Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

M. Said nimekuelewa kuwa hilo la Prof. Othman kuhusu kumconfront Nyerere limeandikwa kwenye kitabu chake; swali la pili hujalibu.

Wewe ulianza kufanya utafiti wa kitabu chako cha Kiingereza lini na ulikamilisha lini hadi kikachapwa mwaka 1998. Yaani ulichukua muda gani kukamilisha uandishi wako wa kitabu cha Abdulwahid Sykes?

Mwanakijiji,

Usijitaabishe bure. Muda wa kuandika kitabu utachangia kipi kipya katika kuijua historia ya uhuru wa Tangnayika? Nakuomba kwa hisani yako niulize maswali yatakayoleta mapya ili mnakasha unoge.

Niwie radhi ndugu yangu.

Mohamed
 
Mkuu Mohamed
Hayo maswali nimekuuliza kwa sababu kwenye kitabu chako ukueleza sababu hasa ya Wazee wa Gerezani Kugharamikia Mwalimu Nyerere, kiasi cha kumlipia pango na mshahara
Kuna kitu ambacho Nyerere alikuwa nacho ambacho kilikuwa zaidi ya Wazee wako Gerezani, lakini kwa sababu zako binafsi huwezi kuzikiri hizo sababu, maana ukizikiri ni kama kuwafanya Wazee wa Gerezani wanafundishwa Ujanja na Wakuja

Mkuu ukweli huwa unajisimamia wala Haupiganiwi,

K,

Huna hamu ya kujua TANU iliingiaje Peramiho? NImekupa "offer" naona umeipuuza.

Wenzako wananiletea ticke kutoka Uhgaibuni, wananilaza "Five Star" wananilipa na
masurufu, siku ya kuondoka wananipa na mazawadi ya mabuku mazuri mazuri ili
wasikie haya. Wewe nakupa elimu ya bure unaikwepa...Au ushaingia woga hutaki
kusikia vipi akina Mhaiki walitolewa Kanisani kuja kujiunga na TANU na wao mwisho
wakawatoa nje wale waliowaingiza...

"UKWELI HUWA UNAJISIMAMIA WALA HAUPIGANIWI"

Mohamed
 
Cha Ajabu Babu yangu kule Rombo wala hawafahamu hawa Wazee wa Gerezani sasa ilikuwaje wao "PEKEE" ndio walikuwa na "Mchango wa Pekee" Katika kuadi Uhuru wa Tanganyika (Rombo ikiwa Sehemu yake) halafu Warombo wenyewe hawaawafahamu hao Pioneers wenyewe LoL! Yataka moyo kusadiki hzi habarii

Albedo,

Kwa kweli ni tabu sana kusadiki haya niliyoandika katika kitabu. Ndiyo maana kilipotoka kitabu hiki kilileta mshindo mkuu. Nimealikwa vyuo vingi sana kwa ajili ya kitabu hiki.

Kila nilipohadhiri niliwaacha wasikizaji wangu na mshangao hata wale ambao wamefika Tanzania na kufanya utafiti katika masuala kama haya.

Nami huwaeleza kuwa kuna watu wengi nchini hawajui. Kwao haya ni mambo mageni kabisa.

Kitabu kimenipa umaarufu kwa kuongeza katika historia ya nchi yetu "new information."

Mohamed
 
K,

Ushakisikia kisa cha TANU Jimbo la Kusini kwenye ngome ya Kanisa Katoliki
iliingiaje na vipi YUsuf Chembera, Salum Mpunga na Sheikh Yusuf Badi
walivyomleta Nyerere Lindi kuishambulia ngome hiyo?

MS

Mzee Mohamed,

Unaweza kutufunulia hii habari ya YUsuf Chembera, Salum Mpunga na Sheikh Yusuf Badi walivyomleta Nyerere Lindi kuishambulia ngome ya Kanisa Katoliki?
 
Mzee Mohamed,

Unaweza kutufunulia hii habari ya YUsuf Chembera, Salum Mpunga na Sheikh Yusuf Badi walivyomleta Nyerere Lindi kuishambulia ngome ya Kanisa Katoliki?

MM,

Insha Allah nitajitahidi:
"TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongoziwa Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri.Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba.TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakatiuongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama chasiasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifakudai uhuru. Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa. Baada yaVita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katikamashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika. Vilevile aliwakusanyawapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao. Ilikuwa kupitia juhudi zakebinafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonjialijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama. Mnonji kwakutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta NangwandaSijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chamacha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa AthumaniLukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyamavya wafanyakazi. Ingawa vyama hivi viwili, yaani TAA na Dockworkersí Unionvilikuwepo katika mji mmoja, siasa za hiki chama cha pili cha wafanyakazibandarini hazikupitia TAA kama ilivyokuwa mjini Dar es Salaam. Hii kidogoilidhoofisha mwamamko wa siasa kwa wananchi. Jimbo la Kusini lilikuwa katikausingizi mzito wakati sehemu nyingine Tanganyika zilikuwa zikipiga hatua kwendambele zikiandaa vita dhidi ya utawala wa kikoloni. Chanzo cha usingizi huumzito huko kusini ulikuwa na asili yake katika historia ya Tanganyika.Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini yaTanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zilesehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yakewakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi yawazalendo. Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumaniulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vyaKiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonariwalikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituovyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya,Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakatiza Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchina viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwaupande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi waowakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni. Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwakusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chiniya himaya ya wamishonari walipupazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baadaya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndaniya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vileshule na hospitali. Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kamamabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu lasiasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislamkufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni waWajerumani. Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyovionaVita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizowa zinakuja tenakwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu. TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwasafari hii Waislam walikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kamawalivyoanzisha vita na Wajerumani. TANU ilipoanzishwa mjini Dar es Salaam nahisia za utaifa zilipokuwa zikipandapole pole katika fikra za wananchi katika sehemu nyingi za Tanganyika, Jimbo laKusini lilikuwa bado usingizini likiishi katika zama za kale. Mnonji na Waziri, kwa sababu ya utu uzima wao, darajayao katika jamii na hasa kutokana na kuhusika kwao katika siasa za pale mjini,walikuwa na nguvu kubwa katika TAA. Wakati TANU imeshachukua nafasi ya TAA,uongozi wa TAA Lindi haukutaka kufungua tawi la TANU. Mtu wa kwanzakuutanabaisha uongozi wa TAA mjini Lindi juu ya mageuzi yaliyokuwa yakitokeaTanganyika na kuanzishwa kwa chama kipya cha siasa mjini Dar es Salaam alikuwaAbdallah Juma Makopa, kijana kutoka Tanga akifanya kazi ya ukarani Posta yaLindi. Makopa aliwaendea Mnonji na Waziri na kuwajulisha kuhusu kuanzishwa kwaTANUmjini Dar es Salaam na aliwashauri waanzishe TANU pale Lindi. Jambo hilolilipingwa moja kwa moja na Mnonji, Waziri, Said Nassoro, Abdallah Mhuji nawanachama wengine wa TAA.Chama cha Waafrika ambacho kilianzishwasiku nyingi mjini Lindi na kwa hakika ndicho kilikuwa chama cha pekeekushughulikia maslahi ya Waafrika sehemu za kusini kilikuwa African WelfrareAssociation ambacho mlezi wake alikuwa John Nevi, Mjaluo kutoka Kenya na katibuwake alikuwa Casian Njunde, Mngoni wa Songea. Makopa aliposhindwa kukishawishikile kikundi cha wazee wa TAA aliwaendea Yusufu Chembera na Rashid SalumMpunga. Chembera alikuwa na umri wa miaka thelathini na nne na Mpunga alikuwakijana wa miaka ishirini na saba. Chambera alikuwa amesoma hadi shule ya msingina Mpunga alikuwa amemaliza madras. Chembera alikuwa akifanya kazi katikakantini ya Lindi Welfare Centre, wakati Mpunga alikuwa dereva wa lorialiyeajiriwa na mfanyabishara wa Kihindi. Makopa aliwashauri Chembera na Mpungajuu ya uwezekano wa kuwahamasisha wananchi wawaunge mkono ili tawi la TANUlifunguliwe pale mjini. Aliwaambia alitaka sana kufanya hivyo yeye mwenyewelakini asingeweza kwa sababu yeye alikuwa mtumishi wa serikali na hakuwaakifahamika sana mjini. Uongozi kama wao ndiyo ungeweza kuaminiwa na wananchina usingetiliwa mashaka. Makopa, Chembera na Mpunga walikubaliana kuwa kabla yakuanza kufanya kampeni waziwazi kwa ajili ya TANU, lazima wawaandikishewanachama wachache kama waasisi wa chama. Mpunga na Chembera walimwandikishakijana mmoja akiitwa Abdallah Faraj na katika muda mfupi waliweza kuwapatatakriban wanachama kumi na tano walioridhia kujiandikisha kama wanachamawaasisi wa TANU.Baada ya kuandikisha wanachama waasisimkutano wa siri uliitishwa katika Welfare Centre ambako ndiko alikokuwaakifanya kazi Chembera. Chembera aliwaeleza kwa ufupi wale wanachama wa mwanzokuhusu malengo na madhumuni ya chama hicho kipya cha siasa. Mkutano huoulichagua kamati ya watu watatu yaani, Makopa, Chembera na Faraj ili kuwakabiliMnonji na Waziri kuwaleza kuwa TAA haipo tena nchini Tanganyika. Lengo lilikuwakuwasadikishia kuwa ilikuwa kazi bure na kupoteza wakati kujaribu kuihuisha TAAmjini Lindi wakati ambapo Tanganyika nzima ilikuwa ikisonga mbele na TANU.Baada ya mjadala mrefu sana na mkali wa wale vijana watatu na ule uongozi waTAA wa wazee, walikubaliana TANU lazima isajiliwe mjini Lindi.Uchaguzi ulifanyika na Shaaban Msangi,kijana wa Kipare akifanya kazi kwa Smith Mc Kenzie, alichaguliwa rais na AhmedSeif, katibu. Mpunga, Chembera, Mnonji na Idd Toto walichaguliwa wajumbe wakamati. Ahmed Seif alikuwa kijana ambaye ndiyo kwanza amemaliza shule, yeyealikabidhiwa kuendesha ofisi kwa niaba ya uongozi. TANU mjini Lindi ilimwajiri ili kukiandaachama kiweza kufanya kazi zake kwa ufanisi. Hassan Mohamed Kinyozi aliajiriwakama mhudumu wa ofisi. Hawa wawili walikuwa ndiyo wafanyakazi wa kwanza wa TANUwaliokuwa wakilipwa mshahara katika Jimbo la Kusini na wakawa miongoni mwawafanyakazi wachache sana walioajiriwa na TANU kwa wakati ule. Mnonji alitoanyumba yake katika mtaa wa Makonde kuwa ofisi ya kwanza ya TANU Jimbo laKusini. Baada tu ya kuanzishwa kwa TANU, Athumani Mussa Lukundu, kiongozi waLindi Dockworkersí Union, aliunganisha chama chake na TANU. Jambo hili, kwaTANU lilikuwa la kuitia moyo sana kwa sababu Dockworkersí Union ilikuwa nawananchama wengi na hatua ile iliongezea TANU nguvu.Baada ya muda mfupi tu toka kufunguliwakwa TANU Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TANU wa mwaka 1955 ulifuatia. Tawi la Lindililikuwa tayari lina uhusiano na makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam, nalilikuwa likitarajia kuhudhuria mkutano huo na kukutana na Julius Nyerere nauongozi mzima wa TANU pale makao makuu Dar es Salaam. Mpunga, mwanachamamuasisi wa TANU, na Ali Ibrahim Mnjale waliteuliwa kuhudhuria mkutano huo kamawajumbe kutoka Jimbo la Kusini. Halmashauri ya TANU ya Lindi iliwaelekezawajumbe hawa wafikishe ombi rasmi kwa makao makuu ili Julius Nyerere ajekufanya ziara kusini kwanza, kukutana na wananchi na kufanya kampeni kwa ajiliya TANU na pili aje kupambana na propaganda dhidi ya TANU zilizokuwazikitawanywa na Yustino Mponda. [1]Mponda akitumia uhusiano wake na serikali ya kikoloni na nafasi yake kamamjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala; na vilevile akitumia ushirikianowake wa muda mrefu na kanisa ambao bila shaka yoyote lilikuwa serikali ndani yaserikali kule kusini, alikuwa ameanza kampeni yake ya kuipinga TANU. Hilililikuwa likiathiri msukumo wa uanachama. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbewaliotumwa na Gavana Twining kwenda Umoja wa Mataifa Februari, 1955 kwa niabaya serikali ya kikoloni kwenda kuipinga. Uongozi wa TANU huko Lindi ulitakaNyerere aende kupambana na Mponda akiwa katika uwanja wake mwenyewe, ndanikabisa ya ngome ya Ukristo wa Kikatoliki katika Tanganyika.Mkutano mkuu wa mwaka wa TANU ulifanyikakatika ukumbi wa Hindu Mandal mjini Dar es Salaam. Siku kabla ya mkutano TANUilimwalika Gavana Edward Twining kwenye tafrija katika Ukumbi wa Arnatouglolakini alikataa kistaarabu na akamtuma Chief Secretary, Bruce Hutt,kumwakilisha. Baada ya mkutano, wakati wajumbe wengine wanaondoka kurudi kwenyemajimbo yao, Mpunga na Mnjawale walibakia nyuma kukutana na uongozi wa makaomakuu wa Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe,Said Chamwenyewe, Oscar Kambona na wengineo. Mpunga na Mnjawale waliwafahamishaviongozi wa makao makuu kuhusu hali mbaya ya siasa Jimbo la Kusini. Mbali nakampeni za kuipinga TANU za Mponda, katika ziara yake Lindi Gavana Twiningaliwatahadharisha Waafriika wa Tanganyika wasijihusishe na ëwafaanya fujowanaotaka kuzusha vuruguí. Twining alikuwa akitoa onyo hili akiikusudia TANUambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka uliopita. Hotuba hii ya Gavana iliwatishawananchi kujiunga na TANU. Mpunga na Mnjawale walisisitiza kuwa kuja kwaNyerere mjini Lindi kulitakiwa haraka sana kukabiliana na vyote viwili, kwanzaile hotuba ya gavana na pili zile kampeni za kupinga TANU zilizokuwazikiendeshwa na Liwali Yustino Mponda. Wakati huo Abeid Amani Karumealiyehudhuria ule mkutano alimwalika Nyerere afanye ziara Zanzibar. Kitu chakustaajabbisha ni kuwa, Nyerere alionekana kuiafiki zaidi ziara ya Zanzibarkuliko ile safari ya kwenda kusini kuiimarisha TANU. Mpunga alimsisitiziaNyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANUkupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzanimkubwa dhidi ya TANU. Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU.Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wotewaliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili. Baada ya kufikiamakubaliano, Mpunga na Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari yaNyerere. Ziara ya Nyerere ilikuwa ianzemuda mfupi kutokea hapo kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku za mwisho za kiangazi.Barabara sehemu ya kusini ya Tanganyika zilikuwa hazipitiki wakati wa masika,zikiitenga kabisa kusini toka sehemu zilizobaki za nchi. Ali Mwinyi Tambwe naRajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi nawoga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.Nyerere na msafara wake ulipokelewa nauongozi wa TANU wa Lindi huko Mbanji, kijiji kidogo nje ya mji. Msafara waNyerere ulipowasili Mbanji ilikuwa kiasi cha saa moja jioni hivi na gizalilikuwa linaanza kutanda. Mbali na Mpunga na wale wajumbe wawili waliokutanana Nyerere mjini Dar es Salaam mwezi uliopita, hakuna hata mtu kati ya umma uleuliokuja kupokea ujumbe kutoka makao makuu ya TANU aliyekuwa anajua Nyerereanafanana vipi. Mpunga, dereva wa lori, alijibagua kutoka kwa lile kundi lawatu akawa amesimama pembeni ili Nyerere apate kumuona. Baada ya Nyerere kumtiaMpunga machoni, Mpunga alimwendeakumsalimu Nyerere, Tambwe na Diwani; kisha aliligeukia lile kundi la watukumtambulisha Nyerere kwa wananchi akilitaja jina lake kwa sauti kubwa. Baadaya hapo aliutambulisha ule ujumbe wa Nyerere. Nyerere na ujumbe wakeulisindikizwa kwa shangwe na kundi la watu hadi ofisi ya TANU kwenye nyumba yaMnonji. Kupakana na ofisi ya TANU ilikuwepo nyumba ya seremala mmoja, Issa binAli Naliwanda. Hii ndiyo nyumba iliyochaguliwa alale Nyerere na ujumbe wake, sikwa sababu ilikuwa nzuri kupita zote. Ilichaguliwa na kupewa heshima hii kwasababu ilikuwa karibu sana na ofisi ya TANU na hivyo basi ilirahisishia TANU kaziya ulinzi wa Nyerere. Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili na Nyerere aliwaombawenyeji wake apelekwe kanisani kwa ajili ya ibada.Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo lafahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi. Lindi ulikuwa mji wa Waislam.Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwaakishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa. Watuwachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindikutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wamjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa nahaja ya kuhudhuria ibada pale kanisani. Hakuna mtu katika uongozi wa TANU waLindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote katiyao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikizaNyerere kanisani ili kumpa ulinzi. Baada ya kujadili suala hilo kwa urefuhatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga nawanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisanina wengine wabakie nje kulinda mlango.Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani yakanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwana Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu. Misa hii ëmaalumí ilidumu katika fikra za wale Wakristowaliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sanaWakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi. Hii huenda ilikuwamara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwaamesimamiwa na Waislam.DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANUkufanya mkutano wa hadhara. Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitishamkutano wa dharura wa tawi uliohudhuriwa na Nyerere na Tambwe. Baada ya mkutanohuo Tambwe alikwenda kumwona DC. Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku yaJumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwakammoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyoWaafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara. Kamwe haijapata kutokea kablaya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hichokujumuika mahali pamoja. Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwawamekaa na wengine wamesimama katika yajua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia. Ili kuhakikisha amani nausalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wamkutano. Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa nifedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao. Uingereza ilikuwaikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, nawakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe. TANUilikuwa imewasili Jimbo la Kusini."

Mohamed
 
Wallah hata sijuia hii shida yote inakupateni kwa kisa gani. Kama hamuamini haya niliyosema sawa hapana tabu. Mimi niliona yaliyokuwemo katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika nikaandika kitabu kueleza upande mwingine. Ikiwa nanyi mmeona haya yangu si kweli basi hakuna neno. Hapana haja ya kutabishana bila sababu.

Mohamed

Hahaha ahahaha! Mohamed Said hakuna anayepata shida wa la tabu kwa simulizi zako, suala linalokuja mpaka mjadala unakuwa mpana ni pale wewe unapoamua kujibu maswali unayoyapenda tu na pia unapotaka references unazozijua wewe tu ndiyo zitumike. Na sielewi kwa nini hoja niiandike mimi nijumuishwe na watu wengine katika majibu. It is a very low thinking and weird kufikiria kila mwenye hoja tofauti na wewe are of some kind wired in some central brain somewhere na hivyo basi they are equal in thinking, judging, deciding etc.
 
Albedo,

Kwa kweli ni tabu sana kusadiki haya niliyoandika katika kitabu. Ndiyo maana kilipotoka kitabu hiki kilileta mshindo mkuu. Nimealikwa vyuo vingi sana kwa ajili ya kitabu hiki.

Kila nilipohadhiri niliwaacha wasikizaji wangu na mshangao hata wale ambao wamefika Tanzania na kufanya utafiti katika masuala kama haya.

Nami huwaeleza kuwa kuna watu wengi nchini hawajui. Kwao haya ni mambo mageni kabisa.

Kitabu kimenipa umaarufu kwa kuongeza katika historia ya nchi yetu "new information."

Mohamed

Mohamed Said

Niko Interested kufahamu Je Wazee wako wa Gerezani walifika hadi kule kwetu TARAKEA? Na kama walifika JE waliwakuta wale Wazee Wangu wa Rombo wanafanya nini? Kwamba hawakuwa na Harakati zozote za Kupambana na Mkoloni? Ni hilo tu
 
Hahaha ahahaha! Mohamed Said hakuna anayepata shida wa la tabu kwa simulizi zako, suala linalokuja mpaka mjadala unakuwa mpana ni pale wewe unapoamua kujibu maswali unayoyapenda tu na pia unapotaka references unazozijua wewe tu ndiyo zitumike. Na sielewi kwa nini hoja niiandike mimi nijumuishwe na watu wengine katika majibu. It is a very low thinking and weird kufikiria kila mwenye hoja tofauti na wewe are of some kind wired in some central brain somewhere na hivyo basi they are equal in thinking, judging, deciding etc.

Nyambala,

Nimefurahi kusikia mambo yote ni sawa.
Ombi.

Mimi Kiingereza changu cha shida naomba ukiandika niandikie Kiswahili kitupu ukinitilia hayo madoido ujumbe wako haufiki sawia.

Mohamed
 
Mohamed Said Usichoshwe na Maswali yangu maana mimi ni wa Kizazi Cha dotcom nina swali jinge

1. TAA ilianzisha lini na Nani? Na nini yalikuwa Malengo ya kwanza ya Uanzilishi wa TAA? ( Hili laweza kujibiwa na Yeyote tu)
2. Je Ilikuwaje Wazee wa Gerezani wamuamini mtu (ambaye walikuwa wanamfahamu kwamba Si chochote si lolote) Urais wa TAA?
 
Mohamed Said

Niko Interested kufahamu Je Wazee wako wa Gerezani walifika hadi kule kwetu TARAKEA? Na kama walifika JE waliwakuta wale Wazee Wangu wa Rombo wanafanya nini? Kwamba hawakuwa na Harakati zozote za Kupambana na Mkoloni? Ni hilo tu

Albedo,

Wazee wangu wa Gerezani hawakufika Mgombani kule alifika mzee wangu mwingine wa Mtaa Chini Moshi Mjini akiitwa Yusuf Olotu pamoja nae walikuwa Mama Bint Maalim, Halima Selengia na wengineo. Soma habari zao hapa chini:

"Historiaya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kama walivyoshiriki wananchi waKilimanjaro haiwezi kamwe kukamilika bila ya kutaja jina la Yusuf Olotu aumaarufu Yusuf Ngozi. Yusuf Olotu ndiye aliyeiwezesha TANU kupata ushindi mkubwakatika uchaguzi wa kura tatu mwaka 1958. Jina hili la Ngozi alilipata kwa kuwaalikuwa akifanya kazi katika kampuni ya kuuza ngozi. Uchagga ilikuwa chini yautawala wa machifu waliokuwa wakijulikana kama Mangi. Baadhi ya machifu hawawalikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria na kwa ujumla wao walikuwa karibu naserikali ya kikoloni kuliko walivyokuwa na wananchi wanaowaongoza. Hali yasiasa katika Jimbo la Kaskazini ilikuwa ngumu na ya kukatisha tamaa. WakatiTANU inakabiliwa na Kura Tatu mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umemalizikakwa wananchi kudhulumiwa haki yao. Japhet Kirilo alikuwa tayari amerudi mikonomitupu kutoka Umoja wa Mataifa alikopeleka madai ya Wameru. Kirilo hakuwa nachochote cha kuwaonyesha Watanganyika. Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye aliyewezakuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo akaienezavijijini. Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf Ngozi ndipo unapokutana na historiaza awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata majina na vyeo na wengine kuwa mawazirikatika Tanganyika huru. Mfano wao ni Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.Ilikuwa ni Yusuf Ngozi pamoja na wazalendo wengine walioifanya TANU ishindeuchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958. Kupitia kumbukumbu zake, halikadhalika, ndipokwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika kama yeye mwenyewe,mashujaa wa kike na wa kiume na wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim, AminaKinabo, Halima Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika nawengineo. Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawalawa machifu wao na kujiweka chini ya TANU. Habariza kuenea kwa TANU Kilimanjaro na matatizo ya Kura Tatu zimeelezwa na YusufOlotu katika mahojiano aliyofanya na mwandishi nyumbani kwake Moshi tarehe 21Januari, 1989. Yusuf Ngozi alimfahamisha mwandishi kuwa ofisi ya CCM Wilaya,miaka michache iliyopita walimuandikia barua kumuomba awape nyaraka zake zoteza mwanzo kuhusu TANU na awaandikie historia ya jinsi chama kilivyoenezwaKilimanjaro na mchango wake binafsi. Kazi hii aliifanya na akakabidhi nyarakahizo kwa CCM. Yusuf Ngozi alimfahamisha mwandishi kuwa alidokezwa kuwa nia yazoezi hilo ilikuwa ni kuweka kumbukumbu za mashujaa wa harakati za uhuru iliwapate kuenziwa na taifa na wale ambao hali zao za kimaisha si nzuri wasaidiwena chama. Yusuf Olotu alifariki dunia tarehe 3 Juni, 1997 akiwa bado anasubiri kuenziwa na kupewa msukumo wamaisha. YusufNgozi hakuwa na elimu bali alikuwa mwananchi wa kawaida aliyethamini utu waMwafrika na mtu aliyechukia dhulma na fedheha ya kutawaliwa. Kilimanjaroilikuwa inasifika kwa kuwa na Waafrika waliokuwa na elimu ya juu kabisa katikaTanganyika. Lakini wasomi hao walishughulishwa zaidi na maslahi yao binafsi.Wengi wao walikuja kujitokeza na kuingia chama cha TANU mwaka 1958 katikauchaguzi wa Kura Tatu. Wakati huo mambo yalikuwa shwari na Waingereza walikuwawamesalimu amri. Yusuf Ngozi labda kwa kuelewa mazingira ya Kilimanjaro alianzakujenga msingi wa TANU si kwa wanaume bali kwa akina mama. Hiki ni kitu azizisana katika historia ya kupigania uhuru. Katika historia ya TANU sehemu ambazochama kilipata nguvu kubwa sana ni zile sehemu ambazo kulikuwa na utamaduni waKiswahili wa vyama vya akina mama kama hapo Moshi mjini, Dar es Salaam, Tanga,Lindi na kwingineko. Joseph Kimalando mmoja katika wale waasisi 17 wa TANU aliogopakuitumikia TANU lakini alijiona amesalimika kuifanyia kazi United TanganyikaParty (UTP) – chama cha Wazungu kilichoundwa kuipinga TANU. Kimalando alitokaTANU na kujiunga na United Tanganyika Party (UTP) na akawa katibu wa chamahicho pale Moshi na Mohamed Kishikio Badi alikuwa Mwenyekiti wake. Yusuf Ngozialiwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTPhadi ikafa. Wanawakewale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi kwenyeofisi ya TANU. Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vyakisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya kadi za UTP nakumpelekea Rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwahawakitaki chama chake cha vibaraka. Yale masharti ya Kura Tatu yaani kipato,elimu na kazi ya maana, kwa wapiga kura na wagombea hayakuwasumbua Wachaggawengi kwani wao walikuwa ni watu waliokuwa na elimu na vipato vya kutosha. Kwamaneno mengine sheria ile (ambayo kwa sehemu nyengine kama vile Bagamoyoilikuwa ngumu) kwa Wachagga ilikuwa nyepesi na hivyo kuruhusika kupiga kurapasi na pingamizi. Lakini kwa bahati mbaya sana iliingia fikra kuwa mashartiyale ya kupiga kura na hasa kile kipengele cha kipato ilikuwa njama ya serikaliya wakoloni kutengeneza orodha ya Wachagga ili wawatoze kodi ya mapato.Wachagga ni wafanya biashara wazuri na watu wenye bidii kubwa katika kilimo.Hiki kipengele cha kipato kiliwaweka wana – TANU wa Uchaggani –wafanyabiashara, wafugaji na wakulima wa kahawa katika hofu kubwa. Hulka yakuthamini mali ilikuwa imefifilisha umuhimu mzima wa watu wa Kilimanjaro kupigakura ili TANU ichukue viti katika Baraza la Kutunga Sheria. Tatizola Uchaggani sasa likawa ni la kipekee. Kazi kubwa hapa ilikuwa ni kubadilishafikra za watu na kuwatoa hofu ya kulipa kodi kwa mali zao na kuwafanya kuonaukweli wa umuhimu wa kuishinda UTP na kumng’oa Mwingereza Tanganyika. Hilililikuwa tatizo ambalo TANU hawakukutana nalo mahali popote katika Tanganyikana wala hawakulitegemea. Hata katika mkutano wa Tabora kujadili juu ya KuraTatu hakuna kumbukumbu yoyote inayoonyesha kuwa kuna Waafrika ambao watashindwakutumia haki yao ya kupiga kura kwa kuwa na fedha nyingi. Tatizo ilikuwa nikinyume chake. Tatizo la TANU katika majimbo mengine lilikuwa ni kuwafanya watuwakubaliane na masharti yale magumu ya kibaguzi katika kupiga kura ili chamakiingie katika uchaguzi. Katika hali ya kawaida mtu angalitegemea kuwawatakaosimama ni wale wasomi wa Makerere kuwaeleza wananchi hali ya mambo namwelekeo wa nchi. Katu, hao hawakusimama. Alikuwa Yusuf Ngozi aliyehamasisha.Alitembea Kilimanjaro nzima na kuwaeleza watu kuwa, kama hawatajiandikishakuipigia kura TANU na kumuunga mkono Julius Nyerere katika vita dhidi yaWaingereza, basi wajue kuwa UTP itashinda na Waingereza wataendelea kuitawalanchi hii. Sehemu nyingine alikuwa akiwafahamisha Waafrika wenye biasharandogondogo kuwa wao vilevile wana kazi na kipato kinachokidhi masharti yaupigaji kura kwani hesabu zao za mwaka zilikuwa zinapita kile kiwango cha paunimia nne. YusufNgozi aliikuta hali hii kwa mafundi cherehani huko Kahe – kijiji kidogo nje yaMoshi. Mafundi hawa walijihesabu hawana kazi ya maana wala kipato cha pauni mianne kwa mwaka. Mzee Yusuf Ngozi aliwasomesha na kuwaonyesha kuwa walikuwa nakazi ya maana na kipato cha kutosha. Hivyo aliwanasihi wasiache kujiandikishana kuipigia kura TANU. Sehemu nyingine Yusuf Ngozi alikuwa na propaganda yakeya kutisha. Alikuwa akiwauliza wananchi kama wao walikuwa wako tayari kuishikatika nchi yenye bendera tatu. Yusuf Ngozi wakati mwingine alikuwa akiachaKiswahili na kuhutubia Kichagga ili ujumbe ufike vuzuri.Katikauchaguzi ule wa Kura`Tatu Jimbo la Kaskazini TANU ilimsimamisha Enesmo Eliufookwa kiti cha Moshi na Sophia Mustapha alisimamishwa Arusha. Yusuf Ngozialiifanyia kampeni TANU kwa ufanisi mkubwa na TANU iliweza kushinda kwa kuranyingi sana na wajumbe wake kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria. TANUilishinda ule uchaguzi wa kura tatu UTP ambayo ilikuwa na nguvu sana huko Tangailikiri kushindwa. David Emmanuel, mwenyekiti wa UTP akitambua ukweli kuwahakukuwa na mategemeo yoyote kwa chama hicho pale Tanga, na kama ishara yapekee kabisa ya ukarimu na moyo wa kutaka maelewano mema, alikusanya samaniyote iliyokuwa ndani ya ofisi ya UTP na kuitunukia TANU. Lucy Lameck mojawapowa wanasiasa maarufu waliopata vyeo na kuwa mawaziri katika Tanganyika huru kwajuhudi za Mzee Yusuf Olotu Ngozi."

Mohamed
 
Albedo,

Wazee wangu wa Gerezani hawakufika Mgombani kule alifika mzee wangu mwingine wa Mtaa Chini Moshi Mjini akiitwa Yusuf Olotu pamoja nae walikuwa Mama Bint Maalim, Halima Selengia na wengineo. Soma habari zao hapa chini:

"Historiaya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kama walivyoshiriki wananchi waKilimanjaro haiwezi kamwe kukamilika bila ya kutaja jina la Yusuf Olotu aumaarufu Yusuf Ngozi. Yusuf Olotu ndiye aliyeiwezesha TANU kupata ushindi mkubwakatika uchaguzi wa kura tatu mwaka 1958. Jina hili la Ngozi alilipata kwa kuwaalikuwa akifanya kazi katika kampuni ya kuuza ngozi. Uchagga ilikuwa chini yautawala wa machifu waliokuwa wakijulikana kama Mangi. Baadhi ya machifu hawawalikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria na kwa ujumla wao walikuwa karibu naserikali ya kikoloni kuliko walivyokuwa na wananchi wanaowaongoza. Hali yasiasa katika Jimbo la Kaskazini ilikuwa ngumu na ya kukatisha tamaa. WakatiTANU inakabiliwa na Kura Tatu mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umemalizikakwa wananchi kudhulumiwa haki yao. Japhet Kirilo alikuwa tayari amerudi mikonomitupu kutoka Umoja wa Mataifa alikopeleka madai ya Wameru. Kirilo hakuwa nachochote cha kuwaonyesha Watanganyika. Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye aliyewezakuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo akaienezavijijini. Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf Ngozi ndipo unapokutana na historiaza awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata majina na vyeo na wengine kuwa mawazirikatika Tanganyika huru. Mfano wao ni Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.Ilikuwa ni Yusuf Ngozi pamoja na wazalendo wengine walioifanya TANU ishindeuchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958. Kupitia kumbukumbu zake, halikadhalika, ndipokwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika kama yeye mwenyewe,mashujaa wa kike na wa kiume na wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim, AminaKinabo, Halima Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika nawengineo. Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawalawa machifu wao na kujiweka chini ya TANU. Habariza kuenea kwa TANU Kilimanjaro na matatizo ya Kura Tatu zimeelezwa na YusufOlotu katika mahojiano aliyofanya na mwandishi nyumbani kwake Moshi tarehe 21Januari, 1989. Yusuf Ngozi alimfahamisha mwandishi kuwa ofisi ya CCM Wilaya,miaka michache iliyopita walimuandikia barua kumuomba awape nyaraka zake zoteza mwanzo kuhusu TANU na awaandikie historia ya jinsi chama kilivyoenezwaKilimanjaro na mchango wake binafsi. Kazi hii aliifanya na akakabidhi nyarakahizo kwa CCM. Yusuf Ngozi alimfahamisha mwandishi kuwa alidokezwa kuwa nia yazoezi hilo ilikuwa ni kuweka kumbukumbu za mashujaa wa harakati za uhuru iliwapate kuenziwa na taifa na wale ambao hali zao za kimaisha si nzuri wasaidiwena chama. Yusuf Olotu alifariki dunia tarehe 3 Juni, 1997 akiwa bado anasubiri kuenziwa na kupewa msukumo wamaisha. YusufNgozi hakuwa na elimu bali alikuwa mwananchi wa kawaida aliyethamini utu waMwafrika na mtu aliyechukia dhulma na fedheha ya kutawaliwa. Kilimanjaroilikuwa inasifika kwa kuwa na Waafrika waliokuwa na elimu ya juu kabisa katikaTanganyika. Lakini wasomi hao walishughulishwa zaidi na maslahi yao binafsi.Wengi wao walikuja kujitokeza na kuingia chama cha TANU mwaka 1958 katikauchaguzi wa Kura Tatu. Wakati huo mambo yalikuwa shwari na Waingereza walikuwawamesalimu amri. Yusuf Ngozi labda kwa kuelewa mazingira ya Kilimanjaro alianzakujenga msingi wa TANU si kwa wanaume bali kwa akina mama. Hiki ni kitu azizisana katika historia ya kupigania uhuru. Katika historia ya TANU sehemu ambazochama kilipata nguvu kubwa sana ni zile sehemu ambazo kulikuwa na utamaduni waKiswahili wa vyama vya akina mama kama hapo Moshi mjini, Dar es Salaam, Tanga,Lindi na kwingineko. Joseph Kimalando mmoja katika wale waasisi 17 wa TANU aliogopakuitumikia TANU lakini alijiona amesalimika kuifanyia kazi United TanganyikaParty (UTP) – chama cha Wazungu kilichoundwa kuipinga TANU. Kimalando alitokaTANU na kujiunga na United Tanganyika Party (UTP) na akawa katibu wa chamahicho pale Moshi na Mohamed Kishikio Badi alikuwa Mwenyekiti wake. Yusuf Ngozialiwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTPhadi ikafa. Wanawakewale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi kwenyeofisi ya TANU. Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vyakisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya kadi za UTP nakumpelekea Rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwahawakitaki chama chake cha vibaraka. Yale masharti ya Kura Tatu yaani kipato,elimu na kazi ya maana, kwa wapiga kura na wagombea hayakuwasumbua Wachaggawengi kwani wao walikuwa ni watu waliokuwa na elimu na vipato vya kutosha. Kwamaneno mengine sheria ile (ambayo kwa sehemu nyengine kama vile Bagamoyoilikuwa ngumu) kwa Wachagga ilikuwa nyepesi na hivyo kuruhusika kupiga kurapasi na pingamizi. Lakini kwa bahati mbaya sana iliingia fikra kuwa mashartiyale ya kupiga kura na hasa kile kipengele cha kipato ilikuwa njama ya serikaliya wakoloni kutengeneza orodha ya Wachagga ili wawatoze kodi ya mapato.Wachagga ni wafanya biashara wazuri na watu wenye bidii kubwa katika kilimo.Hiki kipengele cha kipato kiliwaweka wana – TANU wa Uchaggani –wafanyabiashara, wafugaji na wakulima wa kahawa katika hofu kubwa. Hulka yakuthamini mali ilikuwa imefifilisha umuhimu mzima wa watu wa Kilimanjaro kupigakura ili TANU ichukue viti katika Baraza la Kutunga Sheria. Tatizola Uchaggani sasa likawa ni la kipekee. Kazi kubwa hapa ilikuwa ni kubadilishafikra za watu na kuwatoa hofu ya kulipa kodi kwa mali zao na kuwafanya kuonaukweli wa umuhimu wa kuishinda UTP na kumng'oa Mwingereza Tanganyika. Hilililikuwa tatizo ambalo TANU hawakukutana nalo mahali popote katika Tanganyikana wala hawakulitegemea. Hata katika mkutano wa Tabora kujadili juu ya KuraTatu hakuna kumbukumbu yoyote inayoonyesha kuwa kuna Waafrika ambao watashindwakutumia haki yao ya kupiga kura kwa kuwa na fedha nyingi. Tatizo ilikuwa nikinyume chake. Tatizo la TANU katika majimbo mengine lilikuwa ni kuwafanya watuwakubaliane na masharti yale magumu ya kibaguzi katika kupiga kura ili chamakiingie katika uchaguzi. Katika hali ya kawaida mtu angalitegemea kuwawatakaosimama ni wale wasomi wa Makerere kuwaeleza wananchi hali ya mambo namwelekeo wa nchi. Katu, hao hawakusimama. Alikuwa Yusuf Ngozi aliyehamasisha.Alitembea Kilimanjaro nzima na kuwaeleza watu kuwa, kama hawatajiandikishakuipigia kura TANU na kumuunga mkono Julius Nyerere katika vita dhidi yaWaingereza, basi wajue kuwa UTP itashinda na Waingereza wataendelea kuitawalanchi hii. Sehemu nyingine alikuwa akiwafahamisha Waafrika wenye biasharandogondogo kuwa wao vilevile wana kazi na kipato kinachokidhi masharti yaupigaji kura kwani hesabu zao za mwaka zilikuwa zinapita kile kiwango cha paunimia nne. YusufNgozi aliikuta hali hii kwa mafundi cherehani huko Kahe – kijiji kidogo nje yaMoshi. Mafundi hawa walijihesabu hawana kazi ya maana wala kipato cha pauni mianne kwa mwaka. Mzee Yusuf Ngozi aliwasomesha na kuwaonyesha kuwa walikuwa nakazi ya maana na kipato cha kutosha. Hivyo aliwanasihi wasiache kujiandikishana kuipigia kura TANU. Sehemu nyingine Yusuf Ngozi alikuwa na propaganda yakeya kutisha. Alikuwa akiwauliza wananchi kama wao walikuwa wako tayari kuishikatika nchi yenye bendera tatu. Yusuf Ngozi wakati mwingine alikuwa akiachaKiswahili na kuhutubia Kichagga ili ujumbe ufike vuzuri.Katikauchaguzi ule wa Kura`Tatu Jimbo la Kaskazini TANU ilimsimamisha Enesmo Eliufookwa kiti cha Moshi na Sophia Mustapha alisimamishwa Arusha. Yusuf Ngozialiifanyia kampeni TANU kwa ufanisi mkubwa na TANU iliweza kushinda kwa kuranyingi sana na wajumbe wake kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria. TANUilishinda ule uchaguzi wa kura tatu UTP ambayo ilikuwa na nguvu sana huko Tangailikiri kushindwa. David Emmanuel, mwenyekiti wa UTP akitambua ukweli kuwahakukuwa na mategemeo yoyote kwa chama hicho pale Tanga, na kama ishara yapekee kabisa ya ukarimu na moyo wa kutaka maelewano mema, alikusanya samaniyote iliyokuwa ndani ya ofisi ya UTP na kuitunukia TANU. Lucy Lameck mojawapowa wanasiasa maarufu waliopata vyeo na kuwa mawaziri katika Tanganyika huru kwajuhudi za Mzee Yusuf Olotu Ngozi."

Mohamed

Asante Mo

Ina Maana Hawa Wazee wangu wa Rombo kabla ya 1958 walikuwa Wamelala mpaka walipokuja kuamshwa na akina Olotu? Namaanisha akina Olotu walivyokwenda Mgombani hawakukuta kweli Harakati zozote? Maana Wazee wangu wananiambia kulikuwa na harakati za Kujinasua toka Makucha toka ya Mjerumani
 
Mwita. Umeiona tofauti? Wewe ulipowakalia kooni ukachukuliwa 2nd take. Mimi wazee wangu hawakuwa na uwezo wako wa "kuwakalia kooni" walienda kiungwana na walichojibiwa ndio hicho, ni "repeat". Hapo sasa panakuonesha tofauti ukiwa Muislaam unakuwa treated vipi.

Lakini, kwa sasa nashkuru kuwa sikupelekwa walipopataka wao na siku "repeat" na nikaipata hiyo elimu kwingine tena nna uhakika kwa ubora zaidi. AlhamduliLlah.

Faiza usidhani kumkalia kooni afisa elimu wa mkoa ilikuwa kazi nyepesi hadi useme nilikuwa treated tofauti na wewe. Baada ya kubaini kwamba nilikuwa nimefaulu, mzazi wangu hakukubali kamwe kusikiliza story na uzingatie miaka hiyo nafasi za sekondari zilikuwa chache sana. Nakumbuka wilaya yetu ilikuwa inapata nafasi 106 tu za sekondari, hatukuwa na sekondari ya kutwa wilayani kwetu, tulipigania nafasi hizo chache katika shule za bweni zilizokuwa nje ya wilaya yetu na zile nafasi za shule za kitaifa kama moshi tech, ilboru, ihungo, tabora boys & girls, msalato n.k

Katika kupigania haki yangu ya kusoma, baba yangu alifunga safari toka Tabora alipokuwa akilitumikia taifa- JWTZ, hadi kwa afisa elimu wa mkoa wa Mara, akiwa amepiga kombati mwanzo mwisho!! Afisa elimu hakuwa na namna nyingine zaidi ya kunipeleka shule. Ni bahati mbaya kwamba wazazi wako hawakukomaa, kwahiyo utaona kwamba si suala la kuwa muislamu bali haki yangu ilitaka kuporwa na mzazi wangu akasimama imara kuipigania.

Katika hili Nyerere hahusiki hata kidogo, kwani hata tangu tuanze kutumia namba kwenye mitihani mambo yamebadilika? kama Nyerere ndo alikuwa akitumia u superpower wake kuwadhulmu waislamu, hata baada ya yeye kung'atuka mbona mnadai dhulma bado ipo??
 
Asante Mo

Ina Maana Hawa Wazee wangu wa Rombo kabla ya 1958 walikuwa Wamelala mpaka walipokuja kuamshwa na akina Olotu? Namaanisha akina Olotu walivyokwenda Mgombani hawakukuta kweli Harakati zozote? Maana Wazee wangu wananiambia kulikuwa na harakati za Kujinasua toka Makucha toka ya Mjerumani

Albedo,

Harakati zilikuwako Kilimanjaro akina Mzee Aekaeli Mbowe katoa nyumba yake nzima kufanya ofisi ya TANU. Hiyo nilikuwekea kukuonyesha wazalendo waliokuwa huko kwenu.

Kama nimekuudhi niwie radhi. Naona lugha yako ni ya mapambano zaidi kuliko kujadili tukanufaika sote. Ukifanya subra na mimi
nitakupa mengi na utatoka ndani ya ukumbi ukiwa mjanja kuliko ulivyoingia.

Mohamed
 
WC,

Inaelekea husemi kweli. Ungesoma kitabu changu ungekutana na "Muslim symbols" nyingi ndani lau kama TANU ilifuata "a nationalist secularist ideology." Soma hii:
"Kwa ajili ya wasiwasi huu, viongozi waTANU wa Tanga walimuomba Nyerere wawe pamoja ili ifanywe tawaswil waombe msaadawa Allah awape ushindi dhidi yaa vitimbi vya Waingereza. Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji chaMnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lililokuwa na nguvu sanalikiongozwa na Mmaka Omari kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwakatibu. Mmaka alikuwa kijana aliyekuwa akiendesha mgahawa pale kijijini naAkida bin Dai alikuwa mwashi. Akida aliongoza tawi la vijana wa TANU ambalobaadae lilikuja kujulikana kama Tanga Volunteer Corps (TVC). TVC ilikuwasawasawa na Bantu Group, ambayo wakati huo ilikuwa imekwishaanzishwa huko Dares Salaam na Tabora. Vikundi hivi mbali na kufanya shughuli za propaganda nakuhamasisha wananchi halikadhalika viliifanyia TANU ujasusi. Nyerere naKissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuriakisomo hicho walikuwa Abdallah RashidSembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwanaaliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari.Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh AliKombora."

Nakuongeza na hii nyingine:
"Lakini matukio mawili ya kumbukumbu kubwayalikuwa katika safari ya pili ya Nyerere alipozuru tena Jimbo la Kusini.Kumbukumbu ya kwanza ilikuwa tawaswil aliyosomewa Nyerere na Sheikh Yusuf Badimwenyewe pamoja na Waislam aliowachagua yeye sheikh mwenyewe maalum kwa haflahiyo, pamoja na waliochaguliwa na masheikh wengine.[1] Kumbukumbu ya pili ni ilekaramu iliyoandaliwa kwa heshima yaNyerere na Mussa Athumani Lukundu, kiongozi wa Dockworkersí Union. Hii ilikuwaheshima kubwa aliyoonyeshwa Nyerere, ilikuwa kilele cha upendo na heshima kwaMuislamu yoyote anaweza kumfanyia asiyekuwa Muislamu.Siku ya ukumbusho mkubwa sana mjini Lindiilikuwa siku ya uhuru, tarehe 9 Desemba, 1961. Sheikh Badi, bingwa wa mashairi,aliombwa na TANU kuandika hotuba ya uhuru itakayotolewa na Yusuf Chembera mbeleya DC akiwa kama mwakilishi wa utawala wa Kiingereza uliokuwa ukingíoka. Hotubahiyo ya Sheikh Badi na iliandikwa kwa Kiarabu na Chembera. Akiwa mtoto mdogoChembera alipelekwa kwa Sheikh Yusuf Badi na baba yake kwenda kusoma elimu yadini na aliendelea kuwapo hapo chuoni kwa Sheikh Badi hadi alipohitimu. SheikhBadi hakuona kama ipo hotuba yoyote iliyoandikwa na mwanadamu iliyostahikihafla kama ile ya siku ya kujikomboa kutoka minyororo ya ukoloni. Sheikh Badialimsomea mwanafunzi wake Chembera, dua ya kunut ambayo husomwa na Waislamkatika kila sala ya alfajir. Usiku wa manane wa tarehe 9 Desemba, 1961 ulikuwausiku adhim sana kwa wote wawili, mwalimu na mwanafunzi wake, pale watuwalipokusanyika katika ule uwanja wa gofu na kumsikiliza Chembera akisoma kunutkupokea uhuru wa Tanganyika. Lakini mara tu baada ya uhuru Wakristo walianzakuuchimba ule waliouona kuwa uongozi wa Waislam katika TANU kwa kisingizio kuwauongozi ule haukuwa na elimu. Suleiman Masudi Mnonji alikamatwa na kutiwakizuizini kwa amri ya Nyerere chini ya Preventive Detention Act ya mwaka 1962kwa kile kilichoitwa ëkuchanganya dini na siasaí na Waislam wengine waanzilishiwa harakati za kudai uhuru walitupwa nje ya uongozi."
Na hii ya kuhitimisha:
"Katika mikutano ya TANU katika zile sikuza mwanzo, kabla Nyerere au Bibi Titi kuhutubia umma, Sheikh Suleiman Takadiralikuwa akisimama na kuomba dua. Kwa kawaida alikuwa akisoma ghaibu SuratFatihah, sura ya kwanza katika Qurían Tukufu: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi waRehema, Mwenye Kurehemu. Kila sifa njema ni milki yake Mwenyezi Mungu, Mola waUlimwengu wote. Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Mfalme wa siku ya Hukumu.Wewe tu ndiyo tunayekuabudu na wewe tu ndiyo tunakuomba msaada. Tuongoze katikanjia iliyonyooka, njia ambayo umewaongoza wale uliowaneemesha, si ya waleuliowaghadhibikia wala ya wale waliopotea."Hii ni dua ambayo kwa kawaida husomwa naWaislam kabla ya kuanza jambo lolote la kheri. Wakati Sheikh Takadir akisomadua hii watu walikuwa wima mikono yao juu wakimshukuru Allah. Baada ya hapoNyerere au Bibi Titi, kutegemea na ujumbe maalum uliotaka kutolewa katika sikuhiyo, alikuwa akisimama na kuhutubia.

Mohamed

Mohamed,
Haya ya kuomba dua ndio mchango wa UISLAMU kuleta UHURU wa NCHI yetu? Hizi dua bado zipo na zinaendelea. Kwenye viapo vya teuzi za Rais wetu watu wanashika Quran au Biblia. Haya mambo hayajatusaidia kuzuia wizi, rushwa wala ufisadi! Miji yote unayotaja hapa wakazi wake wengi enzi hizo walikuwa WAISLAMU pia. Ondoa UDINI kwenye hoja zako ili wazee wetu wasijetengwa na jamii zingine wakidhani haya unayoyaandika na kuyahubiri ndio ulikuwa msimamo wao pia. Mwalimu, pamoja na UKRISTO wake unaomtuhumu alijichanganya na kukubalika sana kwa wazee wetu hawa. Baada ya uhuru kupatikana wote wasingekuwa Marais au mawaziri au ulitaka aunde kitu kinachofanana na Baraza la Mapinduzi kule Zanzibar?
 
Huko umekwenda wewe mie haja ni kuonyesha mchango wa wazee wangu katika uhuru wa Tanganyika hata kama historia rasmi hawamo basi angalau watu wawajue kuwa alikuwepo Sheikh Yusuf Badi, alikuwepo Salum Mpunga, alikuwepo Yusuf Chembela nk.

Naona hii inakuuma kidogo lugha ghafla imebadilika si ile ya kutia shaka tena hii ni nyingine.

Zipo nyingi sana kama hizo.

Insha Allah taratibu nitaziweka hapa kwa faida yetu kila itakapobidi.

Ama hilo la udini nishajibu mara kadhaa kuwa mabuku mengi yameandikwa
jinsi Kanisa lilivyosaidia kutokomeza biashara ya utumwa nk. nk.

Sisi hatujasema huo udini.

Iweje leo kuandika mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika iwe udini?

Mohamed
 
MM,

Insha Allah nitajitahidi:
"TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongoziwa Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri.Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba.TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakatiuongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama chasiasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifakudai uhuru. Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa. Baada yaVita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katikamashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika. Vilevile aliwakusanyawapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao. Ilikuwa kupitia juhudi zakebinafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonjialijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama. Mnonji kwakutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta NangwandaSijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chamacha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa AthumaniLukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyamavya wafanyakazi. Ingawa vyama hivi viwili, yaani TAA na Dockworkersí Unionvilikuwepo katika mji mmoja, siasa za hiki chama cha pili cha wafanyakazibandarini hazikupitia TAA kama ilivyokuwa mjini Dar es Salaam. Hii kidogoilidhoofisha mwamamko wa siasa kwa wananchi. Jimbo la Kusini lilikuwa katikausingizi mzito wakati sehemu nyingine Tanganyika zilikuwa zikipiga hatua kwendambele zikiandaa vita dhidi ya utawala wa kikoloni. Chanzo cha usingizi huumzito huko kusini ulikuwa na asili yake katika historia ya Tanganyika.Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini yaTanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zilesehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yakewakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi yawazalendo. Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumaniulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vyaKiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonariwalikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituovyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji. Kutokana mashambulizi haya,Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakatiza Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya fisadi kubwa dhidi ya wananchina viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwaupande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi waowakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni. Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwakusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chiniya himaya ya wamishonari walipupazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baadaya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndaniya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vileshule na hospitali. Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kamamabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu lasiasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislamkufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni waWajerumani. Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyovionaVita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizowa zinakuja tenakwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu. TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwasafari hii Waislam walikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kamawalivyoanzisha vita na Wajerumani. TANU ilipoanzishwa mjini Dar es Salaam nahisia za utaifa zilipokuwa zikipandapole pole katika fikra za wananchi katika sehemu nyingi za Tanganyika, Jimbo laKusini lilikuwa bado usingizini likiishi katika zama za kale. Mnonji na Waziri, kwa sababu ya utu uzima wao, darajayao katika jamii na hasa kutokana na kuhusika kwao katika siasa za pale mjini,walikuwa na nguvu kubwa katika TAA. Wakati TANU imeshachukua nafasi ya TAA,uongozi wa TAA Lindi haukutaka kufungua tawi la TANU. Mtu wa kwanzakuutanabaisha uongozi wa TAA mjini Lindi juu ya mageuzi yaliyokuwa yakitokeaTanganyika na kuanzishwa kwa chama kipya cha siasa mjini Dar es Salaam alikuwaAbdallah Juma Makopa, kijana kutoka Tanga akifanya kazi ya ukarani Posta yaLindi. Makopa aliwaendea Mnonji na Waziri na kuwajulisha kuhusu kuanzishwa kwaTANUmjini Dar es Salaam na aliwashauri waanzishe TANU pale Lindi. Jambo hilolilipingwa moja kwa moja na Mnonji, Waziri, Said Nassoro, Abdallah Mhuji nawanachama wengine wa TAA.Chama cha Waafrika ambacho kilianzishwasiku nyingi mjini Lindi na kwa hakika ndicho kilikuwa chama cha pekeekushughulikia maslahi ya Waafrika sehemu za kusini kilikuwa African WelfrareAssociation ambacho mlezi wake alikuwa John Nevi, Mjaluo kutoka Kenya na katibuwake alikuwa Casian Njunde, Mngoni wa Songea. Makopa aliposhindwa kukishawishikile kikundi cha wazee wa TAA aliwaendea Yusufu Chembera na Rashid SalumMpunga. Chembera alikuwa na umri wa miaka thelathini na nne na Mpunga alikuwakijana wa miaka ishirini na saba. Chambera alikuwa amesoma hadi shule ya msingina Mpunga alikuwa amemaliza madras. Chembera alikuwa akifanya kazi katikakantini ya Lindi Welfare Centre, wakati Mpunga alikuwa dereva wa lorialiyeajiriwa na mfanyabishara wa Kihindi. Makopa aliwashauri Chembera na Mpungajuu ya uwezekano wa kuwahamasisha wananchi wawaunge mkono ili tawi la TANUlifunguliwe pale mjini. Aliwaambia alitaka sana kufanya hivyo yeye mwenyewelakini asingeweza kwa sababu yeye alikuwa mtumishi wa serikali na hakuwaakifahamika sana mjini. Uongozi kama wao ndiyo ungeweza kuaminiwa na wananchina usingetiliwa mashaka. Makopa, Chembera na Mpunga walikubaliana kuwa kabla yakuanza kufanya kampeni waziwazi kwa ajili ya TANU, lazima wawaandikishewanachama wachache kama waasisi wa chama. Mpunga na Chembera walimwandikishakijana mmoja akiitwa Abdallah Faraj na katika muda mfupi waliweza kuwapatatakriban wanachama kumi na tano walioridhia kujiandikisha kama wanachamawaasisi wa TANU.Baada ya kuandikisha wanachama waasisimkutano wa siri uliitishwa katika Welfare Centre ambako ndiko alikokuwaakifanya kazi Chembera. Chembera aliwaeleza kwa ufupi wale wanachama wa mwanzokuhusu malengo na madhumuni ya chama hicho kipya cha siasa. Mkutano huoulichagua kamati ya watu watatu yaani, Makopa, Chembera na Faraj ili kuwakabiliMnonji na Waziri kuwaleza kuwa TAA haipo tena nchini Tanganyika. Lengo lilikuwakuwasadikishia kuwa ilikuwa kazi bure na kupoteza wakati kujaribu kuihuisha TAAmjini Lindi wakati ambapo Tanganyika nzima ilikuwa ikisonga mbele na TANU.Baada ya mjadala mrefu sana na mkali wa wale vijana watatu na ule uongozi waTAA wa wazee, walikubaliana TANU lazima isajiliwe mjini Lindi.Uchaguzi ulifanyika na Shaaban Msangi,kijana wa Kipare akifanya kazi kwa Smith Mc Kenzie, alichaguliwa rais na AhmedSeif, katibu. Mpunga, Chembera, Mnonji na Idd Toto walichaguliwa wajumbe wakamati. Ahmed Seif alikuwa kijana ambaye ndiyo kwanza amemaliza shule, yeyealikabidhiwa kuendesha ofisi kwa niaba ya uongozi. TANU mjini Lindi ilimwajiri ili kukiandaachama kiweza kufanya kazi zake kwa ufanisi. Hassan Mohamed Kinyozi aliajiriwakama mhudumu wa ofisi. Hawa wawili walikuwa ndiyo wafanyakazi wa kwanza wa TANUwaliokuwa wakilipwa mshahara katika Jimbo la Kusini na wakawa miongoni mwawafanyakazi wachache sana walioajiriwa na TANU kwa wakati ule. Mnonji alitoanyumba yake katika mtaa wa Makonde kuwa ofisi ya kwanza ya TANU Jimbo laKusini. Baada tu ya kuanzishwa kwa TANU, Athumani Mussa Lukundu, kiongozi waLindi Dockworkersí Union, aliunganisha chama chake na TANU. Jambo hili, kwaTANU lilikuwa la kuitia moyo sana kwa sababu Dockworkersí Union ilikuwa nawananchama wengi na hatua ile iliongezea TANU nguvu.Baada ya muda mfupi tu toka kufunguliwakwa TANU Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TANU wa mwaka 1955 ulifuatia. Tawi la Lindililikuwa tayari lina uhusiano na makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam, nalilikuwa likitarajia kuhudhuria mkutano huo na kukutana na Julius Nyerere nauongozi mzima wa TANU pale makao makuu Dar es Salaam. Mpunga, mwanachamamuasisi wa TANU, na Ali Ibrahim Mnjale waliteuliwa kuhudhuria mkutano huo kamawajumbe kutoka Jimbo la Kusini. Halmashauri ya TANU ya Lindi iliwaelekezawajumbe hawa wafikishe ombi rasmi kwa makao makuu ili Julius Nyerere ajekufanya ziara kusini kwanza, kukutana na wananchi na kufanya kampeni kwa ajiliya TANU na pili aje kupambana na propaganda dhidi ya TANU zilizokuwazikitawanywa na Yustino Mponda. [1]Mponda akitumia uhusiano wake na serikali ya kikoloni na nafasi yake kamamjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala; na vilevile akitumia ushirikianowake wa muda mrefu na kanisa ambao bila shaka yoyote lilikuwa serikali ndani yaserikali kule kusini, alikuwa ameanza kampeni yake ya kuipinga TANU. Hilililikuwa likiathiri msukumo wa uanachama. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbewaliotumwa na Gavana Twining kwenda Umoja wa Mataifa Februari, 1955 kwa niabaya serikali ya kikoloni kwenda kuipinga. Uongozi wa TANU huko Lindi ulitakaNyerere aende kupambana na Mponda akiwa katika uwanja wake mwenyewe, ndanikabisa ya ngome ya Ukristo wa Kikatoliki katika Tanganyika.Mkutano mkuu wa mwaka wa TANU ulifanyikakatika ukumbi wa Hindu Mandal mjini Dar es Salaam. Siku kabla ya mkutano TANUilimwalika Gavana Edward Twining kwenye tafrija katika Ukumbi wa Arnatouglolakini alikataa kistaarabu na akamtuma Chief Secretary, Bruce Hutt,kumwakilisha. Baada ya mkutano, wakati wajumbe wengine wanaondoka kurudi kwenyemajimbo yao, Mpunga na Mnjawale walibakia nyuma kukutana na uongozi wa makaomakuu wa Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe,Said Chamwenyewe, Oscar Kambona na wengineo. Mpunga na Mnjawale waliwafahamishaviongozi wa makao makuu kuhusu hali mbaya ya siasa Jimbo la Kusini. Mbali nakampeni za kuipinga TANU za Mponda, katika ziara yake Lindi Gavana Twiningaliwatahadharisha Waafriika wa Tanganyika wasijihusishe na ëwafaanya fujowanaotaka kuzusha vuruguí. Twining alikuwa akitoa onyo hili akiikusudia TANUambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka uliopita. Hotuba hii ya Gavana iliwatishawananchi kujiunga na TANU. Mpunga na Mnjawale walisisitiza kuwa kuja kwaNyerere mjini Lindi kulitakiwa haraka sana kukabiliana na vyote viwili, kwanzaile hotuba ya gavana na pili zile kampeni za kupinga TANU zilizokuwazikiendeshwa na Liwali Yustino Mponda. Wakati huo Abeid Amani Karumealiyehudhuria ule mkutano alimwalika Nyerere afanye ziara Zanzibar. Kitu chakustaajabbisha ni kuwa, Nyerere alionekana kuiafiki zaidi ziara ya Zanzibarkuliko ile safari ya kwenda kusini kuiimarisha TANU. Mpunga alimsisitiziaNyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANUkupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzanimkubwa dhidi ya TANU. Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU.Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wotewaliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili. Baada ya kufikiamakubaliano, Mpunga na Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari yaNyerere. Ziara ya Nyerere ilikuwa ianzemuda mfupi kutokea hapo kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku za mwisho za kiangazi.Barabara sehemu ya kusini ya Tanganyika zilikuwa hazipitiki wakati wa masika,zikiitenga kabisa kusini toka sehemu zilizobaki za nchi. Ali Mwinyi Tambwe naRajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi nawoga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.Nyerere na msafara wake ulipokelewa nauongozi wa TANU wa Lindi huko Mbanji, kijiji kidogo nje ya mji. Msafara waNyerere ulipowasili Mbanji ilikuwa kiasi cha saa moja jioni hivi na gizalilikuwa linaanza kutanda. Mbali na Mpunga na wale wajumbe wawili waliokutanana Nyerere mjini Dar es Salaam mwezi uliopita, hakuna hata mtu kati ya umma uleuliokuja kupokea ujumbe kutoka makao makuu ya TANU aliyekuwa anajua Nyerereanafanana vipi. Mpunga, dereva wa lori, alijibagua kutoka kwa lile kundi lawatu akawa amesimama pembeni ili Nyerere apate kumuona. Baada ya Nyerere kumtiaMpunga machoni, Mpunga alimwendeakumsalimu Nyerere, Tambwe na Diwani; kisha aliligeukia lile kundi la watukumtambulisha Nyerere kwa wananchi akilitaja jina lake kwa sauti kubwa. Baadaya hapo aliutambulisha ule ujumbe wa Nyerere. Nyerere na ujumbe wakeulisindikizwa kwa shangwe na kundi la watu hadi ofisi ya TANU kwenye nyumba yaMnonji. Kupakana na ofisi ya TANU ilikuwepo nyumba ya seremala mmoja, Issa binAli Naliwanda. Hii ndiyo nyumba iliyochaguliwa alale Nyerere na ujumbe wake, sikwa sababu ilikuwa nzuri kupita zote. Ilichaguliwa na kupewa heshima hii kwasababu ilikuwa karibu sana na ofisi ya TANU na hivyo basi ilirahisishia TANU kaziya ulinzi wa Nyerere. Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili na Nyerere aliwaombawenyeji wake apelekwe kanisani kwa ajili ya ibada.Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo lafahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi. Lindi ulikuwa mji wa Waislam.Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwaakishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa. Watuwachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindikutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wamjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa nahaja ya kuhudhuria ibada pale kanisani. Hakuna mtu katika uongozi wa TANU waLindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote katiyao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikizaNyerere kanisani ili kumpa ulinzi. Baada ya kujadili suala hilo kwa urefuhatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga nawanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisanina wengine wabakie nje kulinda mlango.Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani yakanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwana Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu. Misa hii ëmaalumí ilidumu katika fikra za wale Wakristowaliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sanaWakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi. Hii huenda ilikuwamara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwaamesimamiwa na Waislam.DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANUkufanya mkutano wa hadhara. Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitishamkutano wa dharura wa tawi uliohudhuriwa na Nyerere na Tambwe. Baada ya mkutanohuo Tambwe alikwenda kumwona DC. Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku yaJumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwakammoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyoWaafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara. Kamwe haijapata kutokea kablaya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hichokujumuika mahali pamoja. Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwawamekaa na wengine wamesimama katika yajua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia. Ili kuhakikisha amani nausalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wamkutano. Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa nifedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao. Uingereza ilikuwaikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, nawakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe. TANUilikuwa imewasili Jimbo la Kusini."

Mohamed

Mzee Mohamed,

Ahsante sana kwa simulizi hii nzuri sana jinsi Nyerere alivyoishambulia ngome ya kanisa katoliki.

Kuna vitu vingi vya kujifunza hapa, nitajaribu kutaja vichache;

1. Imani waliyokuwa nayo waislamu wanaTANU juu ya Nyerere ni kubwa sana, hadi kufikia hatua ya kuingia kanisani kwa mara ya kwanza ili kumlinda.

2.Uaminifu wa Nyerere kwa waTanganyika wenzake ulikuwa ni wa juu sana,hadi kuwasukuma waislamu kutoka Lindi walipohudhuria mkutano wa Tanu dsm wakasisitiza umuhimu wa Nyerere kwenda Lindi haraka sana kujibu hotuba ya Gavana Twining na kujibu mashambulizi ya mkatoliki Mponda.

3.Kiwango cha juu cha ujasiri, weledi na uwezo wa kujenga hoja aliokuwa nao Nyerere, pale palipoonekana kuna ugumu wa kusukuma mbele gurudumu la mapambano ya kupata uhuru aliitwa Nyerere ili kulikwamua, hata mzee karume alimuomba aende unguja!

4.Nyerere hakuwa mdini bali alikuwa na mapenzi ya dhati kwa waTanganyika wenzake hadi kukubali kwenda kuibomoa ngome ya kanisa katoliki huku yeye mwenyewe akiwa mkatoliki.

Kwa ufupi ni hayo niliyoweza kuchuja toka kwenye simulizi hii, kama kuna jengine ambalo sijaling'amua mtaongezea wakuu. Hata Sheikh Mohamed unaweza ukaongezea neno hapo.
 
Umetoa uchambuzi mzuri pasi kifani.

Sasa cha kustaajabisha ni fitna gani iliingia kati ya Nyerere na watu hawa ikaja hata hataki kuwasikia wakitajwa katika historia ya TANU na wengine akawaweka kizuizini?

Karibu tutafikia kilele cha Tanzania Miaka 50 mashujaa hawa walopigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Nyerere wataenziwa?

Mohamed
 
Back
Top Bottom