir kutoka TANU.Wakati haya yote yakitendeka Kanisa ambalo wakati wa kudai uhuru lilijiwekambali na halikutoa msaada wowote sasa likawa linanyemelea kujiingiza katikasiasa likiwa na agenda yake: kuwaweka viongozi Wakristo katika nafasi zauongozi na kuutoa nje ya uongozi Waislam ambao Kanisa liliwaona hawana elimu.[1]Jumuiya za Kiislam kama Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na EAMWS zilikuwasasa zinapigwa vita na serikali ya Nyerere kama vyombo ambavyo havikuwa naumuhimu wowote katika Tanganyika mpya. Katika kumuhakikishia utiifu wao juuyake, Waislam walijitahidi mwisho wa uwezo wao kuziweka taasisi zao kando nachuki za kidini dhidi ya Wakristo. [1]Juhudi hizi hazikuthaminiwa. Serikali ilifanya juhudi za siri kuhakikisha kuwajumuiya zote za Waislam zinapigwa marufuku. [1]Huu ndiyo ukawa mwanzo wa kampeni zakufuta historia ya Uislam katika TANU na mwisho wa Waislam kuwa na sauti katikasiasa baada ya uhuru kupatikana. Baada ya kupatikana kwa uhuru, ile nguvu yaWaislam iliyotumika kupambana na Waingereza kuleta uhuru, ikaonekana hainamaana yoyote na haifai kitu tena. Kuvunjwa kwa Baraza la Wazee ndiyo ilikuwakishiko cha mwisho cha Waislam katika TANU. Baada ya hapo Kanisa lililokuwapembeni wakati wa kudai uhuru sasa likajitokeza waziwazi kuwapiga vita Waislamkatika TANU. Katika kitendo ambacho kanisa halikupata kufanya, Kanisa KatolikiBukoba liliteua wagombea wake wenyewe wapambane wa wagombea Waislamwalioteuliwa na TANU kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Kanisa lilisema limeweka wagombea wake binafsi kwa kuwa wana elimu kupitawagombea wa TANU Waislam. Kampeni kama hii ilifanyika vilevile Kigoma. Hakunaushahidi wowote unaoonyesha kuwa Nyerere, serikali au TANU yenyewe ilichukuahatua zozote dhidi ya Kanisa kwa kuchanganya ëdini na siasaí. Ulipoitishwa Mkutano wa Pili wa WaislamDar es Salaam matatizo haya mazito yaliwekwa kwenye agenda ili yajadiliwe.Mkutano ule ulithibitisha bila wasiwasi wowote kuwa kulikuwapo na njama zasirisiri ndani ya TANU kuhujumu Waislam na njama hizi zikienda sambamba nchinzima na kampeni dhidi ya Waislam na viongozi wa EAMWS.[1] Nyerere alialikwa kufungamkutano ule na Waislam wakamueleza masikitiko yao kwa hali ile iliyojitokeza.Nyerere alizungumza kwa kirefu matatizo ya Waislam na kwa kiasi aliwezakutuliza mambo. Lakini kulikuwa hapana shaka katika fikra za viongozi wa EAMWSkuwa kulikuwa na njama zilizopangwa na Kanisa mahsusi kwa minajili ya kupigavita Uislam na Waislam, uongozi wa Wakristo katika TANU, serikali na Nyererebinafsi akitumika kufanikisha azma hiyo. Uongozi wa Kikristo katika taasisi zaumma sasa ukawa unatumia nguvu za dola kulipa Kanisa madaraka ili liwezekudhibiti serikali na TANU. Tarehe 20 Januari, 1964 kulitokea maasikatika Tanganyika Rifles. Nyerere alirudishwa madarakani na jeshi la Waingerezalililoletwa kumaliza maasi.[1]Baada ya mambo kutulia Nyerere akachukua nafasi hiyo kuwaweka kizuiziniviongozi wa vyama vya wafanyakazi na masheikh maarufu katika Tanganyika. Kesiya uhaini wa wanajeshi ilipofikishwa Mahakama Kuu hapakuwa na ushahidi wowoteule kuwa masheikh walihusika kwa njia moja au nyingine katika uasi waTanganyika Rifles. Uvumi uliokumba mji wa Dar es salaam ni kuwa masheikh haowalikuwa wanapanga njama za kupindua serikali. Shutuma hii kwa masheikh kwahakika ilikuwa ni kiroja. Baada ya hapo, mwanazuoni maarufu, Sharif HusseinBadawiy na mdogo wake Mwinyibaba, walipewa notisi ya kuondoka nchini kamawahamiaji wasiotakiwa. Jaribio la mwanzo la Nyerere kutakakuivunja EAMWS lilikuwa mwaka 1963. Lakini jaribio hilo halikufanikiwa kwasababu ya mpango uliopangwa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir na kutekelezwa naBilali Rehani Waikela, katibu wa EAMWS Tabora. Mwaka huu wa 1963 EAMWS ilifanyamkutano wake katika ukumbi wa Shule ya wasichana ya Aga Khan. Wajumbe wa mkutanohuo walipowasili mjini Dar es Salaam walikuta uvumi kuwa wajumbe wa mkutano waEAMWS watakamatwa na kuwekwa kizuizini. Chanzo cha uvumi huu hakikufahamikalakini haikuwa vigumu kuhisi. Baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Wazee wa TANUmwaka ule ilikuwa wazi kuwa Nyerere alikuwa amewatupa mkono washirika wake wazamani na sasa alikuwa akitafuta wapya ili kujenga upya msingi wake wa siasa.Kutokana na mambo yalivyokuwa yakienda ilikuwa ni dhahiri washirika wake wapyahawatakuwa Waislam.Katibu wa EAMWS Tabora, Waikelaalipowasili Dar es Salaam kuhudhuria mkutano aliitwa na Sheikh Hassan bin Amir.Mufti Sheikh Hassan bin Amir mbele ya Mzee Ali Comorian, alimfahamisha Waikelakuwa kulikuwa na njama zilizokuwa zikipikwa na Nyerere kumuungamiza yeye naTewa Said Tewa ili kuvunja EAMWS ipatikane nafasi ya kuanzishwa jumuiya yaKiislam ya Watanganyika itakayokuwa chini ya wanafiki. Sheikh Hassan bin Amiralimwambia Waikela kuwa harakati za uhuru zilikuwa zinatekwa nyara na Wakristokwa manufaa ya makanisa yao. Sheikh Hassan alimfahamisha Waikela kuwa ni lazimayeye afanye kila linalowezekana ili njama za Nyerere zishindwe. Waikelaalimuuliza Sheikh Hassan bin Amir kwa nini amechaguliwa yeye kufanya kazi ile.Sheikh Hassan bin Amir alimuambia kuwa yeye ana imani na uwezo wake. Baada yamaneno hayo Sheikh Hassan bin Amir alinyanyua mikono yake juu na kumuombea duaWaikela. Nyerere alikuwa anamfahamu Waikela kwa kuwa alikuwa muasisi wa TANU na alikuwa ametoa mchango mkubwa katikakupigania uhuru. Nchi nzima hasa sehemu za Waislamkulikuwa mpango wa serikali wa kuwavunja Waislam nguvu na kuwakatisha tamaa.Waikela, kama ilivyokuwa kwa viongozi wengine wa EAMWS alikuwa anasuguana naMkuu wa Mkoa wa Jimbo la Magharibi, Richard Wambura. Kulikuwa na ujeuri kwaupande wa serikali walipokuwa wanashugulikia matatizo ya Waislam, mbali namategemeo ya Waislam waliyokuwanayo kabla ya uhuru. Subira ya Waikela ilifikiakikomo pale Wambura alipowatukana Waislam katika mkutano wa hadhara. Baada yakuhutubia Wambura, Waikela alipanda jukwaani na akaikumbusha serikali isiwemwizi wa fadhila kwa kusahau jinsi Waislam walivyojitolea muhanga katika kudaiuhuru. Serikali ikachukulia hotuba ya Waikela kama usaliti na yenyekuwashawishi Waislam wasiitii serikali. Ilikuwa katika hali hii Waikela mwanachamashupavu wa TANU alijitoa kwenye chama na akaamua kutumia nguvu zake kuwatumikiaWaislam kupitia EAMWS. Ilikuwa wazi kuwa Nyerere alikuwa na habari za msuguanokati ya serikali na Waislam kule Tabora na mtu ambae alikuwa akihusika namsuguano huo. Siku kabla ya mkutano wa EAMWS, Nyererealiwaalika wajumbe wa mkutano Government House kwa chakula cha usiku. Haowaalikwa walikuwa wajumbe waliochaguliwa mahsusi. Waikela hakuwa mmoja wa haowaalikwa. Nyerere alichukua nafasi ile kuwashauri wajumbe wale waanzishejumuiya ya Waislam wa Tanganyika ichukue nafasi ya EAMWS. Wajumbe hawawalipoleta katika mkutano hoja ya kuanzisha jumuiya ya Waislam wa Tanganyika,Waikela alisimama na kuipinga hoja ile. Alizungumza vilevile kuhusu uadui waserikali kwa Waislam na Uislam. Waikela alimaliza hotuba yake kwa kutoachangamoto kwa wajumbe wamuite Nyerere kwenye ufunguzi wa mkutano ili aje awaeleze wajumbe msimamo wakekuhusu kadhia hii ya chinichini baina ya serikali na Waislam. Baada ya kushindwa kwa hoja ya kuivunjaEAMWS wajumbe wa mkutano ikaonekana kuwa ingekuwa vyema Nyerere aitwe kufungamkutano ule na asomewe makubaliano yaliyofikiwa. Nyerere alifika kufunga ulemkutano na akakutana uso kwa uso na Waikela, ambae alimsomea maazimio yamkutano. Waikela alimfahamisha Nyerere kuwa umoja kwa Waislam ni fardh ñ wajibuwa lazima. Ni kwenda kinyume na maamrisho ya Allah kuwagawa watu. Baada yautangulizi huu Waikela huku akimnyooshea Nyerere kidole alieleza uaduiunaoonyeshwa na serikali dhidi ya Waislam. Waikela alimaliza hotuba yake kwakitisho. Alimwambia Nyerere ikiwa Waislam watamgeuka kupambanana yeye hatakuwana uwezo wa kuwashinda. Nyerere alitulia tuli pembeni mwa Rais wa Baraza laTanganyika la EAMWS Tewa Said Tewa akimsikiliza Waikela. Aliposimama kujibu hotubaya Waikela Nyerere kwa upole alisisitiza msimamo wa serikali wa kutoa haki nausawa kwa raia wake wote. Kwa kiasi fulani Nyerere alikuwa amefanikiwakupunguza joto kati ya Waislam na serikali. Hotuba ya Waikela na ya Nyererezikapewa umuhimu mkubwa katika radio. Waislam wengi wakajitokeza stesheni yagari moshi Tabora kuja kumpokea shujaa Waikela. Alipewa heshima ile kwa kuwa naujasiri wa kuweza kusimama kidete dhidi ya wale waliodhani kuwa wanawezakuwakalia Waislam vichwani. Nyerere alihisi ameumbuka na hili lilimchoma moyosana. Kuanzia hapa Nyerere hakumtazama Sheikh Hassan bin Amir kwa jicho jema.Alingoja nafasi yake ili alipize kisasi. Mwaka ukiofuata, tarehe 20 Januari,1964 jeshi liliasi. Nyerere alichukua fursa ile kuwatia kizuizini masheikh walioonekanawanapinga serikali na viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Waikela alikuwa mmojawa wale waliokamatwa na kuwekwa kizuizini. [1] Nyerere kwa wakati ulehakuwa na nguvu ya kumgusa Mufti Sheikh Hassan bin Amir."

Mohamed
 

Kama vile wewe utaandikiaje TANU isiyo na Julius Nyerere, John Rupia, Oscar Kambona, Joseph Kasella Bantu, Kirilo Japhet, Bhoke Munanka, Paul Bomani,Patrick Kunambi, Pombeah, Mwakangale, Zacharia Madilla, James Malashi, Dominikus Misano, Stanley Kaseko na wengine wengi kama hao! Hao uliowataja walikuwa waislamu, na pengine baadhi yao walitanguliza dini yao kwanza lakini wengi wao walikuwa watanganyika walioungana na watanganyika wenzao wakristu, wahindu na wasio na dini kupigania uhuru wa nchi yao. Wanstahili heshima na kuenziwa si kwa sababu ya dini zao au kabila zao bali utaifa wao.

Oscar Kambona alikuwa Katibu wa kwanza aliyefanya kazi Full time na kulipwa mshahara kutokana na makusanyo ya ada za wanachama. Zuberi Mtemvu alikuwa part time kama walivyokuwa viongozi wengi wa mwanzo, pamoja na Mwalimu.

Amandla......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…