Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mzee Said pamoja na ujuzi wote wa maneno na historia kuna kitu kimoja kiko wazi kuhusiana na hizi 'kazi' zake - amezikariri. Amekariri masimulizi ya utotoni na hata alivyozidi kupata ufahamu zaidi ndivyo hivyo hivyo alivyozidi kuzikariri. Hivyo anachotuelezea ni kile ambacho amekariri kwa kusimuliwa au kujisomea n.k Na hivyo anakirudia na ukiangalia kwa juu juu unaweza kweli kuwa impressed. Tatizo linakuja nipale unapozama chini na kuanza kufuatilia 'kujua'. Kuna tofauti kubwa kati ya kujua na kukariri.
Wapo wanafunzi ambao wanakaririshwa Table na hivyo ukimuambia akuambie table ya 12 anaweza akaiimba yote au 'tebo' ya sita akaiimba yote. Lakini mwanafunzi huyo anaweza asijue kuzidisha kwani ukianzia na table ya 13 au kwenda juu atapata shida au ukianza kuchanganya table na kujumlisha anaweza kushindwa. Lakini mwenye kujua kuzidisha anaweza kujua namna ya kuzidisha namba mbalimbali kwa urahisi kabisa na kwa haraka kuliko hata anayetumia kalamu. Kwa mfano, mtu anajua namba yoyote ukizidisha kwa namba yenye 10, 100, 1000 n.k basi unaongeza tu hiyo idadi ya sifuri na jibu linapatikana.
Kwenye historia au utafiti wa aina kama hii ni hivyo hivyo. Mtu anaweza kukariri matukio muhimu au watu muhimu walifanya nini na ni kile tu ambacho amekaririshwa ndicho pekee anaamini anakijua. Ukijaribu kumtoa tu kwenye kukariri anachanganyikiwa kabisa. Ni sawa na kumuweka swala mbele ya taa ya gari usiku akapigwa macho!
Maswali mengi anayoulizwa Bw. Said na watu wengi tangu kuanza kwa mjadala huu yanahitaji kujua siyo kukariri tu. Kwa mfano, Bw. Said anaweza kusema kuwa "tofauti kati ya Nyerere na Waislamu imeanza baada ya ile congress ya 1963". Sasa hicho ni cha kukariri. Ukitaka kumtoa jaribu kumuonesha kuwa walikuwepo Waislamu kabla ambao walikuwa wanamchukia Nyerere tangu siku ya kwanza ametambulishwa kwao na walimchukia si kwa sababu aliwadhulumu Wailslamu au aliwatendea jambo lolote baya - bali kwa sababu ya Ukatoliki wake. Ukimleta Said kwa hilo anapata shida kwa sababu ni kama kumlazimisha kujua.
Utaona maswali yote anayulizwa majibu yake ni ya kukariri.
SWALI: Kwanini kwa miaka karibu ishirini ambayo ulikuwa unafanyia hii historia 'yako' utafiti hukupata nafasi hata ya kuandika barua kwa Mwalimu Nyerere?
JIBU: Prof. Haroub Othman alishangazwa sana akamwendea Nyerere...
SWALI: Kwanini hadi leo hujawahi kumuuliza au hata kujaribu kwenda kuonana na Mama Maria Nyerere na kumhoji kuhusu Sykes na mtazamo wa Nyerere kuhusu Waislamu wakati akiwa madarakani?
JIBU: Maria Nyerere alikuwa anafahamiana sana na Binti Sudi, Binti Zubeda ambaye alikuwa akiishi mkabala na kwa Bw. Selemani ambaye nje ya nyumba yake tulikuwa tunacheza kombolela!
SWALI: Kwanini kama kweli ulikuwa unataka kuandika historia ya mashujaa 'waliosahauliwa' katika historia hukuwagusa wale ambao hawakuwa Waislamu au wale waliokuwa nje ya Dar?
JIBU: Kama na nyie mna wazee wenu nendeni mkaandike habari zao, miye nimeandika habari za wazee wangu na hiyo ndiyo historia yote ya TAnganyika!
SWALI: Je ni mahali gani ambapo wazee walioshiriki kupigania uhuru walipofanya hivyo kwa sababu ya Uislamu wao na kuwa waliongozwa na imani yao na siyo uzalendo wao kwa Tanganyika na kutaka uhuru uwanufaishe watu wote?
JIBU: Katika kampeni zote zilisomwa dua na Nyerere alikuwa anainamisha kichwa chini ili isomwe Al Fatha na wakati mwingine zilitolewa dua hadi wakatoka machozi!
Sasa mtu ambaye is untrained anaweza kuamini kabisa kuwa Bw. Said anajibu maswali lakini for any objective and trained mind anaweza kuona kuwa maswali hawezi kujibu kwa sababu yatamuondoa kwenye kukariri. Matokeo yake ni kuwa mtazungushana hapo hapo kwenye kukariri hadi mchoke kwa sababu alichokariri yeye ndio ukweli na chochote ambacho kitamfanya afikirie nje ya huko kukariri kutaaribu kabisa. Na ukifikiria sana utaona ni kweli. Wakati mwingine kujiuliza kuhusu kule unachoamini kunaweza kabisa kukusababisha ubadilishe mtazamo wako na kupindua kabisa maisha yako.
Bw. Said akitaka kujua anaweza lakini kujua kuna gharama - na gharama yake ni kuwa kwa kadiri mtu anavyopata ukweli ndivyo anavyoitwa kuufuata na wakati mwingine ukweli ni mgumu sana kuukubali. Ni mtu yule ambaye ana ujasiri wa dhamira yake ndiye pekee anaweza akutafuta ukweli, akauchunguzi na kuuhoji na akiona umethibitika atakuwa tayari kuhama kutoka kuliko alikokuweko.
Ndiyo Yesu alisema mojawapo ya misemo ya kifalsafa ya hali ya juu - 'MTAIFAHAMU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU" Yoh. 8:32 Ukweli unafungua, unawapa watu sababu ya matumaini, unatuliza moyo na unamuinua mtu kutoka katika hali ya kutokujua. UKWELI wa historia yetu haupatikani katika kitabu cha Bw. Said nayeyote ambaye anasoma ataona kuwa hafunguki! Ila anajikuta anasukumizwa kwenye kifungo cha hatari sana kwenye gereza ambalo nje limeandikwa 'UDINI'. Na huyo anaweza kuanza kujikuta anatumikia hii itikadi ya chuki na atafunguliwa tu pale ambapo yeye mwenyewe atakuwa na ujasiri wa kuhoji anachoambiwa, kuuliza maswali sahihi na akiona majibu hayaji kuunda nadharia za kuelezea kwanini majibu hayaji.
Maswali ambayo yameulizwa ambayo karibu yanafikia 50 sasa hayawezi kujibiwa na Bw. Said kwa sababu yanahusiana na kutafuta ukweli. Kwa vile lengo lake siyo kutafuta ukweli bali kukaririsha watu kile alichosikia basi ni vigumu kabisa kumfanya akubali kuwa kuna vitu ambavyo kwa kweli angefanya jitihada kuvijua zaidi. Lakini itakuwaje kama angefanya jitihada hiyo na baadaye kujulishwa vitu ambavyo vingevunja vunja vile alivyokariri?
MM,
Mie si wa kwanza kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Tewa kabla hajafa aliniachia hazina hiyo hapo chini:
Amir, Hassan Sheikh, (Mufti) "Daawat Islamiyya" unpublished paper,1962.
Tewa, S Tewa, "Probe Into the History ofIslam in Tanzania" (unpublished manuscript).
Unadhani kwako wewe kuna mkweli kwetu sisi kumshinda Sheikh Hassan bin Amir?
Nyaraka hizo zipo katika maktaba nyingi Marekani na Ulaya kwa hisani yangu.
Mohamed