Mag3 unakosea sana ndugu yangu, nafasi ndiyo hii itumie. Hiyo nyingine ni Kudra za mwenyezimungu!!No Mohamed Said, no more free ride, nikipata nafasi nitaendelea................
Mag3 unakosea sana ndugu yangu, nafasi ndiyo hii itumie. Hiyo nyingine ni Kudra za mwenyezimungu!!
Na lazima tuwaambie watu kwamba tunawapenda sana ndugu zetu waislamu, lakini huu uchochezi wa Mohamed Said, HAPANA.
Ndugu yangu Kigarama, ni swali la muda tu na ukumbuke kuwa kabla ya kuchangia yabidi usome mambo mbali mbali ambayo yametolewa na washiriki mbali mbali ili usiyarudie tena. Hata hivyo kuna moja muhimu la kulitilia maanani nalo ni kwamba Wazee wa Mohamed walimhitaji Mwalimu Nyerere kuliko alivyowahitaji wao na ni bahati kwao waligundua hilo mapema sana na kumkabidhi Uraisi mara moja. Watu wa muhimu sana walikuwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao ilibidi wateuliwe wawe viongozi wa TANU mikoani na hasa kwenye majimbo muhimu ambako ndiko hasa harakati za kupambana na mkoloni zilikoanzia. Vyama hivyo vya Ushirika vingi vikiwa vimeanzishwa kabla ya TAA na vilitumika kuwahamasisha wananchi kuliko vyama vya wafanyakazi kwa sababu vilikuwa karibu na wananchi walio wengi.
Vyama vya Ushirika vya Wakulima vikuu vilikuwa kama;
Dar es Salaam ilikuwa na wakazi wasiofika 200,000 na hata tukisema asilimia kumi walikuwa wafanyakazi sana sana watafikia watu 20,000. Hii idai ukigawanya kwa vyama vyote ni kwamba wakati Mwalimu Nyerere anachaguliwa kuiongoza TAA, mojawapo ya vyama vya wafanyakazi Dar es Salaam, labda ilikuwa na wanachama wasiofika hata elfu mbili. Sasa linganisha idadi hii na Chama cha Ushirika kama Victoria Federation of Coperative Unions ya Mwanza ambayo tayari ilikuwa na wanachama zaidi ya 30,000.
- Kilimanjaro Co-operative Union Ltd (1933)
- Lake Province Native Growers Association (1949) - baadaye ikaanzishwa Victoria federation of Co-operative Unions
- Bukoba Co-operative Union Ltd. (1950)
- Ngoni Matengo Co-operative Union Ltd. (1936)
- Rungwe African Co-operative Union Ltd. (1949)
Kuna riwaya iliwahi kuandikwa na mtunzi moja mwenye jina la James Hadley Chase ikiwa na title - Believe this and you will believe anything ! Hivyo ndivyo navyovichukulia porojo za Mohamed Said ila tatizo ni kuwa ni porojo zenye hatari kwani zinapandikiza chuki miongoni mwa wananchi. Hapana, lazima aambiwe bila kumung'unya maneno aache mara moja kuivuruga jamii kwa hizi chuki zake na mimi nawaomba wote wenye nia njema na taifa letu kumpa a big NO ! Mbona haorodheshi majina ya hawa vinara walioongoza hivyo vyama vya Uchirika na badala yake amekaa kutusimulia soga za Gerezani ?
Hollywood story-imeandikwa na Pro-Nyerere. Hizi data za kutengenezwa na serikali ya Nyerere, lini mtaziacha?
Kama unataka kujua historia ya nchi inabidi uende kwenye direct sources acheni kufuata data za serikali ya Nyerere. C'mon, let's be honest.
Unayoyasemwa yanasemwa sasa kwa rais jk, yalisemwa kwa bwm na ahm. Nimekuchoka na mipasho yako.
Mwanakijiji,
Maneno ya kumkashifu Nyerere yalikuja baadae sana na yalitokana
na watu waliompokea Dar es Salaam wakawanae baga kwa bega
hadi akafika alipofika.
Baada ya hapo ikawa sasa Nyerere kasahau hisani aliyotendewa.
Akawa anasikika akisema yeye kaikuta TAA imekufa akaifufua,
Dossa alikuwa akimwendesha, TAA kilikuwa chama cha starehe.
Nyerere mwaka 1963 akalivunja Baraza la Wazee wa TANU chini ya
uenyekiti wa Iddi Tulio. Nyerere akawakamata masheikh wengine
hata hawakuwa katika siasa kama Maalim Matar (rafiki kipenzi wa
Abdulwahid) akawatia kizuizini kwa kosa la "kuchanganya dini na siasa."
Nyerere akavunja jumuia za Kiislam kama EAMWS, Al Jamiatul Ismaiyya na
nyinginezo.
Wazee wakapigwa marufuku hata kufika TANU office kama wenyewe
walivyopenda kuita.
Nyerere akajiweka mbali na wale wazee na watu wengine aliokuwanao
katika harakati.
Iddi Tulio kagongwa na gari kafa. Nyerere hakuhudhura maziko yake.
Mshume Kiyate kaugua hadi kafa hakwenda hospitali wala hakuhudhuria
mazishi yake, Sheikh Mohamed`Ramia, Jumbe Tambaza...
Wazee wetu hawakupendezwa na mambo haya.
Chuki ikajengeka dhidi yake.
"Huyu si huyu Nyerere aliyeletwa kwetu na Abdu Sykes kavaa kaptula?
Wazee wakawa wakikutana pembeni wanazungumza lugha hizo.
Ndiyo hadi leo tumefika hapa.
Ni mengi tutaelezana taratibu.
Kila jambo lina sababu yake.
Mohamed
Mag3 unakosea sana ndugu yangu, nafasi ndiyo hii itumie. Hiyo nyingine ni Kudra za mwenyezimungu!!
Na lazima tuwaambie watu kwamba tunawapenda sana ndugu zetu waislamu, lakini huu uchochezi wa Mohamed Said, HAPANA.
Unayoyasemwa yanasemwa sasa kwa rais jk, yalisemwa kwa bwm na ahm. Nimekuchoka na mipasho yako.
Hawa hapa chini vp naona nao historia imewasahau
Nyambala,
Ngoja tusomeshane kidogo.
Umeweka majina bila ya melezo.Ungefanya hivi:
Baada ya kuweka hayo majina ungeeleza na michango yao katika
kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mathalan ungesema huyu fulani mwaka fulani alikuwa ndiye katibu au
rais wa TAA. Katika kipindi cha uongozi wake alifanya kadhaa, kadhaa
lakini historia imemtupa nje.
Sasa wewe umeorodhesha majina tena si kwa "source" yako wewe yaani
"primary source" ila umechukua kutoka "secondary source kisha bila maelezo
unasema kuwa hawa wamesahauliwa.
Sasa swali litakuja. Wamesahauliwa kwenye nini? Kwani hao ni akina nani? nk.
Taratibu tutaelekezana ili mradi hatutukanani.
Mohamed
Umenena mkuuAsante Mungu JF inaelekea kurudi kwenye hadhi yake mijadala ya aina hii ndiyo ilinifanya nikajiunga na hili jamvi lakini kuanzia mwaka 2010 tulivamiwa na kundi la wahuni wasiopenda mijadala yenye afya bali matusi na kejeli.
Mzee Mohamed Said,Fundi Mchundo,Jasusi,FaidaFoxy,WildCard,Mzee Mwanakijiji,Mwita Maranya,Nguruvi3,Mag3 na wengine wote niliowasahau kwa bahati mbaya tafadhali sana tujiepushe na lugha za kuudhi,kejeli au matusi kwa faida ya mjadala.Niseme kweli nimejifunza mambo mengi kupitia kwenu na nina hakika wako wengi pia kupitia michango yenu wamefaidika sana.
Unayoyasemwa yanasemwa sasa kwa rais jk, yalisemwa kwa bwm na ahm. Nimekuchoka na mipasho yako.
nimependa sana hii. Je, unaamini M. Said ameenda kwenye direct sources?
Mohamed Said, kabla sijafanya reference na kucomment, Je historia iliyoandikwa katika kitabu hiki ni sahihi au nayo imepotoshwa??????? Maana imezungumzwa sana hii historia iliyopotoshwa lakini vitabu vilivyopotosha havitajwi. Ila nachokiona from your side ni kwamba you have freedom to choose anywhere ku-cite references zako iwe Tanzania, Cambridge Uni Press, Amazon.com, Marekani u name it. A freedom I suspect is somehow limited to some of us thru branding na unguided limitations.
"Voices from Tanganyika: Great Britian, the United Nations and the decolonization of a Trust Territory, 1946-1961" By Ullrich Lohrmann
Ikiwa mtu kaongea na Ali Sykes ana kwa ana na Ali Sykes ndio alioisaini kadi ya TANU ya Nyerere hivi kweli unataka kutuambia hiyo sio "direct source"? Unanchekesha!
Hii si kama napuuza mchango wa Nyerere hata kidogo lakini ninachosema
hakuwa peke yake kwa hiyo asienziwe peke yake na wenzake watajwe pamoja
na yeye.
Mohamed
Ngoja tusomeshane kidogo.
Umeweka majina bila ya melezo.Ungefanya hivi:
Baada ya kuweka hayo majina ungeeleza na michango yao katika
kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mathalan ungesema huyu fulani mwaka fulani alikuwa ndiye katibu au
rais wa TAA. Katika kipindi cha uongozi wake alifanya kadhaa, kadhaa
lakini historia imemtupa nje.
Sasa wewe umeorodhesha majina tena si kwa "source" yako wewe yaani
"primary source" ila umechukua kutoka "secondary source kisha bila maelezo
unasema kuwa hawa wamesahauliwa.
Sasa swali litakuja. Wamesahauliwa kwenye nini? Kwani hao ni akina nani? nk.
Taratibu tutaelekezana ili mradi hatutukanani.
Mohamed