Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Fundi Mchundo,

Tusivutane kwa hili la Zuberi Mtemvu mimi kanihadithia mwenyewe kuwa yeye aliacha kazi Community Development Department kwa kushauriwa na Nyerere ili ashike nafasi ya ukatibu. Hata hivyo inawezekana pia kuwa pakawa na kugongana kwa kumbukumbu kama tujuavyo TANU wenyewe walipoandika historia yao mengi waliyaacha. Hebu soma hii:
"TANU ilinufaika sana kwa siasa za wastaniza Nyerere, umakini wake na kipaji chake cha kuzungumza. Vilevile harakati kwa ujumla zilinufaika kwa ujasiri waMtemvu na Ally. Wao walitenda mambo kwa ujasiri zaidi. Hawakushughulishwa sana na nadharia katikamaamuzi yao ya siasa. Ilikuwa katika kipindi hiki cha kuijengea TANU misingiimara ya uongozi ndipo Nyerere alimshauri Mtemvu aache kazi serikalini ajiriwena TANU. Mtemvu alikubali ushauri ule na akaacha kazi. Mtemvu akawa katibu wakwanza wa TANU. Mtemvu na Mhando walijukanakama ëwakomunistií na serikali, lakini wao wenyewe hawakuhughulishwa na jinahilo. Hivi ndivyo ilivyokuwa Zuberi Mwinshehe Manga Mtemvu alivyokuja kuwammoja wa viongozi wa juu katika TANU. Tutaona hapo baadaye kisa cha Mtemvukutupana mkono na Nyerere na TANU. Katika siku za mwanzonafasi ya katibu mwenezi ilikuwa ikishikwa na viongozi mbali mbali baina yaMtemvu Denis Phombeah, Oscar Kambona, Iddi Faizi Mafongo na Stephen Mhando.Mtemvu akiwa katibu mwenezi alikuwa na kazi ngumu ya kuwashawishi na kuwashirikishawatu kujiunga na kusajili matawi ya TANU."

Kuna wazalendo umewataja ambao nami nakubaliana na wewe kabisa kuwa historia ya TANU haiwezi kukamilika bila ya kuwataja.

Mimi kama wewe ningependa sana mchango wao ukaelezwa ili waadhimishwe na nimeshauri na kutoa changamoto hapa ukumbini lakini naona hili jambo watu hawana uwezonalo.

Publisher mmoja baada ya kusoma kitabu changu aliniomba niandike short biographies za watu kama Bhoke Munanka, Chief Patrick Kunambi nk. nk. lakini mimi nilimshauri atafute mwandishi mwengine.

Hatujachelewa kazi hii ni muhimu na lazima Insha Allah ifanyike.

Sasa hili la dini. Sisi watu wa pwani Uislam umo hadi katika utamaduni wetu na kwa kuwa TANU iliasisiwa na Waislam hili halikuweza kuepukika.

Ndiyo maana mikutano ya mwanzo ilikuwa ikianza kwa kupigwa "fatha." TANU ikikwama kwenye jambo wanafanya "tawasul" na wakati mwingine wanafunga "saum."

Ndiyo maana Sheikh Hassan bin Amir akiuza kadi za TANU msikitini.

Ndiyo maana Baraza la Wazee wa TANU lilitawaliwa na Waislam.

Huu ndiyo ukweli wa historia ya TANU na ndiyo maana kitabu changu kikavutia wengi kwa kuwa ilikuja na kitu kipya ambacho kilikuwa hakifahamiki kwa wengi.

Nimeweka uzi hapa kuwa katika kongamano moja nilipewa onyo kabla kuwa nisiutukuze Uislam na mie nilopoanza "presentation" yangu nilifungua na "Surat Fatha" nikawaambia Wazungu wale kuwa hii ndiyo dua iliyokuwa ikisomwa kabla ya mikutano ya TANU Mnazi Mmoja kisha Nyerere ndiyo anakaribishwa na Sheikh Suleiman Takadir.

Nakumbuka swali moja waliloniuliza ni kuwa Wakristo walikuwa wapi wakati huo?

Jibu langu nalikumbuka hadi leo: "you find out it will make very interesting topic for reaserch..."


Mohamed
 
WC,

Nimeandika "memoirs" (kumbukumbu) za wazee wangu kuhusu TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

"Style" niliyotumia ni "biographical approach."

Mohamed
Nimekusoma Mohamed. DINI na mashambulizi kwa Mwalimu ambaye amefariki bila kuandika historia ya nchi hii ndiyo yanayotukwaza baadhi yetu. Tukabaki tunajiuliza Mwalimu aliwasahau vipi wazee wako hawa? Washauri tu WAISLAMU wetu wapunguze muda wa kulalamika. Wajipe muda wa kufanya kweli kama kuanzisha mashule, vyuo na hata vyuo vikuu. Wasomeshe watoto wao. Wagombee hizi nafasi za kisiasa tena kwa kuwa unasema Waislamu ni wengi nchi hii wachaguane sana tu. Huo mfumoKristo ni wa kufikirika zaidi kuliko hali halisi.
Waislamu waangalie upya vipaumbele vyao. Nafasi ya KADHI kwa NCHI isiyo na DINI ni kichekesho. Kugawana madaraka, vyeo, ajira, nafasi za elimu kwa misingi ya DINI ni jambo ambalo halipo.
TANZANIA yetu na KATIBA yake mpya ijayo iwe juu ya DINI, VYAMA VYA SIASA, MAKABILA,......Ibaki bila DINI kama Mungu alivyo wetu sote.
 

Sheikh Mohamed said

Maneno mazuri sana hayo. Na hii kazi kwa Takriban miaka ishirini Nguruvi3 na wenzake wanapiga chenga kuandika kitabu katika kujazia zile historia zilizosahaulika za wapigania uhuru wa Tanganyika.

Nimeshukuru na kufurahia sana hitimisho lako.

Allah akubarik sana
 

WC,

Kumbuka kuwa Tanganyika haiwezi kuwa huru pasipo fanyika juhudi za makusudi kuondoa malalamiko ya wananchi wake kwa Serikali. Na haiwezi kusalimika hata kidogo kama dhulma na ufisadi zitashamiri.

Fikiria kutokana na MoU ya kanisa na Serikali ya Tanzania. Kanisa linachukua Tsh 60,000,000,000/ kila mwaka kuanzia 1992 na kuanzia mwaka 2010 wanakwapua 91,000,000,000/= Na kama utabahatika kupitia bajeti ya Tz ya mwaka 2009/2010 na ile ya 2010/2011 kipengele cha misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini. Utaona kanisa linasamehewa pesa nyingi kuliko bajeti nzima ya wizara ya wanawake na watoto. (lithibitishe hili kupitia bajeti hizo).

Sasa kwa dhulma kama hizo je mtasema kuna haki hapo? Na kama hakuna haki je amani itakuwepo hapo?
 

Barubaru,

Amin kwa sote.

Mimi niliikataa ile kazi kwa kuwa nina hakika nisingeitendea haki.

Unajua hata ninapowasikia wachangiaji humu wanajaribu kusema ati kuna wengine wamechangia uhuru huwa nakaa kimya tu lakini najua ndani ya nafsi yangu wachangie harakati kadri ya kuchangia kwao lakini historia ya Tanganyika itakuwa na Abdu Sykes mmoja, Sheikh Hassan bin Amir mmoja, Titi Mohamed mmoja, wao hawatakuwa na zawiyya wala tariqa, wala Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika nk. nk. na huu ndiyo ukweli.

Sasa kwa kujua hivi nikaona bora apatikane mtu mwingine kuandika histroria hiyo.

Fikiria Nyerere kashindwa kunyanyua kalamu wala hata kuigusia historia hii katika maisha yake yote...

Hata pale ulipozuka ugomvi kuhusu mtaa alopewa Kiyate Mshume, hakuthubutu kufungua kinywa kusema, "Mzee Mshume alinisaidia mimi wakati uliokuwa mgumu katika historia ya Tanganyika mpeni heshima yake." Alikaa kimya kama vile hakupata kumfahamu Mzee Mshume.

Sidhani kama kwa sasa kuna atayeweza kuandika historia hii na tatizo lipo katika miaka hii 1950 hadi 1961...

Mohamed
 
Hebu tujiulize leo hii misamaha hii ikiondolewa WAISLAMU watanufaika vipi na hatua hiyo? Gharama za huduma zitolewazo kwenye mahospitali ya makanisa MTANZANIA wa kawaida atazimudu? Hivi misamaha hii ikiondolewa makanisa yatashindwa kuendeleza miradi hii? Waislamu wameshindwa kupata MoU yao kwa miradi kama hii? Au ni ile hulka ya kibinadamu kwamba sote tukose hata kama wewe unakosa fursa hiyo kwa kutojishughulisha au kujibidiisha tu?
Mimi nadhani sio vibaya tukiigana kwa yale mema badala ya kujenga chuki na wivu wa kudumu. Wawekezaji kutoka nje wanapewa vivutio vingi tu hadi vingine vinakera. Au ni kwa kuwa wengi ni WAKRISTO?
 
Ungeniletea solution ya kutatua kwa haraka tatizo la upatikanaji wa huduma za jamii vijijini ningekuelewa...! Hivi hizi huduma za jamii wanapata wakristu tu au hata waislam? Lakini hata na nyinyi kupitia shehe ponda si mmeshapeleka maombi(MoU) yenu? Kama ikikubaliwa mtaendelea kupiga hizi kelele?
 
.

WC,

Si waislam wafaidike bali wananchi wote wa Tanganyika wanufaike na keki ya Taifa. Badala serikali enu kunufaisha makanisa kwanini isitumie pesa hizo kujenga hospital zake na mashule/vyuo vyake na baadae vitumike kwa wananchi wote. Hivi wewe unaona Bora nini kuendelea kupanga kwenye hospitali za Kanisa au kuwa na hospitali/vyuo vya Serikali.

Chukulia kwa nguvu za Serikali yenu katika maendeleo hivi sasa ukijumlisha na pesa hizo za misamaha ya kodi na pesa wanazoipa Kanisa kwa takriban miaka 18 (tokea 1992) kama wangeelekeza kila mwaka mkoa mmoja sasa hivi wangekuwa wamefikia wapi.

Kanisa kama limethubutu na kuweza kujenga hospital/shule/vyuo sasa watashindwaje kuviendeleza.

Siku zote mtu au Serikali makini inaheshimu na kuthamini kitu chake na si cha kuazima.

Je wewe unaonaje hapo..........
 

WC,

Napenda kukujuza kuwa pesa za Mou mpaka sasa takriban miaka 18 ni zaidi ya 1.2 trilion shiling kanisa limekwapua.
Si waislam wafaidike bali wananchi wote wa Tanganyika wanufaike na keki ya Taifa. Badala serikali yenu kunufaisha makanisa kwanini isitumie pesa hizo kujenga hospital zake na mashule/vyuo vyake na baadae vitumike kwa wananchi wote. Hivi wewe unaona Bora nini kuendelea kupanga kwenye hospitali za Kanisa au kuwa na hospitali/vyuo vya Serikali.

Chukulia kwa nguvu za Serikali yenu katika maendeleo hivi sasa ukijumlisha na pesa hizo za misamaha ya kodi na pesa wanazoipa Kanisa kwa takriban miaka 18 (tokea 1992) kama wangeelekeza kila mwaka mkoa mmoja sasa hivi wangekuwa wamefikia wapi.

Kanisa kama limethubutu na kuweza kujenga hospital/shule/vyuo sasa watashindwaje kuviendeleza.
Na kuziacha hizo 1.2 trillioni zitumike kwa manufaa ya watanganyika wote.
Siku zote mtu au Serikali makini inaheshimu na kuthamini kitu chake na si cha kuazima.

Waswahili wanasema '' Nguo ya kuazima haisitiri makalio"

Je wewe unaonaje hapo..........

Turejee kwenye mada hisika.
 

WC,
Napenda kukujuza kuwa pesa za Mou mpaka sasa takriban miaka 18 ni zaidi ya 1.2 trilion shiling kanisa limekwapua.
Kama waislam mna uhakika na ushahidi kweli kiasi hicho kimekwapuliwa na Kanisa na hakijaenda kuendeleza shughuli za jamii basi fungueni kesi mahakamani maana huo ni ufisadi.
Mimi sijali kama huduma ya inatolewa na Kanisa, Msikiti au Serikali as long as sibaguliwi kutokana na dini, kabila etc yangu nitaitumia huduma hiyo. Kwani vyuo /hospitali za kanisa zinabagua waislam? Kama una ushahidi weka hapa.

Ila mimi nina ushahidi kwamba Muslim University of Morogoro ni Chuo cha kupendelea waislam tu si watanzania wote ingawa sidhani hilo lilikuwa ni lengo la serikali walipotoa yale majengo ya TANESCO bure kwa waislam.

Chukulia kwa nguvu za Serikali yenu katika maendeleo hivi sasa ukijumlisha na pesa hizo za misamaha ya kodi na pesa wanazoipa Kanisa kwa takriban miaka 18 (tokea 1992) kama wangeelekeza kila mwaka mkoa mmoja sasa hivi wangekuwa wamefikia wapi.
Hivi hii misamaha ya kodi zinapata taasisi za kanisa tu ? Taasi za waislam hazipati misamaha ya kodi?

Hiyo ndiyo mantiki ya MoU. Huduma zitolewe kwa manufaa ya watanganyika wote.
Serikali ina mchango wake na kanisa lina mchango wake na kwa pamoja wananufaisha watanzania wote.

Je wewe unaonaje hapo..........

Turejee kwenye mada hisika.
Mimi noana MoU ni kitu cha heri sana!
 
Unajua wakuu, mkitaka tusonge mbele kama taifa tuache hizi siasa mfilisi za CCM za kugawa watu kwa makundi na dini zao. Sasa kuna ndugu zangu hapa akina Barubaru mnaona CCM na serikali yake kama ndo adui nambari wani wa uislamu. Hapo hapo mnashindwa kuelewa kwamba hiyo serikali ya CCM kwa mda mrefu (mpaka leo) imekuwa ikiongozwa na waislamu na wasio waislamu. Mfano, leo hii safu karibu yote ya tanzania ya viongozi wa juu ni waislamu (atleast ndivyo wanavyojitambulisha).....Lakini bado tunalia kwa kunyanyaswa na 'mfumo kristo'. Sasa hebu niulize..ukombozi wa waislamu utatoka wapi? Maana wanaopewa nafasi..bado wanaonekana as if wao sio waislamu......I honestly dont understand this!

Sasa 'makafir' kama Masanja hapa tunasema tuungane watanzania wote tuiwajibishe serikali tuliyoichagua. Tunaambiwa tuna chuki na waislamu kwa sababu tunam-attack Kikwete ambaye ni muislamu. Ok, tunasema ngoja tutafute chama mbadala..labda tuone kama kina nafuu..tunaambiwa hicho ni cha wakatoliki kwa sababu kuna Dr. Slaa. Sasa hebu Barubaru twambie...kama watanzania tufanye nini kuondoa hiyo dhulma ambayo waislamu mnalia nayo kila siku? maana you guys it seem you want to eat your cake and have it at the same time. Mfano...taifa letu hata kama ni masikini bado tunaongozwa na sheria. You cant impose your will on others. Sasa jamani mlitaka JK aruhusu mahakama ya Kadhi wakati katiba hairuhusu? People get life jamani....

Mimi naamini, Tanzania challenges zinazotuface hazina dini wala kabila. Mafisadi ni waislamu, wakristo na wasio na dini. Ni hizi mentalities za kutaka special treatment nadhani ndo maana hata hao 'waislamu' wakifika huko madarakani wana-ignore 'kelele' za wenzao maana wanajua kabisa hazina mashiko.

Tuungane tulijenge taifa! Once you consider your self or allow people to define you as a victim of anything-you will always be a victim. Ndo maana hapa watu wanalia na historia ya miaka 50-100 iliyopita, baada ya kuangalia watoto wao na taifa letu tutasonga mbele vipi katika miaka 50 ijayo. Tragic indeed!
 



Brother MS...naomba ufafanuzi kwa hayo hapo juu
 

Ulikataa na umeendelea kukataa kuwa JKN hakuwapa fadhila Waislam...i.e. "usomi"...
 
Brother MS...naomba ufafanuzi kwa hayo hapo juu


Ogah,

Hayo yote hapo juu hayakukaa sawa.

Nia ilikuwa kuwaunganisha Watanganyika wote kwa pamoja kudai uhuru ili pawe na haki na usawa kwa raia wote. Ndiyo maana Abdu Sykes alimtaka Chifu Kidaha David Makwaia achukue uongozi wa TAA 1950 na waunde TANU Chifu Kidaha awe rais wa TANU na wadai uhuru.

Chifu Kidaha alipendekezwa kwa kuamini kuwa Wasukuma ni kabila kubwa na wakiunga mkono harakati kwa kumfuata chifu wao Kidaha harakati zitakuwa na nguvu na chama kitakuwa kimeenea hadi bara.

Chifu Kidaha hakuwa Muislam yeye alisharitadi siku nyingi.

Wazee wangu wamekufa na kinyongo kwa kuwa lile walilotegemea la haki na usawa halikuwa.

Nyerere akawaogopa Waislam akawafanya adui na ndiyo leo tuko katika enzi hii ya mfumokristo.

Soma haya hapa chini kutoka mada niliyotoa Kenyatta University mwaka 2006 uone njama alizokuwa anapanga kuudhohofisha Uislam. Uhuru ushapatikana akawa sasa anaogopa ile nguvu ya Waislam isije ikaelekezwa kwake na kwa Kanisa lake:
"Nyerere did not wantto be seen to be working against these organisations or its leadership. Nyerereneeded a Muslim to spearhead the attack while he worked behind the curtain. Acrisis leading to the disarray of these organisations had therefore to befomented paving way for Nyerere to intervene and in doing so would create anopening to overthrow the independent Muslim leadership and create his ownleaders and a new Muslim organisation which he could manipulate and demandallegiance. The nucleus upon which tobuild his new base had to emanate within the Muslim fabric itself and thechoice of the new leadership had to be perceived as emanating from main stream Muslimsthemselves. Nyerere had by then purged the party of its Muslim leadership and thoseremaining were mere cronies. He had in 1963 soon after independence in 1961abolished the TANU – Elders Council an all Muslim body accusing the elders of‘mixing religion with politics’ this in essence meant mixing ‘Islam withpolitics.’ The vacuum left by theElders Council which was party within the party in TANU was filled by few handpicked Muslims in the powerful Central Committee of the party. These handpicked Muslims in the Central Committee paved the way for Nyerere to bring downthe final blow - that of banning the EAMWS, DaawatIslamiyya, Al Jamiatul fi Tanganyika and other Muslim organisations. But inorder for Nyerere to achieve this he needed a person with charisma, intellect andoratory skills who would be able to publicly speak of the necessity of having anew Muslim organisation with indigenous leadership to replace the EAMWS leadershipunder the Shia – Ismaili Aga Khan. African Muslims in Tanzania Nyerere arguedhave to be led by African leadership because that is what uhuru was all about. Nyerere had set the bait it was now up to themouse to nibble and trigger the trap."

Mohamed
 
Masanja,

Sisi taasisi zetu zilifanyiwa mbinu zikapigwa marufuku na Nyerere akatuundia BAKWATA ambayo ni zao la mfumokristo. Angalia hapa chini:
"Nyerere did not want to be seen to be working against these organisations or its leadership. Nyerere needed a Muslim to spearhead the attack while he worked behind the curtain. A crisis leading to the disarray of these organisations had therefore to be fomented paving way for Nyerere to intervene and in doing so would create an opening to overthrow the independent Muslim leadership and create his own leaders and a new Muslim organisation which he could manipulate and demand allegiance. The nucleus upon which to build his new base had to emanate within the Muslim fabric itself and the choice of the new leadership had to be perceived as emanating from main stream Muslims themselves. Nyerere had by then purged the party of its Muslim leadership and those remaining were mere cronies. He had in 1963 soon after independence in 1961 abolished the TANU – Elders Council an all Muslim body accusing the elders of‘mixing religion with politics' this in essence meant mixing ‘Islam with politics.' The vacuum left by the Elders Council which was party within the party in TANU was filled by few hand picked Muslims in the powerful Central Committee of the party. These hand picked Muslims in the Central Committee paved the way for Nyerere to bring down the final blow - that of banning the EAMWS, Daawat Islamiyya, Al Jamiatul fi Tanganyika and other Muslim organisations. But in order for Nyerere to achieve this he needed a person with charisma, intellect and oratory skills who would be able to publicly speak of the necessity of having a new Muslim organisation with indigenous leadership to replace the EAMWS leadership under the Shia – Ismaili Aga Khan. African Muslims in Tanzania Nyerere argued have to be led by African leadership because that is what uhuru was all about. Nyerere had set the bait it was now up to the mouse to nibble and trigger the trap."

Mohamed


PS: Mfumokristo ndilo zimwi linalowala watoto wa Waislam katika elimu.
Jitahidi kutuelewa.

 
Masanja,

Sisi taasisi zetu zilifanyiwa mbinu zikapigwa marufuku na Nyerere akatuundia BAKWATA ambayo ni zao la mfumokristo. Angalia hapa chini:
"Nyerere did not want to be seen to be working against these organisations or its leadership. Nyerere needed a Muslim to spearhead the attack while he worked behind the curtain. A crisis leading to the disarray of these organisations had therefore to be fomented paving way for Nyerere to intervene and in doing so would create an opening to overthrow the independent Muslim leadership and create his own leaders and a new Muslim organisation which he could manipulate and demand allegiance. The nucleus upon which to build his new base had to emanate within the Muslim fabric itself and the choice of the new leadership had to be perceived as emanating from main stream Muslims themselves. Nyerere had by then purged the party of its Muslim leadership and those remaining were mere cronies. He had in 1963 soon after independence in 1961 abolished the TANU – Elders Council an all Muslim body accusing the elders of‘mixing religion with politics’ this in essence meant mixing ‘Islam with politics.’ The vacuum left by the Elders Council which was party within the party in TANU was filled by few hand picked Muslims in the powerful Central Committee of the party. These hand picked Muslims in the Central Committee paved the way for Nyerere to bring down the final blow - that of banning the EAMWS, Daawat Islamiyya, Al Jamiatul fi Tanganyika and other Muslim organisations. But in order for Nyerere to achieve this he needed a person with charisma, intellect and oratory skills who would be able to publicly speak of the necessity of having a new Muslim organisation with indigenous leadership to replace the EAMWS leadership under the Shia – Ismaili Aga Khan. African Muslims in Tanzania Nyerere argued have to be led by African leadership because that is what uhuru was all about. Nyerere had set the bait it was now up to the mouse to nibble and trigger the trap."

Mohamed


PS: Mfumokristo ndilo zimwi linalowala watoto wa Waislam katika elimu.
Jitahidi kutuelewa.

 
Masanja,

Sisi taasisi zetu zilifanyiwa mbinu zikapigwa marufuku na Nyerere akatuundia BAKWATA ambayo ni zao la mfumokristo. Angalia hapa chini:

PS: Mfumokristo ndilo zimwi linalowala watoto wa Waislam katika elimu.
Jitahidi kutuelewa.


MS,

Hebu niambie hawa elites 'waislamu' tunaowaona leo katika nchi yetu..wao walisoma wapi? wamejazana kwenye uwaziri, U-DC-U-RC, Ubalozi, jeshini, biashara na kwingine kwingi..hwa walipata wapi fursa kama Nyerere alikuwa na njama dhidi ya waislamu? Jibu lako tafadhali kaka.
 
Jibu lake hapo MS litakuwa..."Masanja, Nimekusoma...! Tuendelee na darsa" period.
 
Bismillah,

wanajanvi naona mnazunguka saana pasipo kutuliza vichwa vyenu mkamsoma Mohammed Said vizuri anakotokea na kwa nini amekatalia kipande cha ardhi yake kuwa historia..Na muda mrefu nimekuwa najiuliza kama kuna haja ya kupasua jipu hili lakini nadhani umefika muda muafaka nizungumzie kulikoni...Itakuwa hadithi ndefu kidogo naomba uvumilivu wenu..

Nimemsoma sana Mohammed Said na nadhani lengo lake la awali ni historia ya Wazee wake ktk mchango wa Uhuru wa Tanganyika, wazee ambao baada ya Uhuru leo hii wamesahaulika - FORGOTTEN HEROES - ktk historia ya nchi yetu lakini hakutafuta sababu zaidi ya maelezo alosimuliwa na jamaa zao wenyewe, ama misukosuko ilotokea kuwa sababu ya maswali mengi anayojiuliza lakini hukwepa kipande cha matukio kati ya mwaka 1963 hadi kufikia 1967, matukio ambayo yalisababisha na upande huo huo anaoutetea na muhimu sana kuyaelewa toka upande wa pili ili kuhitimisha.

Mohammed Said anazungumzia wazee wake kina Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Dossa Aziz, Sheikh Mohamed Ramia, Bi Tatu biti Mzee, Dharura biti Abdulrahman, na Sheikh Hassan bin Amir ambao kweli wamesahaulika ktk historia ya nchi yetu na wala hakuna kumbukumbu zao ama baadhi yao Kitaifa..Madai haya ni regit na naweza kuelewa wapi Mohammed Said kasimama dhidi ya historia ya Tanganyika iliyopo ana inayonadiwa sana na waandishi wa vitabu na habari..

Nafikiri hadi hapa wengi tunaweza kukubaliana naye na haswa mtu kama Abdulwahid Sykes, Dosa Aziz wakati watu kama Julius Nyerere, John Rupia, Oscar Kambona, Paul Bomani na wengine kibao ni maarufu hata kwa kizazi hiki kipya wanajua mchango wa watu hawa katika Uhuru wa Tanganyika kupitia historia yetu..Katika hili bila kutaja dini zao nakubaliana sana na Mohammed na ndio maana nikauliuza historia ya Cecil Matola na mbona kiongozi huyu kasaulika?..

Kikubwa anachokosolewa Mohammed Said ni pale alipotengua lengo la awali na kulifanya swala hili kuwa la imani ya dini (conclusion yake) na kwamba hawa viongozi wamesahaulika kwa sababu ni Waislaam ama serikali imepotosha mchango wa Waislaam ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika hivyo kuifanya hoja nzima ya TAA na TANU kuwa ya kidini zaidi ya chama cha siasa...

Nachomuomba Mohammed Said ni kimoja tu ya kwamba, hata historia ya Zanzibar haiwezi kuwa historia sahihi kama hutazungumzia viongozi waarabu wa Hizbu party. Na mtu yeyote kipenzi wa Hizbu anaweza kuja hapa na kudai haoni sababu kwa nini Karume maarufu kuliko Shamte, akatumia hata race card ya kama tunavyowasoma Wazanzibar wengi wakizungumzia Mapinduzi kama ilikuwa njama ya watu weusi dhidi ya Wazanzibar wenye asili ya Kiarabu na kadhalika..Yote haya yanaweza kuwa na ukweli lakini lengo la mwandishi linapokuwa linalenga kuonyesha dhulma fulani ni muhimu sana kwetu kupima hiyo dhulma inayodaiwa kisha tujenge hoja zinazopinga ama kuhalalisha dhulma hiyo..

Mimi nachoweza kumwambia Mohammed Said, historia ulopewa ya wazee wako kuna mengi umefichwa ama wewe mwenyewe umeamua kuiacha pembeni lakini kati ya kundi kubwa la wazee wako toka mwaka 1964 kufikia mwaka 1967 walikuwa tayari wamejitenga na chama TANU, walikuwa tayari wakitaka kufanya Mapinduzi dhidi ya chama TANU ambacho kiliongozwa na Nyerere walikuwemo waislaam wengi sana viongozi vile ivle, na Waislaam karibu mikoa yote walipingana na dhana ama lengo la hawa wazee wako waliojitenga...Hivyo, unapojitoa ktk chama kumbuka pia unapoteza haki zote ulostahili kupewa na historia yako inakuwa na picha tofauti kama ilivyokuwa kwa kina Mtenvu na Kambona.

Hatuwezi kuwa na historia njema ya Kambona zaidi ya kwamba alitaka kuipindua nchi. Na vile vile hatuwezi kuwa na historia nzuri ya kundi la watu walitaka kuanziusha vurugu nchini kwa kutumia sanduku la Udini ila naweza sana kukubaliana na wewe kwamba kuna viongozi wetu waliokuwa na mchango mkubwa sana ktk harakati za Uhuru wetu wamesahauliwa. Hawa ndio wanatakiwa kuitwa mashujaa na hawa ndio wanatakiwa kuenziwa kwa kila sifa ya Uzalendo na hata kusherehekewa ktk Memorial day!.


Nilichoweza kujifunza mimi kutoka vitabu vya Mohammed Said ni kwamba - Historia ya Tanganyika inapotea na ipo haja na sababu kubwa ya vitabu kama cha John Lliffe - A Modern History of Tanganyika kiwe ktk vitabu vinavyotakiwa kufundishwa mashuleni iwe Primary school au Secondary. Lakini haya maswala ya Udini au kutumia Uarabu kudai haki ya Uzanzibar haiwezi kujenga umoja wa kitaifa bali unabomoa hata imani ndogo ya uzalendo iliyokuwepo..Leo hii ukimwambia Mgazija kwamba Waarabu ndio waasisi wa Uhuru wa Zanzibar na Shamte alikaribishwa tu, sijui kama kutakalika.

Maasalaam!
 

Bob,

Mimi sina cha kuongeza ubarikiwe sana kwa hoja zako makini zilizokwenda shule. Sema jamaa akina invisible walishaondoa kale kadude ka thanks..wanatumia fesibuku ambayo wengine hatumo huko!

I wish kaka MS angekusoma na kukuelewa. Kikubwa ni kwamba ukishajenga hoja sensitive kama hii kwa kofia ya imani zetu ni vigumu sana watu kuafiki hoja zako kwa sababu..rightly or wrongly...wengi tunapoteza objectivity kama MS alivyodhihirisha.

In all, I deeply salute your analysis!

Bravo mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…